Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Tatizo hamumjui Makonda. Tulieni kwanza.
Kwani ni mara yake ya kwanza kwa kutoa kauli zenye utata?
1. Ninawafahamu na nitawataja viongozi wote wanao uza madawa ya kulevya!!

2. Ni marufuku kwa wabunge wote kuja Dar wakati vikao vya bunge vinaendelea huko Dodoma!!

3. Ni lazima kwa Wanaume wote wa Dar wakapimwe tezi dume!!
 
Umeanza ujinga wako?

πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…Ujingwa upi na wewe!!! Mmepoa kama piritoni.. chadrama futi sita bado hautaki kujiokoa.. pokea πŸ’‰πŸ’‰πŸ’‰

Acha nianze kuburudika na haya...
Nakanyaga nakwenda.. 2025 huyooo.. na bado.. Tuombeane uzima tuwemo humu kama kawaida.

Makonda oyeee...
Kazi iendeleee
 
Makonda anatisha sana nadhani kwa sasa ndo mtu anayetajwa sana duh jamaa riziki yake ndefu sana
 
Makonda mara zote ni mtu mwenye mawazo finyu.
wa vyovyote Makonda ni mtu wa kitengo aliyevamia siasa.

Ni mtu atakumbukwa kumfanyia vurugu Waziri Mkuu na Makamu wa Rais mstaafu Joseph Sinde Warioba.

Alipokuwa RC Dar, atakumbukwa kwa kupora magari na viwanja vya wafanya biashara kwa kutumia jina la Rais Magufuli.
Aliingia figisu za watu na wanasiasa kubambikwa kesi za madawa ya kulevya.
Hatujasahau uhusika wake kutekwa kwa Mohammed Dewji, Mo.

Suala la kushambuliwa Tundu Lissu, kuna uhusika wa Makinda usiowekwa wazi.

Sasa tuseme tu, je Makonda pamoja na hisia za uchafu ndiye msemaji wa Taasisi ya Uraisi, au ametumwa kunena kuwa kuna watu wanamchafua Rais Samia.?

Kwa vyovyote Makonda anajikweza zaidi ya uwezo wake kisiasa.

Kutoa mawazo mbadala, kwa jambo lolote lile, si kumchafua mtu.

Ni tahadhari tu, kuwa kwa kumtumia Makonda Rais anachafuka zaidi.
 
Should we we wait to hear another leakage of recorded voices? Or even short videos?
that may be the story of next time πŸ’

but for now,
there is a very strong coded message behind a very able RC statement, as I have posed them in style of questions before πŸ’
 
kijana anafanya kazi nzuri, asifitinishwe na wazee wastaafu πŸ’
 
Tarehe 13 mwezi uliopita, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa msimamo wake kama mkuu wa nchi na wa CCM kuhusu 'makundi' na 'watoto' wake kisiasa.

Katika hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, Rais Samia alisema kwa umakini, umadhubuti na wazi kabisa kuwa yeye hana makundi wala watoto ndani ya chama chake na Serikali.

Rais Samia akaenda mbele na 'kuwakemea' wote wanaojitanabaisha kuwa ni watoto wa Mama au wa kundi la Mama. Alihitimisha kuwa viongozi wote kwa ujumla wao ni watoto wake.

Jana, kwenye Maadhimisho ya Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, RC Makonda amesikika akijitanabaisha kuwa yeye ni mtoto wa Rais Samia. Amesikika mara mbili akisema 'Mama yangu' kwenye kauli zake, tena mbele ya Rais Samia.

Kwanini Makonda atofautiane na kukinzana na msimamo wa Rais Samia kwa kujitaja kama 'mtoto wa Mama Samia'? Makonda alilenga au analenga nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…