Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

4sure mkuuu uko sahihi dogo Ana nyota sema anakosa wa kuilinda nyota yake
Bahatimbaya sheikh wetu amekufa ningemshauri aende magomenj kusafisha nyota yake
Mtu akiwadhalilisha wazee huwa anapata aina fulani ya laana kutoka kwa wale wazee mpaka akawaombe msamaha. !

Ile kutubu kwa Kiongozi wa dini haihusiani na makosa uliyowafanyia hao wazee !
Aende akawaombe msamaha hata kama ni wazee hohehahe !
Karma is a bitch !
 
Hiyo kazi maalum Ina faida Gani kwa nchi na wananchi wakati huu maisha ni magumu
 
Askofu kardinali mbariki watu alikuja na Uzi wake eti makondo ndiye raisi wa mwaka 2033, wenye akili tumemkatalia ujingaa na upumbavu wake
 
Huyu nafasi yake pekee anayofiti ni gerezani pekee achana na hizi drama zake anazotumia kuwahadaa masikini hadi wanadhani ni mtetezi wao!
Mliwahi kuyasema haya kwa lowasa, baadaye mkamzungushia mikono.

Mpumbavu tu anayeweza kuwaamini.
 
nani hajui jamaa anaelekea kufanywa mgombea wa rais 2025 , ndiye vp mtarajiwa hivi karibuni , nje mnamwona fala ila CCM ndani ana following na loyal base kubwa sana makonda
 
Sijawahi kuelewa kwanini Makonda huwa anahusishwa na nafasi za juu kabisa za uongozi ikiwemo nafasi ya Rais.

Hivi kumbe nafasi ya Rais ni nyepesi kiasi cha hadi mtu kama Makonda kuishika? Wanaomuwazia hayo huwa mnaangalia nini kwake?
 
Mteuzi ameonyesha udhaifu mkubwa katika kufanya maamuzi.
Makonda amekuwa na mtiririko wa matukio kuanzia alipompiga makofi makamu wa Rais na waziri mkuu mstaafu mzee Warioba anayeheshimika katika jamii na matukio mfululizo yanayomnyima nafasi ya kuwa kiongozi wa maamuzi.
Lakini pamoja na Rais Magufuli kuamua kumweka pembeni kimyakimya bado aliyekuwa msaidizi wake na kachukua nafasi baada ya kifo kadharau maamuzi ya kumuweka pembeni na kumrudisha.
Huo ni udhaifu wa kimaamuzi na kuivunjia heshima hadhi na utukufu wa kiti alichokalia kwa kudra za kifo cha mtangulizi.
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, na kilio na masononeko ya wazee kama Warioba ni laana kwa wahusika.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Makonda yupo vizuri
Tulipofikia Watanzania tunahitaji kiongozi mbabe ili kuwanyoosha hao wavivu na wezi wa mali za umma

Makonda aongezewe cheo..!
Makonda ana msururu wa magari ya kifahari kama sio wizi mtumishi wa umma kapuku aliyekaa kwa mzee sita, ameyapata wapi?

Kabla ya kuwa DC kinondoni makonda alikua anamiliki rav4 ! Ghafla bin vuuuu eti ana nyumba mikocheni! Mikocheni ploti alinunua kwa pesa ngapi.

Makonda ni mwizi nambari oni!
 
Nani anamtengeneza? Tangu tupate uhuru hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu kabisa ametengenezwa. Si Nyerere, si Mwinyi, si Mkapa, si Kikwete, si Magufuli wala si Samia. Viongozi wote huibuka. They emerge. Hawatengengenezwi. Fact.
 
Kazi yake ni kufanya mambo ambayo wana-ccm wengine hawawezi kuyafanya, ambayo ni yale kutoa kauli zenye utata na muksheliii kwa umma
 
Mliwahi kuyasema haya kwa lowasa, baadaye mkamzungushia mikono.

Mpumbavu tu anayeweza kuwaamini.
Na kinyume chake ni kuwa ccm nzima 2015 ilizunguka kwenye kampeni kumtusi na kumdhihaki Lowassa ikiongozwa na JK, Kinana, Nape nk lakini baadae ndio hiyohiyo ikampokea kwa tarumbeta ikiongozwa na Magu, Majaliwa na Bashiru pale Lumumba. Kwa hiyo ni nyie wapumbavu tuu ndio mnaweza kuwaamini hao.
Bangladeshi!
 
Inawezekana Ikawa kweli lakini kudra na hatma IPO mikononi mwa mwenyezi mungu!!

Ya Salim Ahmed Salim yamenifunza mengi,pale mfumo unapomuandaa mtu halafu kudra ya Mwenyezi ikagoma!!
 
Kwa hiyo ni nyie wapumbavu tuu ndio mnaweza kuwaamini hao.
Bangladeshi!
Mpumbavu ni mtu asiyeweza kuutumia ubongo wake kuhoji. Tuliwaona 2015 mkizungusha mikono bila kuhoji kwanini mbowe alifanya ujinga alioufanya.
 
Mama yake aitwe kwenye kamati ya maadili.
 
Makonda ni dodoki la jalalani, hana uongozi uliotukuka wala sifa za kuwa kiongozi mwadilifu.
 
Sijui Moderators mnachoka huyu jamaa anasema Makonda amemuibua Rais Mstaafu wakati aliyetangulia kusema ni Rais Mstaafu kwenye mkutano mkuu?Tulinde hadhi ya hii forum tusilete post za Facebook humu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…