Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Acha kumpa kichwa. Ajue za ndani kama nani?

Anaendeshwa na hulka za upumbavu ndiyo maana anaropoka hovyo.
Tunaelekea mwaka wa 10 mkimtukana Makonda. Since 2015 Makonda anatukanwa lkn yeye anapanda ngazi na kuendelea kupiga kazi.
 
Alilalamika lini?

Fuatililia hasa kipindi kile ndugai katoa kauli ya kupinga kukopa kopa
Pia kwenye ule mkutano wa wanawake chadema
Alipomwambia mbowe kua Kuna watu wapo ndani ya chama wanaompinga sio yeye tu hata Ccm wapo
 
Hi

Hilo nalo lina ukweli pia lakini kubwa ni kumtisha tu yule mama ili aogope atoe pesa kwa vikundi vya kumlinda nje ya mfumo maisha yaende. Tofauti ya alichofanya BASHITE ni sawa tu na Musiba tofauti ni namna ya kufikisha ujumbe tu
Inawezekana je hivyo vikindi kufanya kazi, taarifa wanapata wapi maana wenye taarifa sahihi ni walio kwenye mfumo.
 
Tupunguze chuki za wazi wazi kwa konda
Najua weng hatumpend ila ifike hatua tuache chuki zidi yake tuache afanye kaz
Jf kuna nyuzi zaidi ya 10 juu ya makonda mnaweza zani mnamshusha kumbe ndo mnazidi mpandisha na kumtengenezea jina zaidi na mwisho wa sku atakuja pata cheo kikubwa iv iv
Konda ni mkuu wa mkoa wa Arusha cheo ambacho ni kdg sana ebu wachni apige kaz
 
Maisha ya huyu kijana siku zote ni yale ya kumtegemea mtu wa juu. Hajawahi kuishi maisha ya peke yake.

Tangu anatoka kwao Kolomije, alifika mjini na kukishikisha kwenye familia ya marehemu Samweli Sitta, baadaye akaenda kwa marehemu Edward Lowasa, akahamia kwa kina Riz One, baadaye akamimbilia kwa JPM, na sasa yupo kwa Mama!

Huyu dogo mara zote hupenda kujishikisha sehemu ambayo itampa usalama wa kisiasa. Na akitoka kwa Mama ataangalia sehemu nyingine salama zaidi ya kujishikiza. Na hayo ndiyo maisha yake siku zote. Kiufupi huyu ni mmoja wa waanzilishi wa huu mfumo wa kuishi maisha ya kinafiki na kujipendekeza kwa watu wa ngazi za juu ili kunufaika kisiasa na kiuchumi.
Mimi nafikiri anatafuta namna ya kupewa U-RC Dar. Aweze kuwa karibu na Ikulu kama ilivyokuwa kwa Jiwe. Lengo lake kubwa ni kutaka kuunda kikosi maalum cha kuwatisha na kuwashughulikia wale wote watakaomkwamisha kwenye mipango yao kisiasa kwa kuwatengenezea fitna na hatimae kupata uhalali wa kuwateka kuwapoteza/kuwaondolea uhai. Na hili ni kwasababu Wanasiasa na Watu wengine maarufu wenye nguvu na ushawishi wana makazi ya kudumu Dar. Hivyo kwake itakuwa rahisi kuwashughulikia.

Nafikiri mtakumbuka wale jamaa aliokuwa nao wakati wa uvamizi wa Clouds TV ni wa wapi na hata wale waliomtokea Nape.

Kwa kifupi ni kwamba anataka kupewa kazi na Mama ya kuwashughulikia wale watakaoonekana ni kikwazo awake kuelekea twenty twenty five.
 
Tamko alilotamka Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni tamko mbaya sana na linaleta uchochezi na chuki. Ni aibu kutamka mbele ya kadamnasi ya watu kuwa kuna watu wanamtukana Mhe. Rais. Jambo hili alitakiwa amueleze Mhe. Rais kwa siri kubwa. Mhe. Rais Mkuu wa Mkoa wa Arusha hakufai ni bora umtumbue mapema atakuletea uadui mkubwa na Watanzania. Kikubwa anajipendekeza kwako.
 
Sio bure yeye ndiye anaetumwa!!
 
Wengine wanasema Samia mwenyewe ndiye kamtuma aseme hivyo. Ila yote kwa yote nafarijika sana Makonda anavyoivuruga CCM.
 
Tupunguze chuki za wazi wazi kwa konda
Najua weng hatumpend ila ifike hatua tuache chuki zidi yake tuache afanye kaz
Jf kuna nyuzi zaidi ya 10 juu ya makonda mnaweza zani mnamshusha kumbe ndo mnazidi mpandisha na kumtengenezea jina zaidi na mwisho wa sku atakuja pata cheo kikubwa iv iv
Konda ni mkuu wa mkoa wa Arusha cheo ambacho ni kdg sana ebu wachni apige kaz
Makonda ni mchochezi ametupwa arusha bado anataka kuwa WA dar
 
Huu sio mkakati wa siri wa kuwaondoa watu katika mijadala muhimu kwa wakati huu? Watu wanakuwa "derailed" kwa makusudi ili wasijadili kwa kina mapungufu ya Tume Huru ya Uchaguzi na pia DP kuanza kazi zake rasmi bandarini.

Makonda ni maarufu sana katika kuanzisha mijadala inayohusu matukio ya kwenye mitandao ya kijamii. Kwa hadhi ya hadhira ya jana haikuwa vyema kwake kama fanani kuzungumzia jambo hilo.

Maudhui makubwa aliyopaswa kujielekeza ilikuwa ni kuenzi maisha ya kizalendo ya Edward Moringe Sokoine. Yeye kama Kamishina wa Mkoa alipaswa kujikita zaidi katika hilo, kwa sababu mkoa wake umepewa heshima kubwa kwa kupokea ugeni mkubwa wa kitaifa ili kufanikisha kumbukizi ya shujaa huyu.
 
Makonda anaishi wa fitina, chuki, kujipendekeza na kujifanya yuko karibu na viongozi. Kiufupi ukimuondolea hayo, hana lolote la kumfanya kustahili kupewa nafasi anazopewa.

Bahati mbaya nchi yetu saivi tumeachana na masuala ya merit katika kupata nafasi za juu za uongozi badala yake tunazingatia uchawa, kujipendekeza, fitina, chuki na kujuana.

No wonder in very few years to come tunaweza kuja kuwa failed state kama hatujabadilika.
Acha kumtukana Rais
 
Ndugu zangu Watanzania,

Paul Makonda ni aina ya mtu ambaye Rais yeyote yule anayeingia madarakani hawezi kumuepuka au kutotaka kufanya naye kazi,ni kiongozi ambaye ni ngumu kumuweka kando muda wote. Kwa kiongozi yeyote yule wa ngazi ya Urais ni lazima atatamani tu kuwa na Makonda karibu yake katika kufanya naye kazi.

Hii ni kwa kuwa Paul Christian Makonda ni kiongozi mchapa kazi sana,ni kiongozi mbunifu sana,ni kiongozi mwenye moyo wa kujituma,ni kiongozi mwenye maono na kiu ya maendeleo,ni kiongozi wa kisasa na anayekwenda na wakati,ni kiongozi mwenye roho ngumu na moyo wa chuma katika kuhakikisha kuwa anasimamia kile anachokiamini katika kuwaletea matokeo chanya wananchi.

Paul Makonda ni Mwamba anayekupatia matokeo ya aina yoyote ile unayoyataka wewe kwa wakati husika.,ni kiongozi ambaye ni mwepesi wa kubadilika,anaweza kuwa yeyote yule unayemtaka wewe na katika mazingira ya aina yoyote ile,ni kiongozi ambaye anafiti katika mazingira ya aina yoyote ile,ni kiongozi ambaye anaweza kubadilisha chochote na kwa wakati wowote na kukupatia matokeo unayoyataka wakati wowote ule unaoutaka mwenyewe.

Mwamba Makonda ni kiongozi jasiri anayecheza katika Dunia yake ya ujasiri,viatu vyake vya ujasiri huwezi ukamvalisha mwingine na vikamtosha na kumuenea vyema na kukupatia kile ambacho Mwamba angekupatia., Mwamba ni kiongozi mtiifu na mnyenyekevu sana katika ufanyaji kazi wake na kwa mamlaka ,ni kiongozi mwenye nyota kali sana na ushawishi wa aina yake kwa watu.unaweza ukaziba masikio lakini ukabaki unamtizama kwa picha.jiulize ni kwanini anakubalika kwa kila Rais anayeingia madarakani?

Jibu ni kuwa watu majasiri na wa kaliba ya Paul Makonda ni nadra sana kuwapata katika jamii iliyojaa watu waoga,wanafiki,wambeya,wazushi, wachawi,wachonganishi,wenye kutegemea uchawi na ushirikina katika kufanikiwa ,wenye roho za kwanini na walio tayari kutoa uhai wa mtu kwa ajili ya mali au madaraka.Paul Makonda anabaki kuwa Paul Makonda.hafanani na Hana wa kufanana naye hapa nchini wala wa kufananishwa naye hapa nchini.hana mbadala wake wala wa niaba yake.ni ngumu sana kumpata mtu mwenye kuweza kuvaa viatu vya kila aina na saizi yoyote na uhusika wa aina yoyote na akakubalika kwa namna kubwa anayokubalika huyu Mwamba.

Makonda ni hazina kwa Taifa letu,ni karata ya kipekee sana kwa nchi,chama na serikali yetu. Ni kama komandoo anayetegemewa katika jeshi kuongoza mapambano mahali penye ngome ngumu ya adui.ni kiongozi ambaye wewe mpe kazi na nyenzo halafu muachie akufanyie kazi.ni lazima utapenda Mwenyewe na kutabasamu tu.ndio maana kila anapopewa majukumu ya aina yoyote ile ndani ya chama na serikali huwa analeta matokeo chanya na makubwa.jiulize Mwamba ametokea wapi? Ni wapi amewahi kupwaya? Jibu ni kuwa siku zote amekuwa mshindi na kubakia kileleni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Au kumwaminisha kuwa yeye ni mwema, mwambata na mtetezi kuliko wengine?
Amefanya uchawa hadharani....Kesho Rais akiondoka akaja mwingine huyu wa sasa atamwona Hana thamani, Rais asinamie maneno yake, wanaofanya uchawa watanyooka wenyewe
 
Tamko alilotamka Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni tamko mbaya sana na linaleta uchochezi na chuki. Ni aibu kutamka mbele ya kadamnasi ya watu kuwa kuna watu wanamtukana Mhe. Rais. Jambo hili alitakiwa amueleze Mhe. Rais kwa siri kubwa. Mhe. Rais Mkuu wa Mkoa wa Arusha hakufai ni bora umtumbue mapema atakuletea uadui mkubwa na Watanzania. Kikubwa anajipendekeza kwako.
We mjinga pengine hujui maana ya siasa. Wakati ule Januari jr anamtukana Jpm kwa vikatuni alikuwa anaviweka ikulu!? Kwanini hamtaki kukukubali kwamba Makamba jr na Nape ndo wanamtukana Rais?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Paul Makonda ni aina ya mtu ambaye Rais yeyote yule anayeingia madarakani hawezi kumuepuka au kutotaka kufanya naye kazi,ni kiongozi ambaye ni ngumu kumuweka kando muda wote. Kwa kiongozi yeyote yule wa ngazi ya Urais ni lazima atatamani tu kuwa na Makonda karibu yake katika kufanya naye kazi.

Hii ni kwa kuwa Paul Christian Makonda ni kiongozi mchapa kazi sana,ni kiongozi mbunifu sana,ni kiongozi mwenye moyo wa kujituma,ni kiongozi mwenye maono na kiu ya maendeleo,ni kiongozi wa kisasa na anayekwenda na wakati,ni kiongozi mwenye roho ngumu na moyo wa chuma katika kuhakikisha kuwa anasimamia kile anachokiamini katika kuwaletea matokeo chanya wananchi.

Paul Makonda ni Mwamba anayekupatia matokeo ya aina yoyote ile unayoyataka wewe kwa wakati husika.,ni kiongozi ambaye ni mwepesi wa kubadilika,anaweza kuwa yeyote yule unayemtaka wewe na katika mazingira ya aina yoyote ile,ni kiongozi ambaye anafiti katika mazingira ya aina yoyote ile,ni kiongozi ambaye anaweza kubadilisha chochote na kwa wakati wowote na kukupatia matokeo unayoyataka wakati wowote ule unaoutaka mwenyewe.

Mwamba Makonda ni kiongozi jasiri anayecheza katika Dunia yake ya ujasiri,viatu vyake vya ujasiri huwezi ukamvalisha mwingine na vikamtosha na kumuenea vyema na kukupatia kile ambacho Mwamba angekupatia., Mwamba ni kiongozi mtiifu na mnyenyekevu sana katika ufanyaji kazi wake na kwa mamlaka ,ni kiongozi mwenye nyota kali sana na ushawishi wa aina yake kwa watu.unaweza ukaziba masikio lakini ukabaki unamtizama kwa picha.jiulize ni kwanini anakubalika kwa kila Rais anayeingia madarakani?

Jibu ni kuwa watu majasiri na wa kaliba ya Paul Makonda ni nadra sana kuwapata katika jamii iliyojaa watu waoga,wanafiki,wambeya,wazushi, wachawi,wachonganishi,wenye kutegemea uchawi na ushirikina katika kufanikiwa ,wenye roho za kwanini na walio tayari kutoa uhai wa mtu kwa ajili ya mali au madaraka.Paul Makonda anabaki kuwa Paul Makonda.hafanani na Hana wa kufanana naye hapa nchini wala wa kufananishwa naye hapa nchini.hana mbadala wake wala wa niaba yake.ni ngumu sana kumpata mtu mwenye kuweza kuvaa viatu vya kila aina na saizi yoyote na uhusika wa aina yoyote na akakubalika kwa namna kubwa anayokubalika huyu Mwamba.

Makonda ni hazina kwa Taifa letu,ni karata ya kipekee sana kwa nchi,chama na serikali yetu. Ni kama komandoo anayetegemewa katika jeshi kuongoza mapambano mahali penye ngome ngumu ya adui.ni kiongozi ambaye wewe mpe kazi na nyenzo halafu muachie akufanyie kazi.ni lazima utapenda Mwenyewe na kutabasamu tu.ndio maana kila anapopewa majukumu ya aina yoyote ile ndani ya chama na serikali huwa analeta matokeo chanya na makubwa.jiulize Mwamba ametokea wapi? Ni wapi amewahi kupwaya? Jibu ni kuwa siku zote amekuwa mshindi na kubakia kileleni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Mumeo huyo
 
Back
Top Bottom