Tarehe 13 mwezi uliopita, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Dr. Samia Suluhu Hassan alitoa msimamo wake kama mkuu wa nchi na wa CCM kuhusu 'makundi' na 'watoto' wake kisiasa.
Katika hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, Rais Samia alisema kwa umakini, umadhubuti na wazi kabisa kuwa yeye hana makundi wala watoto ndani ya chama chake na Serikali.
Rais Samia akaenda mbele na 'kuwakemea' wote wanaojitanabaisha kuwa ni watoto wa Mama au wa kundi la Mama. Alihitimisha kuwa viongozi wote kwa ujumla wao ni watoto wake.
Jana, kwenye Maadhimisho ya Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, RC Makonda amesikika akijitanabaisha kuwa yeye ni mtoto wa Rais Samia. Amesikika mara mbili akisema 'Mama yangu' kwenye kauli zake, tena mbele ya Rais Samia.
Kwanini Makonda atofautiane na kukinzana na msimamo wa Rais Samia kwa kujitaja kama 'mtoto wa Mama Samia'? Makonda alilenga au analenga nini?