Kujua kipi useme, useme wapi, wakati gani, na kwenye mazingira gani, kunahitaji akili ya kiwango fulani. Kama huna hiyo akili utabakia kuropoka chochote, wakati wowote na mahali popote.
Rais Samia ameyataka mwenyewe. Hakuna aliyemlazimisha amteue Makonda kwenye nafasi yoyote ile. Haya ni madogo, asubirie makubwa zaidi. Magufuli aliamua kuachana naye kabisa alipokuja kugundua kuwa aliyekuwa anamwamini alikuwa tapeli. Akaenda kugombea ubunge huku akiwadanganya watu kuwa ametumwa na Magufuli agombee ubunge ili ateuliwa kuwa Waziri wa mambo ya ndani. Hayati Magufuli alipoambiwa, aling'aka na kusema kuwa yeye hajamtuma mtu yeyote akagombee ubunge. Ndipo akaomba arudi kwenye ukuu wa mkoa, marehemu akamkatalia katakata, wakati huo akiwa tayari amefikishiwa taarifa kuwa jamaa amewatapeli GSM nyumba kwa kuwadanganya kuwa Rais alikuwa ameomba wamjengee, kumbe ni yeye ndiye aliyekuwa anahitaji kujengewa nyumba. Hapo akawa takataka mbele ya JPM.
Samia, takataka aliyoitupa mtangulizi wake, ameiona lulu. Asubirie kashfa zitakazompata kwa kupitia huyu mtu. Atapora magari, fedha na nyumba za watu kwa kutumia jina la anayemwita eti ni mama yake. Rais ameyataka mwenyewe, hajajua kuwa tumbili huwa hafugiki.