Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kuwa Disemba 09, 2024 wakati Tanzania itakapokuwa inaadhimisha Miaka 63 ya Uhuru, Mkoani Arusha kutafanyika Kongamano kubwa la maombi la kuombea Mkoa wa Arusha dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoikumba mkoa huo
Makonda ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Arusha, akisema katika maadhimisho hayo kutafanyika pia matembezi maalum kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yakijumuisha Viongozi hao wa dini na wananchi wa mkoa wa Arusha.
"Tutatembea kwa pamoja maeneo mbalimbali mkoani Arusha tukiwa na bendera, tukitamka maneno ya baraka na maombezi kwa Mkoa wetu wa Arusha tukiombea amani, baraka, biashara zetu pamoja na kizazi tukitakacho mkoani Arusha." Amesema Mhe. Makonda.