Paul Makonda: Tutakachofanya Tarehe 9 Disemba jijini Arusha hata wakisema ni uchawi poa tu

Wacha nianze kusali na kufunga ili roho mtakatifu awe nami ili nikiudhuria huko siku hiyo ni kukemea tu mpaka wadudu wote wakimbie mkoa
 
Dini ipo kwaajili ya kuwakupambaza wajinga, safi sana mkuu wa mkoa hiyo ni karata nzuri sana unaicheza.
 
Uyu promota wampeleke Ruvuma uko
Hivi sisi wa Ruvuma unatuonaje? Kwanza umeishawahi kufika huku kweli?

Mheshimiwa anatimiza wajibu aliotumwa na Rais Hata akija huku kwetu atatimiza wajibu huo huo!!!
 
Bashite ni tapeli!

Unanunua bendera laki Moja ndogo na kubwa elfu kumi?

Hizo fedha,ungenunulia watoto yatima vyakula na nguo,ungebarikiwa
 
Dini ipo kwaajili ya kuwakupambaza wajinga, safi sana mkuu wa mkoa hiyo ni karata nzuri sana unaicheza.
Hakika .
Ipo siku moja nitawasimulia kisa Cha Mimi kwenda chimbuko letu lilipo na kusikia sauti ya babu zangu waliokufa miaka mingi wakiongea .

Ni hapo nikajua walinidanganya eti wanaenda Janattu Firdaus kumbe wamba wapo hapa hapa bongoland tunakula vumbi wote Ila wao wameamua kujificha machoni petu sisi wandewa
 
Unawanyima ulanzi ila unaenda janattu firdaus kwa mamilioni🤣🤣🤣
 
Ni ujinga Sana bro.

Hapo nikamkumbuka baba yangu mkubwa aliishi Sana nje ila kila mwisho wa mwezi alikuwa anatuma laki na ushee eti wanunue nyama waziweke kwenye makao makuu ya ukoo kwakuwa wazee wetu watakuwa wanakula .

Sasa ile nyama ikawa inawekwa Ila wamba hawaili ikioza waangalizi wanaiondosha .

Ulipokuwa utaratibu wake enzi za isis tunavyokuwa ,matapeli wa ukoo wakaanza kuwa na ratiba na ile hela ya mzee kila ikitumwa matapeli wa ukoo wanaikula ,hawanunui kwaajili ya mizimu .

Sasa baba mkubwa alivyorudi akagundua kupitia maafisa usalama wa ukoo kuwa kuna wandewa walikuwa wanaikula ile hela na mizimu wanaikaushia ,alimaindi kichizi ,akarudi majuu mpaka wa leo no simu Wala call kwa ndunguze alimaindi kichizi kisa mizimu haipewi msosi .

Sasa ni hapo nikaanza kugundua hii dunia ishi tu ukifa ni kuwa unapewa uwezo wa kutoonekana mbele za Wana wanaishi ndiyo maana hata baba mkubwa alivyokuwa anatoa hela ili mizimu ile bado mizimu ilikuwa inaona aibu kula ile nyama ikidhani ikila tutajua kumbe washikaji hawakufa wapo bado .

Bro ,Mambo ya dini na mizimu ni vichekesho vya dunia tuliandaliwa ili tusikae bila kucheka kidogo
 
Hahaha mimi huwa sina mda nayo kabisa .
 
Wasisahau Kuifanya CCM Maombi Wawaache Tabia ya Kuiba Kura na Kukata Majina ya Wagombea wa Upinzani

Katika historia ya siasa za Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikikabiliwa na shutuma mbalimbali kuhusu tabia yake ya kuiba kura na kukata majina ya wagombea wa upinzani. Hii ni hali ambayo imeleta wasiwasi mkubwa kwa wananchi na kuathiri uaminifu wa mchakato wa uchaguzi. Ni muhimu kuelewa sababu za matatizo haya na namna ya kuyatatua ili kuimarisha demokrasia nchini.

Kwanza, ni muhimu kuzingatia kwamba uchaguzi ni msingi wa demokrasia. Wananchi wanapopiga kura, wanakuwa na fursa ya kuchagua viongozi wanaowakilisha matakwa yao. Hata hivyo, tabia ya kuiba kura inakandamiza sauti ya wapiga kura na inawanyima haki yao ya kuchagua. Kila uchaguzi unapoandaliwa, kuna ripoti za kuibiwa kura, ambapo matokeo ya uchaguzi yanapindishwa ili kulinda maslahi ya CCM. Hali hii si tu inakatisha tamaa wapiga kura, bali pia inawakatisha motisha wagombea wa upinzani.

Aidha, kukata majina ya wagombea wa upinzani ni kitendo kingine kinachochangia kuharibu mchakato wa uchaguzi. Wakati wa uchaguzi, ni lazima wagombea wote wawe na fursa sawa ya kushiriki. Hata hivyo, mara nyingi tumeshuhudia majina ya wagombea wa upinzani yakikatwa bila sababu za msingi. Hii inadhihirisha hila za CCM katika kuhakikisha kwamba upinzani hauwezi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi. Wananchi wanahitaji kuwa na uelewa wa kina kuhusu mchakato huu na umuhimu wa uwazi na haki katika uchaguzi.

Katika nchi nyingi, kuna mifumo ya uwazi na usimamizi wa uchaguzi ambayo inasaidia kuzuia udanganyifu. Hapa Tanzania, kuna haja ya kuimarisha mifumo hii ili kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa wa haki. Serikali inapaswa kuanzisha mikakati ambayo itasaidia kuongeza uaminifu wa mchakato wa uchaguzi. Hii ni pamoja na kuweka wakaguzi huru ambao watafuatilia mchakato mzima wa uchaguzi ili kuhakikisha kwamba kila hatua inazingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Pia, ni muhimu kwa wananchi kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi. Wakati watu wanaposhiriki kwa wingi, inakuwa vigumu kwa vyama vya siasa, ikiwemo CCM, kujaribu kuiba kura au kufanya udanganyifu. Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba kura zao zina nguvu na zinaweza kubadilisha hali ya kisiasa nchini. Kwa hivyo, ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba tunashiriki katika uchaguzi na kupiga kura zetu bila woga.

Kufanya maombi kwa CCM kuacha tabia hizi mbovu ni hatua muhimu, lakini ni muhimu pia kuangalia hatua za kisheria ambazo zinaweza kuchukuliwa dhidi ya wale wanaohusika na udanganyifu wa uchaguzi. Serikali inapaswa kuwa na sera kali dhidi ya wale wanaoshiriki katika vitendo vya kuiba kura au kukata majina ya wagombea wa upinzani. Hii inaweza kujumuisha adhabu za kifungo au faini kali kwa wale wanaopatikana na hatia.

Pia, vyombo vya habari vina jukumu muhimu katika kuhabarisha umma kuhusu vitendo vya udanganyifu katika uchaguzi. Wanahabari wanapaswa kuwa na uhuru wa kutafuta na kuripoti habari, bila hofu ya kudhuriwa. Hii itasaidia katika kupeperusha mwanga juu ya matatizo yanayoikabili demokrasia nchini na kuhamasisha wananchi kuchukua hatua.

Kwa kumalizia, ni wazi kwamba tabia ya kuiba kura na kukata majina ya wagombea wa upinzani inahitaji kushughulikiwa kwa dhati. Ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kwamba uchaguzi wa haki unafanyika. Tunapaswa kuwashawishi viongozi wetu wa CCM kuacha vitendo hivi na kuhakikisha kwamba demokrasia inachukua mkondo wake. Kwa kufanya hivyo, tutaunda mazingira rafiki ya kisiasa ambayo yatafaidisha kizazi cha sasa na kijacho. Hii ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa wananchi wote.
 
Wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kuwa Disemba 09, 2024 wakati Tanzania itakapokuwa inaadhimisha Miaka 63 ya Uhuru, Mkoani Arusha kutafanyika Kongamano kubwa la maombi la kuombea Mkoa wa Arusha dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoikumba mkoa huo

Makonda ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Arusha, akisema katika maadhimisho hayo kutafanyika pia matembezi maalum kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yakijumuisha Viongozi hao wa dini na wananchi wa mkoa wa Arusha.

"Tutatembea kwa pamoja maeneo mbalimbali mkoani Arusha tukiwa na bendera, tukitamka maneno ya baraka na maombezi kwa Mkoa wetu wa Arusha tukiombea amani, baraka, biashara zetu pamoja na kizazi tukitakacho mkoani Arusha." Amesema Mhe. Makonda.

SOCIAL ENTERTAINER
 
Ni vizur pia tutubu Kwa ajili ya wizi wa kura na uenda Mungu Alisha geukia ukutani Kwa dhambi ya wizi wa kura na kutekana na kuuana Kwa iyo tuombe Toba Kwa Kwa Chama
 
Wakuu,

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kuwa Disemba 09, 2024 wakati Tanzania itakapokuwa inaadhimisha Miaka 63 ya Uhuru, Mkoani Arusha kutafanyika Kongamano kubwa la maombi la kuombea Mkoa wa Arusha dhidi ya changamoto mbalimbali zinazoikumba mkoa huo

Makonda ametoa kauli hiyo alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoani Arusha, akisema katika maadhimisho hayo kutafanyika pia matembezi maalum kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha yakijumuisha Viongozi hao wa dini na wananchi wa mkoa wa Arusha.

"Tutatembea kwa pamoja maeneo mbalimbali mkoani Arusha tukiwa na bendera, tukitamka maneno ya baraka na maombezi kwa Mkoa wetu wa Arusha tukiombea amani, baraka, biashara zetu pamoja na kizazi tukitakacho mkoani Arusha." Amesema Mhe. Makonda.

Mungu asubiri makongamano unaweza kuomba hata chooni!
 
Mpe maskini kileo asahau shida zake,Mungu anawajua walio wake.Ukijifanya una hofu ya Mungu ni vyema matendo yako yaendane na hiyo hofu ya Mungu.Toba ya kweli ni muhimu sana kwa ajili ya maisha yajayo.
 
Back
Top Bottom