Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

Paul Makonda: Wananchi walioikimbia Dar warudi, Mauti hauikimbii. Siku ya Jumapili, kila mtu afanye fujo awezavyo na kupiga kelele na vigeregere!

Kujua takwimu sio ndio kuishinda Corona bali ni kifuata taratibu na maelekezo ya serikali ili kuepukana na Corona, ivi takwimu hujui kama zinaleta hofu pia Mana watu watazidi kuogopa na kushindwa kuendesha shughuli za maendeleo ya familia na taifa,Mungu ibariki Tanzania


Hofu hiyo kwa hapa bongo tu?

Kwa hiyo mataifa mengine wanaotoa takwimu wao hawajaliona hilo?!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ruhusa ya maambukizi ya kijamii ili kutengeneza hard immunity...
Watakaokufa na wafe watakaobaki na waishi...
Za kuambiwa....
 
Huyu bwana anajua Sana kwenda na biti amuwaziae kutumbuliwa akapimwe akili.
Ndugulilie akwenda na biti ilipigwa blues akacheza reggae out,mollel na mwigulu wakadaka step ya blues in.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewaelekeza Watu wote waliofunga Hotel, Migahawa na sehemu za biashara kutokana na hofu ya Corona kuzifungua na kuanza kazi kama kawaida huku akiwataka waendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata maelekezo ya Wizara ya Afya.

RC Makonda ametoa wito pia kwa Wale waliokimbilia mikoani kwa kuhofia Corona kuhakikisha wanarudi na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.

Aidha RC Makonda ametangaza siku ya Jumapili ya wiki hii kuwa siku ya Sherehe na Shukrani kwa Mungu kwa kutukinga na Janga la Corona ambapo ameeleza kuwa atafurahi kuona kila mmoja anasherekea siku hiyo.

“Rais Magufuli ametupa siku tatu za kumshukuru Mungu wetu, naamini kila mmoja atafanya ibada ya Shukrani lakini mimi nimeomba Jumapili kila Mtu apige shangwe na vigelegele ikiwa ni ishara ya Shukrani kwa Mungu wetu kwa Makuu aliyotutendea.

"Mtakumbuka historia ya Wana wa Israel walichofanya kwenye ukuta wa Yerico, kwahiyo kama wewe una mziki wako nyumbani piga kelele uwezavyo na Tarehe 25 tunaendelea kuchapa kazi kama kawaida” Amesema RC Makonda
 
Corona imeisha bila takwimu kujulikana.
Pia miili ya marehemu haipimwi Corona kwa sababu wameshakufa huwezi kuwasaidia.
Basi Pandemic imeisha, watalii wataanza kuja. Mashirika ya ndege, siwezi kuyataja hapa, yana bookings za watalii wetu mpaka December. Yaani ndege zimejaa.
 
Back
Top Bottom