Paul Makonda: Watu wanaendekeza Uchawi na Majungu

Kakwambia chumbani amejuaje thamani ya waganga imepanda mwamba? Anajuaje mwenendo wa bei ya uchawi? Kama sio mshirika basi ni ewura wao
 
IMG_6103.jpeg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Maneno hayo yamesemwa na Mwamba wa kaskazini Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara.siku ya jana ya jumapili pale alipopewa nafasi ya kuzungumza na kusalimu katika kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya kaskazini kati.katika kustaafu kwa Dkt Solomoni Jakob Massangwa.

Ambapo Mwamba Mwenyewe Paul Makonda amesema kwa sasa watu wanaendekeza sana uchawi na Majungu na hata kumsahau mwenyezi Mungu.amesema mfano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi thamani ya waganga wa kienyeji imepanda sana ukilinganisha na thamani ya watumishi wa Mungu .

Amesema ya kuwa kwa sasa magari ya VX yaani yale ya thamani yanapishana kwa waganga wa kienyeji.

Amelitaka kanisa kusimama katika nafasi yake na kuwaombea viongozi wote. Amewataka watu wote pia kumrudia Mungu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
kweli nmeamini wachawi ndo
wanaolia kwa sauti kwenye misiba aiseeee
 
Muhalifu anawezaje kwashawishi watu watende mema,ni nani atachukuwa usahuri wake?
 
Acha Majungu yako wewe.

Jivike akili asilia, achana na uchawa. Fanya uchunguzi huyo unayemsemea ili umfahamu ni mtu wa namna gani

Yaani mshirikina ambaye alifanya mipango ya kumpeleka mganga mpaka ikulu, leo anachukia ushirikina?
 
Ulikuwepo wakati wa kumpeleka huyo mganga?
 
Swali lako halina msingi. Panua uelewa.

Mambo yote unayoyajua, ulikuwepo hapo hapo yalipokuwa yanatendeka?

Kwa aina ya maswali yako, hata leo hii nikisema kuwa Rais Samia alizaliwa mwaka 1960, utaniuliza kama nilikuwepo wakati anazaliwa!!!
 
Jibu swali acha kuleta mifano ya kijinga isiyoendana kabisa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Maneno hayo yamesemwa na Mwamba wa kaskazini Paul Christian Makonda Kijana Jasiri kusini mwa jangwa la Sahara.siku ya jana ya jumapili pale alipopewa nafasi ya kuzungumza na kusalimu katika kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya kaskazini kati.katika kustaafu kwa Dkt Solomoni Jakob Massangwa.

Ambapo Mwamba Mwenyewe Paul Makonda amesema kwa sasa watu wanaendekeza sana uchawi na Majungu na hata kumsahau mwenyezi Mungu.amesema mfano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi thamani ya waganga wa kienyeji imepanda sana ukilinganisha na thamani ya watumishi wa Mungu .

Amesema ya kuwa kwa sasa magari ya VX yaani yale ya thamani yanapishana kwa waganga wa kienyeji.

Amelitaka kanisa kusimama katika nafasi yake na kuwaombea viongozi wote. Amewataka watu wote pia kumrudia Mungu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kuhusu uchawi bashite ni muumini no1
 
Ni mcha Mungu
Mshirikina, muuaji na mporaji wa mali za watu, ni mcha mungu!! mungu gani? Au ninyi mna mungu wenu mnayemjua ambaye ni mungu wa uovu? Fanyeni ujinga wote lakini msimkufuru Mungu. Mjue kuwa kila kufuru, inawatengenezea laana.
 
Back
Top Bottom