Hamjambo!
Kwa upande wangu, Paulo aka Sauli ninamchukulia kama mwandishi mashuhuri aliyepewa nafasi na Dola la Rumi Kwa Siri Ili kubadili uelekeo wa Ukristo na kuufanya uwe upagan.
Paulo/Saul: kiasili ni Myahudi
Raia; Warumi
Elimu: Farisayo, elimu ya juu ya Dini ya kiyahudi.
Paulo hakuwahi kuonana na Yesu popote kipindi Yesu yupo Hai.
Utume wa Paulo ni mission Kwa sababu zifuatazo;
1. Paulo alikuwa adui wa Wakristo wa mwanzoni.
Lakini akapiga U-turn Kwa kile alichosema ametokewa na mtu aliyejitambulisha Kwa Jina la Yesu.
2. Paulo hakuwahi kumwona Yesu popote kipindi Yesu akiwa Duniani.
Hata hoja yake ya kutokewa na Yesu kimiujiza akiwa anaenda Dameski Haina uthibitisho. Ni ushuhuda binafsi. Ni sawa na hawa manabii wakileo wanaosema wametokewa na Yesu.
Hata waliokuwa na Sauli/Paulo hawakumwona Wala kuisikia Sauti ya Yesu ila Paulo anadai alitokewa na kusikia sauti.
3. Hakuna mantiki ya Yesu kumchagua Paulo wakati walikuwepo wanafunzi kumi na Moja waliobakia aliowafundisha Kwa miaka miitatu...
Ndio maana hata wanafunzi wa Yesu walimchukulia Paulo kama Mamluki wa Waroma. Hasahasa Petro.
4. Paulo alienda kinyume na Mafundisho ya Yesu hasa yanayohusu Torati ya Musa.
Paulo ndiye mhusika pekee aliyeipotosha Biblia na kuipa mrengo wa kipagani.
Mafundisho ya sabato
Kumfanya Yesu Mungu
Kuruhusu kula chakula chochote n.k.
5. Wakati huo Injili ilikuwa haijaandikwa. Paulo hajakutana na Yesu kipindi Yesu akiwa Duniani. Paulo anakinzana na wanafunzi wa Yesu. Kwa vyovyote vile mazingira ya Paulo kuwa na mafundisho Halisi ya Yesu uwezekano ni mdogo sana.
6. Paulo ndiye aliyesema Mamlaka zote zinatoka Kwa Mungu. Na watu waheshimu mamlaka. Fundisho ambalo sio kweli. Alikuwa akitetea Dola la rumi Kwani yeye alikuwa raia wa Roma ingawaje alikuwa myahudi.
Sio Kila Mamlaka inatoka Kwa Mungu.
Zipo mamlaka dhalimu, zakishetani, katili na zakinyama ambazo hazitoki Kwa Mungu.
Mafundisho hayohayo ya kikafiri hutumika na Dola nyingi dhalimu kutawala watu kishenzi na kimabavu.
Paulo angekuwa sio Jasusi la kiroma Wala asingesema hayo. Angesema, mamlaka zinazofuata haki zinatoka Kwa Mungu huku zile zinazofanya udhalimu zikitoka Kwa yule muovu.
7.;Paulo ndiye Mhusika pekee aliyeandika Falsafa za kuwafanya wasililizaji na wasomaji wa maandiko yake kuacha kupigania mambo ya mwili na kukazana na mambo ya roho..
Lengo lake ni kuwafanya watu waache kujikita na mambo ya ulimwengu Ili Dola la rumi lizidi kustawi na kutawala bila shida.
Acha nipumzike
Sikiliza kwa makini maneno unayoyasema dhidi ya Paulo si mapya, ni hoja zile zile ambazo zimekuwa zikitumiwa na wapinzani wa injili kwa karne nyingi. Lakini ukweli wa Mungu hauwezi kubadilishwa kwa porojo za wanadamu. Hii ndiyo injili yenyewe, iliyojaa nguvu na upako wa Roho Mtakatifu.
Kwanza, unasema Paulo alikuwa jasusi wa Rumi. Ikiwa kweli alikuwa jasusi, basi ajabu iliyoje kwamba fundisho lake liligeuza ulimwengu mzima? Jasusi gani anayeweza kufundisha kwamba “Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, akazikwa, na siku ya tatu akafufuka” (1 Wakorintho 15:3–4) na kwa injili hiyo watu maelfu wapate wokovu? Je, Dola la Rumi lingependa injili ambayo ilivunja sanamu zao, ilipiga vita upagani wao, na kuhubiri Mungu mmoja wa kweli? La hasha! Paulo hakutumikia Rumi, alitumikia Yesu Kristo aliye hai.
Unasema Paulo hakumuona Yesu. Ndiyo maana anajitambulisha kama “mtume aliyezaliwa kabla ya wakati” (1 Wakorintho 15:8). Lakini kumbuka, hata mitume wengine walikuwa wanashuhudia kwa macho; Paulo alipewa neema ya kipekee kushuhudia kwa roho. Na uthibitisho wake siyo maneno matupu ni maisha yake. Alipigwa viboko, alifungwa magerezani, aliteswa, na hatimaye akakatwa kichwa kwa ajili ya Kristo. Je, jasusi wa Rumi angekataa mali, heshima na ulinzi wa dola ili afe kifo cha aibu kwa ajili ya jina la Yesu?
Unasema Paulo alipotosha injili kwa kwenda kinyume na Torati. Lakini kumbuka, Yesu mwenyewe alisema: “Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato.” (Mathayo 12:8). Yesu ndiye aliyetimiza Torati na manabii. Paulo hakupindua, bali alieleza kwa Mataifa kwamba wokovu si kwa matendo ya sheria bali kwa imani ndani ya Yesu Kristo (Warumi 3:28). Huu ni ukweli wa injili kwa maana kwa matendo ya sheria hakuna mwili utakao hesabiwa haki mbele za Mungu.
Unasema Paulo alitetea mamlaka ya kiserikali kwa sababu alikuwa Mroma. Hapa tena unapotosha. Warumi 13 inasema mamlaka zinatoka kwa Mungu ili kuzuia uovu na kulinda haki. Lakini pale mamlaka zinapopinga Mungu, Paulo mwenyewe alikataa kutii. Angalia: aliteswa, alifungwa, aliuawa na utawala wa Roma. Kama alikuwa mnafiki wa dola, kwa nini dola hiyo hiyo imkata kichwa?
Kwa hiyo hoja zako haziwezi kusimama mbele ya ukweli. Paulo hakubadilisha injili, bali aliihubiri kwa nguvu zote na kwa upako wa Roho Mtakatifu. Ndiyo maana hata Petro alisema: “Ndugu yetu mpendwa Paulo ameandika kwa hekima aliyopewa” (2 Petro 3:15). Mitume walimkubali, kanisa la kwanza lilimkubali, na hadi leo injili anayoihubiri imeokoa mamilioni ya roho duniani kote.
Ukweli ni huu: Yesu Kristo ndiye msingi, Paulo ni chombo tu. Yesu Kristo ndiye kanisa, Paulo ni mtumishi tu. Yesu Kristo ndiye mwokozi, Paulo ni shahidi tu. Na leo hii sauti ya injili inalia kwa nguvu: Yesu Kristo ni Alfa na Omega, Mwana wa Mungu aliye hai, na yeyote akimwamini hataangamia bali atakuwa na uzima wa milele!