PAYE kwa Wafanyakazi imepunguzwa kutoka 9% hadi 8%. Kodi kwenye marupurupu imeondolewa; hatua hii itaongeza mshahara!

Nampongeza mama Samia, anayo dhamira ya kweli ya kuipigania maslahi ya wafanyakazi...madaraja na vyeo ni hatua nzuri kwa wafanyakazi
 
Malimbikizo ya Mishahara yanalipwa mwezi huu wa tano, pia ni jambo la kushukuru, lkn pia 1% imepunguzwa.
Ahsante mama.
 
Nyie ndo mnalalamika mkienda kwenye Taasisi za serikali mkapewa huduma mbovu haya Mambo ya kuwalipa vizuri watumishi yanaleta motisha katika kazi mtu anakua na bidii kwa sababu kazi anayofanya inamfanya aishi maisha mazuri kwa kupewa stahiki zake kwa wakati.kuja na hoja eti Kuna watu Hawa ajira uko mtaani ndo iwe sababu ya kutowaongezea mishahara watumishi ni ufinyu wa upeo katika kufikiri. Kwa sababu serikali inaajiri kwa kufuata majirani na imishaajiri inajukumu la kuboresha mishahara na mazingira ya kazi kwa mtumishi wake
 
Malimbikizo ya Mishahara yanalipwa mwezi huu wa tano, pia ni jambo la kushukuru, lkn pia 1% imepunguzwa.
Ahsante mama.
Ignorance and brainwashed addiction drive the crooks into the lioness din in which the flesh is devoured without expectations.
 
Hapa kwenye kodi za magari ndo janga kuu kabisa.Kodi kubwa kuliko hata gharama za kutengeneza gari kiwandani.
Magari yafaa yaingie bure Ili kukuza uchumi kupitia kodi na ajira.
 
Malimbikizo ya Mishahara yanalipwa mwezi huu wa tano, pia ni jambo la kushukuru, lkn pia 1% imepunguzwa.
Ahsante mama.
Kwani mwanzo malimbikizo yalikuwa hayalipwi?

Hujasikia uhakiki wa wafanyakazi hewa na vyeti feki bado kukamilika?

Jipe moyo hewa
 
Nyerere baba yetu wa taifa alifanya mengi mazuri lakini kama ilivyo kwa binadamu hakuna mtu asiye na kasoro. Miongoni mwa kasoro hizo ni kujenga nchi ambayo serikali ndiyo kila kitu, na kuiita nchi hiyo ya wakulima na wafanyakazi. Matokeo yake serikali yetu ni miongoni mwa serikali kubwa sana kimatumizi, na zaidi ya asilimia 75 ya makusanyo ya TRA yanalipa mishahara ya wafanyakazi wa serikali.

Mi mwenyewe mfanyakazi wa serikali lakini sometimes linapokuja suala la nchi ni upuuzi kuangalia maslahi binafsi. Hapa kazini kwangu taasisi ya umma kuna magari ya serikali yanapigwa mnada. Nilimuuliza dreva yana shida gani haya magari hadi mnayapiga mnada, jibu lake lilinihakikishia kwamba hii nchi bado sana aisee. Yaani gari moja linalopigwa lilikuwa gari la kutumia bosi wetu wa zamani lakini alipokuja mwingine akataka la kwake jipya. Hilo la zamani zima kabisa ila ndio hivyo halitumiki tena inabidi lipigwe mnada.

Nirudie tena, hizo ni pesa za walipa kodi, na walipa kodi wenyewe orijino ukiona jinsi wanavyojibana ili walau biashara zao ziende licha ya uchumi tepetevu msingekuwa na hizo hulka za matumizi mabovu ya pesa za walipa kodi. Kama suala la kutoa huduma za serikali liwe transaction, kwamba daktari wa hospitalini alipwe kulingana na thamani ya huduma yake, mwalimu, nesi, polisi, n.k, vivyo hivyo, mi naona ni sawa tu. Na ndivyo serikali inavyopaswa kuendeshwa kwa tija na itafutwe model ya kuquantify tija ya kila sekta ya umma kifedha, na wafanyakazi wa kila sekta walipwe kulingana na tija yao. Ila kwa sasa haiko hivyo, wengi wa wafanyakazi wa umma huduma zao hazilingani na mishahara wanayolipwa. Matokeo yake nchi haina uwezo wa kuongeza mishahara wakati huo huo itekeleze miradi ya maendeleo.
 
Serikali imepunguza kodi ya PAYE kutoka 9% na sasa itakuwa 8%

Punguzo hili litasababisha mshahara kuongezeka kadhalika kodi kwenye marupurupu imeondolewa.

Kazi Iendelee!
Hii 1% cut inawahusu watu wa kima cha chini. Kama wewe unapata mshahara kuanzia laki 540000. Endelea na kazi.
 
Hi ni moja ya ahadi yangu nitakokuwa mgombea wa Urais.......ha ha ha ha ha ha. Nimeliona miaka mingi sana hili. Tukipunguza Kodi ya MAGARI, Magari mengi yataongezeka, mafuta yatanunulika sana, vipuri, matengenezo na kadhalika. Importation tax ya magari nchi hii inaumiza mno. Japo madhara ya magari mengi ni uchafuzi wa mazingira.
 
Serikali imepunguza kodi ya PAYE kutoka 9% na sasa itakuwa 8%

Punguzo hili litasababisha mshahara kuongezeka kadhalika kodi kwenye marupurupu

Je hii ni kwa wafanyakazi sekta zote au wa umma tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…