PDPC: Leo ni Siku ya Mwisho ya Usajili wa hiyari kwa Wachakata Taarifa Binafsi

PDPC: Leo ni Siku ya Mwisho ya Usajili wa hiyari kwa Wachakata Taarifa Binafsi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,183
Reaction score
2,100
Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 (Sura ya 44), taasisi au mtu yeyote anayeshughulika na ukusanyaji au uchakataji wa taarifa binafsi nchini Tanzania anatakiwa kujisajili na Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC). Kushindwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria ambao unaweza kupelekea adhabu.

Adhabu kwa Kutokujisajili au Ukiukaji wa Sheria

Kifungu cha 63.-(1) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria

hii, anatenda kosa na pale ambapo hakuna adhabu mahususi iliyoainishwa, atakapotiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki moja na isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja

(2) Baada ya mtu kutiwa hatiani kwa kosa lolote chini ya Sheria hii, mahakama inaweza kuamuru kukamatwa kwa vifaa vyake vyenye taarifa binafsi vilivyohusika katika kutenda kosa.

Umuhimu wa Kujisajili

Kujisajili na PDPC sio tu ni hitaji la kisheria, bali pia ni hatua muhimu ya kuonyesha uwajibikaji na kujenga uaminifu kwa wateja na wadau wengine.

Inasaidia kuhakikisha kuwa taarifa binafsi za watu zinalindwa ipasavyo na zinachakatwa kwa mujibu wa sheria.

Ni kina nani hasa wanaopaswa kujisajili?

Wanafaa kujisajili:

1. Taasisi za Umma – mfano: wizara, mamlaka, halmashauri, taasisi za elimu, hospitali za serikali, n.k.

2. Kampuni na Mashirika Binafsi – mfano: kampuni za biashara, huduma za afya, taasisi za kifedha (mabenki, bima), nk.

3. Sekta ya Hospitality – hoteli, nyumba za wageni, kampuni za tours & travel, n.k., ambazo hukusanya taarifa za wateja kama majina, namba za pasipoti, anwani, mawasiliano, au taarifa za malipo.

4. Asasi za Kiraia (NGOs) – zinazokusanya taarifa za wanufaika, wafanyakazi, au wahisani.

5. Huduma za kidijitali – mitandao ya kijamii ya ndani, apps, websites zinazokusanya taarifa binafsi za watumiaji.

6. Vyombo vya habari – vinavyohifadhi au kuchakata taarifa binafsi kwa namna yoyote.

7. Shule, vyuo, na taasisi za mafunzo – zinazohifadhi taarifa za wanafunzi, walimu, n.k.

8. Watoa huduma za afya – hospitali, vituo vya afya, kliniki binafsi.

Jinsi ya Kujisajili

Taasisi au mtu anayehusika na ukusanyaji au uchakataji wa taarifa binafsi anatakiwa:

1. Kutembelea tovuti ya PDPC: PDPC

2. Kusajili akaunti ya taasisi au mtu binafsi.

3. Kujaza fomu ya usajili kwa usahihi.

4. Kuwasilisha fomu hiyo kwa ajili ya mapitio na kuidhinishwa na PDPC.

Ni muhimu kukamilisha usajili huu kabla ya tarehe 30 Aprili, 2025, ili kuepuka adhabu zinazoweza kutolewa kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom