PEMBA: Achapwa Mikwaju Kula Mchana Mwezi mtukufu wa Ramadhan

Aksante kwa maneno yako na uelewa wako na watu kama wewe wenye uelewa mlitakiwa muiongoze hii hiyo jamii yenu. Si hawa wanaojichukulia sheria mikononi (nobody is perfect sir)

AKSANTE MJADALA MZURI
 
Habari wanabodi.

Huyu ndg amenusurika kifo baada ya kukutwa akila chakula mchana wakati ndg zetu katika Imani Waislam wakiwa katika mfungo.

Walitokea wasamaria wema wakaweza kumnusuru maana huenda angeweza kupoteza Maisha.

Hii imetokea hapa Pemba.

My take : Ndugu zetu Waislam tujaribu kuwa wavumilivu katika wakati huu wa mfungo, sidhani kama inaruhusiwa kutoa HUKUMU kwa jambo lolote.

Nawatakia swaumu njema.

 
Du hapa naona anayeabudiwa ni mungu njaa binadamu tunavyohukumiana je Mungu angekuwa na yeye anatuhukumu kimwendokasi kama waliofanya hawa duniani tusingebaki
 
Hii ni mbaya sana. Kama wewe umefunga, mtu mwingine kula kunazuiaje swaumu yako? Si ndio kipimo kizuri kuwa japo waona chakula, lakini imani yako inashinda tamaa? Kuna dini/imani kweli hapo penye mtu kupigwa na walio ktk mfungo kwa 'kosa' la kula? Tunajua kwa nini huyo mtu kala chakula hadharani mwezi wa mfungo? Je kama amekula sababu ya ugonjwa(vidonge,vidonda vya tumbo), lililofanyika ni sahihi?

Kuna taarifa pia ya makahaba kupigwa bakora na maustaadh. Hapa pia pana kasoro. Unatoka vp nyumbani kwako na swaumu yako hadi kinondoni au sinza makaburini kwenda kuwapiga wanaojiuza? Ni haki mtu apigwe kwa kuwa tu anajiuza? Je ni kweli kuwa kila anayefunga hatendi dhambi siku nzima?

Watu maskini tunasumbuka sana na dini. Haya mambo huwezi kuyasikia wala kuona katika jamii za kisomi na zilizoendelea. Dini ni umaskini tu. Maskini mpe dini imfariji.
 

seriously???????
 
Aksante kwa maneno yako na uelewa wako na watu kama wewe wenye uelewa mlitakiwa muiongoze hii hiyo jamii yenu. Si hawa wanaojichukulia sheria mikononi (nobody is perfect sir)

AKSANTE MJADALA MZURI
Na wewe kawahubirie hao wenzio wanachoma moto vibaka na watoto kwa ajili ya wizi wa mifukoni. WAMEPATA WAPI HAKI YA KUCHUKUA SHERIA MKONONI
 
Dini inapochangamana na wahuni huzaliwa kitu hatari sana ambacho ni ushetani wenye jina la dini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…