Hakika, Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni! Ni ile kauli ya Mama Anaupiga Mwingi usidhani ni msemo tu, sasa hebu tazama jinsi Mama alivyoweka historia katika maslahi ya watumishi wa umma ndani ya muda mfupi tu tangu ashike hatamu.
Uchumi wa Dunia unapoyumba hakuna nchi inayobaki salama. Baada ya athari za COVID19, tayari Dunia imeingia katika suala la mgogoro wa Urusi na Ukraine. Licha ya changamoto hizi kiuchumi Rais
Rais Samia ameweza kuonyesha umahiri mkubwa kwa kufanya haya katika sekta ya utumishi wa umma;
1. Nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wote wa umma ikiwemo wa kima cha chini.
2. Kupunguza kodi(PAYE) kwa kuifikisha 8% na kupandisha kiwango cha chini cha kukatwa kodi, suala hili lilipoteza kiwango cha takribani Bilioni 14 ya fedha zilizopaswa kukusanywa na serikali.
3. Katika mifuko ya hifadhi ya jamii kupandisha kiwanga cha malipo ya mkupuo kwa kufikia asilimia 33 kutoka 25% iliyokataliwa na wadau mwaka 2018.
4. Kupandishwa madaraja WATUMISHI laki moja tisini elfu na miatano sitini na mbili~ 190,562 (Kwa wasioelewa, hii imeigharimu Serikali kiasi cha takribani TZS BILIONI 39.6).
5. Taasisi zote zenye uhitaji wa wafanyakazi kupewa vibali vya ajira mpya na kutolewa vibali kwa watumishi walioomba kubadilisha vituo na kwenda kuongeza taaluma kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma.
6. Kuanzia Mwezi March 2021 hadi January 2022, Rais Samia amewezesha ulipwaji wa madeni na malimbikizo ya watumishi wa umma wapatao 65,391, madeni yenye thamani ya takribani TZS BILIONI 90.7.
7. Kuondolewa kwa mzigo wa tozo ya 6%(VALUE RETENTION FEE) kwa watumishi waliokuwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Kiwango hiki cha 6% kimekuwa mzigo mzito kwa watumishi hususani vijana wanaotoka Vyuo Vikuu, Rais Samia atakumbukwa sana kwa hili.
8. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya watumishi. Hii inatupa hamasa watumishi kutoa huduma bora na kuhakikisha wananchi wanapewa wanachostahiri.
Itoshe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameweka rekodi ya aina yake kama Mkuu wa nchi anayejali watumishi wa umma. Tumuunge mkono tujenge nchi yetu.