Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Mkazi wa Kijiji cha Nohli, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akihifadhi mazao juu ya paa la nyumba kama alivyokutwa kijijini. PICHA: IBRAHIM JOSEPH (Nipashe)
Tumekuwa tukiona mara kwa mara Rais John Magufuli akiagiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Na tumeona miradi mbalimbali ikitekelezwa kwa kasi kubwa na kwa haraka karibu kila kona ya nchi. Ni katika mwanga wa haya yanayoendelea na katika kufikiria jinsi gani ya kuweka mfumo unaoweza kujiendesha na kuwa wa kudumu (haya yasije kuisha Rais akimaliza muda wake 2025). Hii itakuwa ni sehemu moja ya Rais kuacha alama ya kudumu ya utendaji wake mahili wa kuhalakisha maendeleo ya haraka ya Taifa letu. Haya ni mawazo yangu tu naamini wengine wanaweza kukosoa, kuongezea, kusahihisha na hata kuleta mawazo bora zaidi na labda wahusika wanaweza kupata mawazo na wao wenyewe na wakayaongeza haya na hatimaye tukawa na kitu kizuri ambacho tunaweza tukaona kikiacha alama kuwa na sisi tuliwahi kuwepo. Lengo hasa ni kuhakikisha kuwa tunatengeneza kitu sambasamba na mfumo wa kawaida wa bajeti – kitu ambacho tayari kimetokea – na sasa kukifanya kiwe rasmi.
JINA LA MFUKO
(Kiingereza) Tanzanian National Reconstruction and Development Fund TNRDF/TANAREDEF
(Kiswahili) Mfuko wa Maendeleo na Ujenzi Mpya wa Taifa Tanzania– MUMT
Mfumo uanzishwe kwa agizo la Rais au kwa Sheria ya Bunge.
Lengo la Mfuko:
- Kukusanya fedha zote ambazo zitakuwa nje ya Bajeti ya Taifa kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia, na kuendeleza miradi maalum ya maendeleo.
- Mfuko utajiwekeza katika maeneo makubwa matatu:
- Ujenzi wa nyumba nafuu (affordable housing) lengo ikiwa ni kuwaondoa wananchi wa Tanzania ndani ya miaka 10 kutoka kwenye nyumba za udongo, nyasi na tembe. Msingi mkubwa ni nyumba za vijijini. Lengo ni kuingiza nyumba za matofali ya kuchoma na vigae zisizopungua 500,000 kwa mwaka ifikapo 2025. Ifikapo 2030 Tanzania iwe imeondoka na nyumba za ujima.
- Ujenzi wa shule za kisasa za msingi kwenye maeneo ambayo bado yana shule zilizochakaa na ambazo ni aibu ya Taifa.
- Uunganishwaji wa barabara za wilaya na wilaya.
- Kufadhili miradi yoyote yenye manufaa kwa umma inayohitajika kwa haraka na ambao ukamilishaji wake hauwezi kuzidi zaidi ya mwaka mmoja. Miradi hiyo yaweza kupendekezwa na chombo chochote n ahata mtu yeyote lakini ni lazima iridhiwe na Rais na Mfuko. Kwa hili, Mfuko unaweza kuweka utaratibu wa kukaribisha maombi ya ufadhili kutoka mtu, taasisi, au chombo chochote kile. Mfuko hautatoa ufadhili kwa miradi au taasisi binafsi isipokuwa kama ni lengo 4.
- Kutoa ufadhili au udhamini wa kifedha kwa makampuni ya Kitanzania (ambayo yanamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania) ambayo yanataka kupanua biashara zake au masoko yake katika eneo lolote la Afrika ya Mashariki na Kati (maeneo ya EA au SADC). Kwa lengo hili mfuko utaanzisha Tanzanian Overseas Private Investment Corporation (TOPIC). Lengo kubwa la eneo hili la mfuko ni kufanya makampuni ya Tanzania kupenya na kustawi. Taratibu zinaweza kuwekwa kwa jinsi gani makampuni hayo yatarudisha ufadhili huo wa mfuko (ama kama mikopo ya bei nafuu au katika mfumo wa kodi na ada mbalimbali). Mfano wa kitu kama hiki ni kampuni ya Overseas Private Investment Corporation (OPIC) ya Marekani.
Uendeshaji wa Mfuko:
Mfuko huu unaweza kuanzishwa kwa njia mbili – kwa haraka kwa kutumia Agizo la Rais au kwa kutumia utungwaji wa sheria utakaoweka utaratibu wa uendeshaji wa mfuko huu. Lengo kubwa ni kuruhusu ‘flexibility” ya mfuko kuweza kufanya kazi zake. Lakini vyovyote vile itakavyokuwa:
- Mfuko utasimamiwa na Rais au Makamu wa Rais
- Wajumbe wake watatoka Pande zote za Muungano
- Wajumbe wake wataangalia uwiano wa kijinsia
- Usiwe na wajumbe zaidi ya 10 na Kura ya Rais au Makamu wa Rais itakuwa na veto
- Wajumbe watatumikia miaka mitatu na inaweza kurudiwa mara moja tu kwa kila mjumbe (kwa kikomo cha mihula miwili).
- Uteuzi wa wajumbe utazingatia fani za uhandisi, sayansi, usimamiaji miradi, utawala na sheria. Na kila mjumbe atakuwa na kura moja.
- Mjumbe hatoteuliwa kama anashika nafasi yoyote ya kisiasa (ama ya kuteuliwa au kuchaguliwa) ukiondoa Rais na Makamu wa Rais. Na mjumbe yeyote atakayepata nafasi ya kisiasa atapoteza nafasi yake.
- Taratibu za mafao na marupurupu ya wajumbe yataanishwa katika uundwaji wa mfuko.
- Mfuko utakuwa na Mkaguzi wake wa Ndani (internal auditor) lakini pia kwa wakati wowote ule na kwa kawaida utakuwa ni sehemu ya ukaguzi wa kawaida au usio wa kawaida wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
- Mapato na Matumizi ya mfuko kila mwaka hadi senti ya mwisho yatakuwa yanawekwa hadharani na kwenye miradi inayotekelezwa na mfuko.
- Fedha zote zinazokusanywa kutoka katika kesi za ufisadi na uhujumu uchumi au zile zinazotaifishwa
- Fedha zote zinazotokana na makubaliano ya maridhiano kama zile za makanikia au kesi za kimataifa ambazo Tanzania inashinda
- 2% ya mapato yote ya mauzo ya madini (yaani, kila yanapouzwa madini ndani na nje asilimia 2 inaenda kwenye mfuko huu)
- 1% ya mapato yote ya utalii
- Mfuko unaweza kuwekeza kiasi cha fedha (ambacho hakitazidi 15% ya fedha za mfuko) na kujipatia mapato kwa njia hiyo.
Kadha wa kadha.
BARUA PEPE