Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,601
- 34,760
Tukipata Uhuru Stiegler Gorge ilijulikana kama chanzo kizuri cha nishati.Mojawapo ya mambo ambayo yananikera kimipango ni kuwa bado hatujatengeneza mipango inayotangulia matarajio yetu. Yaani, mipango yetu mingi ina malengo ya kukidhi mahitaji ya sasa. Haiangalii projection ya miaka kama hamsini mbeleni. HIvyo, mara zote tunajikuta tunakimbiza kukutana na mahitaji badala ya kuyatangulia. Mradi wa Umeme wa Stiegler's Gorge labda ni wa kwanza ambao kukamilika kwake kutakuwa kumetangulia kwa kiasi kikubwa mahitaji yetu.
Mgao wa umeme wa akina ''Sumaye na Mkapa'' uliibua hoja ya Stiegler Gorge, tuna kumbu kumbu hapa JF si wazo jipya hata kidogo. Hivyo si suala tulilotangulia bali tumechelewa
Tulichelewa kwasababu ya kutoona mbali. Mwaka 1986 Songo songo ilikuwa tayari.
Hatukuwa na mipango ya muda mrefu kati ya gesi na Hydro Power station
Ndiyo maana awamu ya nne ilikuwa gesi mara mpango ukapotea sasa ni Stiegler
Ninachokubaliana nawe ni kuwa hatuna utamaduni wa kuona mbali.
Leo tungekuwa tunauza nishati nchi zote za Afrika mashariki na kati kama tungekaa na kufikiria kuhusu Hydro ya Stiegler pamoja na gesi.