Pendekezo Chanya: Rais Magufuli aanzishe Mfuko wa Ujenzi Mpya na Maendeleo wa Taifa (MUMT)

Pendekezo Chanya: Rais Magufuli aanzishe Mfuko wa Ujenzi Mpya na Maendeleo wa Taifa (MUMT)

Nilikua sijaisoma yote,kumbe umeweka na source ya mapato..waoh mawazo mazuri..nilidhani sisi ndio tujitolee kuchanga...
 
Labda huo mfuko Rais asiwe na nguvu ya kisheria kuugusa, maana mifano ya mifuko inayokusanya pesa moja kwa moja kutoka kwa wafanyakazi tunajua ipo kwenye hali gani.
 
Hili wazo nilikuwanalo lakini upande wa slums na ghettos za mjini kuanzia airport hadi manzese, kinondoni, kawe, Tandale etc..zivyunjwe zote zipangiliwe upya ziwekwe barabara, miundombinu, streetlights, play grounds etc...
 
Hays mamifuko ndiyo kuwatengenezea jukwaa lawatu kupiga mafungu!! Hakuna cha mfuko hapa tutafika hivihivi
Ni masuala ya usimamizi na mipango. Hutengenezi mfuko tu hivi hivi watu watapiga. Lakini sasa hivi upige ngoja ukamatwe.. na jamaa kasema hana tena "msamaha"..
 
View attachment 1241124

Mkazi wa Kijiji cha Nohli, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akihifadhi mazao juu ya paa la nyumba kama alivyokutwa kijijini. PICHA: IBRAHIM JOSEPH (Nipashe)
​
Na. M. M. Mwanakijiji

Tumekuwa tukiona mara kwa mara Rais John Magufuli akiagiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Na tumeona miradi mbalimbali ikitekelezwa kwa kasi kubwa na kwa haraka karibu kila kona ya nchi. Ni katika mwanga wa haya yanayoendelea na katika kufikiria jinsi gani ya kuweka mfumo unaoweza kujiendesha na kuwa wa kudumu (haya yasije kuisha Rais akimaliza muda wake 2025). Hii itakuwa ni sehemu moja ya Rais kuacha alama ya kudumu ya utendaji wake mahili wa kuhalakisha maendeleo ya haraka ya Taifa letu. Haya ni mawazo yangu tu naamini wengine wanaweza kukosoa, kuongezea, kusahihisha na hata kuleta mawazo bora zaidi na labda wahusika wanaweza kupata mawazo na wao wenyewe na wakayaongeza haya na hatimaye tukawa na kitu kizuri ambacho tunaweza tukaona kikiacha alama kuwa na sisi tuliwahi kuwepo. Lengo hasa ni kuhakikisha kuwa tunatengeneza kitu sambasamba na mfumo wa kawaida wa bajeti – kitu ambacho tayari kimetokea – na sasa kukifanya kiwe rasmi.

JINA LA MFUKO

(Kiingereza) Tanzanian National Reconstruction and Development Fund TNRDF/TANAREDEF
(Kiswahili) Mfuko wa Maendeleo na Ujenzi Mpya wa Taifa Tanzania– MUMT

Mfumo uanzishwe kwa agizo la Rais au kwa Sheria ya Bunge.

Lengo la Mfuko:
  • Kukusanya fedha zote ambazo zitakuwa nje ya Bajeti ya Taifa kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia, na kuendeleza miradi maalum ya maendeleo.
  • Mfuko utajiwekeza katika maeneo makubwa matatu:
  • Ujenzi wa nyumba nafuu (affordable housing) lengo ikiwa ni kuwaondoa wananchi wa Tanzania ndani ya miaka 10 kutoka kwenye nyumba za udongo, nyasi na tembe. Msingi mkubwa ni nyumba za vijijini. Lengo ni kuingiza nyumba za matofali ya kuchoma na vigae zisizopungua 500,000 kwa mwaka ifikapo 2025. Ifikapo 2030 Tanzania iwe imeondoka na nyumba za ujima.
  • Ujenzi wa shule za kisasa za msingi kwenye maeneo ambayo bado yana shule zilizochakaa na ambazo ni aibu ya Taifa.
  • Uunganishwaji wa barabara za wilaya na wilaya.
  • Kufadhili miradi yoyote yenye manufaa kwa umma inayohitajika kwa haraka na ambao ukamilishaji wake hauwezi kuzidi zaidi ya mwaka mmoja. Miradi hiyo yaweza kupendekezwa na chombo chochote n ahata mtu yeyote lakini ni lazima iridhiwe na Rais na Mfuko. Kwa hili, Mfuko unaweza kuweka utaratibu wa kukaribisha maombi ya ufadhili kutoka mtu, taasisi, au chombo chochote kile. Mfuko hautatoa ufadhili kwa miradi au taasisi binafsi isipokuwa kama ni lengo 4.
  • Kutoa ufadhili au udhamini wa kifedha kwa makampuni ya Kitanzania (ambayo yanamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania) ambayo yanataka kupanua biashara zake au masoko yake katika eneo lolote la Afrika ya Mashariki na Kati (maeneo ya EA au SADC). Kwa lengo hili mfuko utaanzisha Tanzanian Overseas Private Investment Corporation (TOPIC). Lengo kubwa la eneo hili la mfuko ni kufanya makampuni ya Tanzania kupenya na kustawi. Taratibu zinaweza kuwekwa kwa jinsi gani makampuni hayo yatarudisha ufadhili huo wa mfuko (ama kama mikopo ya bei nafuu au katika mfumo wa kodi na ada mbalimbali). Mfano wa kitu kama hiki ni kampuni ya Overseas Private Investment Corporation (OPIC) ya Marekani.

Uendeshaji wa Mfuko:

Mfuko huu unaweza kuanzishwa kwa njia mbili – kwa haraka kwa kutumia Agizo la Rais au kwa kutumia utungwaji wa sheria utakaoweka utaratibu wa uendeshaji wa mfuko huu. Lengo kubwa ni kuruhusu ‘flexibility” ya mfuko kuweza kufanya kazi zake. Lakini vyovyote vile itakavyokuwa:
  • Mfuko utasimamiwa na Rais au Makamu wa Rais
  • Wajumbe wake watatoka Pande zote za Muungano
  • Wajumbe wake wataangalia uwiano wa kijinsia
  • Usiwe na wajumbe zaidi ya 10 na Kura ya Rais au Makamu wa Rais itakuwa na veto
  • Wajumbe watatumikia miaka mitatu na inaweza kurudiwa mara moja tu kwa kila mjumbe (kwa kikomo cha mihula miwili).
  • Uteuzi wa wajumbe utazingatia fani za uhandisi, sayansi, usimamiaji miradi, utawala na sheria. Na kila mjumbe atakuwa na kura moja.
  • Mjumbe hatoteuliwa kama anashika nafasi yoyote ya kisiasa (ama ya kuteuliwa au kuchaguliwa) ukiondoa Rais na Makamu wa Rais. Na mjumbe yeyote atakayepata nafasi ya kisiasa atapoteza nafasi yake.
  • Taratibu za mafao na marupurupu ya wajumbe yataanishwa katika uundwaji wa mfuko.
  • Mfuko utakuwa na Mkaguzi wake wa Ndani (internal auditor) lakini pia kwa wakati wowote ule na kwa kawaida utakuwa ni sehemu ya ukaguzi wa kawaida au usio wa kawaida wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
  • Mapato na Matumizi ya mfuko kila mwaka hadi senti ya mwisho yatakuwa yanawekwa hadharani na kwenye miradi inayotekelezwa na mfuko.
Vyanzo vya Fedha za Mfuko
  • Fedha zote zinazokusanywa kutoka katika kesi za ufisadi na uhujumu uchumi au zile zinazotaifishwa
  • Fedha zote zinazotokana na makubaliano ya maridhiano kama zile za makanikia au kesi za kimataifa ambazo Tanzania inashinda
  • 2% ya mapato yote ya mauzo ya madini (yaani, kila yanapouzwa madini ndani na nje asilimia 2 inaenda kwenye mfuko huu)
  • 1% ya mapato yote ya utalii
  • Mfuko unaweza kuwekeza kiasi cha fedha (ambacho hakitazidi 15% ya fedha za mfuko) na kujipatia mapato kwa njia hiyo.
Yatokano:

Kadha wa kadha.

BARUA PEPE
Mwambieni aimarishe NSSF yetu kwanza na watulipe mafao yetu ya mkupuo Kama watangulizi wake. Mifuko hiyo mengine isubirie kwanza manake mafao ni hela zetu na yeye huko hawezi tembelea.
 
Vyanzo vya mapato ya mfuko

* Fedha zote zinazokusanywa kutoka katika kesi za ufisadi na uhujumu uchumi au zile zinazotaifishwa

* Fedha zote zinazotokana na makubaliano ya maridhiano kama zile za makanikia au kesi za kimataifa ambazo Tanzania inashinda

Nimelipenda wazo mzee wangu, kwakua umeruhusu michango, kukosoa, mimi sinalo la kukosoa bali pingamizi katika nukta hizo mbili.

Fedha hizi ni fedha za msimu ambazo iwapo tutaboresha usimamizi wa miradi vizuri na kuziba mianya inayopelekea uwepo wa vyanzo hivyo, Ni bora basi tukajikita katika nukta nyingine.

Aidha
Kianzishwe chanzo kingine mfano, kodi itokanayo na mapato ya wananii wa tasnia zote, uigizaji, uchekeshaji na uimbaji.

Hili litajenga taswira kuu moja na ambayo licha ya kusaidia wananchi bali itaongeza mwamko wa wananchi katika kupenda sanaa ya ndani.

Kwa wakati huo huo wasanii watakua wakirejesha shukrani kwa watu ambao wamewapatia kipato ( Kama vungu la kumi au zakka ya kiaina).

Pili, mapato yatokanayo na michezo ikiwamo mpira wa miguu, kikapu, tenesi, Pete, nk. hili pia litaleta kuamiliana kule kule kati ya mashabiki na wachezaji.

Naomba kuwasilisha
 
Idea hii ili ifanye kazi, lazima taasisi za utafiti ambazo zipo na zina technology nzuri ya kujenga nyumba za bei nafuu zihusishwe.
Pengine hata na vyuo vyetu vya uhandisi na usanifu wa majengo.
Lakini ili tufike kwenye lengo, wananchi ni lazima wawe sehemu ya kuondoa tatizo hili. Kwa maana kuwa wanaweza kufundishwa technology rahisi, wakajenga nyumba zao, na baadhi ya mambo yakafanywa na huo mfuko unaopendekezwa. Kama ni machine za kutolea matofali. Kama ni watu wa mipango miji ili nyumba zijengwe kwa mpangilio etc

Mwisho wa siku, sisi kama watanzania tusipoamia kufanya hivyo, hakuna mwingine atakayefanya. Na nafikiri usomi wetu utakuwa na maana zaidi ikiwa tunaweza kufanya vitu vya maana kwa gharama nafuu, vinavyoendana na mazingira yetu
 
Vyanzo vya mapato ya mfuko

* Fedha zote zinazokusanywa kutoka katika kesi za ufisadi na uhujumu uchumi au zile zinazotaifishwa

* Fedha zote zinazotokana na makubaliano ya maridhiano kama zile za makanikia au kesi za kimataifa ambazo Tanzania inashinda

Nimelipenda wazo mzee wangu, kwakua umeruhusu michango, kukosoa, mimi sinalo la kukosoa bali pingamizi katika nukta hizo mbili.

Fedha hizi ni fedha za msimu ambazo iwapo tutaboresha usimamizi wa miradi vizuri na kuziba mianya inayopelekea uwepo wa vyanzo hivyo, Ni bora basi tukajikita katika nukta nyingine.

Aidha
Kianzishwe chanzo kingine mfano, kodi itokanayo na mapato ya wananii wa tasnia zote, uigizaji, uchekeshaji na uimbaji.

Hili litajenga taswira kuu moja na ambayo licha ya kusaidia wananchi bali itaongeza mwamko wa wananchi katika kupenda sanaa ya ndani.

Kwa wakati huo huo wasanii watakua wakirejesha shukrani kwa watu ambao wamewapatia kipato ( Kama vungu la kumi au zakka ya kiaina).

Pili, mapato yatokanayo na michezo ikiwamo mpira wa miguu, kikapu, tenesi, Pete, nk. hili pia litaleta kuamiliana kule kule kati ya mashabiki na wachezaji.

Naomba kuwasilisha
Halafu huitaji hata kuchukua kiasi kikubwa tu; asilimia ndogo tu (chini ya 10)...
 
Idea hii ili ifanye kazi, lazima taasisi za utafiti ambazo zipo na zina technology nzuri ya kujenga nyumba za bei nafuu zihusishwe.
Pengine hata na vyuo vyetu vya uhandisi na usanifu wa majengo.
Lakini ili tufike kwenye lengo, wananchi ni lazima wawe sehemu ya kuondoa tatizo hili. Kwa maana kuwa wanaweza kufundishwa technology rahisi, wakajenga nyumba zao, na baadhi ya mambo yakafanywa na huo mfuko unaopendekezwa. Kama ni machine za kutolea matofali. Kama ni watu wa mipango miji ili nyumba zijengwe kwa mpangilio etc

Mwisho wa siku, sisi kama watanzania tusipoamia kufanya hivyo, hakuna mwingine atakayefanya. Na nafikiri usomi wetu utakuwa na maana zaidi ikiwa tunaweza kufanya vitu vya maana kwa gharama nafuu, vinavyoendana na mazingira yetu
THis is exactly my point.. hatuwezi kufikiliwa kila siku na watu wengine! Teknolojia ipo. Hivi watu wamewahi kujiuliza Marekani chini ya miaka 300 imeweza kujenga nusu ya bara zima.. kuna vijinyumba, nyumba, majumba na mahekalu.. Sasa sisi nini kinatushinda. Na ukienda Marekani utaona kuwa nyumba zote asilimia 80 zinafanana.. jiulize kwanini.. hata majengo ya biashara na maofisi.. utaona yamefanana..
 
Kabla ya kuuanzisha huo mfuko ambao unaonekana unabeba mambo mengi kwa wakati mmoja, yafaa kujiuliza

1. Kwa sasa tuna vyombo gani katika hizo sekta.
2. Changamoto zake ni nini?

3. Huu mfuko mpya utazindoa vipi?

4. Utawala bora upo? Kama upo umeshindwa vipi kuyatekeleza hayo yanayopendekezwa kwenye mfuko mpya?

5. Kwa kuwa wameshindwa wapo tayari kukaa pembeni na kuwapa nafasi wengine?

6. Huyu CAG ataweza kweli kufanya hiyo kazi kama anadhibitiwa kwa sasa kuzikagua baadhi ya sehemu.? Ama pia atapewa mipaka.
7. Magawanyo wake utakuwa vipi hasa tukizingatia baadhi ya viongozi wamekuwa na upendeleo dhahiri?

Ushauri; sioni haja ya kuwa na mfuko wenye majukumu lukuki wakati kwa sasa zipo taasisi mahususi zikifanya kazi.
Tunaweza fanya kwa zile zinazo simamiwa kwa namna tofauti. Tuige kama vile TANROADS,TARURA,(TARUWASA),REA walau imetupo matokea chanya kwa muda mfupi. Ukitazama hivi vyombo uniformity imekuwa kubwa sana hivyo kupelekea utekelezaji wa miradi iliyochini yao kufana.

Rais aendelee kuimarisha taasisi zilizopo ili ziweze kujenga dira ya haya unayotamani kutokea kwa kutengeneza majina mapya ya usimamizi.
 
Rais aendelee kuimarisha taasisi zilizopo ili ziweze kujenga dira ya haya unayotamani kutokea kwa kutengeneza majina mapya ya usimamizi.

Ni maswali mazuri na ya msingi. Hata hivyo, kuanzishwa kwa taasisi moja au nyingine hakuondoi umuhimu au ulazima wa kuwepo kwa taasisi nyingine. Jambo la maana ni kuhakikisha tu kuwa taasisi hizi haziingilian au hazifanyi mambo yale yale na kusababisha redundancy. Taasisi nyingine zitaweza kufanya kazi kama kawaida. Chukulia kwa mfano hospitali. Kwanini kuna kitengo cha Dharura au cha Ajali, au cha Magonjwa ya Moto wakati zipo idara mbalimbali labda zinashughulikia mambo yale yale.

Uwepo wa idara ya dharura (ER) au ile ya maumivu makali (Trauma Center) una lengo la kushughulikia mambo yale ambayo yanahitaji uangalizi wa pekee wa mabingwa na labda suala la muda ni la muhimu. Kwa mfumo wetu wa sasa Rais anaweza kusababisha mambo mengi endapo atatangaza hali ya dharura chini ya Emergency Powers. Si mfumo mzuri na ni wa dharura kweli kweli (kama wakati wa vita au majanga ya kitaifa).

Sasa suala la mfuko huu ni kama kuunda idara ya ER ya utendaji wa serikali. Magonjwa mengine yataendelea kutibiwa na idara na madaktari wake...
 
Duh!

Nje ya mada kidogo...

Naona sijui watu wamekua au sijui ni nini....ila mpaka kufikia hapa hakuna aliyeli-pooh pooh wazo la Mwanakijiji?

Maajabu haya.

Nikirudi kwenye hoja, wazo ni zuri kabisa.

Kwa ujumla, sioni ubaya wake.
 
Duh!

Nje ya mada kidogo...

Naona sijui watu wamekua au sijui ni nini....ila mpaka kufikia hapa hakuna aliyeli-pooh pooh wazo la Mwanakijiji?

Maajabu haya.

Nikirudi kwenye hoja, wazo ni zuri kabisa.

Kwa ujumla, sioni ubaya wake.
Unajua wakati mwingine mantiki Ni vigumu kuipinga. Kwa sababu Hili Ni suala la kujaribu kutatua tatizo. Tayari Rais anaonekana kufanya baadhi ya haya na kwa Hili ataweza kwenda mbali zaidi.
 
Mkuu

1. Sijaona mahali panapoeleza ikiwa ujenzi wa nyumba ( Ukiacha shule na barabara) utakuwajeJe, wananchi watakopeshwa hizo nyumba? kuna mahali nadhani sijaelewa, ufafanuzi tafadhali

2. Kuanzisha miradi 3 (Nyumba, shule na barabara) kwa mazingira yetu ni wazo baya.
Hatuna utamaduni wa kufanya tathmini( evaluation) ya mradi mmoja mmoja.
Kuwa na miradi 3 itakuwa vurugu na mwanzo wa kupoteza uelekeo

Kwanini Mkurabita na ''MEMKU'' havikufanikiwa kuondoa umasikini na kujenga shule?
Kuna tathmini yoyote iliyowahi kufanya ili kujua mafanikio au kushindwa kwake?

3.Wajumbe watoke pande mbili za muungano.
Hapa ni kuingiza politics bila sababu
Kwanini tulikuwa na Mkurabita halafu Mkuza huko upande mwingine.

4. Rais au Makamu kuwa na 'veto'
Hiyo ni kuondoa nguvu ya ushindani wa mawazo. Ikiwa ni project ya umma kura ya veto ni ya nini?

5. Mafao na marupu rupu ya wajumbe yatapangwa.
Kwanini kusiwe na waajiriwa kama taasisi nyingine ili kuondoa vurugu za marupu rupu.
Je, tunajifunza nini kutoka bodi kama za Utalii!

6. Vyanzo viwe fedha kama za ufisadi
Mahakama ya mafisadi imefikia wapi?
Kwanini tunaamini '' ufisadi'' utakuwa sustained. Je, tumekata tamaa ya kupigana na ufisadi?

7. Kwanini vikao Bunge vinavyochukua fedha nyingi visipunguzwe ili zielekezwe katika miradi.

8. Ni bora kutafuta chanzo cha fedha cha uhakika kuliko kutegemea ufisadi.
Mfuko wa Mbunge ufutwe ni chanzo cha uhakika kuliko kusubiri fedha za wezi ikiwa watakamatwa!

9. NHC imeshindwa (kwa mujibu wako)
Je imeshindwa kama taasisi au imeshindwa kusimamiwa kama taasisi na wenye dhamana.

10. Kuna mikoa (naomba niudhi watu) kama Kilimanjaro, nyumba za nyasi zinafutika kuliko maeneo mengine nchini. Ni kwanini iwe hivyo na siyo Dodoma au Singida?

Nini siri ya mafanikio yao! na kwanini isifanyike analysis ya kujua chanzo cha mafanikio yao!

11. Kwanini tusifute kodi kwa vifaa vya ujenzi kama ilivyo kwa matrekta ili kuwawezesha wengi kujenga nyumba (affordable)

12. Tumetumiaje taasisi kama chuo cha ardhi kutafuta suluhu ya ''affordable house''
 
Back
Top Bottom