Mkuu
1. Sijaona mahali panapoeleza ikiwa ujenzi wa nyumba ( Ukiacha shule na barabara) utakuwajeJe, wananchi watakopeshwa hizo nyumba? kuna mahali nadhani sijaelewa, ufafanuzi tafadhali
Hili hapa ni suala la kupanga tu vizuri tu. Ninaposema serikali (kupitia mfuko wetu huu) ishiriki kweny ujenzi wa nyumba na kuwasaidia watu kutoka kwenye nyumba za tembe mengi yanaweza kufanyika.
- Kwa mfano, kuanzisha mashirika ya umma kama
Fannie Mae na
Freddie Mac (mashirika ya Serikali Kuu ya Marekani) ambayo yanatoa udhamini kwa mabenki na taasisi za fedha kuhakikisha kuwa watu wenye kipato cha chini wanaweza kuaccess mikopo ya ununuzi wa nyumba. Kama hawa mabepari waliokubuhu waliona kuwa mfumo wa soko na sekta binafsi peke yake haiwezi kuharakisha accessibility ya home ownership naamini hata sisi mabepari uchwara tunaweza kufikiria kitu.
- Serikali inaweza ikajenga nyumba (kwa gharama ya asilimia 100) lakini ikatumia njia ya "lease to own" au "rent to own" na vijana wanaoanza ajira za kudumu wakawa wanapewa kipaumbele. Lengo ni kuhakikisha kuwa vijana hawa ndani ya miaka kama 20 hii wanaweza kuzimiliki nyumba hizi au hata kutransfer mkopo wao kwenye nyumba ya serikali (kwa mfano kama wakihama mahali).
- Serikali kwa kushirikiana na taasisi binafsi inaweza kuweka mpango kwa mfano wa kusaidia watumishi wake ambao wana miaka kama 15 kabla ya kustaafu kuweza kuanza kumiliki nyumba ambazo serikali itakuwa imezijenga. Wanaendelea kufanya kazi huku wanalipia nyumba mahali fulani; siku ile wanastaafu utumishi wa umma au hata kwenye taasisi ambayo serikali imeingia nayo mkataba watu hao wanakabidhiwa funguo za nyumba zao kwenye miji ya chaguo lao (wanaokenda kustaafia)
- Kwa watu wa vijijini hili linaweza kwenda kuwa moja kwa moja kwa serikali kujenga na kutransfer hizi nyumba kwa watu binafsi kwa punguzo kubwa la fedha ikiwemo kwa mfano kutaka kuwepo na "sweat equity". Kama mkulima anaweza kulima, akipewa nafasi ya kuchoa maji, kubeba mbao, au kufyatua matofali yanayolipiwa na serikali anaweza kuwa na umiliki. TUnaweza kujifunza kupitia taasisi kama
Habitat for Humanity.
- kuna namna nyingi za kuweza kulifanya hili na nina uhakika tuna vichwa vya kutosha kuweza kufikiria mechanisms ya hili.
2. Kuanzisha miradi 3 (Nyumba, shule na barabara) kwa mazingira yetu ni wazo baya.
Hatuna utamaduni wa kufanya tathmini( evaluation) ya mradi mmoja mmoja.
Kuwa na miradi 3 itakuwa vurugu na mwanzo wa kupoteza uelekeo
Kwanini Mkurabita na ''MEMKU'' havikufanikiwa kuondoa umasikini na kujenga shule?
Kuna tathmini yoyote iliyowahi kufanya ili kujua mafanikio au kushindwa kwake?
Haya peke yake si sababu ya kutosha kutoanzisha kitu kingine. Bila ya shaka kabla ya kuamua kufanya kitu kama hiki ni muhimu kuangalia ni wapi tunataka hasa kutoa msaada. Na katika hili ni lazima kuwe na tathmini ya miradi mbalimbali ambayo imejaribiwa na kushindikana na kuangalia wapi tunaweza kuiboresha na wapi huu mfuko utakuja na kusaidia. Naomba uzingatie kuwa lengo la mfuku huu siyo "REPLACEMENT" BALI "SUPPLEMENT".
3.Wajumbe watoke pande mbili za muungano.
Hapa ni kuingiza politics bila sababu
Kwanini tulikuwa na Mkurabita halafu Mkuza huko upande mwingine.
Bahati nzuri au mbaya siasa ni sehemu ya maisha ya kitaifa na ya jamii yeyote ile. Siyo kila kuingiza siasa mahali ni jambo baya. Suala la muhimu ni kuona umuhimu wa kufanya hivyo. Kwa mfano, kama mfuko utataka kufanya mambo sehemu yoyote ya Zanzibar itakuwa ni makosa kukosa hata mjumbe mmoja katika watendaji wa mfuko huo. Huu ni mfumo wetu tuliojijengea Tanzania na si siasa tu ni utaratibu wa kawaida. Kwa hiyo hili la kuhusisha sehemu zote za Muungano siyo tu ni la lazima lakini haliepukiki. Isipokuwa kama tunasema haya matatizo ni ya bara tu na Zanzibar waje na mfumo wao (kitu ambacho kinawezekana kabisa). Tukifanya hivyo tutakuwa bado tumefanya siasa.
4. Rais au Makamu kuwa na 'veto'
Hiyo ni kuondoa nguvu ya ushindani wa mawazo. Ikiwa ni project ya umma kura ya veto ni ya nini?
Lengo la 'veto' hapa siyo siasa tu bali ni kulazimisha maamuzi. Veto haitumiwi kiholela tu bali pale inapotokea kuna kufungamana kwa kura. Lengo ni kuhakikisha kuwa maamuzi yanafikiwa na hatua zinachukuliwa na siyo mijadala isiyokoma. Kwa hiyo hata matumizi ya hiyo veto yatawekwa bayana si lazima kwenye kila jambo veto itakuwa ni ya lazima. Hili si jambo kubwa kivile.
5. Mafao na marupu rupu ya wajumbe yatapangwa.
Kwanini kusiwe na waajiriwa kama taasisi nyingine ili kuondoa vurugu za marupu rupu.
Je, tunajifunza nini kutoka bodi kama za Utalii!
Hili ndio maana nilisema vile utaratibu wowote wa ajira utawekwa. Marupurupu (benefits) ni taratibu za kawaida za ajira. Sasa ukimwajiri mtu utampa mshahara na maslahi yake mengine. Sioni tatizo kwanini hili lisiwekwe. La maana tena ni kuhakikisha tu kuwa kila kitu kinawekwa utaratibu mzuri na kuondoa marupurupu yasiyo ya lazima au ambayo yanaua lengo lenyewe. Lengo ni kujifunza hata yaliyotokea kwenye bodi ya utalii na sehemu nyingine ambapo marupurupu yalikuwa ni sababu kubwa ya ufisadi katika taasisi.
6. Vyanzo viwe fedha kama za ufisadi
Mahakama ya mafisadi imefikia wapi?
Kwanini tunaamini '' ufisadi'' utakuwa sustained. Je, tumekata tamaa ya kupigana na ufisadi?
Haya ni mapendekezo tu. Ufisadi upo na utakuwepo kwa kadiri ya kwamba wanadamu bado wapo. Hata tuudhibiti kiasi gani bado utakuwepo na hasa kama hali ya uchumi wetu itaendelea kukua. Sasa kwa kadiri tunavyoudhibiti vile vile tunatumia mifumo kuhakikisha fedha zinarudi kwa Watanzania. Sizungumzii hatua kama ya kuzungumza na watuhumiwa. Nazungumzia mfumo wa kawaida hata wa mahakama ambapo baada ya watu kukutwa na hatia, mali za kutaifishwa au kufilisiwa au kupigwa faini sehemu ya hizo fedha (hata zote ikiwezekana) zinaenda kwenye huu mfuko.
7. Kwanini vikao Bunge vinavyochukua fedha nyingi visipunguzwe ili zielekezwe katika miradi.
Pendekezo murua. Siyo tu vikao, hata idadi ya wabunge na mawaziri na watendaji wengine inaweza kupunguzwa. Sidhani kama kwa nchi kama ya kwetu kuna sababu ya kuwa na wabunge wengi tulionao. Tanzania kiukweli kabisa hiitaji wabunge zaidi ya 200. Fyekelea mbali wabunge 100 unaokoa kiasi kikubwa, unatumbukiza kwenye mfuko.
8. Ni bora kutafuta chanzo cha fedha cha uhakika kuliko kutegemea ufisadi.
Mfuko wa Mbunge ufutwe ni chanzo cha uhakika kuliko kusubiri fedha za wezi ikiwa watakamatwa!
Hii ingefutwa siku ya kwanza tu baada ya kupitishwa mfuko huu. Niliyapanga haya madudu enzi zile na bado sijaona sababu yake. Lengo lake ni sawa na hili lakini bahati mbaya ilikuwa ni namna ya kumpa mbunge 'ujiko' fulani hivi.
9. NHC imeshindwa (kwa mujibu wako)
Je imeshindwa kama taasisi au imeshindwa kusimamiwa kama taasisi na wenye dhamana.
Imeshindwa katika pande zote - kama taasisi (lengo na muundo wake ulibadilika) na pia umeshindwa kama wenye dhamana ya ujenzi wa nyumba. Binafsi, NHC ingekuwa absorbed na mfuko huu (chini ya mfuko) labda kwa kutekeleza jibu langu la kwanza hapo juu kuhusu mashirika ya serikali.
Nitaendelea kujibu yale maswali mengine baadaye. Ngoja nijenge nchi ya Trump kwanza wakati naifikiria nchi yangu.