Nafikiri moja ya matatizo yanayotufanya tusiendelee ni kutaka vitu vianze kufanywa juu na viongozi.
Tunaona watu wakijipanga wenyewe, au kwa kupitia kwa wabunge wao wapitushe sheria za kuanzisha vitu, inakuwa haitishi.
Mpaka vitu vitoke kwa rais.
Ndiyo maana sasa hivi utasikia watu wengi sana wanamlikia Magufuli.
Kwa mambo anayotakiwa na asiyotakiwa kufanya.
Hii ni tabia ya jamii ambayo haiamini mifumo yake, inaamini katika njia za mkato na kumtumia strongman aliye juu kabisa.
Hili ni tatizo. Tunalemaza mifumo. Vitu vingine watu wanatakiwa wafanye wenyewe, vingine wanatakiwa wajipange kushinikiza wabunge wao sheria zitungwe.
Hata huyo rais mwenyewe inakuwa vizuri zaidi akitia saini miswada iliyopitishwa na bunge, si kujiundia vitu tu kwa presidential decree.
Kimsingi unachopendekeza kingefanya vizuri iwapo BRN ingeendelezwa na kuboreshwa. BRN ilijikita kwenye tija katika UZALISHAJI na utafutaji wa rasilimali ili kutekeleza miradi/mipango ya kimkakati ya nchi. Hiki unachopendekeza kimejikita kwenye matumizi ya tulichonacho bila kubainIsha tunakiongezaje. Kama nchi, tatizo kubwa lipo kwenye tija katika uzalishaji.BRN ulikuwa Ni utapeli fulani
View attachment 1241124Na. M. M. Mwanakijiji
Mkazi wa Kijiji cha Nohli, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akihifadhi mazao juu ya paa la nyumba kama alivyokutwa kijijini. PICHA: IBRAHIM JOSEPH (Nipashe)
Tumekuwa tukiona mara kwa mara Rais John Magufuli akiagiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Na tumeona miradi mbalimbali ikitekelezwa kwa kasi kubwa na kwa haraka karibu kila kona ya nchi. Ni katika mwanga wa haya yanayoendelea na katika kufikiria jinsi gani ya kuweka mfumo unaoweza kujiendesha na kuwa wa kudumu (haya yasije kuisha Rais akimaliza muda wake 2025). Hii itakuwa ni sehemu moja ya Rais kuacha alama ya kudumu ya utendaji wake mahili wa kuhalakisha maendeleo ya haraka ya Taifa letu. Haya ni mawazo yangu tu naamini wengine wanaweza kukosoa, kuongezea, kusahihisha na hata kuleta mawazo bora zaidi na labda wahusika wanaweza kupata mawazo na wao wenyewe na wakayaongeza haya na hatimaye tukawa na kitu kizuri ambacho tunaweza tukaona kikiacha alama kuwa na sisi tuliwahi kuwepo. Lengo hasa ni kuhakikisha kuwa tunatengeneza kitu sambasamba na mfumo wa kawaida wa bajeti – kitu ambacho tayari kimetokea – na sasa kukifanya kiwe rasmi.
JINA LA MFUKO
(Kiingereza) Tanzanian National Reconstruction and Development Fund TNRDF/TANAREDEF
(Kiswahili) Mfuko wa Maendeleo na Ujenzi Mpya wa Taifa Tanzania– MUMT
Mfumo uanzishwe kwa agizo la Rais au kwa Sheria ya Bunge.
Lengo la Mfuko:
- Kukusanya fedha zote ambazo zitakuwa nje ya Bajeti ya Taifa kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia, na kuendeleza miradi maalum ya maendeleo.
- Mfuko utajiwekeza katika maeneo makubwa matatu:
- Ujenzi wa nyumba nafuu (affordable housing) lengo ikiwa ni kuwaondoa wananchi wa Tanzania ndani ya miaka 10 kutoka kwenye nyumba za udongo, nyasi na tembe. Msingi mkubwa ni nyumba za vijijini. Lengo ni kuingiza nyumba za matofali ya kuchoma na vigae zisizopungua 500,000 kwa mwaka ifikapo 2025. Ifikapo 2030 Tanzania iwe imeondoka na nyumba za ujima.
- Ujenzi wa shule za kisasa za msingi kwenye maeneo ambayo bado yana shule zilizochakaa na ambazo ni aibu ya Taifa.
- Uunganishwaji wa barabara za wilaya na wilaya.
- Kufadhili miradi yoyote yenye manufaa kwa umma inayohitajika kwa haraka na ambao ukamilishaji wake hauwezi kuzidi zaidi ya mwaka mmoja. Miradi hiyo yaweza kupendekezwa na chombo chochote n ahata mtu yeyote lakini ni lazima iridhiwe na Rais na Mfuko. Kwa hili, Mfuko unaweza kuweka utaratibu wa kukaribisha maombi ya ufadhili kutoka mtu, taasisi, au chombo chochote kile. Mfuko hautatoa ufadhili kwa miradi au taasisi binafsi isipokuwa kama ni lengo 4.
- Kutoa ufadhili au udhamini wa kifedha kwa makampuni ya Kitanzania (ambayo yanamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania) ambayo yanataka kupanua biashara zake au masoko yake katika eneo lolote la Afrika ya Mashariki na Kati (maeneo ya EA au SADC). Kwa lengo hili mfuko utaanzisha Tanzanian Overseas Private Investment Corporation (TOPIC). Lengo kubwa la eneo hili la mfuko ni kufanya makampuni ya Tanzania kupenya na kustawi. Taratibu zinaweza kuwekwa kwa jinsi gani makampuni hayo yatarudisha ufadhili huo wa mfuko (ama kama mikopo ya bei nafuu au katika mfumo wa kodi na ada mbalimbali). Mfano wa kitu kama hiki ni kampuni ya Overseas Private Investment Corporation (OPIC) ya Marekani.
Uendeshaji wa Mfuko:
Mfuko huu unaweza kuanzishwa kwa njia mbili – kwa haraka kwa kutumia Agizo la Rais au kwa kutumia utungwaji wa sheria utakaoweka utaratibu wa uendeshaji wa mfuko huu. Lengo kubwa ni kuruhusu ‘flexibility” ya mfuko kuweza kufanya kazi zake. Lakini vyovyote vile itakavyokuwa:
Vyanzo vya Fedha za Mfuko
- Mfuko utasimamiwa na Rais au Makamu wa Rais
- Wajumbe wake watatoka Pande zote za Muungano
- Wajumbe wake wataangalia uwiano wa kijinsia
- Usiwe na wajumbe zaidi ya 10 na Kura ya Rais au Makamu wa Rais itakuwa na veto
- Wajumbe watatumikia miaka mitatu na inaweza kurudiwa mara moja tu kwa kila mjumbe (kwa kikomo cha mihula miwili).
- Uteuzi wa wajumbe utazingatia fani za uhandisi, sayansi, usimamiaji miradi, utawala na sheria. Na kila mjumbe atakuwa na kura moja.
- Mjumbe hatoteuliwa kama anashika nafasi yoyote ya kisiasa (ama ya kuteuliwa au kuchaguliwa) ukiondoa Rais na Makamu wa Rais. Na mjumbe yeyote atakayepata nafasi ya kisiasa atapoteza nafasi yake.
- Taratibu za mafao na marupurupu ya wajumbe yataanishwa katika uundwaji wa mfuko.
- Mfuko utakuwa na Mkaguzi wake wa Ndani (internal auditor) lakini pia kwa wakati wowote ule na kwa kawaida utakuwa ni sehemu ya ukaguzi wa kawaida au usio wa kawaida wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
- Mapato na Matumizi ya mfuko kila mwaka hadi senti ya mwisho yatakuwa yanawekwa hadharani na kwenye miradi inayotekelezwa na mfuko.
Yatokano:
- Fedha zote zinazokusanywa kutoka katika kesi za ufisadi na uhujumu uchumi au zile zinazotaifishwa
- Fedha zote zinazotokana na makubaliano ya maridhiano kama zile za makanikia au kesi za kimataifa ambazo Tanzania inashinda
- 2% ya mapato yote ya mauzo ya madini (yaani, kila yanapouzwa madini ndani na nje asilimia 2 inaenda kwenye mfuko huu)
- 1% ya mapato yote ya utalii
- Mfuko unaweza kuwekeza kiasi cha fedha (ambacho hakitazidi 15% ya fedha za mfuko) na kujipatia mapato kwa njia hiyo.
Kadha wa kadha.
BARUA PEPE
Mkuu
1. Sijaona mahali panapoeleza ikiwa ujenzi wa nyumba ( Ukiacha shule na barabara) utakuwajeJe, wananchi watakopeshwa hizo nyumba? kuna mahali nadhani sijaelewa, ufafanuzi tafadhali
2. Kuanzisha miradi 3 (Nyumba, shule na barabara) kwa mazingira yetu ni wazo baya.
Hatuna utamaduni wa kufanya tathmini( evaluation) ya mradi mmoja mmoja.
Kuwa na miradi 3 itakuwa vurugu na mwanzo wa kupoteza uelekeo
Kwanini Mkurabita na ''MEMKU'' havikufanikiwa kuondoa umasikini na kujenga shule?
Kuna tathmini yoyote iliyowahi kufanya ili kujua mafanikio au kushindwa kwake?
3.Wajumbe watoke pande mbili za muungano.
Hapa ni kuingiza politics bila sababu
Kwanini tulikuwa na Mkurabita halafu Mkuza huko upande mwingine.
4. Rais au Makamu kuwa na 'veto'
Hiyo ni kuondoa nguvu ya ushindani wa mawazo. Ikiwa ni project ya umma kura ya veto ni ya nini?
5. Mafao na marupu rupu ya wajumbe yatapangwa.
Kwanini kusiwe na waajiriwa kama taasisi nyingine ili kuondoa vurugu za marupu rupu.
Je, tunajifunza nini kutoka bodi kama za Utalii!
6. Vyanzo viwe fedha kama za ufisadi
Mahakama ya mafisadi imefikia wapi?
Kwanini tunaamini '' ufisadi'' utakuwa sustained. Je, tumekata tamaa ya kupigana na ufisadi?
7. Kwanini vikao Bunge vinavyochukua fedha nyingi visipunguzwe ili zielekezwe katika miradi.
8. Ni bora kutafuta chanzo cha fedha cha uhakika kuliko kutegemea ufisadi.
Mfuko wa Mbunge ufutwe ni chanzo cha uhakika kuliko kusubiri fedha za wezi ikiwa watakamatwa!
Imeshindwa katika pande zote - kama taasisi (lengo na muundo wake ulibadilika) na pia umeshindwa kama wenye dhamana ya ujenzi wa nyumba. Binafsi, NHC ingekuwa absorbed na mfuko huu (chini ya mfuko) labda kwa kutekeleza jibu langu la kwanza hapo juu kuhusu mashirika ya serikali.9. NHC imeshindwa (kwa mujibu wako)
Je imeshindwa kama taasisi au imeshindwa kusimamiwa kama taasisi na wenye dhamana.
- TUnaweza kujifunza kupitia taasisi kama Habitat for Humanity.
Hili ni swali zuri lakini pia ni swali lenye udhanifu mwingi. Mikoa kama Kilimanjaro haina maana ina nyumba bora kwa kila mtu na kwamba haiitaji kuinua kiwango cha nyumba za watu wake. Bila ya shaka kuna maeneo ambayo watu wamejenga na sababu zinazojulikana na watu wengine wanaweza kujifunza kutoka huko. Nina bahati ya kupita pita pande hizo na unaweza kuna maendeleo makubwa ya nyumba na changamoto zilizopo.Mkuu
10. Kuna mikoa (naomba niudhi watu) kama Kilimanjaro, nyumba za nyasi zinafutika kuliko maeneo mengine nchini. Ni kwanini iwe hivyo na siyo Dodoma au Singida?
Sidhani kama kuna siri; ukitaka kufuata siri yao kwa kila mkoa uige itachukua muda mrefu sana kuweza kufanikiwa.Nini siri ya mafanikio yao! na kwanini isifanyike analysis ya kujua chanzo cha mafanikio yao!
11. Kwanini tusifute kodi kwa vifaa vya ujenzi kama ilivyo kwa matrekta ili kuwawezesha wengi kujenga nyumba (affordable)
12. Tumetumiaje taasisi kama chuo cha ardhi kutafuta suluhu ya ''affordable house''
Kama nchi hatuwezi kukata tamaa kupambana na umaskini tulionao ni jukumu la serikali kuwa na Taasisi imara/mathubuti wakati ikiwaletea wananchi wake maendeleo.
Tunaweza fanya kwa zile zinazo simamiwa kwa namna tofauti. Tuige kama vile TANROADS,TARURA,(TARUWASA),REA walau imetupo matokea chanya kwa muda mfupi. Ukitazama hivi vyombo uniformity imekuwa kubwa sana hivyo kupelekea utekelezaji wa miradi iliyochini yao kufana.
Rais aendelee kuimarisha taasisi zilizopo ili ziweze kujenga dira ya haya unayotamani kutokea kwa kutengeneza majina mapya ya usimamizi.
Wazo zuri mkuu sema utekelezaji wake utakuwa finyu,ni kama REA ina lengo zuri lakini Umeme tu hapo bagamoyo tu hakuna,nenda mwandege tu umeme hakuna,nenea vikindu karibu na DSM umeme hakuna,kama Tanesco wamewapa REA wasambaze umeme vijijini,mbona tu DSM tu umeme hakuna maeneo mengi? Hii si aibu kwa Tanesco?View attachment 1241124Na. M. M. Mwanakijiji
Mkazi wa Kijiji cha Nohli, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma akihifadhi mazao juu ya paa la nyumba kama alivyokutwa kijijini. PICHA: IBRAHIM JOSEPH (Nipashe)
Tumekuwa tukiona mara kwa mara Rais John Magufuli akiagiza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Na tumeona miradi mbalimbali ikitekelezwa kwa kasi kubwa na kwa haraka karibu kila kona ya nchi. Ni katika mwanga wa haya yanayoendelea na katika kufikiria jinsi gani ya kuweka mfumo unaoweza kujiendesha na kuwa wa kudumu (haya yasije kuisha Rais akimaliza muda wake 2025). Hii itakuwa ni sehemu moja ya Rais kuacha alama ya kudumu ya utendaji wake mahili wa kuhalakisha maendeleo ya haraka ya Taifa letu. Haya ni mawazo yangu tu naamini wengine wanaweza kukosoa, kuongezea, kusahihisha na hata kuleta mawazo bora zaidi na labda wahusika wanaweza kupata mawazo na wao wenyewe na wakayaongeza haya na hatimaye tukawa na kitu kizuri ambacho tunaweza tukaona kikiacha alama kuwa na sisi tuliwahi kuwepo. Lengo hasa ni kuhakikisha kuwa tunatengeneza kitu sambasamba na mfumo wa kawaida wa bajeti – kitu ambacho tayari kimetokea – na sasa kukifanya kiwe rasmi.
JINA LA MFUKO
(Kiingereza) Tanzanian National Reconstruction and Development Fund TNRDF/TANAREDEF
(Kiswahili) Mfuko wa Maendeleo na Ujenzi Mpya wa Taifa Tanzania– MUMT
Mfumo uanzishwe kwa agizo la Rais au kwa Sheria ya Bunge.
Lengo la Mfuko:
- Kukusanya fedha zote ambazo zitakuwa nje ya Bajeti ya Taifa kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia, na kuendeleza miradi maalum ya maendeleo.
- Mfuko utajiwekeza katika maeneo makubwa matatu:
- Ujenzi wa nyumba nafuu (affordable housing) lengo ikiwa ni kuwaondoa wananchi wa Tanzania ndani ya miaka 10 kutoka kwenye nyumba za udongo, nyasi na tembe. Msingi mkubwa ni nyumba za vijijini. Lengo ni kuingiza nyumba za matofali ya kuchoma na vigae zisizopungua 500,000 kwa mwaka ifikapo 2025. Ifikapo 2030 Tanzania iwe imeondoka na nyumba za ujima.
- Ujenzi wa shule za kisasa za msingi kwenye maeneo ambayo bado yana shule zilizochakaa na ambazo ni aibu ya Taifa.
- Uunganishwaji wa barabara za wilaya na wilaya.
- Kufadhili miradi yoyote yenye manufaa kwa umma inayohitajika kwa haraka na ambao ukamilishaji wake hauwezi kuzidi zaidi ya mwaka mmoja. Miradi hiyo yaweza kupendekezwa na chombo chochote n ahata mtu yeyote lakini ni lazima iridhiwe na Rais na Mfuko. Kwa hili, Mfuko unaweza kuweka utaratibu wa kukaribisha maombi ya ufadhili kutoka mtu, taasisi, au chombo chochote kile. Mfuko hautatoa ufadhili kwa miradi au taasisi binafsi isipokuwa kama ni lengo 4.
- Kutoa ufadhili au udhamini wa kifedha kwa makampuni ya Kitanzania (ambayo yanamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania) ambayo yanataka kupanua biashara zake au masoko yake katika eneo lolote la Afrika ya Mashariki na Kati (maeneo ya EA au SADC). Kwa lengo hili mfuko utaanzisha Tanzanian Overseas Private Investment Corporation (TOPIC). Lengo kubwa la eneo hili la mfuko ni kufanya makampuni ya Tanzania kupenya na kustawi. Taratibu zinaweza kuwekwa kwa jinsi gani makampuni hayo yatarudisha ufadhili huo wa mfuko (ama kama mikopo ya bei nafuu au katika mfumo wa kodi na ada mbalimbali). Mfano wa kitu kama hiki ni kampuni ya Overseas Private Investment Corporation (OPIC) ya Marekani.
Uendeshaji wa Mfuko:
Mfuko huu unaweza kuanzishwa kwa njia mbili – kwa haraka kwa kutumia Agizo la Rais au kwa kutumia utungwaji wa sheria utakaoweka utaratibu wa uendeshaji wa mfuko huu. Lengo kubwa ni kuruhusu ‘flexibility” ya mfuko kuweza kufanya kazi zake. Lakini vyovyote vile itakavyokuwa:
Vyanzo vya Fedha za Mfuko
- Mfuko utasimamiwa na Rais au Makamu wa Rais
- Wajumbe wake watatoka Pande zote za Muungano
- Wajumbe wake wataangalia uwiano wa kijinsia
- Usiwe na wajumbe zaidi ya 10 na Kura ya Rais au Makamu wa Rais itakuwa na veto
- Wajumbe watatumikia miaka mitatu na inaweza kurudiwa mara moja tu kwa kila mjumbe (kwa kikomo cha mihula miwili).
- Uteuzi wa wajumbe utazingatia fani za uhandisi, sayansi, usimamiaji miradi, utawala na sheria. Na kila mjumbe atakuwa na kura moja.
- Mjumbe hatoteuliwa kama anashika nafasi yoyote ya kisiasa (ama ya kuteuliwa au kuchaguliwa) ukiondoa Rais na Makamu wa Rais. Na mjumbe yeyote atakayepata nafasi ya kisiasa atapoteza nafasi yake.
- Taratibu za mafao na marupurupu ya wajumbe yataanishwa katika uundwaji wa mfuko.
- Mfuko utakuwa na Mkaguzi wake wa Ndani (internal auditor) lakini pia kwa wakati wowote ule na kwa kawaida utakuwa ni sehemu ya ukaguzi wa kawaida au usio wa kawaida wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
- Mapato na Matumizi ya mfuko kila mwaka hadi senti ya mwisho yatakuwa yanawekwa hadharani na kwenye miradi inayotekelezwa na mfuko.
Yatokano:
- Fedha zote zinazokusanywa kutoka katika kesi za ufisadi na uhujumu uchumi au zile zinazotaifishwa
- Fedha zote zinazotokana na makubaliano ya maridhiano kama zile za makanikia au kesi za kimataifa ambazo Tanzania inashinda
- 2% ya mapato yote ya mauzo ya madini (yaani, kila yanapouzwa madini ndani na nje asilimia 2 inaenda kwenye mfuko huu)
- 1% ya mapato yote ya utalii
- Mfuko unaweza kuwekeza kiasi cha fedha (ambacho hakitazidi 15% ya fedha za mfuko) na kujipatia mapato kwa njia hiyo.
Kadha wa kadha.
BARUA PEPE
Sijaelewa haupo kwa sababu haujafika au haupo kwa sababu watu hawajamudu kujiunganishia?Wazo zuri mkuu sema utekelezaji wake utakuwa finyu,ni kama REA ina lengo zuri lakini Umeme tu hapo bagamoyo tu hakuna,nenda mwandege tu umeme hakuna,nenea vikindu karibu na DSM umeme hakuna,kama Tanesco wamewapa REA wasambaze umeme vijijini,mbona tu DSM tu umeme hakuna maeneo mengi? Hii si aibu kwa Tanesco?
Haupo kwasababu fedha zinazokusanywa zinaishia kwenye matumbo na mifuko ya watu na wanashindwa kufanya malengo ya kuanzisha mradi(hawatimizi malengo yaliyokusudiwa ,fedha zinaishia katika upembuzi yakinifu,usanifu wa kina,warsha ,makongamano na semina elekezi),miradi mingi inasuasua.Sijaelewa haupo kwa sababu haujafika au haupo kwa sababu watu hawajamudu kujiunganishia?