"Dan Zwangendaba, post: 33232253, member: 223542"]
Aidha kwa upande wa matumizi, matatizo makubwa tuliyonayo ni kutokuwepo kwa rasilimali fedha yenye kutosha kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati (ikiwemo hii unayoipendekeza) na matumizi yasiyoendana na thamani halisi ya fedha (value for money).
Mkuu, rasilimali ''fedha' tunayo. Kinachokosekana ni mawazo na mipango mizuri, matumbo na si wananchi
Kwa mfano, wazo wa MM la mfuko, bila kutumia mchumi mwenye certificate linawezekana japo kwa nyumba 1000 kwa mwaka kwa uchache sana.
Mfuko unaweza kuanza na mabilioni bila kuchukua chochote hazina au kwingine.
Fikiria tuna Wabunge 357 na kila mmoja anapata pesa za mfuko wa jimbo, pesa zisizofanyiwa audit wala sheria ya kuzitumia.
Kwa ujinga ujinga tu tufanye kuwa kila mbunge anapata 50 milioni. Je, ni kiasi gani hicho
Fikiria pesa wanazolipwa wabunge kwa kukaa katika viti tu kwa siku mara 357, ni kiasi gani!
Kuna sababu gani Bunge likae miezi miwili ikiwa tumeona miswada inapitishwa usiku mmoja?
Fikiria, Wabunge zaidi ya 100 wanatoka Zanzibar.
Kwanini wakae Dodoma kujadili mambo yasiyo ya muungano kwa miezi miwili au mitatu. Kwanini Bajeti ispangwe wakatanguliza ya muungano kisha wakaondoka.
Tungeokoa pesa kiasi gani?
Inawezekaje serikali ikawa na pesa za kuwakopesha mashangingi ambayo hulipa takribani nusu na nusu nyingine ni ruzuku kutoka kodi zetu, halafu taukashindwa kujenga nyumba za bei nafuu hata 1000 kwa mwaka?
Muhimu zaidi ni kujiuliza kwa gharama zote hizo kwanini hatusikii wazo kama hili la MM bila kujali uzuri au ubaya wake. Kwanini hakuna idea katika gharama kubwa kama hiyo?
Ni muda kiasi gani unatumika kusifiana, kujadili namna ya kufunga JF , kujadili kufutiana ubunge badala ya kujadili mawazo ya kuboresha maisha ya wananchi kama ujenzi wa nyumba nafuu!
Eneo jingine linalosikitisha ni ruzuku za vyama. Hivi chama kisichoweza ku generate income kwa nguvu zake kinaweza kuwa na wazo la ujenzi wa nyumba za bei nafuu!
Kuna Bodi za mashirika ambazo sijui hasa zaina kazi gani. Bodi ya Utalii imesaidiaje kukuza utalii kiasi kwamba Mauritius inapata watalii sawa na Tanzania. !
Wazo la MM inaweza kuonekana ''impractical' hasa kwa kuangalia mapato ya mfuko.
Ukitumia darubini iliyotengenezwa Korea kaskazini utaona wazo hilo linawezekana kabisa