Pendekezo: Itungwe sheria ya upimaji wa DNA kwa mtoto. Sheria iwe lazima pindi tu mtoto anapozaliwa

Shetani sio kiumbe shetani ni matendo....
Sawa, ikiwa ni hivyo, ushetani uko kwa jinsia zote.
Kama ambavyo sio wanawake wote wanabambikizia watu mimba/watoto hali kadhalika kuna wanaume matendo yao utafikiri ndio wakufunzi wa chuo cha uovu. Ni kwa sababu hiyo hua sipendi kujumuisha watu kwenye jambo moja.
 
Hakika hili nalo litazamwe wabongo wengi wanapenda vitu vyepesi vyepesi, DNA ipimwe baada tu ya Mtoto kuzaliwa.
 
Watu wapime DNA, kila wakati ndoa inapopata mtoto kabla mtoto hajakua wala kujitambua, mama mtu apeleke mtoto kwa baba yake mapema, na kama ni kulea kwa hiari mwanaume aliyesingiziwa mtoto ndiyo aamue mwenyewe.

Hii itasaidia kupunguza ukatili katika ndoa na familia pale ambapo mwanaume anahangaija kulea na baadae inakuja kugundulika mtoto si wake.

Pia itapunguza watoto wa mitaani pale ambapo watoto watafahamiana na wazazi wao mapema na wazazi kuanza kuwajibika juu yake.

Pia itasaidia wanawake kuwa waaminifu kwenye ndoa zao.

Pia itasaidia kulinda haki ya mwanaume katika ndoa maana huu uonevu umeenea Africa na watu wanaona kama ni hali ya kawaida na kumbe ni ukatili wa kijinsia.
 
Nakubaliana na wewe katika hili lakini kwa hili lililopo mezani wahanga wanabakia kuwa wanaume
 
Ujinga wewe garbage in garbage out unapooa kuwa makini sio unaoa kienyeji au kuzaa hovyo na mi garbage in yako kisha unakuja Sumbua mtoto kupima DNA

Ujinga tu huo
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ garbage..
Huyu mtu anatumia kiungo gani kufikiria.
Mbona maoni yake hayaingii akilini. πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hakika hili nalo litazamwe wabongo wengi wanapenda vitu vyepesi vyepesi, DNA ipimwe baada tu ya Mtoto kuzaliwa.
Kamwambie mama yako na baba yako na wewe mwende mkapime DNA kuthibitisha kama wewe ni mtoto wao au la na kama
hawakukuokota jalalani ulipotupwa na mama yako malaya original ambaye hakutaka mtoto wao wakakulea kama mtoto wao wakati sio hiyo siri walikuficha Ili ukajue siri iliyojificha kwenye Pandora box kujua wewe sio mtoto wao sio wa baba yako wala mama yako ni mtoto wa majalalani

Waburuze wazazi wako mahakamani mkapime DNA uthibitishe kama hao ni wazazi wako? sio kesi

Wakionekana sio kamtafute baba yako na mama yako majalalani
 
Itafaa mtoto akizaliwa paternity test ifanyike pamoja na maternity test.

Kuna documentary niliangalia, inasema zamani kipindi binadamu tunaishi kama hunters and gatheres, tulikuwa tunaamini kwenye usawa wa hali ya juu(egalitarianism).

Watu walikuwa hawawazi wake zao wametembea na nani, mtoto analelewa na kabila zima.
Kulikuwa na kabila linaitwa 'Bari' huko Venezuela, kwao wanaume wote wanaoshiriki ngono na mwanamke kipindi cha ujauzito wake, watawajibika kama baba wa mtoto.

Na wanasayansi wanasema hii njia ilitusaidia sana, kwasababu mtoto akiwa na walezi wengi, uwezekano wa kuishi mpaka utu uzima unaongezeka, jamii yetu ya binadamu inaepukana na kutoweka.

Nadhani huu msemo wa 'Kitanda hakizai haramu' ni wa wahenga wa zama hizo, zama ambazo hata haya mambo ya DNA hayakuwepo.
Huu msemo tunaufafanua bila muktadha wa wakati ulipotokea.
 
Mbona unavuruga mada!?
Jamaa kasema mtoto apimwe akishazaliwa inamaana hapo inazungumziwa suala la mwanaume kaona mkewe ana mimba na akaitunza mimba hadi mtoto kuzaliwa.

Suala la mtoto kuokotwa na mke kubeba mimba huku ukimuona anajifungua na mtoto kumbe sio wako vinaingilianaje!??
We jamaa niaje aisee!?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nakubaliana na wewe katika hili lakini kwa hili lililopo mezani wahanga wanabakia kuwa wanaume
Ni kweli, lakini ni kama unajikita zaidi kwenye matokeo kuliko kuangalia chanzo cha tatizo kiongozi, niliuliza awali kwenye post yangu ya mwanzo kabisa, kama mwanamke anabambikia mwanaume mwingine mimba inamaana kuna mwanaume mwingine amempatia mimba kimagendo, sahihi? Sasa wakati tunataka kumlaumu na kumuona huyo mwanamke ana ushetani, huyu mwanaume inakuaje abaki salama bila kamisheni yake ya ushetani?

Wanaume wote wangejitambua unafikiri hao wanawake wangepata hizo mimba za kuwabambikia watu?
 
Nadhani huu msemo wa 'Kitanda hakizai haramu' ni wa wahenga wa zama hizo, zama ambazo hata haya mambo ya DNA hayakuwepo.
Huu msemo tunaufafanua bila muktadha wa wakati ulipotokea.
Waafrika kwa hilo libaki hivyo hivyo tusiige wazungu kuna hekima kubwa sana kwenye hilo ambayo ni only African Tradition leaders Philisophers waweza fafanua sio wazungu na DNA test hopeless philosophy zao za kujua mtoto wa nani

Eneo hilo waafrika tuko mbali kuliko wazungu tuna akili kuwashinda nobody has copyright of knowledge
 
Mke wa mtu anayetongozwa na kukubali kulala na mwanaume mwingine asiye mumewe huyo ni shetani........vivo hivyo kwa mume wa mtu
 
I
Ivi we una Wajina wanawake au unawaskia, mwanamke anaamua ni nani atazaa nae, anajua mwanaume aliyempatia mimba anajua kila kitu.

Kinachofanya mwanamke abambikize mimba ni masuala ya kiuchumi mwanamke akiona unahela na una uwezo wa kulea mimba vizuri na pia unaweza kulea mtoto vizuri basi anakubali kuolewa na wewe ila watoto anazaa na mwanaume mwenye muonekano ili apate watoto wazuri we kazi yako ni kulea na kuandikishwa jina Kwenye vyeti tu πŸ˜‚
 
HAyo ni mambo ya zamani, we unaona kwa maisha ya sasa na mambo yanayoendelea huku mjini ni sawa af unasema tunaakili we Acha kutudharaulisha hivyo hayo maswala ya kitanda hakizai haramu ilikuwa ni mambo ya zamani kuleta hali ya kuridhika kulea mtoto anayezaliwa katika nyumba husika bila migogoro.
Kwa zamani ilikuwa rahisi mana wanawake walikuwa na heshima tofauti na wasasa ambao wanaweza kuchafukwa wakaanza kejeli na kusema kwanza huna mtoto hapa we ni Mlezi tu.

Zamani chakula mavazi na gharama za maisha zilikuwa affordable tofaut na maisha ya sasa hali ngumu unalea mtoto baadae anaenda kwao af unabaki mikono mitupu what a foolish philosophy is that.!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…