Pendekezo: Itungwe sheria ya upimaji wa DNA kwa mtoto. Sheria iwe lazima pindi tu mtoto anapozaliwa

Pendekezo: Itungwe sheria ya upimaji wa DNA kwa mtoto. Sheria iwe lazima pindi tu mtoto anapozaliwa

Endelea kuficha hivyo hivyo ila siku ukibainika, ukipona sana ni kuivunja familia yako, yaani hayo yatakuwa ni madhara yenye haueni kwako.
Weeeh tumewaheshimisha kwa kuwapa watoto halafu bado mnatusimanga! Mara paaap DNA imekosewa, ya Khamis kapewa Juma! Msitafute matatizo nyie viumbe, leeni watoto wenu.
 
Kwa taarifa yako kwetu kwa upande wa kaka tuna watoto wawili wazungu.mapacha wakati sisi weusi tulikubali kama watoto wetu kuwa kitanda hakizai haramu

Tukasema hao watoto wanafanana na bibi mzaa bibi wa bibi wa bibi alikuwa mzungu tukataifisha .Tukawa tunakisubiri kitokee kidume koko kijitokeze kiseme hao ni watoto wake tukionyeshe cha mtema kuni.Tukasema hakuna cha DNA test wala nini ni watoto wetu wa ndani ya ndoa

Tunafurahi kwenye familia yetu tuna wazungu watoto wetu
Mmeamua kumtesa shemeji yenu kisakolojia!!
 
Unalea mtoto kwa taaabu, Halafu baada ya miaka mitano mama mtu Tena kwa kujiamini kabisa anakwambia "huyu mtoto sio wako" na hapo unakuta umejinyima kufanya mambo Kibao... Halafu kirahisi rahisi tu unakuja kuambiwa huyo mtoto hakuhusu serious?

Hivi nyie wenzangu mnafikiri kwa kutumia kiuongo gani?? Yaani hamfikiri kabisa mental damage inayoweze kumkuta mwanaume kutokana na paternity fraud? Au ndio Yuko katika nyakati ambazo mwanaume ni kama gogo tu lolote baya likimkuta ni sawa tu?
Siyo kwamba mtoto hakuhusu,mtoto anakuhusu sana hata ukitaka maji ya kunywa unaweza mtuma si umemlea mwenyewe, sema DNA inakuonesha hiyo siyo damu yako yaani huyo mtoto hajatoka kiunoni mwako! Hayo sijui ya majina ya mtoto DNA hayamuhusu,DNA yeye ana deal na damu kwa damu,tena DNA huwa hataki kabisa hata kujua majina ya wahusika,maana inaweza leta conflict of interest!!
 
Maboresho hayo ni mazuri ila sasa kile kipengere cha kwamba mwanaume au baba wa mtoto anaapishwa mahakamani ETI KWAMBA HATA KAMA MTOTO ATAJULIKANA SIO WANGU BASI NITAMUHUDUMIA MAHITAJI YAKE YOTE.
Hiki kipengele kimetubana na hata umekosekana umuhimu wa PARTENITY TEST
 
Siyo kwamba mtoto hakuhusu,mtoto anakuhusu sana hata ukitaka maji ya kunywa unaweza mtuma si umemlea mwenyewe, sema DNA inakuonesha hiyo siyo damu yako yaani huyo mtoto hajatoka kiunoni mwako! Hayo sijui ya majina ya mtoto DNA hayamuhusu,DNA yeye ana deal na damu kwa damu,tena DNA huwa hataki kabisa hata kujua majina ya wahusika,maana inaweza leta conflict of interest!!
Mantiki nzima ya hii comment yako ni nini hasa? maana nimesoma mara mbili mbili kujua ulichokusudia kulenga lakini nimetoka kapa..

Kuhusu suala la mtoto kutokukuhusu pale mama mtoto anapoamua Hilo linawezekana sana na huna la kufanya...

Yaani unaambiwa kabisa "huyu mtoto baba yake ni Fulani Wala sio wewe, na kwanzia sasa nampeleka kwa baba yake wa kumzaa sitaki aendelee kuteseka kwenye mikono yako(na hapo unakuta hujawahi hata kumtesa), na kweli anaenda wewe unabaki unalia tu hapo huku ukiigusa psychological trauma...

Endelea kujidanganya kwamba eti kwa sababu umemlea basi wewe ndio utakuwa na mamlaka naye siku zote....
 
Tunatakiwa kuwasanua madogo sasa hivi
Utakuwa tagged kama adui mkubwa wa jamii kwanzia kwa hao madogo mpaka kwa mishangazi kwamba unawaharibia vijana wao wa kiume kwa kuwafundisha "toxic masculinity"

Wewe acha tuendelee kuushudia tu jamii ikitengeneza kizazi Cha wanaume wanaokuja kuwa watumwa wa wanawake na watakaoteswa na wanawake mpaka basi...
FB_IMG_1726837582687.jpg
 
Naunga mkono hoja. Na nikikuta nimechomekewa naomba gharama zangu zote zirudi, siui mtu wala nini!
 
Ni vyema sana sana kukaa kimachale, kwa sisi tuliotendwa vibaya na ndoa, mioyo yetu ipo na status ya “auto pilot” yani hata usipodhamiria, inamwangalia mwanamke kwa Machame!
Mkuu kama ulitendwa na Mwanamke kwa kubambikiziwa mtoto, basi kaa ukijua kwa asilimia kubwa na wwe una mtoto wako wa damu sehemu kapewa mwanaume mwingine anamlea bila kujua kama wake! Ni swala la muda tu mtakutana, wwe mshukuru Mungu kwa kila jambo!!
 
Habari wakuuu..,....

Hali ilipofikia sio kuzuri.......palipofikia tena sio kwa kuoneana aibu.......watu wanalia kwa kutoa milio wengine wanalia kwa vibration na wengine wagugumia ndani ndani......

Siku hizi kitanda kinazaa haramu kwa kuwa wanandoa wameamua kuwa wana haramu......

Kwa hali ilipofikia sio tena kufumbiana macho tuambiane ukweli wa mambo.........

Hii ni dhuruma kubwa inafanyika lakini watu wanaiona ni kawaida.......


Hili pendekezo Tu......

NB;
Mzee wa miaka 62 ajitoa uhai baada ya kugundua wanae watano aliowalea sio wa kwake......imetokea huko Kenya....
kabisa mkuu tena huduma itolewe bure ili iwe haki kwa wote
 
Back
Top Bottom