Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Pendekezo: Kitengo cha Upelelezi kitolewe Polisi

Kweli inawezekana kama FBI ya USA, kuna gharama lakini kupata haki inahitaji gharama!!
Kiundwe kitengo chenye watu mahili, wenye uwezo wa kupeleleza na kushitaki bila urasimu wa DPP.
Wanatakiwa wawe wataalam, wanasheria, engrs, saicologist, madocs, watu wa nyanja mbali.
Wawe ni wataalamu wa security, kutoka vitengo vya aina hiyo, wataalamu wa IT ilikurahisisha investigation!!
Wasibanwe na MaRPC na wakubwa wengine wawe huru kupeleleza mahali popote bila vizuizi kama FBI.
Asante kwa wazo zuri, walifanyie kazi!!
 
Hebu jaribu kufikiria mathalani kesi ya Eric Kabendera, huu ni mwezi wa 6 akisota rumande kutokana na kesi "aliyobambikiwa" kukosa dhamana, mbaya zaidi kila anapokwenda mahakamani hao mapolisi, ambao pia ndiyo waendessha mashitaka, wanadai kuwa upelelezi haujakamilika...............

Haya ni mateso tu wanataka kuwapa watanzania, kwa kuwa haiwezekami kesi kukosa kukamilisha upelelezi kwa zaidi ya miezi 6!
 
Wacha jeshi lifanye kazi yake
Kwani unapungukiwa nini upelelezi kuwa polisi?

Upelelezi gani? Watu wanatekwa, wanauawa, na maovu kibao. Hakuna upelelezi zaidi ya kuwabambika watu kesi. Jeshi la polisi lijirekebishe maana watu wanazidi kukosa imani
 
Hilo niwa zuri! Kazi ya police ibaki kuzuia kupambana na kukamata waharifu.
Hii itapunguza hata lawama kwa jeshi letu la police. Harafu kila kosa liwe na limitation time ywa kupereteza. baada ya hapo km upererezi bado mtuhumiwa apewe dhamana arudi kujenga taifa wakati uchunguzi ukienderea.
 
Hii ajenda ingewekwa kwenye mdaharo wa kitaifa. Badara ya kubaki hum jf. Harafu somo hili lifundishwe vyuoni watu waaprai kusomea uchunguzi yaani... local investigation, cantry investigation, international investigation and other!
 
Kati ya uhuru ambao umepitiliza ni namna mitandao inavoriport masuala ya shughuri za police wakiwa kazini, jamani hivi vyombo vya ulinzi wanafanya kazi katika mazingira magumu saaana, nchi hisipokuwa makini tunaweza kuwa na Trespassers wengi na tujue uharifu mwingi sana unaanzaga na connections za ndani, ata majumbani kwetu kwa wale wenye walinzi 70% ya uharifu unaanziaga nyumbani kwako, either kwa kukosa umakini au kushiriki, kwa hiyo mi naamini kwa sabbu kila kitu kinaenda kisheria we must keep respect, maana panaweza kuwa na jambo kubwa la uharifu lakini tukawaintrupt vyombo vyetu vya usalama kufanikisha kazi yao.

Tukumbuke kila mmoja anakitu chake ndani mwake no matter how close you are....ila pana vyombo vya usalama ambavyo vina intelligence unit, nayasema haya kwa experience tuviamini vyombo vyetu vya usalama, na wao sio malaika, lakini hisiwe kigezo cha kuintrupt kazi zao. Tukitengeneza huu utamaduni kuna uharifu mwingine utakuwa unaskilizia kwenye mitandao, kakamatwa mtu kwa ajili ya kusaidia upelelezi sisi huku tunaanza kupiga kelele kwenye mitandao....kiukweli tunakwamisha kazi za vyombo vyetu vya usalama.

Take my words, ata katika jamii yako tu, ata katika familia ikiwa tunatengeneza culture ya kwamba kila suspects are wrong, siku moja utakosa uvumilivu utapoitiwa mtoto wako wa kumzaa rdhanded katika tukio. Tuchukue hatua Make Tanzania safe, This is our Nation.
 
Ingelikuwa vizuri tukajiuliza ni nini kilichotufanya tukaanzisha vitengo vingine kama vile Takukuru, Railway Polisi,nk. Naunga mkono kuwa Investigation iwe kitengo maalum na polisi iwe yenyewe. Majukumu yake mbona yanawatosha??
 
Itakuwa vema kuwa na hicho Kitengo ambacho kitafanya upelelezi baada ya kupata/kupewa information ambayo yaweza kutoka Police. Kitengo hakitaweza kumkamata mshukiwa wa uhalifu mpaka pale kitakapo kuwa na ushahidi usio na shaka kwa ajili ya kuwasilisha mahakamani. Kwa namna hiyo mahabusu watapungua na pia msululu wa mashauri yasiyo kwisha mahakamani utapungua pia.
 
Moja ya mambo ambayo yanaturudisha nyuma ni pamoja na hiki kitengo kinachoitwa cha upelelezi ambacho hadi sasa ni sehemu ya Jeshi la Polisi.

Na mara nyingine unakuta kuna tukio ambalo Polisi wanahusika na kitengo kinatakiwa kufanya upelelezi. Nadhani ni wakati sasa kukiondoa iwe taasisi inayojitegemea kama zilivyo taasisi kama hizi nchi nyingine.

Ina maana hata Rwanda wanatuzidi kufikiri vizuri. Rwanda mwaka 2018 wamekiondoa kitengo hicho Polisi na kuunda taasisi mpya inayo itwa RIB (Rwanda Investigation Bureau).

Nadhani Magufuli na Baraza lake wanaweza, jambo hili litakuwa muarobaini wa kesi nyingi ambazo zinawatesa wananchi kwa kusubiria upelelezi.

Tanzania Bureau of Investigation.
Watenda kazi walewale labda kama unataka kubadiri jina na jengo. Labda Hoja ya msingi ungesema labda sheria flani na flani ibadrishwe ili kuboresha utendaji wake. Sasa sijui ndugu yangu nini kilifanyika hiyo nchi kiasi kwamba ikatuzidi akili.
 
Kuna matukio kadhaa ambayo polisi wamehusika na wamechunguzwa na CID na wakapatikana na makosa na kufikishwa mahakamani.

Huwezi kuwaondoa CID ndani ya jeshi la polisi ni kama vile MP ambao wapo kwenye jeshi.

Hizi ni idara zinazojitegemea ndani ya majeshi hayo yaani law enforcement agenciea na wana wajibu wa kuwachunguza askari polisi na raia (kwa CID) na wanajeshi kwa MP kunapotokea tatizo lolote likiwemo la la kinidhamu kwa wanajeshi.

Kwa jeshi la polisi hakuna haja ya kuwaondoa kwani tayari wao (CID) wanavaa kiraia.

Au labda kuna sababu ingine unayoona kuna ulazima wa kuwatenga kabisa au unamaanisha wawe independent yaani hawawajibiki kwa IGP isipokuwa waziri wa mambo ya ndani?

Fafanua kidogo.
 
Yaani bora hata ungeitaja nchi nyingine hapo tofauti na Rwanda Mkuu kwani hakuna nchi ambayo inachukiwa na Watanzania kama ya Rwanda japo ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania ina mengi ya Kujifunza kwa Rwanda hata kuliko Rwanda ambavyo inaweza Kujifunza kwa Tanzania. Na Kitu kikubwa ambacho Watanzania wanaweza Kujifunza kutoka kwa Taifa la Rwanda na hasa Wanyarwanda ni namna gani ya Kutumia ' Akili ' vizuri katika Kujieletea Maendeleo. Binadamu wote tuna Akili ila Akili za Wanyarwanda zinatumika mahala sahihi na kwa wakati sahihi na pia kwa malengo yaliyo sahihi kabisa. Chuki ya Watanzania kwa Wanyarwanda na Taifa lao la Rwanda wangeigeuza iwe ni Upendo na Imani Kwao basi leo wangekuwa mbali mno na Wanyarwanda siyo Wachoyo wa Kukupa ' Maarifa ' kama wakijua au ukijijua Wewe ni ' Popoma Mwandamizi ' kabisa. Ukiichukia Rwanda na Wanyarwanda ni lazima tu utakuwa na matatizo makubwa ya ' Akili ' na pengine unahitaji Tiba ya haraka Mirembe.

Long live Rwanda!
rwanda ni nchi maskini sana kwa bottom ikitoka burundi inafuata rwanda hapa east africa, pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka bado ni dogo sana ukilinganisha na wa TZ, watumie akili zao kwanza kuondoa umaskini
 
Moja ya mambo ambayo yanaturudisha nyuma ni pamoja na hiki kitengo kinachoitwa cha upelelezi ambacho hadi sasa ni sehemu ya Jeshi la Polisi.

Na mara nyingine unakuta kuna tukio ambalo Polisi wanahusika na kitengo kinatakiwa kufanya upelelezi. Nadhani ni wakati sasa kukiondoa iwe taasisi inayojitegemea kama zilivyo taasisi kama hizi nchi nyingine.

Ina maana hata Rwanda wanatuzidi kufikiri vizuri. Rwanda mwaka 2018 wamekiondoa kitengo hicho Polisi na kuunda taasisi mpya inayo itwa RIB (Rwanda Investigation Bureau).

Nadhani Magufuli na Baraza lake wanaweza, jambo hili litakuwa muarobaini wa kesi nyingi ambazo zinawatesa wananchi kwa kusubiria upelelezi.

Tanzania Bureau of Investigation.

Soma pia: Jaji Mkuu achukizwa na wapelelezi wanaokamata mtuhumiwa kabla ya kukamilisha upelelezi
Hapo umenena kwani kama kipo polis na sometimes polisi wanahusika na matukio afu hao hai wanapewa kazi ya kujipeleleza hahaha uhalifu utaendelea kama kikiendelea kuwekwa kwenye jeshi la polisi Bora kitolewe na iwe taasisi ya kujitegemea
 
Hii kitu ni very Logical mkuu, big up sana.
Wakuu Malcom Lumumba Chige Mzee Mwanakijiji JokaKuu My Son drink water hebu pitieni uzi huu
Kwa maoni yangu, suala sio kukiondoa kitengo kutoka Jeshi la Polisi, bali kutenganisha nini kiwe chini ya Jeshi la Polisi na nini kisiwe chini ya Jeshi la Polisi!

Tuchukulie Marekani kwa mfano! Pamoja na Law Enforcement Agencies zingine (za ndani) lakini maarufu zaidi ni FBI n Local Police, kama vile NYPD, LAPD and the like!

Kuwepo kwa Federal Bureau of Investigation (FBI) hakujafanya Local Police wasiwe na Investigation na hata Intelligence Units.

Tatizo la Kitengo cha Upelelezi Jeshi la Polisi ni kukusanya mambo yote na kuyaweka kwenye kapu moja na matokeo yake, inatokea kukosekana kwa competency!

Unashangaa tu from nowhere, Askari aliyekuwa kituo fulani, anahamishiwa Investigation!!

Sijui ndo vile Nabii hakubaliki kwao, lakini nilicheka sana siku Mama angu anarudi home na kusema amehamishiwa Central, Kitengo cha Upelelezi!!

Sikuwahi kumuona ratiba zake zikibadilika ili hatimae nifahamu kwamba Mama yangu hatimae ameenda kuchukua mafunzo maalumu ya upepelezi! Miaka kadhaa baadae, mara nasikia yupo upande wa Prosecution... ikawa Kisutu na yeye, yeye na Kisutu!!

Inawezekana kabisa kwamba sijui lolote kuhusu mambo ya ukachero ndo maana nilikuwa nashangaa ule Ukachero wa mama yangu mzazi!!

Maana yangu ni kwamba, Kitengo cha Upelelezi kinaweza kuendelea kuwepo pale Jeshi la Polisi, lakini wajikite kwenye mambo ya kipolisi zaidi, na mambo mengine mazito ndiyo yanaweza kutengenezewa kitengo kinachojitegemea kama ilivyo kwa RBI.

Lakini hiyo peke yake haitoshi! Kama hakuna complete autonomous, bado wala haitasaidia! Na sio tu kuwa na complete autonomous bali kuwa na complete autonomous away from the political sphere!

Hilo la kushindwa kuwa na a complete autonomous from political sphere ndio chanzo cha kushindwa ku-deliver kwa taasisi zetu nyingi.

Lingine ambalo ni muhimu sana ni watu kuwa na weledi! Hili lisipokuwepo, basi hata ukianzisha taasisi inayojitegemea haitasaidia kwa sababu wakati hivi sasa polisi wenyewe kwa wenyewe wanafichiana maovu, na hao wengine watakuwa wanafichiana vile vile!

But on top of that, ni kufahamu kwamba wapo hapo ili kutenda haki! Hilo lisipokuwepo, basi hicho kinaweza kugeuka ni kitengo kingine cha kushughulikia wakosoaji!!

Yote hayo yamekosekana kwenye kitengo cha upelelezi cha sasa ndo maana tunaona mambo yapo hovyo hovyo! Hapo hapo walipo wakiamua kufanya hayo, basi kitengo hicho hicho cha sasa kinaweza ku-deliver!!
 
Wakianzisha hiyo agency kuna sheria zitatungwa kuanzisha hiyo taasisi nazani mapungufu yote yataelezwa
Watenda kazi walewale labda kama unataka kubadiri jina na jengo. Labda Hoja ya msingi ungesema labda sheria flani na flani ibadrishwe ili kuboresha utendaji wake. Sasa sijui ndugu yangu nini kilifanyika hiyo nchi kiasi kwamba ikatuzidi akili.

Sent from my HTC Desire 626GPLUS dual sim using JamiiForums mobile app
 
kama wasi wasi ni polisi kuhusika na uhalifu kisha wajipeleleze,basi una sababu ya msingi sana,lakini kwasababu hii sio taaluma yako,ngoja tukukumbushe kwamba wanaokamata mharifu ndio polisi hao hao,ni rahisi zaidi kuvuruga ushahidi kama mhusika ni mwenzao.

kwahiyo hapa ni kama umeyafunika mavi na taulo,si kwamba umeyaondoa kabisa.

labda sasa useme na shughuli ya kukamata wapewe hao hao wapelelezi.yaani unaripoti polisi,polisi wanatoa taarifa kwa wapelelezi mliowaamini ndio wakakamate na kisha kupeleleza.

ukiona kitu cha hovyo sehemu,na hakuna anayejishughulisha nacho,1~kina ufanisi zaidi katika ubovu wake huo,2~si kweli kwamba ni kibovu,3~kina kazi nyingine tofauti na unayoijua.
 
Back
Top Bottom