Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Nakuelewa🙏
 
MAKONDA hakufuta kauli yake..kwamba BUNGENI WANAJADILI UMBEA TU/HAKUNA LOLOTE LA MSINGI WANALOFANYA. KUNA GENGE LA WAHUNI NA WACHUMIA TUMBO TU kwa sauti ya H.Polepole. Nadhani umeongea point sana ila watakuja mbu mbu mbu fulani wabinafsi kupuuzia hoja muhimu hizi
 
Sasa huyo kijana mbona alijaribu kugombea ubunge huo huo?

Muhimu ni waingie wabunge Mahiri.

Waingie wabunge Wachache chini ya 100 Nchi nzima,

Viti maalum vifutwe.

Posho na mishahara iwe chini ya 5ml, anayeona ndogo asigombee ubunge.
 
Misri ni Afrika pia.

Afrika imebarikiwa Kwa Kila kitu, ni kama tu mtoto wa tajiri, ni Wachache Huwa na akili ya utafutaji, sababu Wana Kila kitu.
Africa inaponzwa na ubinafsi na choyo ,,
Hivi vitu 2 tukiweza kuvishinda basi Africa itakuwa mbali sn..

Viongozi wetu tuliowaamini na kuwapa mamlaka 90% sio waaminifu na wengi wana sifa hizo nilizozitaja..
--ubinafsi
--choyo.

Mtu mmoja ana mahela chumba kizima na bado anaendelea kuiba pesa za umma,, kwa maslahi yake binafsi .
Pesa zote za kazi gani?
Wakati wengine wanakufa njaa?
Mashule hayana walimu,,
hospital hakuna dawa,,
gharama za maisha zinapanda nk.
Hivi wanaona faraja gani kujilimbikizia mapesa ya umma kwa maslahi binafsi na family zao?.
Kila kukicha wanatengeneza drama mpya mradi tu waweze kukwapua mali za umma na kodi zetu wananchi.

Kweli Trump alikuwa sahihi,, AFRICA A SHIT HOLE.
 
Trump na wenzie ndio wanaoiba madini ya Africa Kwa kuhonga viongozi wetu.

Akae kimya.
 
Trump na wenzie ndio wanaoiba madini ya Africa Kwa kuhonga viongozi wetu.

Akae kimya.
viongozi wetu Africa kukubali kuhongwa na kuiuza Africa,

inadhihirisha ukweli wa maneno ya Trump.
Kwani hata baadhi ya machifu wa kiafrika waliwauza babu zetu kwa wazungu wakati ule wa utumwa.
.kwahyo kauli ya Trump sio ya kuikejeli..

Africa a shit hole.
 

26 March 2024
Mvomero, Morogoro
Tanzania

DAS / Katibu Tawala - Mtumishi Wa Umma Huwezi Kuwa Bilionea Kwa Ajira Ya Umma, Labda Uwe Mwizi, kibaka na jambazi wa mali za umma


View: https://m.youtube.com/watch?v=-6VNHQvMgTM
Katibu tawala DAS alikuwa akizungumza na kada mbalimbali za watumishi wa umma kama waalimu, wauguzi n.k na kusisitiza kwa mshahara huu wa mtumishi wa umma utaishia kusomesha watoto, kula na kujenga nyumba.

Ila huwezi kuwa bilionea na kama mtumishi unataka kuwa bilionea acha kazi yako ya umma na kwenda kuwa mfanyabiashara huko ndipo utajiri halali ulipo na utatimiza matamanio ya kuwa bilionea ....

DAS Katibu tawala mzalendo wa wilaya ya Mvomero Morogoro ndugu Saidi Nguya akawasifia waalimu kuwa hawazeeki maana ajiri yao ktk utumishi wa umma hawana nafasi ya kuiba kiasi kuwa miaka mingi baadaye wanaonekana hawajazeeka kama wale wanafunzi waliopitia mikononi mwao, ila angali wale wezi wanazeeka kwa mioyo yao kusongwa na hatia ya kuiba mali za umma....

ndugu Saidi Nguya anasema ukiona mtumishi wa umma ni tajiri basi ni mwizi na jambazi mkubwa wa kupora mali za umma ....
 
Sasa huyo kijana mbona alijaribu kugombea ubunge huo huo?

Muhimu ni waingie wabunge Mahiri.

Waingie wabunge Wachache chini ya 100 Nchi nzima,

Viti maalum vifutwe.

Posho na mishahara iwe chini ya 5ml, anayeona ndogo asigombee ubunge.
sahihi kabisa, kwasasa ubunge umekuwa ni sehemu ya kuchukulia pesa za bure kazi hakuna
 
PAMOJA SANA!
... wakilipwa viwango vinavyoendana na vipato halisi vya wapiga kura watajikita zaidi Katika kuikwamua nchi na umasikini na kudhibiti mfumko wa bei!
 
Hongera sana madiwani Mkoa wa Mara kupendekeza mshahara wa mbunge ipungue Ili nao wapate posho za vikao.
 
Mbunge unamlipa milioni 5 yote kwa kazi gani kubwa anayofanya?

Milioni 2 tu ilitosha.
 
Dola elf 2,000 kwa mwezi sawa na dola 12,000 kwa mwaka. Arifu bora ilipwe hiyo 18m officially.

Ukiwalipa 5m watakuibia hadi mkeo!!
 
Kwa hayo mawazo yako unadhani watumishi wa TRA wangelipwa kama walimu je hali ingekuwaje?? Unajua majukumu ya wabunge lkn? Usifikiri ni kukaa tu pale bungeni na sikiliza zile hotuba, wanazo kazi nyingi tu nje bunge, utasikia kamati ya LAKI, PAC nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…