Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Kwa hayo mawazo yako unadhani watumishi wa TRA wangelipwa kama walimu je hali ingekuwaje?? Unajua majukumu ya wabunge lkn? Usifikiri ni kukaa tu pale bungeni na sikiliza zile hotuba, wanazo kazi nyingi tu nje bunge, utasikia kamati ya LAKI, PAC nk.
KAZI ya mbunge haifikii Ile ya mkulima kuamka saa 9 usiku na kushika jembe la mkono akalima Hadi sasa 11 jioni.

Mshahara wa mbunge usizidi 5ml. Hata pungufu ya hapo, ni sawa.
 
Salaam, Shalom!!

Niliwahi kuandika thread isemayo, Wabunge wafanyabiashara matajiri wanasimamia Maslahi ya nani bungeni?

Haijaisha miezi SITA tangu kuandikwa thread hiyo, tayari Kuna tetesi kuwa Wabunge wamejiongezea posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 15 Kwa mwezi.

Mbunge anayeona posho na marupurupu ya ml 13 kuwa haitoshi, huyo hawezi kamwe kutosheka. Na watu Hawa, lazima ni matajiri wakubwa walioacha biashara zao na kwenda bungeni wakidhani bungeni Pana maslah binafsi ya kiuchumi.

KAZI ya ubunge ni KAZI ya season, Si ajira ya kudumu, lazima uwe na KAZI Yako ,bungeni unaenda kutetea Maslahi ya wananchi, wabunge wanaodhani kuwa ubunge ni ajira ndio wanatuletea shida.

Pale Uingereza, mbunge anapanda treni ya umma kwenda bungeni, gari yake binafsi anatumia akiwa jimboni kwake na umma hawajibiki kumlipia mambo lukuki kama huku.

Mshahara na marupurupu usizidi ml 5 Kwa mwezi, na mbunge lazima awe na KAZI yake, bungeni pasifanywe ajira.

Wabunge wapande mabasi kama raia wengine waendapo Dodoma, Kodi zetu zisitumike kulipa mshahara wa dereva, mbunge akitaka gari, akopeshwe na alipe Yeye mwenyewe na ajigharamie gharama za mafuta.

Tunachagua wabunge Ili wasaidie wananchi tupate bima walau za watoto chini ya miaka mitano iliyofutwa Ili kujazia pesa za kulipa wabunge ml 18 Kwa mwezi na kulipa wake wa wastaafu.

Wabunge oneni Aibu na muwe na huruma Kwa wananchi.

FAIDA ZA KULIPA MISHAHARA YA WABUNGE CHINI YA ML 5 KWA MWEZI.

1. Itasaidia wabunge wazalendo kuingia bungeni.

2. Itapunguza wizi wa kura.

3. Itasaidia kujipunguzia Serikali Mzigo kuhudumia wabunge, Badala yake, pesa hizo zitasaidia kulipa posho walimu mashuleni Ili wafundishe Kwa Ari na morali zaidi.

Hivi wabunge jiulizeni, bodaboda, matching guys ,wakulima, wavuvi ambao Kwa mwezi hawapati hata laki 5 Kwa mwezi, wamepata wapi uwezo kuwalipeni wabunge 399 , milioni 18 Kwa mwezi=7 bilion?

Mkiendelea na uroho huo, tutasusia mikutano yenu na hatutowapigia kura!!

KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa, wabunge wamedhihirisha wazi kuwa hawaangalii maslah ya Wananchi maskini, wanajiangalia wao na familia zao.

Pia wabunge wazuiwe kujiongezea mshahara bila kupata ridhaa ya walipakodi.

Karibuni 🙏
Mkuu, tatizo hapo ni kwamba; wabunge wenye neno ni wengi, wakiwemo Mawaziri, ambao wana sauti na ushawishi mkubwa Bungeni, hivyo kupelekea wabunge kuwa na maslahi makubwa kuzidi wenye taaluma muhimu mara 10 zaidi yao na hivyo kupelekea wenye taalumu muhimu nao kuingia kwenye siasa. Ukiangalia kwa jicho la tatu, utaona Serikali inatoa hongo kwa Mbunge kwa kuwapa maslahi mazuri ili nayo isibuguziwe na matumizi yake. Matokeo yake ndio hayo
 
Umeogea jambo zuri kabisa ila sijui unamwambia nani? Maana chama tawala ndo kimeamua iwe hivyo
Dawa ni kuandamana kwa Amani mbona wataeleweka tu? hii si sawa hata kidogo binafsi naamini ni swala la muda tu wananchi watapaza Sauti
 
Bando milioni 5 ni nyingi sn, isizidi milioni 2 tupate watu wa kweli wanaotaka kujitolea kutumikia wananchi na siyo hawa wala rushwa
 
Kama ml 5 ni kubwa, ml 18 ni kubwa kiasi Gani?

Na wananchi tukihoji, wanatwambia kuwa wanafanya hayo Kwa ridhaa yetu.

Unajiuliza, lini Mimi mkulima ambaye ninaweza kulima shamba nikatumia gharama, mvua isinyeshe nikapata HASARA, lini nimeridhia mbunge alipwe ml 18 Kwa mwezi Kutoka Kodi nilipayo?
Mishahara inatakiwa ipungue haswa
 
Kwa sasa kitita cha fedha kwa mbunge :

Mshahara wa mbunge ni zaidi ya bilioni moja akitumika miaka 5 (miezi 12 x 5 ) ktk kikokotoo:


Mchanganuo wa mshahara wa miaka mitano wa mbunge ni Bilioni 1 na milioni themanini :

Shilingi 18,000,000 x miezi 12 = 216,000,000

Shilingi 216,000,000 × miaka 5 =1,080,000,000

  • Bado hapo pia anapokea allowance za vikao vya bajeti
  • Ziara za mafunzo Dubai, India n.k
  • Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge PAC, LAAC, Mambo ya Nje na ulinzi usalama n.k
  • Marupurupu ya mkopo wa gari n.k
  • Bima ya Afya kwa mbunge hospitali VIP Class n.k
  • Pensheni ya mkupuo akimaliza ubunge miaka
Bando rushwa, mkopo bilioni 1 analipa milioni 500 pekee
 
Sasa matajiri shida, masikini shida, solution ni nini?

Nadhani bado mleta mada ana hoja nzuri tu. Maana mwisho wa siku, mbunge anagombea kwa kupitia chama cha siasa ambacho kina sera zake nk.

Huu uozo unaanzia kwenye chama. Wanapotaka kupitisha miswada yao hovyo na kifisadi, haijalishi mbunge ni mtu wa aina gani. Hata akiwa bubu bado anafaa kabisa.

Mwisho wa siku wananchi ndiyo waamuzi wenye kutakiwa kuwawajibisha.
Tukiamua tunaweza, haya majangili yanalipwa pesa nyingi haswa
 
Ndo maana nakubaliana na mleta mada. Pale kwenye point yake #1 anasema mishahara ikiwa 5m au less, itatupatia wabunge wazalendo.

Kwa kiasi kikubwa yuko sahihi, kwasababu kabla hata hawajajiongezea mishahara, tayari walikuwa wanalipwa pesa nyingi. Kwa tajiri mkubwa, hawezi kupoteza muda wake kwa ajili ya milioni 5 kwa mwezi.

Kwasababu huwa wanatumia pesa nyingi kuweza kuchaguliwa, na kwahiyo ni kama biashara hapo wanawekeza kwenye ubunge.

Kwa muda atakaokuwa bungeni akitoka ana zaidi bilioni. Na hapo labda ametumia milioni 100 kuupata ubunge.
Mshahara ukiwa 1.5M tutapata wawakilishi wa kweli, kwanza kwa nchi masikini kama hii hata Rais wa nchi mshahara wake hautakiwi kuzidi milioni 3
 
Hawa matajiri kwanini hawajitolei?

Mbunge tajiri, Abuud au kishimba, bungeni anachukua posho au mshahara wa KAZI Gani?

Wabunge matajiri wanatakiwa wajitolee, wakatae posho na mishahara, watumie pesa zao kulipa madreva wao, wajigharamie mafuta nk nk.

Ikiwa hakuna tajiri hata mmoja mbunge bungeni aliyekataa posho na mshahara,

Jua kuwa hakuna tajiri hapo, wote mafisi tu!!

Utajiri wao Si wa HAKI!!

Utajiri wao ungekuwa wa HAKI, wangeridhika.
Ubunge ni eneo la kwenda kutajirikia na siyo sehemu ya kutumikia wananchi
 
Hilo halikwepeki,

Ikiwa kura zinaibwa wazi wazi bila kificho,

Inamaana IPO siku, drug dealer au muuza bangi anaweza kuwa kiongozi mkubwa wa Nchi Kwa kununua kura Kwa pesa chafu Ili akajilipe bungeni au wizarani.

Ikiwa tumeshindwa kufuata HAKI kuongoza nchi,

Ifike time wananchi tuchukue hatamu!!
Nakubaliana na wewe tuamke
 
Mkuu naomba nikuongezee hili "kwasasa mbunge anakunja 18M kwa mwezi badala ya 13M"
 
KAZI ya mbunge haifikii Ile ya mkulima kuamka saa 9 usiku na kushika jembe la mkono akalima Hadi sasa 11 jioni.

Mshahara wa mbunge usizidi 5ml. Hata pungufu ya hapo, ni sawa.
2M inamtosha maama vitu vingi anapata bure.
 
Back
Top Bottom