Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Upo Sawa kabisa. Ila nani atamfunga huyu paka kengere? Chakula chake anapanga yeye mwenyewe na pia ndiye anayetupangia tule nini, tulipe nini, tufanye nini, tusifanye nini n.k. Yeye kashika mpini wa upanga.
 
Still ume propose pumba ili bidi na wao wairate kama mishahara mingine
 
Ifike wakati tufutilie mbali viti maalum, sijui wabunge wa kuteuliwa. Ili tubane matumizi tujifunge mkanda.
Wabunge walipwe kama wafanyakazi wengine wa serikali hapi tutajua wabunge wa dhamiri ya kweli au wabunge matumbo yao na.masaburi.

Wanakula pesa nyingi sana ya jamhuri bila kazi ya maana huu ni unyonyaji hawalipi kodi hawana elimu wengine ni mahoyahoya tuu .
 
Salaam, Shalom!!

Niliwahi kuandika thread isemayo, Wabunge wafanyabiashara matajiri wanasimamia Maslahi ya nani bungeni?

Haijaisha miezi SITA tangu kuandikwa thread hiyo, tayari Kuna tetesi kuwa Wabunge wamejiongezea posho na marupurupu Yao Kutoka ml 13 Hadi ml 15 Kwa mwezi.

Mbunge anayeona posho na marupurupu ya ml 13 kuwa haitoshi, huyo hawezi kamwe kutosheka. Na watu Hawa, lazima ni matajiri wakubwa walioacha biashara zao na kwenda bungeni wakidhani bungeni Pana maslah binafsi ya kiuchumi.

KAZI ya ubunge ni KAZI ya season, Si ajira ya kudumu, lazima uwe na KAZI Yako ,bungeni unaenda kutetea Maslahi ya wananchi, wabunge wanaodhani kuwa ubunge ni ajira ndio wanatuletea shida.

Pale Uingereza, mbunge anapanda treni ya umma kwenda bungeni, gari yake binafsi anatumia akiwa jimboni kwake na umma hawajibiki kumlipia mambo lukuki kama huku.

Mshahara na marupurupu usizidi ml 5 Kwa mwezi, na mbunge lazima awe na KAZI yake, bungeni pasifanywe ajira.

Wabunge wapande mabasi kama raia wengine waendapo Dodoma, Kodi zetu zisitumike kulipa mshahara wa dereva, mbunge akitaka gari, akopeshwe na alipe Yeye mwenyewe na ajigharamie gharama za mafuta.

Tunachagua wabunge Ili wasaidie wananchi tupate bima walau za watoto chini ya miaka mitano iliyofutwa Ili kujazia pesa za kulipa wabunge ml 18 Kwa mwezi na kulipa wake wa wastaafu.

Wabunge oneni Aibu na muwe na huruma Kwa wananchi.

FAIDA ZA KULIPA MISHAHARA YA WABUNGE CHINI YA ML 5 KWA MWEZI.

1. Itasaidia wabunge wazalendo kuingia bungeni.

2. Itapunguza wizi wa kura.

3. Itasaidia kujipunguzia Serikali Mzigo kuhudumia wabunge, Badala yake, pesa hizo zitasaidia kulipa posho walimu mashuleni Ili wafundishe Kwa Ari na morali zaidi.

Hivi wabunge jiulizeni, bodaboda, matching guys ,wakulima, wavuvi ambao Kwa mwezi hawapati hata laki 5 Kwa mwezi, wamepata wapi uwezo kuwalipeni wabunge 399 , milioni 18 Kwa mwezi=7 bilion?

Mkiendelea na uroho huo, tutasusia mikutano yenu na hatutowapigia kura!!

KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa, wabunge wamedhihirisha wazi kuwa hawaangalii maslah ya Wananchi maskini, wanajiangalia wao na familia zao.

Pia wabunge wazuiwe kujiongezea mshahara bila kupata ridhaa ya walipakodi.

Karibuni 🙏
Acha kuchekesha.
Uliona wapi mtu akajipunguzia mshahara?

Ili uweze kupunguza hio mishahara lazima tuwe na katiba mpya ambayo itakuwa na heshima na usawa kwa waalimu mpaka wabunge. Ila kwa katiba hii kuongelea mishahara ya wanasiasa ni kujaza tu server ya Max Melo
 
Acha kuchekesha.
Uliona wapi mtu akajipunguzia mshahara?

Ili uweze kupunguza hio mishahara lazima tuwe na katiba mpya ambayo itakuwa na heshima na usawa kwa waalimu mpaka wabunge. Ila kwa katiba hii kuongelea mishahara ya wanasiasa ni kujaza tu server ya Max Melo
Sasa Katiba mpya itaandikwa bila mapendekezo na maboresho Toka Kwa wananchi?
 
26 March 2024
Mvomero, Morogoro
Tanzania

DAS / Katibu Tawala - Mtumishi Wa Umma Huwezi Kuwa Bilionea Kwa Ajira Ya Umma, Labda Uwe Mwizi, kibaka na jambazi wa mali za umma


View: https://m.youtube.com/watch?v=-6VNHQvMgTM

Katibu tawala DAS alikuwa akizungumza na kada mbalimbali za watumishi wa umma kama waalimu, wauguzi n.k na kusisitiza kwa mshahara huu wa mtumishi wa umma utaishia kusomesha watoto, kula na kujenga nyumba.

Ila huwezi kuwa bilionea na kama mtumishi unataka kuwa bilionea acha kazi yako ya umma na kwenda kuwa mfanyabiashara huko ndipo utajiri halali ulipo na utatimiza matamanio ya kuwa bilionea ....

DAS Katibu tawala mzalendo wa wilaya ya Mvomero Morogoro ndugu Saidi Nguya akawasifia waalimu kuwa hawazeeki maana ajiri yao ktk utumishi wa umma hawana nafasi ya kuiba kiasi kuwa miaka mingi baadaye wanaonekana hawajazeeka kama wale wanafunzi waliopitia mikononi mwao, ila angali wale wezi wanazeeka kwa mioyo yao kusongwa na hatia ya kuiba mali za umma....

ndugu Saidi Nguya anasema ukiona mtumishi wa umma ni tajiri basi ni mwizi na jambazi mkubwa wa kupora mali za umma ....

Mshahara wa katibu tawala sh ngapi?
 
Back
Top Bottom