Pendekezo: Posho na mshahara wa mbunge, usizidi milioni 5 Kwa mwezi

Kwa hayo mawazo yako unadhani watumishi wa TRA wangelipwa kama walimu je hali ingekuwaje?? Unajua majukumu ya wabunge lkn? Usifikiri ni kukaa tu pale bungeni na sikiliza zile hotuba, wanazo kazi nyingi tu nje bunge, utasikia kamati ya LAKI, PAC nk.
KAZI ya mbunge haifikii Ile ya mkulima kuamka saa 9 usiku na kushika jembe la mkono akalima Hadi sasa 11 jioni.

Mshahara wa mbunge usizidi 5ml. Hata pungufu ya hapo, ni sawa.
 
Mkuu, tatizo hapo ni kwamba; wabunge wenye neno ni wengi, wakiwemo Mawaziri, ambao wana sauti na ushawishi mkubwa Bungeni, hivyo kupelekea wabunge kuwa na maslahi makubwa kuzidi wenye taaluma muhimu mara 10 zaidi yao na hivyo kupelekea wenye taalumu muhimu nao kuingia kwenye siasa. Ukiangalia kwa jicho la tatu, utaona Serikali inatoa hongo kwa Mbunge kwa kuwapa maslahi mazuri ili nayo isibuguziwe na matumizi yake. Matokeo yake ndio hayo
 
Umeogea jambo zuri kabisa ila sijui unamwambia nani? Maana chama tawala ndo kimeamua iwe hivyo
Dawa ni kuandamana kwa Amani mbona wataeleweka tu? hii si sawa hata kidogo binafsi naamini ni swala la muda tu wananchi watapaza Sauti
 
Bando milioni 5 ni nyingi sn, isizidi milioni 2 tupate watu wa kweli wanaotaka kujitolea kutumikia wananchi na siyo hawa wala rushwa
 
Mishahara inatakiwa ipungue haswa
 
Bando rushwa, mkopo bilioni 1 analipa milioni 500 pekee
 
Tukiamua tunaweza, haya majangili yanalipwa pesa nyingi haswa
 
Mshahara ukiwa 1.5M tutapata wawakilishi wa kweli, kwanza kwa nchi masikini kama hii hata Rais wa nchi mshahara wake hautakiwi kuzidi milioni 3
 
Ubunge ni eneo la kwenda kutajirikia na siyo sehemu ya kutumikia wananchi
 
Nakubaliana na wewe tuamke
 
Mkuu naomba nikuongezee hili "kwasasa mbunge anakunja 18M kwa mwezi badala ya 13M"
 
KAZI ya mbunge haifikii Ile ya mkulima kuamka saa 9 usiku na kushika jembe la mkono akalima Hadi sasa 11 jioni.

Mshahara wa mbunge usizidi 5ml. Hata pungufu ya hapo, ni sawa.
2M inamtosha maama vitu vingi anapata bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…