PENDEKEZO: Rais Samia atangaze rasmi tarehe 17 Machi iwe Sikukuu ya kitaifa kumuenzi Hayati Magufuli

PENDEKEZO: Rais Samia atangaze rasmi tarehe 17 Machi iwe Sikukuu ya kitaifa kumuenzi Hayati Magufuli

Tunapoelekea katika hio siku muhimu ya kuenzi kifo cha JPM, ni vyema huu mwaka Mh SSH akaitangaza rasmi hio siku kuwa sikukuu ya kitaifa, ili kuenzi mema na makubwa kabisa aliyo yafanya Hayati Dr. Magufuli.

17 march: Magufuli Day

Kwenu wakereketwa...View attachment 2526364View attachment 2526379
Kumbukumbu za viongozi wote wa kitaifa walioaga dunia zingewekwa katika siku moja tu, yaani wote wakumbukwe katika Sikukuu ya Mashujaa. Hakuna haja ya kuwa na utitiri wa sikukuu nyingi katika nchi maskini kama yetu.
 
Pokea ushauri huu wenye AKILI.

Waasisi wote nchini waliotangulia mbele za HAKI wanatakiwa kukumbukwa Kwa siku walizozaliwa na Si siku walizofariki.

Hii italeta BARAKA Kwa Nchi.

1. JK Nyerere akumbukwe Kwa siku ya Kuzaliwa kwake.

2. Benjamin Mkapa akumbukwe Kwa siku ya Kuzaliwa kwake.

3. Viongozi wote waliofia madarakani kama KARUME na MAGUFULI yahitaji mjadala wa kitaifa juu ya namna Gani ya kuwakumbuka.

Amen.
Kwani Rais kufa akiwa madarakani ni umaarufu?
 
Naunga mkono hoja,ila iwe siku moja tu kuwaenzi viongozi wote,Nyerere,Karume,Sokoine,Mkapa,Magufuli na wengineo
 
Naunga mkono hoja,lkn isiwe siku ya mapumziko,iwe siku ya kufanya kazi sana,na ikiwezekana iwe siku ya kujitolea,
 
Tunapoelekea katika hio siku muhimu ya kuenzi kifo cha JPM, ni vyema huu mwaka Mh SSH akaitangaza rasmi hio siku kuwa sikukuu ya kitaifa, ili kuenzi mema na makubwa kabisa aliyo yafanya Hayati Dr. Magufuli.
Hili ombi lielekeze kwa Mstaafu asiyestaafu
 
Naunga mkono hoja,ila iwe siku moja tu kuwaenzi viongozi wote,Nyerere,Karume,Sokoine,Mkapa,Magufuli na wengineo
 
Kwani Rais kufa akiwa madarakani ni umaarufu?
Kiongozi kufia madarakani Si umaarufu,

Ni suala la kulichukua Kwa uzito wake maana laeza fungua mlango mbaya juu ya nchi.
 
Tukiruhusu kila Rais anayekufa iwe siku ya mapumziko, siku moja tutajikuta Rais anakufa kizembe ili wapate kupumzika bure.
 
Back
Top Bottom