PENDEKEZO: Rais Samia atangaze rasmi tarehe 17 Machi iwe Sikukuu ya kitaifa kumuenzi Hayati Magufuli

PENDEKEZO: Rais Samia atangaze rasmi tarehe 17 Machi iwe Sikukuu ya kitaifa kumuenzi Hayati Magufuli

Sijui ni kwa nini waimba mapambio wengi wa marehemu, hawana akili.

Hata kama kweli angekuwa amefanya mambo makubwa ya maana (mpaka sasa hakuna cha pekee kizuri kikubwa alichofanya ambacho watangulizi wake hawakufanya, ila yapo mabaya mengi ambayo alifanya ambayo watangulizi wake hawakufanya na watakaofuata hawatayafanya), mtu hajiulizi baada miaka 100 au 200 mbele itakuwaje kama kila Rais siku yake ya kufariki itakuwa ni mapumziko. Mkiwa na marais 50 waliofariki, maana yake muwe na siku 50 za mapumziko (ongeza na siku nyingine za mapumziko ambazo zipo), si litakuwa Taifa la wendawazimu?

Hiyo heshima amepewa Mwalimu Nyerere na Karume basi. Hakuna Rais mjinga atakayetangaza siku nyingine ya mapumziko eti kumuenzi marehemu. Watakumbukwa siku zao za kufariki kama ilivyokuwa birthdays zao walipokuwa hai.

Wewe huzuiwi, kutegemeana na mazuri aliyokutendea kama mtu binafsi, unaweza hata mwezi mzima March, kila mwaka ukaufanya uwe mwezi wa mapumziko.

Bora umesema kweli, wasipoelewa hawataelewa kamwe.
 
Tunapoelekea katika hio siku muhimu ya kuenzi kifo cha JPM, ni vyema huu mwaka Mh SSH akaitangaza rasmi hio siku kuwa sikukuu ya kitaifa, ili kuenzi mema na makubwa kabisa aliyo yafanya Hayati Dr. Magufuli.

17 march: Magufuli Day

Kwenu wakereketwa...View attachment 2526364View attachment 2526379
Wewe, mkeo, watoto wako na mabata na kuku uwafugao siku hiyo mkusanyike ukumbini mwenu mle, mnywe na msaze, tayari litakuwa bonge moja la sherehe na litaleta gumzo nadhani mwendazake atakusikia na kukubariki.
 
Tunapoelekea katika hio siku muhimu ya kuenzi kifo cha JPM, ni vyema huu mwaka Mh SSH akaitangaza rasmi hio siku kuwa sikukuu ya kitaifa, ili kuenzi mema na makubwa kabisa aliyo yafanya Hayati Dr. Magufuli.

17 march: Magufuli Day

Kwenu wakereketwa...View attachment 2526364View attachment 2526379
Siku hiyo atakuwa anazikwa tena na tena. Si unaona Lissu alikuja kumzika tena?. Ni heri isiwepo tu.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
šŸ•°ļøšŸ’Æ sio mjinga na mshamba kiasi hiko
 
Tunapoelekea katika hio siku muhimu ya kuenzi kifo cha JPM, ni vyema huu mwaka Mh SSH akaitangaza rasmi hio siku kuwa sikukuu ya kitaifa, ili kuenzi mema na makubwa kabisa aliyo yafanya Hayati Dr. Magufuli.

17 march: Magufuli Day

Kwenu wakereketwa...

View attachment 2526364View attachment 2526379
Kwa mkapa tusisahau ndio baba wa mageuZi yote unayoyaona baada ya utawala mzee mwinyi ambae alifanya kazi kubwa kuboresha uchumi baada ya vita nk
 
Wanajifanya wanamuenzi Mwalimu lakini mawazo na mafundisho yake yote wameyatia kapuni. Sasa wanafanya vivo hivyo na Hayati JPM. TUACHE UNAFIKI
 
Back
Top Bottom