Pengine kuna siku tutakutana na wapendwa wetu tena

Pengine kuna siku tutakutana na wapendwa wetu tena

Kifo kinatuachia majonzi makubwa ni maumivu. Nimejariwa uwezo flani kuna siku uchungu ulinikaba sana nikasema hapana kwa kipawa hiki nakitumia kumuita mama yangu mzazi niongee nae japo nisikie sauti...... Kilichonikuta marehemu wetu nao roho zao zinawauma kwa yanayoendelea duniani na yanayotutokea. Tuwaombee sana marehemu roho zao zipumzike kwa amani na kama kuna uwezekano tuungane nao siku moja paradiso!.
alikuja mama? nielekeze namna ulifanya nna jambo nataka kudiscuss na marehemu mmoja hivi
 
Nimejifananisha na huyo mtoto. Imagine Huyo Mama Akija Kufariki Huyo Mtoto Itakuwaje?! Aliyeimba Kifooo Kifoo Kifo Hakina Huruma Alikuwa Sahihi 100/- R.I.P Father & Mother
FB_IMG_17272901627409592.jpg
 
Kuna siri kubwa sana kwenye kifo.. Kifo ni fumbo lisilo na majibu mpaka leo hii
M'miss mtu aliye hai lakini yuko mbali nawe! Huyu mnaweza kuja kuonana lakini sio mfu.. Ambapo kwa baadhi ya imani tutakuja kuonana nao huko huu mbinguni siku ya kiama..tena si katika mwili huu wa damu tena!

Hakuna hapa ambaye hajawahi kufiwa.. Kifo kinauma sana! Kifo ni kichungu kwa wale wapendwa wetu waliotuacha wakati bado tunawahitaji sana
Wazazi
Kaka/dada
Mjomba/shangazi
Mume/mke
Watoto ndugu na jamaa

Unabaki na wengine ambao hawatoshi kuvaa viatu vyao.. Kuna wakati unajikuta unawakumbuka mpaka unakosa pozi.. Sometimes hata usingizi hupati
Unazikumbuka zile nyakati za furaha
Nyakati za upendo mkuu
Nyakati uliposhikwa mkono na kupata nguvu mpya na tumaini jipya wakati ulishakata tamaa na kuona maisha hayana maana tena!
Pengine hayo maisha yatarudi tena
Pengine uchungu mkubwa ule utatoweka milele
Hakuna ndoto mbaya kama nyota uko na mpendwa wako aliyekeisha fariki halafu unashtuka na kujikuta uko pekeyako kitandani hayupo na huwezi kumuona tena

Tumeumbiwa kifo na hatujui siku wala saa ya kuachana milele na wapendwa wetu.. Tunao muda mchache wa kukaa nao
Hivyo basi
Tuwapende sana
Tuwasaidie sana
Tuwape kila faraja wanayostahili
Tuwape furaha na mambo mengine yote mema mazuri na bora kabla hatujaachana nao milele
Tuombeane mwisho mwema na maisha mengi mazuri
Jr™
Safarini ArushaView attachment 3107792
Mimi nafikiri hakuna maisha baada ya kifo.

Na wala binadamu hana kitu kinachoitwa "roho" ambacho kinaendelea kuishi baada ya kifo.

Huu ni ukweli mchungu.

Binadamu, kama walivyo wanyama wengine, anazaliwa, anaishi na mwisho anakufa na kufutika.

Hakuna kuzaliwa tena, hakuna kukutana na wapendwa, hakuna kwenda mbinguni/motoni, hakuna kufufuka siku ya kiama. Ukifa ndio mwisho wako.
 
Surat Kafirun
"Lakum deenukum waliya deeni"

Mtume aliwaambia makafiri ...."Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu"

Kwenye hili suala la kifo ni fumbo ambalo utatuzi wake upo kwenye imani zetu za dini

Mfano mimi naamini tutakufa na kuzikwa kwa muda usiojulikana kisha siku ya Qiyama ambapo Allah atatufufua kwa ajili ya hesabu na hukumu ndio maana ikaitwa judgement day >> when Allah will decide how people will spend their afterlife.

Ila kwa upande wa pili wao wanaweza wasiamini kwamba tutafufuliwa baada ya kufa, wanaweza wakaamini kwamba mtu akishakufa anaenda kwenye pumziko la milele.....
 
Ukitaka usiwaze sana mambo ya nini kitatokea baada ya kifo, hakikisha Kwa kadri unavyoweza, hauhusiki na kifo Cha mtu yeyote.

Pili, kadri upatapo nafasi, tenda wema, usiumize wengine.

Mwisho, usikabidhi mtu mwingine jukumu la furaha yako, usiwaze kabisa delegation kwenye hili jambo.

Pambana sana kwenye jitihada za kuwa na maisha bora bila kupoteza furaha yako kwenye mchakato.

Tulikuja bila kitu, tutaondoka bila kitu vile vile.

Hayo ya huko mbele au nini kitatokea tukifa, yatajipanga yenyewe.
 
Mtani kifo ni mwanzo sio mchakato.. Death is a state not a process .. Waliowahi kunusurika kifo wanajua hili.. Huko kifoni ni mbali sana barabara ni ndefu haina mwisho halafu haina watu wala wanyama
🤣🤣🤣🤣🤣Umeanza ongea story za vijiwe vya wakereketwa
 
Hivi undugu ni jambo la limwili ama la karoho?
Mwili ni kasha la muda liharibikalo
Kuna kupumzika kwa amani na kupumzika kusiko kwa amani (walio kundi hili walikufa pasipo siku zao za kufa kufika) na baadhi ya makabila au koo mizimu yao husumbua sana ndugu waliobaki hai kutafuta haki yao, kama kuna utatanishi hufanywa tambiko kabla au baada ya mazishi ili kuumaliza nguvu,

Mshana fanya ulete mada inayozungumzia jinsi ya kuishi na kuzifatisha nguvu za kiroho kwa yale chanya, watu wengi wana hiyo nguvu ila wanaipuuza hawajui kuiishi
Mada nzuri sana naahidi nitafanya hivyo rafiki
 
Hivi undugu ni jambo la limwili ama la karoho?
Mwili ni kasha la muda liharibikalol
Kifo kinatuachia majonzi makubwa ni maumivu. Nimejariwa uwezo flani kuna si

Mimi nafikiri hakuna maisha baada ya kifo.

Na wala binadamu hana kitu kinachoitwa "roho" ambacho kinaendelea kuishi baada ya kifo.

Huu ni ukweli mchungu.

Binadamu, kama walivyo wanyama wengine, anazaliwa, anaishi na mwisho anakufa na kufutika.

Hakuna kuzaliwa tena, hakuna kukutana na wapendwa, hakuna kwenda mbinguni/motoni, hakuna kufufuka siku ya kiama. Ukifa ndio mwisho wako.
Roho ni nishati hai.. Haikuumbwa na haiwezi kuharibiwa
 
Attachments

Nachukia hizi habari za KIFO yaani Kama KIFO kingekuwa mtu hakika ningekiua mimi mwenyewe

Sikujuaa kuwa inachukua nusu ya maisha yako kumsahau mpendwa wako inaumiza sana [emoji24][emoji24]

Wewe KIFO wewe umelaaniwa sanaaa
 
Kwanza inatisha, waliokufa sio wenzetu tena huwa wanakuja kwa ukali na kwa kuogopesha bora umuote ndotoni sio kumuita aroo
Kabisa uko sahihi,, kuongezea tu marehemu wanatuona na matendo yetu hapa duniani sasa wanapokuja lazima akurekebishe akuonye na akushauri sasa kasheshe marehemu awe alikua mkali mbona utajuta.
 
Kifo kinatuachia majonzi makubwa ni maumivu. Nimejariwa uwezo flani kuna siku uchungu ulinikaba sana nikasema hapana kwa kipawa hiki nakitumia kumuita mama yangu mzazi niongee nae japo nisikie sauti...... Kilichonikuta marehemu wetu nao roho zao zinawauma kwa yanayoendelea duniani na yanayotutokea. Tuwaombee sana marehemu roho zao zipumzike kwa amani na kama kuna uwezekano tuungane nao siku moja paradiso!.
kama kuna roho ipo sehemu inasikia, inaona huyo mtu hajafa ni mzima

Mhubiri 9:5​

Maana, walio hai hujua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui chochote. Hawana tuzo tena; hata kumbukumbu lao limesahauliwa kabisa.
 
Duuh mmenikumbusha mbali kipindi cha uhai wangu!!
Nimemiss sana kuishi ila ndio hivyo tena
 
Unajidanganya mwenyewe
Ukichukia kufa tafsiri rahisi wew unachukia kuishi.
Maana kifo ni sehemu ya maisha.
Na usipokipenda kwa moyo wako wote unakosa ladha ya kuishi .

Umenikumbusha sana kipindi cha uhai wangu

Nachukia hizi habari za KIFO yaani Kama KIFO kingekuwa mtu hakika ningekiua mimi mwenyewe

Sikujuaa kuwa inachukua nusu ya maisha yako kumsahau mpendwa wako inaumiza sana [emoji24][emoji24]
 
Kuna siri kubwa sana kwenye kifo.. Kifo ni fumbo lisilo na majibu mpaka leo hii
M'miss mtu aliye hai lakini yuko mbali nawe! Huyu mnaweza kuja kuonana lakini sio mfu.. Ambapo kwa baadhi ya imani tutakuja kuonana nao huko huu mbinguni siku ya kiama..tena si katika mwili huu wa damu tena!

Hakuna hapa ambaye hajawahi kufiwa.. Kifo kinauma sana! Kifo ni kichungu kwa wale wapendwa wetu waliotuacha wakati bado tunawahitaji sana
Wazazi
Kaka/dada
Mjomba/shangazi
Mume/mke
Watoto ndugu na jamaa

Unabaki na wengine ambao hawatoshi kuvaa viatu vyao.. Kuna wakati unajikuta unawakumbuka mpaka unakosa pozi.. Sometimes hata usingizi hupati
Unazikumbuka zile nyakati za furaha
Nyakati za upendo mkuu
Nyakati uliposhikwa mkono na kupata nguvu mpya na tumaini jipya wakati ulishakata tamaa na kuona maisha hayana maana tena!
Pengine hayo maisha yatarudi tena
Pengine uchungu mkubwa ule utatoweka milele
Hakuna ndoto mbaya kama nyota uko na mpendwa wako aliyekeisha fariki halafu unashtuka na kujikuta uko pekeyako kitandani hayupo na huwezi kumuona tena

Tumeumbiwa kifo na hatujui siku wala saa ya kuachana milele na wapendwa wetu.. Tunao muda mchache wa kukaa nao
Hivyo basi
Tuwapende sana
Tuwasaidie sana
Tuwape kila faraja wanayostahili
Tuwape furaha na mambo mengine yote mema mazuri na bora kabla hatujaachana nao milele
Tuombeane mwisho mwema na maisha mengi mazuri
Jr™
Safarini ArushaView attachment 3107792
Umenifanya nime mkumbuka rafikiyangu tuliye soma wote primary school ni miaka 5 imepita tangu aondoke katika uso wa dunia …… katika maisha kuna moment huwa zinatokea nakupita …. Tushukuru MUNGU kwa kila jambo
 
Back
Top Bottom