Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Mimi nimeacha hata kusali sikuizi maana hata kanisa nalo limekuwa afta money. They just care about sadaka na si kuwa mfano katika jamii
Kwani unasali kwa faida ya nani? Anayetakiwa kuwa mfano katika jamii ni wewe muumini, sasa unakimbia ili uishi upagani? Think twice
 
Wewe hama hata leo, wewe ni mbegu iliyotupwa kwenye mwamba, sisi wenye imani na kanisa Katoliki tunasonga mbele, na hatakuja kupata rais Mprotestanti,nafikiri hatujui hasira yenu inatokana na nini,
 
Atoe maoni yake asilisemee kanisa yeye sio msemaji wa kanisa
Pengo ndio bosi wa jimbo katoliki la Dar, mojawapo ya majimbo ya kwanza Tanzania. Ndio maana wakati wa mageuzi ya misa, huwa tunalitaja jina lake.

Kauli yake inatuwakilisha sisi wakatoliki wa jiji la Dar, mamlaka yake yanatambulika popote pale duniani ambapo unafanyika mkutano wa viongozi wa kanisa katoliki.

Kardinali Pengo sio mtu mdogo kama mnavyodanganyana humu JF.
 
Porojo nyiingi na kiingereza cha kuchovyachovya hakitabadilisha ukweli ndugu.PAPA SI MUNGU NA ROMA SIYO MBINGUNI.kwaheri
 
Kwani Niwemugizi alitoa msimamo wa kanisa?
 
Mkuu ungeelewa kardinali anapatikana vipi usingeandika upuuzi kama huu uliouandika.

Ungeelewa heshima yake kidini usingejisumbua kuandika mambo ambayo huyafahamu.

Kardinali sio mtu mdogo sana kama unavyodhani, kama mnavyoongea mkiwa kijiweni kwenu.
Papa alijiudhulu ndie yeye.Acha habari za kusaidikika km vile kitu haifikiki.Akishajiona akili yake inapoteza uwezo anaweza kiri mwenyewe.Na ikizidihadi kushindwa jitambua kuwa ana shida.Papa anaweza mweka bench na kumtafutia kazi mbadala.
 
Kila mara anakuja na kuleta msimamo mi niliacha kumwamini kuanzia swala la mahakama ya kadhi pamoja na katiba mpya
 
Mange ameshawaelekeza nini cha kufanya?[emoji13] [emoji13] [emoji13] je mkimtoa Pengo nani achukue nafasi yake?mwenyekiti wa maisha?RL? TL? FM?[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Pengo nae ni mwananchi wa Tanzania, ana uhuru wa kutoa maoni
Ni kweli ila alijipambanua kwa kumpinga Askofu Mwenzake eti yeye ndiye anatoa msimamo wa kanisa wakati sio kweli ?

Pengo ni Kardinal wangu ila kanikwaza sana.
 
Pengo ndio Godfather wa Pombe..
mnamuona Pengo mnafiki basi siku akifa ndo mtatamani afufuke..
ndio mtu pekee anaeweza kumbishia Pombe kitu na akasikia..
Tunahitaji kuwa na kiongozi Imara wa kiroho ,kauli zake kwa kweli zimekuwa na mnyukano sana ,hata baba mtakatifu Benerdicto alijiuzuru Upope baada ya kuona yu mgonjwa na amepoteza nguvu nadhani ili ni sahihi kwa Kardinal pamoja na nguvu aliyo nayo kwa Pombe
 
Acha ubabaishaji bwana kama Wewe ni RC FAKE

Mimi nimezaliwa mkatoliki, baba, mama na ndugu zangu wote ni RC

Lakini kwa hiii tabia ya Pengo kulinajisi kanisa...hapa mzee hafai na Mungu amuadhibu kwa kadri ya matendo yake maovu.
Huyo hajui hata mafundisho ya kanisa achane naye
 
Ni bora Pengo ,MTU kama ngwajima kazama kabisa siasani
 
Pengo nae ni mwananchi wa Tanzania, ana uhuru wa kutoa maoni
Sasa kwanini wengine wakitoa maoni yao anawaka? Niwemugizi alitaja wapi kuwa mahubiri yake siku ile ni msimamo wa kanisa katoliki? Mbona amewashwa tu na askofu mwingine aliyeko kwenye jimbo ambalo ni mbali mno na jimbo la pengo?
 
Papa alijiudhulu ndie yeye.Acha habari za kusaidikika km vile kitu haifikiki.Akishajiona akili yake inapoteza uwezo anaweza kiri mwenyewe.Na ikizidihadi kushindwa jitambua kuwa ana shida.Papa anaweza mweka bench na kumtafutia kazi mbadala.
Mkuu, msiwe kama mbumbumbu wa kisiasa, sio kila mtu awe na mawazo au fikra kama zenu.

Askofu Pengo kiumri ni mkubwa, lakini sio kigezo cha kugeuka kupelekeshwa na mawazo yote ya vijana ambao bado wanajiona wakamilifu kimawazo na kimaono.

Kustaafu atastaafu yeye mwenyewe lakini yupo sawa kabisa kwenye suala la kupinga mawazo ya askofu wa Rulenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…