Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Mnabaki kucheka kwa sababu mnazama kwenye mada nyepesi sana. Nyinyi kuwa watu wa madhehebu mengine mbali na ukatoliki sio kigezo cha kejeli zenu kuwa ndio uhalisia wa mambo.

Mambo ya kiroho husomewa shuleni miaka na miaka, sio mambo yenye kufanana na hizi mada nyepesi za kina Lema na Muro.
 

Kwanini unasema hivyo? Cardinal alieleza kitu sahihi...msimamo wa kanisa unatolewa na TEC na sio Askofu mmoja mmoja. Maaskofu ni raia kama raia wengine. Pengine sio wote wanakubaliana na hali ya sasa. Tusilazimishe wote wakubaliane na Chadema au matakwa ya upinzani.

Ninakubaliana umuhimu wa katiba mpya. Ila mbinu za medani wanazotumia wapinzani hazitawafikisha popote. Maana sijaona mtu anayepiga ngumu ukutani bila kuumiza mkono wake.
 
Kiboko yake Gwajima
Mbona alipomtukana Pengo aliishia kutembelea wheel chair nenda kamuulize na uite Waandishi Wa habari mwende nao kwa gwajima mumuulize swali moja tu kuwa je utarudia tena kuuliza kuwa pengo kala maharage gani? Au muulizeni swali lolote kuhusu pengo muone atakavyonywea Kama kamwagiwa tindikali.Pengo namba ingine hawezi chezewa na vitoto Kama gwajima. Nendeni mkamuhoji gwajima hata Kwa swali dogo tu kuwa any comment baada ya pengo kumjibu niwemugizi unasemaje gwajima uone atakavyoruka.
 
Hivi Tanzania Sasa hivi Kidney beans bei yake sio ghali sana!
 
Miezi kadhaa iliyopita,mmoja wa maaskofu nguli na wabobezi aliwahi kumuhoji kadinali pengo,aliuliza kama Pengo anajua nani alimroga

Askofu Gwajima aliyejipatia umaarufu kwa kuondoa mapepo na uchawi,aliuliza swali hilo hasa baada ya Pengo kutoa hoja ambazo kila mtu zilimshangaza na kuhoji weledi wake

Namuuliza Askofu Pengo,je alishamjibu Gwajima? Maana inawezekana katika ulimwengu wa Roho,Askofu Gwajima amewaona watu wanaomroga Askofu Pengo,na ni jukumu lake kumtafuta Gwajima ili amsaidie
 
Teh! Teh!

Ila jamaa kama kweli vile,karogwa
 

Can't they contain matters in the catholic church? kwa nini waonyeshe udhaifu huu ndani ya kanisa? Hata ukimya ni silaha kubwa sana , wakionyeshana kiburi au kutoheshimiana ina maana kuwaonyesha waumini wao tofauti zao? Bado nasisitiza kuwa haya ni mambo yaliyostahili kujadiliwa ndani kwa ndani kisha tamko la Kanisa Katoliki kutolewa bila ya ku-affect personality ya mtu. halafu Elimu itolewe makanisani nani mkubwa ki utaratibu wa kanisa Tanzania au say ORGANIZATIONAL CHART YA KANISA KATOLIKI
 
Uzuri Ni kuwa Maaskofu wa RC wanateuliwa na Papa mwenyewe La sivyo Pengo angewatoa! Pengo msione anaongea sauti ya upooole yule Jamaa can eat you inside out kama Piranha! Namfahamu Vizuri, Muulizeni kama Anawajua Ma-Jesuit "The Children of Ignatias Loyola, Pedro Arupe na Vencent Keefe" Atajua Namjua ila yeye sio mmoja wao!
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Haina katiba iliyoandikwa lakini ina mila na desturi zinazofuatwa kikamilifu, mfumo mzuri wa kimahakama na hukumu zake kama rejea,wewe hayo Tanzania yapo?

Kwamba kiongozi hata akitoka nje ya ndoa ikajurikana anaachia ngazi bila hata kushinikizwa! Kuongoza nchi kwa mfumo wa uingereza hamtaweza kamwe.

Nchi ambayo wahujumu wakubwa wa nchi bado wamo serikalini kama wabunge! Uingereza hao wangekuwa wanaozea jela,mko madarakani kwa mujibu wa katiba leo mnajifanya hamjui umuhimu wa katiba! Shetani wakubwa nyie.
 
Pengo ndio Godfather wa Pombe..
mnamuona Pengo mnafiki basi siku akifa ndo mtatamani afufuke..
ndio mtu pekee anaeweza kumbishia Pombe kitu na akasikia..
Basi hafanyi hilo jukumu lake vizuri, kuna pengo
 
Umehangaika sana kujibu hoja moja
Protocol za kanisa katoliki tofauti na za chadema ambako kila mtu msemaji Nassari msemaji lema msemaji Mchungaji msigwa msemaji Sugu msemaji bavicha wasemaji kijo bisimba msemaji nk
 
Sawa, lakini hapo hajatoa maoni yake binafsi. Yule mwingine ndio hii statement ilimfaa.

Naunga mkono kauli aliyoitoa pengo kwa niaba ya Kanisa.
Pengo hana mamlaka ya kuongea kwa niaba ya kanisa, ukae ukilijuwa hili vyema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…