Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Huyu mzee ana mahaba na JPM na msimamo wake umekuwa wazi tangu kampeni za urais hadi sasa. Sasa anataka awape maneno ya kusema maaskofu wenzake. Hata hivyo na yeye aliyoyasema, kama kweli kayasema, ni maoni yake na si ya kanisa.
 
Kiukweli huyu jamaa nilitokea kumchukia Sana, ni Kati ya viongozi WA kanisa wanaosababisha nisiende kanisani siku hizi, nikiamini ni wapiga dili tu.
 
Hivi wewe bwanamdogo unasimamia nini hasa ?
Najiuliza hivi huyu Yehodaya ni muumini wa dini yeyote? kama ndio, ni dini ipi hiyo ambayo miongozo yake inaruhusu waumini wake kufanya hiki anachokishauri huyu member hapa kwenye hizi comment zake hapo chini, kwenye hiyo thread inayomuhusu mh Lissu?

YEHODAYA said:
Waziri huwa anasaini mikataba ya tender iwe ya ujenzi au yoyote? Magufuli Kill these idiots


Tundu Lissu: Aliyevunja Mkataba wa ESCEL ni rais Magufuli
 
Huyu mzee ni mnafiki sana shida yake ni udini tu kipindi ambacho ikulu inakuwa na viongozi wa dini nyengine.
 

Askofu Niwemugizi alitoa mawazo yake kama yeye na siyo kama TEC na it was crystal clear. Sasa Kardinali Pengo anaposema alichosema siyo msimamo wa Kanisa Katoliki ana maana gani au hakuwahi kusikia alichosema Askofu Niwemugizi? Otherwise, ninachoona ni kama kuna mgawanyiko wa kifikra kwenye TEC kati ya wale wanaotaka Katiba Mpya na wale ambao wanaridhika na Katiba ya 1977 na hawaoni umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya. Kama hii ni kweli tafsiri yake ni kwamba TEC inaweza kuwa katika mgawanyiko kati ya maaskofu ambao ni "conservative" na "progressive".
 
Thread closed...wanaomshambulia mkuu pengo wasome hapa...

Siyo kweli. Askofu alionyesha kabisa yalikuwa mawazo yake labda kama kila anachosema askofu huwa ni tamko la TEC au jimbo lake kitu ambacho siyo kweli pia.
 
Nafikiri, hata hicho alichosema yeye kwamba Katiba IJE BAADAE nao usiwe msimamo wa RC,bali msimamo wake binafsi
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Awe Pengo awe mwanya katiba kwanza
 
Swali kwa kadinali je katiba na bombadia kipi kinafanya watu wafe njaa na kukosa elimu? Kipi ni cha muhimu zaidi?
 
Hamjamuelewa Pengo. Kasisitiza kuwa kuna utaratibu wa kanisa kuhusu kutoa matamko ya kisiasa. Sasa wapinga kila kitu wanakuja na mipash yao. Kwani pengo kasosea wapi? kwani Pengo kasema hataki katiba mpya?
Dragoon, nafahamu misimamo na itikadi zako kuhusu siasa zetu na sishangai kwa ulichosema.

Kadinali Pengo amezungumzia hili kama nani? Ask.Niwemugizi alikuwa wazi kwa kusema 'haya ni maoni yangu binafsi, sio ya Kanisa', wananchi na vyombo vya habari tulimwelewa vizuri.

Sasa shangaa, Pengo anaibukia wapi kwa suala ambalo halijaleta mkanganyiko wowote. Kama maoni ya Ask. Niwemugizi yangekuwa yameleta mkanganyo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kupitia Katibu wake au Rais wake Askofu Ngalalekumtwa wangekuwa wameshalitolea ufafanuzi. Sasa Pengo anaibuka ghafla na anapata mwanya wa kupenyeza maoni yake! Ningemwelewa Ask. Pengo kama angetoa maoni yake binafsi kuhusu Katiba mpya bila kuzungumzia hoja ya Ask. Niwemugizi.

Vv
 
Na iko ndo kinaonekana wazi kabisa
 
Na majibu ya pengo siyo ya kanisa pia
 
Hakika.Maana niliuliza hapa mtu akivunja katiba nini kinafuata?Hakuna aliyejibu.Kama iliyopo tu inavunjwa na ni kawaida wala anayevunja hashtuki,hata ikiwekwa katiba gani haitasaidia kitu.
Ndio maana tunataka katiba ili akivunja achukuliwe hatua sahivi rais yuko juu ya katiba
 
Ni sawa na makonda anavyo jiona kuwa yeye ndo Maui wa wakuu wa mikoa yote tanzania
 
Uingereza haijawahi kuwa na katiba na haina mpango wa kuwa na katiba lakini ni nchi iliyoendelea.Katiba sio kipaumbele cha maendeleo
Umewahi kuona uingereza video ya rushwa inasambaa na mty bado anateuliwa kuwa kiongozi kwenye chama?
 
Nafikiri,hata hicho alichosema yeye kwamba Katiba IJE BAADAE nao usiwe msimamo wa RC,bali msimamo wake binafsi

Kama yeye anaweza kusema hivyo, kwa nini wengine wakitoa mawazo yao binafsi anaibuka ibuka?
 

Tutamwitia Gwajima, ndiye anamuweza huyu mzee
 

Naona kama Kardinali alikuwa out of context kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…