Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Uko nje ya mada, mtoa mada haongelei kuongea na cm na papa, halafu by the way who is papa?we unamuona papa mtu muhimu sana? Huu bado ni utumwa wa fikra


Kama uko nje ya Kanisa Katoliki siyo mtu muhimu lkn kwa Wakatoliki bilioni 1.23 ni Mkuu wao na maamuzi yake yanaathiri maisha yao, hivyo usiunderestimate nguvu yake, kwa mfano mimi Bibi yangu Kijijini anasali kila siku kama Kardinali akisema kitu hawezi kuhoji wala kumpinga, kwa mfano Kardinali akimwambia achague CCM atafanya hivyo kwake yeye ni mtumishi wa Mungu sasa watu kama Bibi yangu wako wengine Tanzania!
 
Sikupenda kujibu pia ila Mhashamu Pengo hupaswi kupingana na maaskofu wenzio. Inafaa asifanye unafiki sisi waumini msitugawe kwa kutetea misimamo isiyo sawa. Kweli hautaki katiba ? Je mh rais akiruhusu katiba mchakato uanze uta- goma au utaendeleza unafiki WA kusema katiba ni muhimu?

Hatujasahu makasisi wakuu walikula pesa ya rugemalira. Hujatoa tamko. Askofu kutoa mawazo yake ya kutaka haki unapaniki? Hakuna awezaye kuufuta ukatoliki ivo inafaa kusimamia haki. Inani yangu kwako inayumba baba Askofu
 
Mwanahabari Huru

Askofu Pengo unafiki sio sehemu yetu wakatoliki, sikutaka kuandika chochote kuhusiana na wewe, mimi nimebatizwa katika RC nimekuwa muumini mkubwa, nimesoma shule ya Upadri St Mary's Seminary, ninaijua Rc.
Kama hukutaka kuandika chochote kuhusiana na yeye, sasa hii thread ni ya nini?, si ungeendelea kukaa kimya
Kwa maneno haya "mimi nimebatizwa katika RC" tayari ishaonesha wewe sio mkatoliki
 
Kwa Wakatoliki Kardinali ni mtumishi wa Mungu, anateuliwa na Mungu baada ya kushukiwa na roho Mtakatifu hivyo sauti yake ni Sauti ya Mungu kwa Wakatoliki!
Jee ni kweli kwamba kila wakati watumishi wa Mungu huwa na Roho mtakatifu. Kama Yuda Iskariote alikuwa anaiba kwenye fuko la sadaka tena Kristo mwenyewe akiwepo, ni kwa nini tuamini hawa kina Pengo hawawezi kuwa na udhaifu?

Unakumbuka Kristo alimwambia Mtume Petro "rudi nyuma Shetani"?
 
Hapo kuhusu Gwajima ni uwongo mkubwa. Pengo hajawahi mshitaki Gwajima.

Pia kumbuka maelezo ya Pengo yalikuwa kwamba anafafanua kuwa kauli ya Niwemugizi siyo ya kanisa kwani tayari ulikuwa na hiyo argument iliyohitaji ufafanuzi
Acheni ushabiki wa kijinga hvi unajua mfumo wa uongozi RC yeye alikua anafafanua kama Nan?Ufafanuzi wake ni maelezo yake binafsi Kama ilivyokua kwa askofu wa Ngala na wala hasimami kma kanisa!!!Msemaji Mkuu wa kanisa ni raisi wa TEC na sio vingnevyo.Ajaribu kuficha mahaba yake kwa chama tawala
 
Kumbe nawe zwazwa hivi! Kuongea na papa ndo nini?unaweza ukawa na kiongozi mkubwa hata kuishi nae lakn ukawa jinga tu,hata wewe ni jinga sana..


Siyo swala la ujinga au werevu ni swala la power, kuna Wakatoliki wengi Tanzania ambao hawawezi kuhoji ushauri wa Kardinali wao, kwao ni mtumishi wa Mungu na akisemacho kina baraka za Mungu, hivyo ndivyo ilivyo!
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Huna point..unaleta vitu viwil tofaut..jamaaa hajaongelea Pengo anakaa na nan au kula na nani..hivi mbona kuna watu vichwa maji kiasi hiki..yan maji kabisa..MAJI TAKA
Chadema upepo umebadilika...2020 mtalia zaidi
 
Hatawew pia ni mtumishi wa mungu na unahaki sawa na papa
Usipumbazike mungu ni mmoja na kwake sote tutarejea


Ni kweli labda kwa Mungu hkn tofauti ingawaje sina uhakika na hilo lkn Kanisa Katoliki limeanzishwa na Binadamu na siyo Yesu, Yesu hakuanzisha Kanisa lolote!
 
Kama hukutaka kuandika chochote kuhusiana na yeye, sasa hii thread ni ya nini?, si ungeendelea kukaa kimya
Kwa maneno haya "mimi nimebatizwa katika RC" tayari ishaonesha wewe sio mkatoliki
Another idiot at work.Kwa hyo neno kubatizwa halitumiki ktk kanisa au umezoea sacrament tu?Jengeni hoja zenye tusiwe maboga hata kwenye mambo ya msingi.
 
Mwanahabari Huru

Askofu Pengo unafiki sio sehemu yetu wakatoliki, sikutaka kuandika chochote kuhusiana na wewe, mimi nimebatizwa katika RC nimekuwa muumini mkubwa, nimesoma shule ya Upadri St Mary's Seminary, ninaijua Rc.

Nimesikitishwa sana na kauli zako za kipuuzi, zilizo jaa unafiki, tumekusikia sana ukijipambanua kuwa wewe si muumini wa mabadiliko, tuambie upande wako ni UPI.

Askofu wangu Pengo umemjibu Askofu Niwemugizi alie jitokeza hadhalani na kusema watanzania wanataka katiba mpya, umefufuka ulikotoka na kumshambulia Askofu kuwa katiba au maneno ya Askofu sio msimamo wa RC lakini hakusema kuwa ni msimamo wa RC. Lakini unajua Askofu Niwemugizi si msemaji wa Rc, maana yake alisema kama Mawazo yake kikatiba, na wewe unamjua msemaji wa RC ulitaka kutafuta uhalali wa kujibu mashambulizi la watawala, of target.

Naona umetoka kwa kasi sana kujibu shambulizi hill!,! Lakini hutoki hadhalani kuonya matukio ya kuuwawa kwa watanzania na kutupwa kwenye maji wakiwa wamefungwa mikono Nyuma, wanaopigwa Risasi kama kina tundu Lissu, kuonya viongozi wanao toa maneno ya kibaguzi na kikabila, huwezi kuonya kufokea au kushauri, kazi yako imekuwa ni kujibu mashambulizi kwa wanao ikosoa serikali,

Au unavyeti feki? Unamiliki Mali zisizo halali? Kiongozi wa kiroho unashindwa kujua nini wajibu wako? Sio mala ya kwanza kupingwa na maaskofu wenzio akiwepo Gwajima na kupelekana mahakamani ambapo Askofu Gwajima alikushinda kesi.

Viongozi wa dini simamieni haki na sio unafiki kujipendekeza kama mnataka ubunge, au teuzi za kina mama Lwakatale sawa, Hata mkitaka usemaji wa Ccm nafasi za kina polepole.

Swali la Kizushi: WATU WASIOJULIKANA WANATOKEA RWANDA PREY FOR TUNDU LISSU

We ndo tunda La waseminari wapumbavu. Wajinga na wasiojitambua waliowahi kusoma huko kama kweli ulisoma. Unaujua unafiki unalijua Kanisa Katoliki. Ungelijua na hata ungemjua Pengo vizuri na historia yake usingekuja hapa na dhehebu lako La kichadema kumkashfu Baba Kardinali. Kanisa katoliki lina utaratibu tena makini wenye kuchimba the „Urstoff „ of what is seen now. Pengo kama mshauri wa Baba Mtakatifu anapaswa kuweka Sawa hoja kwa niaba ya Kanisa La Tanzania. Na kumbuka kaulizwa.

Na ndo mana hata Balozi wa Baba Mt naye akaongelea hilo. Hawana Siasa za kijinga kama wewe eti Mseminary WA zamani. Askofu wa Ngara naye kama mtz ana haki ya kusema. Lakini cheo chake kinambana asije akaonekana anasema in the name of the Catholic Church of Tanzania na pia ya wakatoliki walio chini yake. Mana Ndani humo wapo ambao vipaumbele vyao (kidemokrasia na pia kistrategy Sio katiba ). Chadema mmekuwa bendera fuata upepo mpaka mnasahau kuwa standard ya nini Liwe na nini kitangulie haipo kwako.

Serikali ya Tz kwa maoni ya pengo Sio katiba. Ni madawa. Ni uchumi. Ni Elimu nk. Mwaka Wa Pili sasa bado Siasa. Lini tutafanya Kazi. Katiba gani itafanyiwa mchakato bila fedha tena Sio fedha ya kitoto. Sera ya chama cha Mapinduzi wanajua wao nini wafanye. Na ndo magufuli anafanya. Kanisa haliwezi kuwa nyuma ya wajinga kama wewe. Maauji gani ya ajabu. Haya ambayo mnayatangaza kipropaganda.

Alikufa Sokoine. Mchana Kazi. Mnataka katiba lakini Leo hamuheshimu hata iliyopo. UHURU wa maoni. Yani mjinga kweli ni mjinga. Kila Mtu manataka kumtumia. Wewe ni mwanaliamsha dude Nenda huko kasali. Huko kwetu ni Sheria na kama Tamko litatoka Sio kadiri ya wewe bali ya UKWELI
 
Kurekebusha katiba ya chama chenu mmeshindwa mtaweza ya nchi!
....Acha ujuha, tunazungumzia katiba ya nchi kwa watanzania 50 mill, hivi unajua watanzania walioko kwenye vyama ni wachache kuliko wasio na vyama? Mkiwa majukwaani mnahubiri utaifa na uzalendo, huku vichochoroni mnakomaa na chama chenu cha makanikia.
 
Ni kweli labda kwa Mungu hkn tofauti ingawaje sina uhakika na hilo lkn Kanisa Katoliki limeanzishwa na Binadamu na siyo Yesu, Yesu hakuanzisha Kanisa lolote!
Kanisa limeanzishwa na Kristo ila madhehebu ndiyo yameanzishwa na wanadamu. Paulo alikemea sana madhehebu lakini bila madhehebu hakuna maslahi kwa wanaoutumia Ukristo kama biashara.

Kuna enzi Kanisa Katoliki lilikuwa linauza vyeti vya msamaha wa dhambi. Leo tuna Manabii na Mitume ambao wanatembelea magari ya kifahari na kuishi kwenye majumba ya kifahari yanayofanana na wauza madawa ya kulevya, huku baadhi ya waumini wao hata nauli ya kwendea kwenye ibadi hawana na mlo wa siku moja kwao ni shida!
 
Pale mapema ilinichukua muda kidogo ili nimuelewe Pengo. Baada ya muda nikaweza kumuelewa Pengo kama alicho kitamka ni kutofautisha Kanisa/Catholic na Siasa
 
Siyo kweli! Mleta Mada hawezi kulielewa Kanisa Katoliki na mambo yake jinsi linavyofanya kazi kuliko Pengo kwani hana access yoyote!
Usichanganye Kanisa Katoliki na Imani kwa ujumla wake, Kanisa Katoliki limeanzishwa na Binadamu ni Dola kamili kama vile Serikali ya Tanzania na halina uhusiano na Yesu kwani Yesu hakuanzisha Kanisa lolote lile hapa Duniani!

Hivyo kusema mleta Mada analielewa Kanisa Katoliki klk Kardinali wa Kanisa Katoliki ni sawa na kusema Kubenea anailewa Dola ya Tanzania kuliko WM Majaliwa!
Pengo sio siri tena wakatoliki wamemchoka sana, kawaangusha sana.Kipindi ch akutaka kumsikia huwa anapotea sana km lipumba. Mapadri wake alikuwa wazi kabisa kila mahali hawaitaki tena ccm. Sio muda utasikia shinikizo watu wakimtaka papa amtoe na kumwekwa kwa wazee. Sijui km hatosusia kanisa.
 
Mawazo yako sio sheria. Albadir itakuwa imekupitia sio bure
 
Ni kweli labda kwa Mungu hkn tofauti ingawaje sina uhakika na hilo lkn Kanisa Katoliki limeanzishwa na Binadamu na siyo Yesu, Yesu hakuanzisha Kanisa lolote!
Sitaki kuzungumzia kanisa manatutatofautiana
Lkn kma kiongozi akienda kinyume na uadilifu hatumtii na ataambiwa
kwasababu atapoteza watu wengine sema ametumia njia gani kumuambia sasa ilo mimi cjui
 
Kardinali Policarp Pengo si Msemaji wa kanisa katoliki. Hata maneno yake si msimamo wa kanisa pia.
 
Back
Top Bottom