Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

PENIELA SEASON 3

EPISODE 8

MTUNZI : PATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Padre alitumia zaidi ya dakika hamsini ndani ya chumba cha John.Walionekana kuongea na baadae akamuombea na kumpaka mafuta usoni baadae Padre akatoka.

“ Ndugu zangu kama nyote mnavyofahamu kwamba kutokana na ugonjwa wake ndugu yetu hatakuwa na maisha marefu sana kwa hiyo basi nimempatia huduma ya mwisho kabla ya mwenyezi Mungu kumuita.John Mwaulaya amekubali kwa hiari yake kubatizwa na amekuwa mpya tena . John ametubu dhambi zake zote na kwa mamlaka niliyopewa na kanisa nimemuondolea dhabi zake. Amepokea komunyo takatifu na Yesu yuko ndani yake.Kwa sasa hata kama akiitwa na Mungu dakika yoyote tuna hakika atakuwa sehemu salama.Kitu cha msingi ni kuzidi kumuombea ili hata atakapoondoka katika maisha haya aweze kupokelewa Mbinguni” akasema Padre na kuwabariki wote kisha Peniela akamrudisha nyumbani kwake.


ENDELEA…………………

Mlio wa simu ulimstua Mathew toka usingizini .Haraka haraka akaichukua simu yake na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Eva

“ Hallow Eva? Akasema Mathew
“ Mathew habari za asubuhi? Bado umelala?
“ Ahsante sana kwa kuniamsha Eva.Nilikuwa katika usingizi mzito sana.Kuna habari gani? Akauliza Mathew
“ Mathew nimekupigia kukupa taarifa kuhusiana na ile kazi uliyoniomba nikufanyie.Kuna kitu cha ajabu ambacho kimetokea na kunishangaza sana.Hakuna taarifa zinazoonyesha mawasiliano ya simu ya wale wazee kwa muda wa miezi sita ya mwisho kabla hawajauawa.Taarifa hizo zimefutwa kabisa katika kumbu kumbu kwa hiyo ni vigumu kufahamu walikuwa wakiwasiliana na akina nani kabla hawajafariki.Hii imenishangaza sana Mathew.” Akasema Eva.Mathew akakaa kimya kidogo na kusema
“ Thank you Eva.
“Kuna chochote kingine nikusaidie? Akauliza Eva
“ No thank you Eva.Nikihitaji msaada tena nitakujulisha.Ila nashukuru sana kwa msaada huu mkubwa” akasema Mathew na kukata simu.
“ Kwa miezi sita hakuna taarifa za mawasiliano ya simu za wazee wale.Ni wazi taarifa hizi zimeondolewa makusudi kabisa na lengo hapa ni kumficha Yule mtu ambaye alikuwa nyuma yao.Watu hawa wako makini sana kwani walifahamu fika uchunguzi ungefanyika na yangefuatiliwa mawasiliano kati ya wazee wale na mtu huyo angefahamika na ndiyo maana wakawahi kufuta kabisa kumbu kumbu zote za mawasiliano .Lakini hata hivyo kuna njia nyingine ya kuweza kumfahamu mtu huyo ni nani.Ngoja turudi sasa katika lile wazo la Anitha la kumchunguza Habib ambaye anatajwa kutaka kununua karatasi zile.Nina hakika kupitia yeye basi tunaweza kugundua jambo Fulani.Nina rafiki yangu katika shirika la ujasusi la C.I.A yeye anaweza akanisaidia sana katika jambo hili kwani C.I.A wamejipenyeza karibu kila kona ya dunia na ni rahisi sana kumfuatilia mtu yeyote Yule” akawaza Mathew na kutoka mle chumbani.Tayari Anitha alikwisha amka kitambo na alikuwa jikoni akiandaa mlo wa asubuhi.Mida hiyo ilipata saa moja na dakika kumi na saba za asubuhi
“ Hallow Anitha” akasema Mathew huku akifungua kabati na kutoa chupa ya mvinyo akamimina kidogo katika glasi akagugumia yote.Anitha akamtazama na kusema
“ Is something bothering you? I know you.Ukinywa mvinyo kama hivyo lazima kuna jambo linalokusumbua.” Akasema Anitha
“ nataka kuchangamsha mwili tu ,naona umechoka sana” akajibu Mathew.Anitha akaacha shughuli aliyokuwa akiifanya akamtazama Mathew na kusema
“ Ulionana na John jana? Anaendeleaje? Alikuitia jambo gani? .
Mathew akaongeza tena mvinyo katika glasi akanywa na kusema
“ Nothing important.Hali yake si nzuri na kwa mujibu wa uchunguzi wa madaktari john anasumbuliwa na saratani ya ubongo kwa hiyo hakuna tegemeo la kupona.Aliniita na kuniomba msamaha kwa kitendo kile cha kuiteketeza familia yangu vile vile akanitaka nimlinde Peniela na kuhakikisha anakuwa salama siku zote.Thats all” akasema Mathew na kunywa funda lingine la mvinyo.
“ Anything from Kigomba? Akauliza Mathew

“ hakukuwa na simu ya maana aliyopiga tena zaidi ya kuwapigia simu waanwake wawili na akamuahidi mmoja wao kwamba anakwenda kulala kwake.Vile vile alimpiga simu mke wake na kumweleza kwamba hataweza kurejea nyumbani usiku ule kutokana na kuwa na kikao kizito.Kigomba anaonekana ni mpenda wanawake sana.”akasema Anitha

“ Usimweleze jaji Elibariki chochote kuhusiana na simu hizo za Kigomba alizowapigia wanawake wengine,si unajua anavyompenda peniela.By the way Eva amenipigia simu muda si mrefu na amenipa taarifa kuhusiana na kazi ile niliyomuomba anisaidie kuifanya.Hakuna kumbu kumbu zozote za mawasiliano za wazee wale kwa miezi sita kabla ya kufariki kwao.Zimefutwa kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumficha huyo ambaye walikuwa wakiwasiliana naye.Kwa sababu hiyo basi tunarejea katika lile wazo lako la kumchunguza Habib ambaye anatajwa kutaka kuzinunua karatasi zile.”akasema Mathew

“ Nina rafiki yangu mmoja anafanya kazi katika idara ya ujasusi ya marekani C.I.A.Nina hakika anaweza akatusaidia katika suala hili.” Akasema Mathew halafu akaongozana na Anitha hadi ofisini na kumpigia simu huyo rafiki yake afanyaye kazi katika shirika la ujasusi la marekani.Baada ya sekunde kadhaa mwanadada mmoja akaonekana katika luninga kubwa iliyokuwa ukutani.
“ hallow Mathew” akasema mwanadada Yule mwenye asili ya afrika

“ hallow Kerry.habari za siku ?
“ habari nzuri sana .habari za Tanzania?
“ Tanzania kwema.Samahani kwa kukusumbua Kerry,ninashida naomba unisaidie”
“ Bila samahani Mathew.Nikusaide nini?

“ Kuna mtu mmoja ambaye ninahitaji unisaie kumchunguza.Anaitwa Habib soud ni raia wa Saudi Arabia.Ninataka kufahamu kama ana mawasiliano na mtu yeyote kutoka Tanzania.Kuna jambo ninalichunguza na yeye amejitokeza katika picha .Najua ni kinyume na taratibu zenu za kazi lakini naomba unisaidie Kerry,Ni muhimu sana kwangu” akasema Mathew..Kerry akaonekana kufikiri kidogo kisha akasema
“ sawa Mathew nitakusaidia.Nisubiri dakika mbili.”akasema Kerry na kukata simu
“ Unapofanya kazi kama hizi kuna ulazima wa kuwa na marafiki wengi toka katika mashirika mbali mbali ya kijasusi na kipelelezi duniani ili unapohitaji taarifa Fulani basi inakuwa rahisi sana kuipata.Mimi nina marafiki karibu katika mashirika mengi makubwa ya ujasusi duniani.C.I.A,KGB,MOSSAD,MSS la china,BND ujerumani,MOIS Iran,na mengine mengi” Akasema Mathew na mara Kerry akarejea hewani
“ Mathew huyu Habib Soud ni mtu ambaye amekuwa katika orodha ya watu wanaochunguzwa na C.I.A kwa kufadhili vikundi vya kigaidi.Habib ana utajiri mkubwa sana na inasemakana anautumia utajiri huo katika kufadhili ugaidi.Baba yake alikuwa ni mfadhili wa siri wa Alqaeda na aliuawa na vikosi vya Marekani .” akasema Kerry na kusogeza tena taarifa nyingine katika tablet yake.

“ C.I.A tumekuwa tukimfuatilia pia mawasiliano yake .kwa upande wa Tanzania taarifa zinaonyesha kwamba amekuwa na mawasiliano ya mara na mtu mmoja anaitwa Rosemary Mkozumi.Huyu aliwahi kuwa mke wa rais wa Tanzania na ana taasisi yake inayojishughulisha na miradi mbalimbali ya kuwawezesha akina mama kiuchumi .Kupitia taasisi hii amekuwa akipata wadhili toka sehemu mbali mbali duniani na mmojawapo wa wafadhili wa taasisi hii ni Habib.Amekuwa akitoa pesa nyingi kama misaada kwa taasisi hii kwa dhumuni la kuwawezesha wanawake kiuchumi.Habib anafanya hivi ili kuificha ile dhana kwamba anafadhili makundi ya kigaidi.Mathew hizo ndizo taarifa ninazoweza kukupa kwa sasa kuhusiana na habib.Sisi bado tunaendelea kumchunguza na kama kuna lolote ambalo unaona linaweza likatusaidia katika kupata ushahidi wa kutosha kuhusu Habib kujihusisha na makundi ya ugaidi basi naomba unitaarifu mara moja na endapo utahitaji tena msaada wowote mimi niko tayari kukusaidia muda wowote.” Akasema Kerry

“ Kerry nakushukuru sana kwa msaada wako huo mkubwa.Endapo nitapata jambo lolote la kumuhusu Habib katika uchunguzi wangu nitakutaarifu mara moja” akasema mathew na kuagana na Kerry akata simu.Muda huo huo jaji Elibariki akaingia mle ofisini

“ Kuna taarifa yoyote mpya imepatikana? Akauliza jaji Elbarki
“ Ndiyo jaji.Kuna taarifa tumezipata .Kwanza ni kutoka kwa Eva.hakuweza kupata taarifa zozote za mawasiliano za mzee Mustapha na Ktwana.Inaoenaka zimefutwa kabisa kwa makusudi.Tumewasiliana na trafikiyangu mmoja aanayefanya kazi katika shirika la ujasusi la marekani na ametutaarifu kwamba mtu ambaye alitajwa kutaka kuzinunua karatasi zile zilizoibwa ikulu Habib soud amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rosemary Mkozumi mke wa rais mstaafu Deus Mkozumi.Amekwenda mbali zaidi na kusema kwamba Habib amekuwa akiifadhili taasisi inayoongozwa na bi Rosemary kwa kuimwagia mabilioni ya fedha .” Mathew akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Jana tumemsikia Dr Joshua akimtaja adui yake namba moja katika mpango wa kuiuza package ni Deus mkozumi.Leo tena tunasikia kwamba mke wa Deus mkozumi anapokea mamilioni ya fedha toka kwa mtu anayedaiwa kuufadhili ugaidi.Hapa kuna picha inajengeka.Ninapata picha kwamba package hiyo anayotaka kuiuza Dr Joshua ilikuwepo hata wakati wa uongozi wa Deus na anaifahamu fika na ndiyo maana amekuwa kinyume na mpango wa Dr Joshua wa kutaka kuiuza.Pili nina hakika kabisa kwamba hata hizo karatasi zilizoibwa zilikuwepo ikulu wakati wa uongozi wa Deus na nina hakika kabisa kwamba Rosemary kwa kuwa naye alikuwepo ikulu wakati huo alifahamu uwepo wa karatasi hizo.Ninaweza kutamka bila wasi wasi kwamba Rosemary ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango wa kuziuza karatasi zile.Kumbu kumbu za mawasiliano za mzee Kitwana na mzee Mustapha zimefutwa kwa sababu ya kumficha ili asijulikane kama alikuwa akiwasiliana nao.” Akasema Mathew akawaangalia akina Anitha na kusema
“ kama Habib anashukiwa kuufadhili ugaidi basi ni wazi alihitaji sana karatasi zile ili kuweza kuzitumia kanuni zilizomo ndani yake katika kutengeneza kirusi hicho hatari ili kitumike katika mashambulio ya kigaidi.Hii ni sababu pekee ambayo ilimfanya Habib kutaka kuzinunua karatasi zile kwa mabilioni ya fedha.Mnaona namna picha inavyojengeka? Akauliza Mathew

“ Nakubaliana nawe kabisa Mathew.Maelezo uliyoyatoa yanatoa taswira ya wazi ya namna Rosemary Mkozumi alivyohusika katika uibwaji wa karatasi zile ikulu.Kwa mantiki hiyo basi Rosemary naye atakuwa ni mtu wa muhimu sana kwetu .Kuna mambo mengi ambayo tutahitaji kuyafahamu kutoka kwake.” Akasema Anitha

“ Jamani kuna jambo na mimi naomba niliseme.” Akasema jaji Elibariki
“ Ninamfahamu huyu Rosemary Mkozumi .Alikuwa ni mke wa rais mstaafu Deus Mkozumi lakini baada ya Deus kumaliza awamu yake ya pili ya uongozi walitengana.Hakuna sababu iliyowekwa wazi kuhusiana na kutengena kwao.Rosemary anamiliki jumba kubwa la kifahari ufukweni mwa bahari na vile vile anamiliki pia biashara nyingine nyingi kubwa kubwa.Ni mwanamke tajiri na mpaka sasa haijawekwa wazi utajiri wake ameupataje.Ninaweza kukubaliana na maneno ya mathew kwamba Rosemary aliingiwa na tamaa ya pesa na akaamua kusuka mpango wa kuziuza karatasi zile. Edson alitumiwa tu katika kuziiba lakini maelekezo yote yalitoka kwa Rosemary.” Akasema jaji Elibariki na mara ikasikika kengele ya getini.
“ Ngoja nikaangalie nani anagonga” akasema Mathew na kutoka

“ Is Mathew ok? Akauliza jaji Elibariki baada ya Mathew kutoka.Aligundua kwamba Mathew hakuwa sawa.
“ There is must be something bothering him.Jana usiku alipigiwa simu na peniela kwamba john Mwaulaya anamuhitaji.Aliondoka na kwenda hospitali kuonana na John.Nimemuuliza ni kitu gani John alichomuitia lakini bado hajanipa jibu la kweli.Amekuwa akificha ficha.Ninamfahamu Mathew ,kuna jambo aliambiwa na John” Akasema Anitha

“ Umesema alikwenda kuonana na John mwaulaya? Jaji Elibariki akashangaa
“ ndiyo alikwenda kuonana naye jana usiku na….” kabla Anitha hajaendelea akaingia Mathew akiwa ameongozana na peniela.Jaji Elibariki na peniela walipoonana wakajikuta wakikumbatiana kwa nguvu na kupeana mabusu

“ Are you ok my love?akauliza jaji Elibariki

“ I’m ok Elibariki.What about you,are you ok?

“ I’m ok peniela” akasema jaji Elibariki .Anitha na Mathew wakatazamana wakatabasamu

“ karibu sana peniela” akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.mambo yanakwendaje hapa?
“ mambo yanakwenda vizuri .Anaendeleaje John? Akauliza Mathew
“ Bado hali yake si nzuri.Jana ulipoondoka hali ilizidi kuwa mbaya akaomba tumtafutie padre.Tulifanikiwa kumpata Padre kwa usiku ule na akampatia huduma ya kiroho kumuandaa kwa lolote linaloweza kutokea.Nimeondoka kule saa kumi na moja alfajiri bado hali yake haikuwa nzuri.Nimewapigia tena simu madaktari kabla sijaja huku na wakaniambia kwamba kwa sasa hali yake imezidi kuwa mbaya .Anything can happen at anytime.” Akasema peniela na chumba kikawa kimya.Mathew akauvunja ukimya

“ Tuko pamoja Peniela katika wakati huu mgumu” jaji Elibariki na Anitha wakamuhakikishia peniela kwamba wako pamoja naye pia

“ Ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu.Nimepita hapa ili kufahamu ni kitu gani kinachoendelea kwani toka jana hatukuwasiliana.Vipi ule mpango wetu ulifanikiwa? Akauliza Peniela

“ Ulifanya kazi kubwa sana jana na kila kitu kimeenda vizuri kama tulivyopanga Tayari tunaweza kufuatilia kila kinachofanyika katika simu ya Dr Kigomba.Mfano jana tumeweza kusikia maongezi yote aliyoongea na Dr Joshua akiwa afrika ya kusini.Vile vile tunaweza kufahamu kila mahala aliko Dr Kigomba endapo atakuwa ameivaa ile saa” akasema Anitha na kumuelekeza Peniela namna program ile inavyofanya kazi.Akayafungua maongezi ya simu kati ya Dr Kigomba na Dr Joshua na wote kwa pamoja wakayasikia.
“kumbe Yule mzee ni mtu katili sana.Amekwenda afrika ya kusni shingo upande.Kwake yeye fedha ni muhimu sana kuliko uhai wa binadamu tena mtoto wake mwenyewe” akasema peniela kwa hasira

“ kwa mujibu wa maongezi yao inaonekana wanajiandaa kuifanya biashara hii haraka iwezekanavyo.Alimuachia Dr Kigomba jukumu la kuhakiki kama fedha tayari imekwisha ingia katika akaunti zao za siri nje ya nchi na mara tu wakihakikisha kwamba fedha yote imelipwa basi wataikabidhi hiyo package.Mtu wa muhimu na wa kuchunga sana hapa ni Dr Kigomba kwani ndiye atakayefanya makabidhiano kwa niaba ya Dr Joshua Kwa vile tayari tuna uwezo wa kumfuatilia Dr Kigomba .Peniela unatakiwa ukae karibu sana na Dr Kigomba.Ongeza ukaribu pia na Kaptain Amos ambaye mko naye team SC41 na yuko timu moja na akina Kigomba .Katika team SC41 mmejipanga vipi katika kuichukua hiyo Package? Akauliza Mathew
“ Jana walikuja watu watano kutoka makao makuu ya team SC41 Marekani na dhumuni lao kubwa ni kuja kusimamia suala hilo la uchukuaji wa hiyo Package na kuondoka nayo.Leo kutakuwa na kikao cha watu wote wa team SC41 kwa ajili ya kuweka mikakati ya mwisho kuhusiana na package hiyo.Team SC41 wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaipata package hiyo na katika operesheni hiyo wanatutegemea sana sisi wawili mimi na captain Amos.
"
“ Mpaka sasa hivi hujafanikiwa kufahamu kilichomo ndani ya hiyo Package? Akauliza Anitha

“ Hapana bado.Mpaka sasa hakuna ajuaye ndani ya hipo package kuna nini.Nmejaribu kuwadadisi wale jamaa waliotoka Marekani lakini hawako tayari kuweka wazi.”
“ Ok vizuri.Basi utaendelea kutufahamisha mipango yote ya team SC41 kuhusiana na package hiyo Kitu cha muhimu sana kuzingatia jihadhari wasije wakagundua kwamba unashirikiana nasi” akasema Mathew
“ Ninalifahamu hilo na niko makini sana katika kuhakikisha kwamba hawagundui lolote.Hata nijapo huku huwa ninatumia mbinu za hali ya juu sana. Ili nisiweze ku…..” Peniela akastushwa na mlio wa simu yake.Akaitazama ikiita akaogopa kuipokea.

“Mbona hupokei simu? Akauliza Mathew
‘ Its Josh.Yuko kule hospitali” akasema Peniela kwa wasi wasi
“ Pokea ufahamu anataka kukwambia nini.Yawezekana ana jambo la muhmu sana la kukwambia”akasema jaji Elibariki .Peniela akabonyeza kitufe cha kupokelea na kuweka simu sikioni

“ hallow Josh ” akasema.Zikapita sekunde kadhaa bila ya Josh kuongea kitu
“ Josh are you there? Akauliza peniela
“ Peniela where are you? Akauliza Josh
“ Josh kuna nini?
“ Naomba uje mara moja hapa hospitali” akasema Josh na kukata simu.Peniela akapatwa na wasiwasi mwingi

“ Is everything ok peniela? Akauliza Mathew
“ Josh ananitaka nifike haraka hospitali .Sijui kuna nini.I’m so scared.”akasema Mathew

“ Usiogope peniela .Yawezekana kuna jambo la msingi analokuitia..I’ll take you there.” Akasema Mathew

“ No thank Mathew I can manage” akasema peniela

“ Peniela uko katika mstuko na ni hatari sana kuendesha gari ukiwa katika hali hiyo.Naomba usiweke ubishi katika hilo.Nitakupeleka hospitali.Anitha endelea kumfuatilia Dr Kigomba na kama kuna jambo lolote la dharura utanitaarifu mara moja” akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akavaa kisha akaongozana na Peniela akamuendesha kuelekea hospitali.
“ Anitha ninakubaliana nawe kwamba mathew leo hayuko sawa sawa.Kuna jambo linalomsumbua kichwa chake.” Akasema jaji Elibariki.

“ Ninavyofahamu mimi,Mathew na John Mwaulaya ni maadui wakubwa.Ni John mwaulaya aliyeiteketeza familia ya Mathew.Siku zote Mathew alikuwa akitafuta nafasi ya kulipiza kisasi kwa John Mwaulaya na ndiyo maana aliponiambia kwamba John amemuita hospitali nilistuka sana .Lakini tumuache kwanza atulie na atatueleza “akasema Anitha
Mathew na Peniela wakawasili hospitali.Safari yao haikuwa na maongezi mengi kwani Peniela alionekana kuzama katika mawazo na Mathew hakutaka kumsumbua

“ Mathew ahsante sana .Ulikuwa sahihi.Nisingeweza kuendesha gari kwa hali hii.Miguu inanitetemeka ” akasema Peniela huku akifungau mlango na kushuka wakaelekea katika jengo alikolazwa john.Mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa ni Josh.Macho yake yalionekana kuwa mekundu .Peniela akazidi kujawa na wasi wasi.Josh alipomuona akamfuata na kumkumbatia

“ Peniela I’m sorry.He’s gone.John is gone”akasema Josh.Peniela akaishiwa nguvu na kuzirai.Haraka haraka akachukuliwa na kupelekwa kupatiwa huduma ya kwanza .Wakati Peniela akiendelea kupatiwa huduma ya kwanza simu ya Mathew ikaita.Alikuwa ni Anitha

“ hallow anitha.Nilikuwa katika harakati za kukupigia simu kukufahamisha mambo ya huku .Kuna habari gani hapo? Akaulzia Mathew
“ Dr Joshua amempigia simu Dr Kigomba muda si mrefu.Flaviana is gone.She’s dead.” Akasema peniela .Ilimchukua Mathew zaidi ya dakika moja kutamka lolote

“ How’s Elibariki?
“ ameishiwa nguvu.Nimempeleka chumbani kupumzika.”akasema Anitha

“ Ok Endelea kumpa uangalizi wa karbu sana.Huku nako mambo si mazuri.John is gone too” akasema Mathew



TUKUTANE SEHEMUJAYO…

.
 
SEASON 3

SEHEMU YA 10


MTUNZI 😛ATRICK.CK

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nimefanikiwa kuonana tena na John na katika dakika zangu za mwisho nimejikuta nikishindwa kutekeleza mpango wangu wa kulipiza kisasi.Hali yake nilivyoiona jana ilikuwa mbaya na mimi mwenyewe nikamuonea huruma .Alikiri kosa lake na nikakubali kumsamehe.John alinieleza mambo makubwa na mazito sana na ninapaswa kumshukuru sana kwa kunichagua mimi niyafahamu mambo yale.Amekufa na siri nyingi kubwa kubwa na laiti kama ningepata muda wa kutosha wa kuongea naye angeweza kunieleza mambo mengi makubwa zaidi lakini ninashukuru hata kwa hili alilonieleza.Kitu kingine kizuri ni kwamba katika dakika za mwisho za uhai wake alipata huduma ya kiroho na kama maandiko yanavyosema hata kama tukiwa na dhambi nyingi kiasi gani tukifanya toba ya dhati Mungu hutuondolea dhambi zote na kutufanya wapya tena.Mungu amrehemu na ampe pumziko la milele” akawaza Mathew wakati akikaribia sana kufika katika baa ya Eva



ENDELEA…………………………….



Mathew aliwasili katika baa ya Eva.Watu hawakuwa wengi sana.Wengi wa waliokuwepo hapa mida hii walikuwa wakipata supu,kwani sifa nyingine ya baa hii ni kuwa na supu nzuri .Mathew aksshuka garini na moja kwa moja akelekea katika ofisi ya Eva,akagonga mlango , Eva akamruhusu aingie.
“ Hallow Eva” akasema Mathew

“ Karibu sana Mathew.” Akasema Eva
“ Ahsante Eva..Niambie kuna kitu chochote ulichokipata? akauliza Mathew huku akivuta kiti na kuketi.Eva akasubiri hadi Mathew alipoketi na kutulia kisha akasema
“ Ulipoondoka niliacha shughuli zote na kulishughulikia lile suala uliloniomba.Kuna jambo nimeligunuda ambalo linaweza kuwezesha kupata nafasi ya kuingia ndani ya nyumba ya Rosemary na ukafanya uchunguzi wako.” Akasema Eva
“ Ahsante sana Eva.Umegundua nini? akaulzia Mathew kwa shauku ya kutaka kulifahamu jambo hilo.
“ Baada ya kuachana na Mzee Deus Mkozumi,Rosemary aliingia katika mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa aliyewahi kuwa waziri wa kilimo katika serikali ya Deus Mkozumi anaitwa Henry Alois Chibuma.” Akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Henry Chibuma ni mmoja kati ya waliokuwa mawaziri vijana sana katika serikali iliyopita na anasemekana kuwa na utrajiri mkubwa.Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba mke wa ndoa wa henry alikwisha farikiki dunia na ana mtoto wake mmoja tu aitwaye Naomi.Huyu ni muathirika wa dawa za kulevya na kwa sasa anafungiwa ndani ya jumba kubwa lenye ulinzi mkali ili asiweze kutoka wala kuonekana.Taarifa zinasema kwamba Henry ndiye chanzo cha mwanae kuathirika na dawa hizo kwani yeye pia alikuwa ni muingizaji na mtumiaji mkubwa wa dawa hizo .Nina hakika tukimpata Naomi tukaongea naye tunaweza kufahamu mambo mengi sana na hii inaweza ikawa ni njia rahisi ya kumpata Henry atakayetupeleka kwa Rosemary..” Akasema Eva.
“ Unasema waziri Henry naye ni muingizaji na mtumiaji wa dawa za kulevya? Akauliza Mathew
“ Ni kweli Mathew.Henry ni muingizaji mkubwa sana wa dawa za kulevya hapa nchini lakini nakuwa vigumu kumtia nguvuni kutokana na mtandao walio nao.Ndiyo maana nilikutahadharisha toka awali kwamba watu hawa ni hatari sana.Hata wakati akiwa wazidi alikuwa akijihusisha na biashara hii” akasema Eva
“ Huyu Naomi umeweza kuipata historia yake japo kwa ufupi? Akauliza Mathew
“ Ndiyo nilifanikwa kupata historia yake.Ni binti wa miaka kumi na tisa sasa na inasemekana alishindwa kuendelea na masomo kutokana na kuathirika na dawa hizo.Pili rafiki yake wa kiume alipigwa risasi na watu wasiojulikana.Inaaminika aliuawa kwa amri ya Henry. Naomi anaishi maisha ya upweke mkubwa ndaniya jumba hilo alimofungiwa.Nina hakika tukienda kuonana naye atatusikia na atakubali kushirikiana nasi.Nimefanikiwa kupata hadi jina la Daktari anayemtibu anaitwa Dr Marina.Huyu ni daktari toka hospitali kuu ya taifa kitengo cha kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya. ” Akasema Eva.Mathew kama kawaida yake hutumia muda kidogo kutafakari kila jambo kabla ya kufanya maamuzi akainama akatafakari na kusema
“ Sawa Eva twende tukaonane na Naomi.Lakini kabla ya kwenda huko lazima tuhakikishe tumejiandaa vya kutosha kwani kama ulivyosema kuna ulinzi katika jumba hilo.Nina hakika hatutaruhusiwa kuonana na Naomi kwa hiyo tunaweza kulazimika kutumia nguvu.” Akasema Mathew.Naomi akainuka akafungua kasiki lake lililoko ukutani ambalo huhifadhia silaha kwa matumizi ya dharura akamuita Mathew aangalie silaha ambazo zingeweza kuwasaidia.Mathew akachagua silaha na vifaa ambavyo vingeweza kuwasadia halafu bila kupoteza muda wakaingia katika gari la Mathew na safari ya kuelekea kwa Naomi ikaanza.
“ Nadhani sasa umeanza kupata picha ya watu wanaomzunguka Rosemary ni watu wa namna gani.Mtandao wao ni mkubwa na hatari.Henry anajihusisha na biashara nyingi haramu ikiwemo uingizaji wa dawa za kulevya lakini kumtia hatiani inakuwa ni mtihani mgumu kwa sababu wamezishika karibu sekta zote muhimu.Wana watu wao ndani ya jeshi la polisi,hata ndani ya usalama wa taifa kuna watu wao kwa hiyo ni rahisi sana kwao kujua chochote kinachoendelea dhidi yao na wakajihami.Ndiyo maana nilikutahadharisha toka mapema kwamba unatakiwa uwe makini sana unapomfuatilia Rose .” akasema Eva

“ Nimeamni maneno yako Eva,lakini dhumuni kuu la kazi yetu ni kushughulika na watu kama hawa. Hatupaswi kuwaogopa hata kidogo.Lazima tuhakikishe watu kama hawa ambao wanakwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi wanafikishwa katika vyombo husika.Endapo tukiogopa kupambana nao siku moja nchi hii itashindwa kukalika kwani itakuwa ikiongozwa na genge la wahuni na wahalifu.Wewe mwenyewe uliniambia kwamba Rosemary anafikiria kuwania urais.Kwa nguvu ya pesa,ushawishi na mtandao mkubwa alio nao akipata nafasi hiyo ya kugombea anaweza akawa rais,sasa hebu pata picha mtu kama Rosemary akiwa rais wa nchi hii nini kitatokea? Hatupaswi hata kidogo kuacha jambo kama hilo likatokea.Lazima tupambane naye kwa kila nguvu na uwezo tulio nao.Binafsi nina roho ngumu kama jiwe na huwa siogopi kitu chochote zaidi ya Mungu pekee” akasema Mathew.Eva akatabasamu na baada ya muda akasema
“ Mathew naomba nikuulize kitu na tafadhali naomba unijibu”

“ Uliza va usijali”
“ Ni jambo gani ambalo unalichunguza?

“ Eva , mimi na wewe tumekuwa karibu kwa muda mrefu sana na kila pale ninapokuwa na tatizo nimekuwa nikikukimbilia wewe kwa msaada.Natamani sana nikueleze nini ninachokichunguza lakini ninaomba unipe muda kidogo ili niliweke vizuri suala hili na kisha nitakueleza kila kitu.” Akasema Mathew

“ Don’t you trust me? Akauliza Eva
“ I do trust you with my life Eva” akasema

“ No you don’t.Kama unegkuwa unaniamini usingesita kunieleza kile unachokichunguza.Mathew ninaweza kuwa na msaada mkubwa sana kwako tofauti na unavyodhani.Au unahisi kwamba ukinieleza jambo hilo ninaweza kuvujisha siri na kuharibu uchunguzi wako? Akauliza Eva
“ Si hivyo Eva.Ninakuamini sana na ndiyo maana nimekwambia kwamba nipe muda kidogo na nitakueleza kila kitu .Naomba ufahamu vile vile kwamba bado ninahitaji sana msaada wako.” Akasema Mathew aliyekuwa makini katika usukani
“ Sawa Mathew..” akajibu Eva kwa shingo upande na safari ikaendelea kimya kimya.Baada ya muda Eva akauliza

“ That woman,Anitha is she your girlfried? Akauliza Eva na kumfanya Mathew atabasamu
“ Kwa nini umeuliza ?
“ Nimehisi tu kwamba anaweza akawa ni mchumba wako kwa namna mnavyopendana.” Akasema Eva na Mathew akatoa kicheko
“ Anitha si mpenzi wangu na wala hatuna mahusiano yoyote mengine zaidi ya kazi.Unaponiona mimi na Anitha tuko mahala basi ujue ni kazi tu inafanyika na hakuna lingine.Mimi ni kazi tu mambo hayo ya mapenzi nilikwisha achana nayo muda mrefu.Toka familia yangu ilipoteketea sitaki tena kuijingiza katika mahusiano mengine.” Akasema Mathew
“ Mathew ni miaka sasa imepita toka litokee tukio lile.Usiendelee kujitesa tafadhali.You have to move on.Au bado una mpango wa kulipa kisasi kwa waliofanya kitendo kile? Do you know them? Akauliza Eva.Mathew akanyamaza kidogo kisha akajibu
“ Ni kweli ni miaka mingi imepita sasa lakini bado picha za tukio lile zinanijia akilini kila siku na ninaona ni kama tukio lile limetokea jana.Nimejitahidi sana kulisahau tukio lile lakini nimeshindwa.Bado linanitesa na nitateseka hadi siku ninaingia kaburini.Kuhusu kulipiza kisasi ni kweli nilikuwa na mpango huo lakini kwa sasa nimeachana nao.Sintolipiza kisasi kwani aliyefanya kitendo kile tayari amekwisha fariki dunia na ni Mungu pekee atakayemuhukumu” akasema Mathew
“ Kwa hiyo ulimfahamu? Ni nani huyo shetani? Akauliza Eva

“ It doesn’t matter for now.Eva kama hutajali naomba tusiendelee kuliongelea suala hilo”

“ Sawa Mathew na samahani kwa kukukumbusha mbali lakini kuhusu kuingia katika mahusiano mengine hili sintaacha kukukumbusha kwani umri unakwenda sana.Promise me you’ll think about that” akasema Eva.Mathew akatabasamu na kusema

“ Ok Eva.I’ll think about it” akajibu Mathew na safari ikaendelea.
Waliwasili katika mtaa lilipo jumba analoishi Naomi.Ni jumba kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa wa rangi nyeupe.Haikuwa rahisi kwa mtu aliyeko nje kuona chochote kilichomo ndani ya jumba lile kutokana na ukuta ule mkubwa.Kilichoonekana ukiwa nje ni bati zuri la rangi ya bluu.
“ Ni hapa” akasema Eva.Mathew akalitazama jumba lile na kupunguza mwendo wa gari na kusimama katika geti.Wakashuka na kubonyeza kengele na mlango mdogo wa geti ukafunguliwa na mtu mmoja aliyevaa mavazi meusi aliyeonekana kushangazwa sana na ujio wa akina Mathew
“ Habari zenu? Akawasalimu

“ Nzuri.Habari za hapa? Wakajibu Mathew na Eva kwa pamoja
“ Niwasaidie nini ? Akauliza Yule jamaa.
“ Sisi ni wanasihi tumetoka katika hospitali ya taifa kitengo cha kuhudumia waathirika wa dawa za kulevya.Tumetumwa hapa na Dr Marina kwa ajili ya kumfabnyia unasihi Naomi.” Akasema Mathew.Yule jamaa akastuka kidogo
“ Ninamfahamu Dr Naomi lakini mbona hakunitaarifu kama kuna watu watakuja hapa leo?Isitoshe huwa anakuja mwenyewe iweje leo atume watu wengine?

“ Una namba zake za simu? Akauliza Mathew

“ Ndiyo ninazo.” Akajibu Yule jamaa
“ mpigie na atakupa maelekezo.” Akasema Mathew na yule jamaa akaingiza mkono mfukoni akatoa simu na kuanza kuzitafuta namba za Dr Marina.Wakati ameiinamia simu yake Mathew akamfanyia ishara Eva na kwa kasi ya umeme Eva akampiga Yule jamaa pigo moja la haraka na kumpeleka chini.Mathew akamuwahi pale chini na kumkaba kabala hadi akapoteza fahamu.Eva akachungulia ndani na hakuona mtu mwingine yeyote.
“ Its clear.No body is here! Akasema Eva kisha Mathew akamvuta Yule jamaa na kumuigiza ndani akamficha katika maua.Akaichukua simu ya yule jamaa kisha wakaelekea katika mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni.Wakagonga lakini hakuna mtu aliyejibu.Wakagonga tena na safari hii mlango ukafunguliwa na msichana mmoja aliyeonekana kama ni mfanyakazi za ndani.Alistuka sana alipowaona akina Mathew akawasalimu kwa uoga.
“ Naomi yuko wapi? Akauliza Mathew
“ Yuko chumbani kwake” akajibu Yule msichana
“ Tupeleke haraka chumbani kwake.” Akasema Mathew kwa ukali na yule msichana akawaongoza hadi katika mlango wa chumba cha Naomi
“ Chumba cha Naomi ni hiki hapa.” Akasema Yule msichana na mara sauti ikasikika toka ndani
“ Chiku unaongea na nani huko ?
Yule msichana akawafanyia akina Mathew ishara kwamba sauti ile ni ya Naomi.
“ Naomi kuna wageni wamekuja kukutembelea.” Akasema Chiku
“ Waambie waondoke.Sihitaji kuonana na mtu yeyote Yule.Nani kawaruhusu waingie humu? Akauliza Naomi kwa ukali toka ndani.Eva akamnong’oneza jambo Chiku akasema
“ Naomi ni watu toka hospitali wanataka kukuona”
“ Nimekwambia waambie waondoke zao.Leo si siku ya tiba” akasema Naomi

“ Eva she’s not going to open” akasema Mathew na kuupiga teke mlango ukafunguka wakaingia ndani.Naomi alistushwa sana na kitendo kile akapiga ukulele mkubwa.Mathew akamfuata na kumtuliza
“ Naomi naomba tafadhali usipige kelele.Hatuko hapa kwa ajili ya kukudhuru.Tuko hapa kwa ajili ya kukusaidia” akasema Mathew.Naomi akawatazama Mathew na Eva halafu akauliza

“ Kwani ninyi ni akina nani?
Mathew akamgeukia Eva aliyekuwa amemshikilia Chiku Yule mtumishi wa ndani

“ Mfungie bafuni huyo” akasema Mathew na Eva akamchukua Chiku akaenda kumfungia katika bafu la Naomi,akamsachi na kuhakikisha hana simu wala kifaa chochote cha mawasiliano .
“ Naomi naomba usituogope tafadhali.Sisi si wanasihi kama tulivyojitambulisha.Sisi ni maafisa toka idara ya usalama wa taifa.Ninaitwa Mathew na Yule dada anaitwa Eva.Tumekuja hapa kuzungumza nawe mambo kadhaa lakini dhumuni kubwa likiwa ni kukusaidia” akasema Mathew

“ Nitaaminije kama unasema kweli? Ninyi si watu wa mtandao wa baba?
“ Hapana sisi si watu wa mtandao baba yako.Tuamini Naomi tuko hapa kwa lengo la kukusaidia.Lakini tutakusaidia endapo na wewe utakuwa tayari kutusadia.” Akasema Mathew
“ Mnataka kunisaidia kivipi? Akauliza Naomi

“ Tunataka kukutoa katika maisha haya unayoishi sasa na kukusadia kuanza maisha mapya na uweze kutimiza ndoto zako za maisha.Naomi tunafahamu kila kitu kuhusu historia yako .Ulikuwa ni msichana mwenye akili sana darasani na ulikuwa na malengo mengi ya maisha yako kwa siku za usoni lakini malengo na ndoto zote za maisha yako zilikatishwa baada ya kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.Tunafahamu ni baba yako ndiye aliyesababisha haya yote yatokee.Tunafahamu anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya . Tunafahamu amekufungia humu ndani na hataki utoke kabisa nje ili watu wafahamu hali yako.Unaishi maisha ya upweke mkubwa humu ndani.Naomi tunataka kukusaidia ili uweze kuachana na maisha haya upate tiba upone na uendelee kutimiza ndoto zako.” Akasema Mathew.Naomi akashindwa kujizuia akaanza kulia.Eva akamfuata akakaa pembeni yake na kumbembeleza.

“ Nyamaza kuliza Naomi.Historia yako inaumiza sana .Tutakusaidia Naomi ..Naomba usiendelee kulia ili tuongee kwani muda wetu ni mfupi sana hapa kwako.” Akasema Eva.Naomi akafuta machozi na kusema

“ Nawaona ninyi ni kama malaika mliokuja kunikomboa.Kwa miaka minne sasa nimekuwa nikiishi kama mfungwa ndani ya jumba hili.Sina hamu tena ya kuendelea kuishi kwani siioni tena thamani yangu.Hakuna mtu anayenipenda tena wala kunijali.Yote hii imesababishwa na mimi kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.” Akasema Naomi huku akiendelea kububujikwa na machozi
“ Ilikuaje ukajiingiza katika matumizi ya dawa hizi za kulevya? Akauliza Mathew.Naomi akamtazama na kusema
“ Ni frank.Huyu ndiye aliyenishawishi mimi kujiingiza katika dawa za kulevya.”
“ Frank ni nani?
“ Alikuwa boyfriend wangu,kwa sasa amekwisha fariki alipigwa risasi.”
“ Pole sana” akasema Eva
“ Haikuwa dhamira ya Frank mimi kujiingiza katika maisha haya ya dawa za kulevya kwani alikuwa ananipenda sana lakini huu ulikuwa ni mpango wa baba niwe hivi.”
“ Mpango wa baba yako? Kivipi? Akauliza Mathew

“ Baba alimtumia Frank aniingize katika matumizi ya dawa za kulevya.Niligundua kwamba baba alikuwa anamtumia Franki katika biashara ile kwa hiyo akamtumia yeye kunishawishi niingie katika matumizi hayo ya dawa za kulevya.”
“ Naomi tunafahamu kwamba baba yako anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya na ni mtumiaji pia lakini hatuelewi ni kwa nini akuingize na wewe katika matumizi haya ya dawa za kulevya wakati anazifahamu athari zake? Akauliza Mathew

“ Ni kwa sababu ninafahamu mambo yake mengi.Ninazifahamu siri zake nyingi.Baba alihusika katika kifo cha mama na nilipoligundua niliumia sana na nilimuweka wazi kwamba lazima nihakikishe ninamfikisha katika vyombo vya sheria.Hapo ndipo ugomvi kati yangu na baba ulipoanza na ndipo alipomtumia Frank kuningiza katka dawa za kulevya ili nichanganyikiwe akili yangu nisiweze kufanya kile nilichokusudia kukifanya.Baada ya kuona nimeathirika vibaya Frank aliumia sana na alikuwa tayari kwenda kutoa siri hii ndipo alipouawa kwa risasi na watu wa baba.Nilichukuliwa na kufungiwa humu ndani na katika miaka yote hii minne sijawahi kutoka kwenda nje ya nyumba hii.Nikitoka humu chumbani ninakaa hapo bustanini na si nje ya hapo. Baba amenitafutia daktari wa kunitibu na ameweka hadi walinzi na hakuna yeyote anayeruhusiwa kuingia ndani humu zaidi ya daktari wangu tu.Ninaishi maisha magumu sana na ndiyo maana ninawaona ninyi ni kama malaika mliokuja kunikomboa kama kweli lengo lenu ni hilo” akasema Naomi

“ Naomi sisi tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo ili uweze kurejea katika maisha yako ya kawaida.”
“ Tafadhali naombeni msiniache humu ndani.Mkiondoka ondokeni na mimi” akasema Naomi
“ usijali Naomi tutaondoka nawe.Lakini kabla ya yote kuna jambo ambalo tunahitaji sana msaada wako.” Akasema Mathdew
“Tunafahamu baba yako anajihusisha na mambo mengi ya haramu ikiwemo na biashara hii ya dawa za kulevya.Tumekuwa tukimfuatilia kwa muda na tumegundua kwamba anao mtandao mkubwa wa watu wanaojishughulisha na mambo mengi ya hatari. Kwa sasa baba yako na mtandao wake wanajihusisha na jambo moja kubwa na la hatari lenye kuhatarisha uhai wa mamilioni ya watu duniani.Tunatafuta namna ya kuweza kumzuia yeye na mtandao wake wasiweze kutekeleza mpango wao huo lakini njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa kupitia kwako.” Akasema Mathew
“ NInamfahamu baba yangu .Ana roho ya kishetani.Ni mkatili kupindukia.Yeye ndiye aliyenifanya mimi kuishi maisha ya namna hii.Simpendi na ninatamani kama siku moja ningekuwa na uwezo ningemuua.”akasema kwa uchungu Naomi huku akilia

“ Basi usilie Naomi .Hili tutalimaliza.Tunachokuomba ni ushirikiano wako.Baba yako kwa sasa yuko katika mahusiano ya kimapenzi na mke wa rais mstaafu.nadhani unalifahamu hilo”
“ Ndiyo ninalifahamu hilo na kuna nyakati huwa wanakuja wote kunitazama” akajibu Naomi

“ Basi Yule mama ndiye kiongozi wa mtandao alimo baba yako.Mambo mengi anayoyafanya baba yako yanaratibiwa na Yule mama kwa hiyo tunataka kuingia ndani ya jumba la Yule mama na kufanya uchunguzi lakni mtu pekee anayeweza kutuingiza humo ni baba yako kwa hiyo tunaomba utusaidie tuweze kumpata baba yako”
“ Mnataka niwasaidiaje? Akauliza Naomi

“ Tunataka uwasiliane naye na kumtaka afike hapa nyumbani haraka sana kwamba una tatizo na akisha fika sisi tutamtia mikononi mwetu na atatupeleka katika jumba hilo la Rosemary kufanya uchunguzi wetu.Wewe tutakuchukua na kukupeleka sehemu salama,tutakutafutia tiba na tutakupatia ulinzi na tutakusaidia kwa kila namna tuwezavyo kuhakikisha kwamba unakuwa na maisha mazuri na ya uhuru” akasema Mathew

“ Kwa kweli natamani sana baba yangu akamatwe na afungwe gerezani maisha au ikiwezekana anyongwe kabisa lakini ninashindwa namna ya kuwasaidia.Kwanza mimi na baba yangu hatuna mahusiano mazuri na siwezi kuwasiliana naye kwa sababu sina mawasiliano yoyote humu ndani.Sina simu wala kitu chochote cha kuniwezesha kuwasiliana na watu huko nje.” Akasema Naomi.Mathew akatoa simu ya Yule mlinzi aliyepoteza fahamu

“ Simu hii ya mlinzi wa getini.Wasiliana na baba yako.Tafuta namna ya kumfanya aweze kufika hapa mara moja” akasema Mathew na Naomi akaishika ile simu huku mikono ikimtetemeka akazitafuta namba za baba yake na kupiga



MPANGO WA MATHEW UTAFANIKIWA ?
 
SEASON 3

SEHEMU YA 38

MTUNZI : PATRICK.CK

Ni saa sita za usiku sasa bado jaji Elibariki chukuswa yuko sebuleni akiendelea kupitia kitabu chake cha sheria .Katika meza ndogo kulikuwa na vitabu vingine zaidi ya saba vya sheria.Aliendelea kufungua ukurasa baada ya ukurasa.Alionekana kuwa na mawazo mengi mno.Wakati akiendelea kupitia kurasa za kitabu kile mke wake akaingia pale sebuleni akiwa na kikombe cha kahawa, akakiweka mezani halafu akainama na kumbusu mumewe.

“ You need to take a rest now.Tommorow is your big day” akasema Flaviana mwanamke mwenye uzuri wa kipekee.Elibariki akakifunika kitabu chake na kumtazama mkewe ,akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kusema

“ Natamani sana nipumzike lakini sina hakika kama nitapata usingizi.”
Mke wake akamuangalia kwa makini halafu akasema
“ Kuna jambo nataka nikuulize mume wangu”
“ Uliza usihofu ”
“ Najua kesi hii ni moja kati ya kesi kubwa na ngumu kwako.Hukumu unayotarajia kuitoa kesho inasubiriwa kwa hamu kubwa sana na umma wa watanzania.Wewe ni jaji na nina imani maamuzi yako utakayoyachukua ni sahihi kabisa,lakini swali langu ni je Yule msichana ana hatia?
Swali lile lilionekana gumu sana kwa jaji Elibariki.Akainama akafikiri kidogo halafu akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kumtazama mkewe.

Hakukuwa na nafasi tena ya kukaa ndani ya chumba cha mahakama kutokana na watu kujaa.Ni siku ya hukumu ya kesi ya mauaji inayomkabili mmiliki wa maduka makubwa ya mavazi ya Penny Fashion,Peniela Salimote.Kesi hii iliyovuta hisia za watu wengi na kuwafanya wafurike ili kuja kusikia hukumu ilikuwa inaonyeshwa moja kwa moja katika runinga.ILikuwa ni kesi ya kwanza kubwa kurushwa moja kwa moja katika runinga.Katika kila kona ya nchi watu walikuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya kesi hii ambayo hukumu yake ilikuwa inasubiriwa na watu wengi.

Ndani ya chumba cha mahakama ilikuwepo familia ya rais ikiongozwa na mke wa rais,Dr Flora Johakim ambaye alikuwa ameambatana na binti zake wawili Flaviana na Anna.Familia ya Edson Kobe kijana anayedaiwa kuuliwa na Peniela nayo ilikuwepo mahakamani hapo ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka.Familia ya Edson na ile ya rais zilikuwa ni familia rafiki kwa muda mrefu sana.Kwa upande wa Penny hakukuwa na ndugu yake yeyote aliyefika mahakamani pale zaidi ya rafiki zake wachache.

Tayari mtuhumiwa amekwisha ingizwa mahakamani na aliyekuwa akisubiriwa ni jaji anayeisikiliza kesi ile aweze kuingia na kuisoma hukumu.Wakati wakimsubiri Jaji aingie,Jason Patrick mwanasheria anayemtetea Penny alikuwa akibadilishana mawili matatu na mteja wake .
“ Jason,kabla hukumu haijaanza ninaomba nikwambie kitu.” Akanyamaza kidogo na kuendelea.

“ Nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.Umenisimamia katika kesi hii kwa kila namna ulivyoweza.Najua chochote kinaweza kikatokea siku ya leo hivyo nakuomba endapo ikitokea nikakutwa na hatia na kufungwa kifungo cha maisha au kifo uhakikishe yale yote niliyokuandikia katika karatasi unayatimiza.Wewe ni zaidi ya rafiki.Wewe ni ndugu yangu pekee ninayekutambua.Ninakukabidhi kila kilicho changu endapo mambo yataenda kinyume na matarajio yetu." Akasema Penny huku machozi yakimtoka
“ Penny naomba usikate tamaa hata kidogo.Nimepambana vya kutosha kuhakikisha kwamba tunashinda kesi hii lakini kama mambo yataenda tofauti na matarajio yetu hautakuwa ni mwisho.Nitapambana hadi nihakikishe haki imepatikana.” Akasema Jason na mara jaji akaingia.

NIMEONA NIWAFARIJI KIDOGO😀😀😀😎😎😎😎😎😉
Unatisha kwa UTANI HUU!
 
Au kama Vipi Tuongezee Speed hii Haitoshi Foleni ni Kubwa

7963b64d5bc33f930a54564907401e9a.jpg


Fanya Week tu LEGE tuko hoi
x=45
 
Hatari sana!!
Mkuu LEGE heshima yako Master!
Ama kweli vitabu vina Siri kubwa sana, tusichoke kusoma [emoji122][emoji122][emoji122]
 
PENIELA

SEASON 4

EPISODE 1


MTUNZI : PATRICK.CK



ILIPOISHIA SEASON 3


“ Elibariki nakushukuru sana kwa kunitoa usingizini.Sikujua kama nina maadui wakubwa namna hii tena walio karibu kabisa na mimi na ambao wangeweza hata kunimaliza sekund e yoyote .Kuanzia sasa wewe ndiye utakayekuwa mshirika wangu mkuu.I’ll give back to you all that I took from you.Nisaidie tuimalize biashara hii na ninakuahidi kwamba uakuwa ni mtu mkubwa sana. kuna jambo ambalo sikuwa nimelifikiria lakini kwa sasa limekuja akilini.I’ll make you the next president of Tanzania”
Jaji Elibariki alibaki mdomo wazi akimkodolea macho Dr Joshua asiamini kile alichoambiwa.

“ Umesema nini mzee? akauliza
“ kwa mambo uliyonifanyia jaji umenifanya nikuthamini ghafla kuliko watu wote kwani bila wewe ningeendelea na mipango yangu yote bila kufahamau chochote na mwisho wangu ungekuwa ni wa aibu kubwa.Ni wewe ambaye nilikuwa nimekuweka katika kundi la adui zangu wakubwa lakini ndiye umekuja na kunifumbua macho.kwa hili ulilolifanya nimesema kwamba nitakufanyia kitu ambacho sikuwa nimekusudia kukifanya.Nitakufanya uwe rais wa jamhuri ya muunganowa Tanzania.” Akasema Dr Joshua.jaji Elibarki machozi ya furaha yakamdondoka.

“ is this true Dr Joshua?
“ Ndiyo Elibarik.Uwezo huo ninao na nitafanya hivyo na hakuna anayeweza kunizuia kufanya hivyo.I’ll make you a very powerfull man in this country na nina hakikani wewe ambaye utaweza kuendelea kuyalinda maslahi yangu.Nilikuwa nafikiria sana ni nani ambaye ninaweza nikampa nchi na akaendelea kuyalinda maslahi yangu lakini nashukuru nimekupata wewe.Nina hakika wewe ni mtu sahihi kabisa na unafaa.”Akasema Dr Joshua.Jaji Elibariki akainuka na kwenda kumpa mkono akamshukuru

“ Dr Joshua sikuwahi kufikiri kuhusu jambo kama hili ! akasema kwa furaha jaji Elbariki
“kwa hiyo kama halikuwa katika ndoto zako anza sasa kuota kwamba umekuwa rais wa Tanzania kwani jambo hili linakwenda kutimia.Nitakuelekeza nini cha kufanya muda utakapofika lakini lazima ukae ukijua kwamba wewe ndiye utakayekuwa rais wa Tanzania baada ya mimi kuondoka madarakani.Lakini pamoja na hayo kuna jambo nataka nikuombe”

“Jambo gani Dr Joshua?
“ Samahani lakini kwa kulisema hili kabla hata hatujamzika Flaviana mkeo lakini ni ukweli ulio wazi kwamba Kwa sasa baada ya Falivana kututoka utabaki mwenyewe na kwa kuwa bado kijana lazima utaoa tena lakini mimi lengo langu kubwa ni kutaka familia yangu iendelee kukaa katika neema ya uongozi kwahiyo basi ninakutaka ujenge mazoea ya karibu na Anna mbaye naye kwa sasa yuko mwenyewe baada ya mpenziwake kufariki.Ninajua umenielewa ninaposema hivyo kwani ninataka utakapokuwa rais yeye awe ni mke wa rais na familia yetu iendelee kutawala.Unalionaje wazo hili? Akauliza Dr Joshua
“ Hilo ni wazo zuri Dr Joshua lakini naomba uniachie kwanza jambo hilo nilitafakari na kulifanyia kazi na nitakupa majibu”akasema Elibarik,.Dr Joshua akafungua mlango na kumuita msaidizi wake akamuomba amuite Dr Kigomba ambaye alifika mara moja .Dr Joshaua akamuangalia kwa macho makali kwa sekunde kadhaa kisha akasema
‘ Kigomba give me your phone” .Huku akishangaa Dr Kigomba akachukua simu yake na kumpatia Dr Joshua.

” Kuanzia sasa hautaitumia simu hii utatafuta simu nyingine.Vua na hiyo saa mkononi”akaamuru Dr Joshua
“ Dr Joshua whats going on? Akauliza Dr Kigomba kwa wasiwasi.

“ Kigomba nadhani umekwisha fahamu nini kinaendelea.Nilikupa kazi ya kumchunguza peniela na badala yake ukaanzisha mahusiano naye.Ulifanya kosa kubwa sana Kigomba”
“ Nani kakueleza habarihizo dr Joshua?
“ Kigomba tayari ninafahamu kila kitu kwa hiyo hakuna haja ya mabishano. Siku zote nimekuwa nkikuonya kuhusiana na udhaifu wako kwa wanawake lakini hukutaka kunisikia.”
“ Dr Joshua sikuelewi una maanisha nini” akasema Dr Kigomba.Dr Joshua akamtazama kwa macho makali na kusema
“ Kigomba unafahamu Peniela ni nani? Unafahamu ni kitu gani alichotufanyia kupitia kwako?
“ hapana Mr President.”akajibu Dr Kigomba

“ Peniela ni nyoka mkubwa na tayari ameunganisha simu yako katika program yao na wanasikia kila kitu unachokiongea kupitia simu yako.Kama hiyo haitoshi alikupa saa hii kama zawadi uivae lakini kwa taarifa yako saa hii imefungwa kifaa maalum ambacho kina uwezo wa kuwaonyesha kila mahala ulipo.Tumshukuru sana Elibariki ambaye ametufumbua macho na kama si yeye tusingeweza kujua chochote kinachoendelea” akasema Dr Joshua.Kigomba alibaki kimya akiwatazama.
“ I’m sorry Mr President,sikuwa ninafahamu lolote kuhusiana na alichokifanya Peniela.” Akasema Dr Kigomba

“ Kigomba mimi na wewe tutakuwa na maongezi yetu baadae lakini kwa sasa naomba nikufahamishe kwamba mipango yetu yote imekwisha gundulika na kama tusipochukua hatua za tahadhari angali bado mapema basi hatutaweza kufanikiwa.Cha kwanza tunachotakiw a kukifanya ni kumuhamisha kwa siri Hussein na ujumbe wake mapema kesho asubuhi na kesho hiyo hiyo jioni kila kitu kikamilike na Hussein aondoke nchini haraka na baada ya hapo tutaendelea na zoezi la kumsaka mtu aitwaye Mathew ambaye huyu ndiye adui yetu mkubwa sana kwa sasa.”akasema Dr Joshua

“Mr President ninaomba niuliz……………”Dr Kigomba akataka kuuliza swali lakini Dr Joshua akamzuia
“ Kigomba hakuna muda wa maswali sasa hivi.Anza sasa hivi kushughulikia hoteli ya kuwahamisha Hussein na ujumbe wake.Tutaongea baada ya mambo yote kukamilika” Akasema Dr Joshua na Dr Kigomba akatoka mle chumbani
Jaji Elibarikina Dr Joshua waliendelea na maongezi na ilipotimu saa tisa za usiku wakaagana.
“ Nenda kalale jaji kesho tuna siku ndefu sana.Kesho tutamzika Flaviana na kisha tutaendelea na mchakato mwingine.Tutaongea zaidi kesho lakini nakushukuru sana jaji.” Akasema Dr Joshua na kumuongoza jaji Elibariki kuelekea katika chumba maalum cha wageni

ENDELEA SEASON 4


Dr Joshua akarejea sebuleni kwake na kuketi sofani akavuta pumzi ndefu halafu akavua koti na kulegeza tai .Alihisi joto .Mambo aliyoelezwa na jaji Elibariki yalimchanganya mno.

“ I’m confused .Totaly confused !!!.... akawaza na kuinuka akaenda katika kabati kulimokuwa na chupa kadhaa za pombe kali akachukua moja akamimina katika glasi akagugumia yote na kukunja sura kutokana na ukali wa pombe ile,halafu akaenda moja kwa moja chumbani kwake ,akavua tai na kuitupa kitandani akasimama kwa sekunde kadhaa akionekana kujawa na mawazo mengi mara ghafla akaibinua m eza kwa hasira na kumwaga kila kilichokiwa juu yake
“ Aaaagghhhh…!!!!” akapiga ukulele kwa hasira huku akihema mfululizo,na uso wake ukiwa umeloa jasho.Mara mlango wake ukagongwa kwa nguvu akainuka na kwenda kuufungua akakutana na sura zenye wasi wasi za walinzi wake.

“ Is everything ok Mr President?..akauliza mmoja wao.
“ I’m fine guys..I’m ok dont worry” akajibu Dr Joshua
“ Are you sure Mr President?

“ Vijana nimewaambia I’m ok..Nimekunywa kidogo pombe kali ili kuondoa mawazo ya kifo cha mwanangu mpendwa .Msijali vijana wangu I’m fine ,so if you’ll excuse me I n eed to be alone” akasema Dr Joshua na kuufunga mlango wake akaketi sofani na kuinamisha kichwa akaweka mikono kichwani
“ Mambo aliyonieleza jaji Elibariki ni mazito na magumu kuyaamini lakini kwa namna alivyonieleza nalazimika niamini ila nimestushwa mno kusikia eti Peniela ametumwa kwangu na kikundi kiitwacho Team SC41 kwa lengo la kunichunguza na kuhakikisha wanakipata kirusi Aby” akawaza na kuivuta akilini sura ya Peniela

“ Hivi kweli Peniela anaweza akanifanyia hivi alivyosema Elibariki ? Sura yake ya kimalaika iliyojaa mahaba haionyeshi kabisa kama ni msichana anayeweza kufanya hayo aliyoyasema Elibariki.Peniela ni mwananmke nnayempenda mno ,tayari ameniin gia katika kila mshipa wa mwili wangu na ndiyo maana inaniwia ugumu sana kuamini maneno aliyoyasema Elibariki juu yake.” Kichwa cha Dr Joshua kikaendelea kuuma kwa mawazo mengi .Akayakumbuka maneno fulani aliyoambiwa na jaji Elibariki
“ Peniela ambaye umekuwa ukimuona kama malaika wako hakupendi hata chembe na ndiye anayeongoza mipango yote ya kukuangamiza.Anatumiwa na Team Sc41 ambao nio waliompa mafunzo na wakamuunganisha kwako makusudi kabisa wakimtumia Captain Amos.Walikuwa na lengo moja tu la kukipata kirusi Aby.Nakuhakikishia tena mheshimiwa rais kwamba Peniela ni mwanamke hatari sana ambaye hana mapenzi yoyote kwako bali anatumiwa kukumaliza.Kama huamini hiki ninachokwambia usichukue hatua zozote na utaona kitakachotokea.Peniela ni nyoka mwenye sumu kali ,anautumia uzuri wake ili kupata kile ambacho yeye na team yake wanakitaka kwa manufaa yao.Amekuwa akiwalaghai kimapenzi watu mbali mbali na mmoja wao ni katibu wako Dr Kigomba”
Dr Joshua akahisi kama vile kichwa kinapigwa na kitu kizito alipoyakumbuka maneno haya ya jaji Elibariki

“ Natamani nisimuamini Elibariki lakini kwa mambo aliyonieleza yananilazimisha nimuamini.Kwanza ni kweli nilimpata Peniela kwa kumpitia Captain Amos.Hakuna aliyekuwa analifahamu hili zaidi yangu na Amos.Kwa Elibariki kulifahamu hili ananilazimisha niamini kuwa kile anachokisema kinaweza kuwa kweli.Kitu kingine ni kuhusu Peniela na Kigomba kuwa katika mahusiano.Sikuwa nikilifahamu hili lakini Elibariki amenifumbua macho na hata Kigomba ameshindwa kukataa mbele yangu kwamba ana mahusiano na Peniela.Kitendo cha kufuatilia mawasiliano ya Kigomba na kujua nyendo zake zote kinanifanya niamini yale aliyonieleza Elibariki yanaweza kuwa kweli.Ni wazi Peniela anahusika katika jambo hili na kama alivyosema Elibariki ni kwamba Peniela anatumia uzuri wake kufanikisha mambo yake.Oh !! Peniela ..Peniela !! Why she did this to me?!! Alinipofusha kwa penzi lake zito nikajiona nimepata malaika kumbe niko na shetani mtoa roho.I’m so stupid to trust her that much.Kwa nini sikuwa mwangalifu na kuligundua hili toka mapema?..Dr Joshua akauma meno kwa hasira

“ Sijui nitampa nini jaji Elibariki kwa jambo hili kubwa alilonifanyia la kuwasaliti wenzake na kuja kunipa siri hizi ambazo zimenitoa katika usingizi mzito ulionifanya nisijtambue kwa kufunikwa na blanketi la penzi la Peniela.Kumbe nilikuwa najikaanga mwenyewe na mafuta yangu bila kujua.Hayakuwa maamuzi mepesi kuwasaliti wenzake na kuja kwangu na kwa hili I must reward him na zawadi kubwa kuliko zote ambayo naweza kumpatia ni kumfanya awe rais ajaye wa Tanzania.” Akasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani

“ Yes ! I will make him a president of Tanzania.Uwezo huo ninao na Elibariki anafaa kabisa.Anaweza akakalia kiti vizuri na zaidi ya yote atakuwa anafuata yale yote nitakayokuwa namuelekeza.Hata kama kuna mambo mengi mabaya nimeyafanya wakati wa uongozi wangu akija mtu kama Elibariki atayafukia yote na nitaendelea kukaa kwa amani na salama nikitumia utajiri wangu.” Akaendelea kuwaza Dr Joshua halafu akamkumbuka Peniela
“ Oh Peniela sijui nikufanye nini pindi nikikuweka mikononi mwangu lakini pamoja na yote uliyonifanyia bado taswira yako imekitawala kichwa changu.Ninahisi yawezekana akawa anatumia uchawi kwani sijawahi kuchanganyikiwa kwa mwanaume yeyote kama alivyonichanganya Peniela namna hii.Ninamuwaza kila dakika japokuwa bado ninahasira naye..” akawaza Dr Joshua na kuanza kukumbuka namna alivyokutana na Peniela



2012 JOHANNESBURG – AFRIKA YA KUSINI


Mkutano mkubwa wa siku sita wa kujadili athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa nchi masikini duniani ulikuwa unafanyika katika jiji la Johannesburg Afrika ya kusini.Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Joshua ambaye alitarajiwa kutoa hotuba katika mkutano huo.
Akiwa jijini Johannesburg Dr Joshua alifikia katika hoteli ya kifahari ijulikanayo k ama four season hotel
Kazi ya kwanza aliyoifanya Dr Joshua akwa jijini Johannesburg ni kukutana na jumuia ya watanzania waishio nchini Afrika ya kusini Katika mkutano na wanajumuiya hao Dr Joshua aliwaasa wakumbuke kuwekeza nyumbani na vile vile kuzingatia sheria za nchi wanakoishi.Kwa upande wao watanzania waishio afrika ya kusini walimueleza rais changamoto wanazokutana nazo nchini afrika ya kusini ambazo rais aliwaahidi kuzifikisha sehemu husika ili zipatiwe majibu.Baada ya mkutano kumalizika Dr Joshua akaondoka akarejea hotelini alikofikia.
Tayari ilikwisha timu saa kumi na moja jioni.
Akiwa chumbani kwake amejipumzisha,Captain Amos daktari wa familia ya rais akaingia

“ Hallow Mr President” Amos akamsabahi Rais
“ Hallow Amos” akasema Dr Joshua .Captain Amos akaiendea chupa ya mvinyo mezani na kumimina katika glasi mbili akampatia moja Dr Joshua

“ Maneno uliyoyaongea katika kikao chako na wanajumuiya ya watanzania waishio afrika ya kusini yamewagusa sana na kwa namna walivyoguswa nina imani yale yote uliyowaeleza watayafanyia kazi.” Akasema Captain Amos
“ Niliona niwakumbushe umuhimu wa kuwekeza nyumbani na kuijenga nchi yao .Wengi wao wakiwa huku nje ya nchi husahau kabisa kwao.Tuachane na hayo, mambo yanakwendaje? Have you found me something? I’m getting bored in here”

“ Tena ni hilo lililonileta kwako mheshimiwa” akasema Amos na kumfanya Dr Joshua atabasamu

“ Tell me the good news Amos” akasema Dr Joshua
“ Good news is that I’ve found you something very special.Utakubaliana nami utakapomuona” akasema Amos
“ Nakuamini Amos.Ukimsifia mwanamke namna hiyo basi ni kifaa hasa.Tell me who is she?
Captain Amos akanywa funda moja la mvinyo na kusema

“ Her name is Peniela.Ni mtanzania ambaye amekuja Afrika ya kusini kibiashara .Anamiliki maduka makubwa mawili ya nguo na urembo.Nakuhakikishia Mr President she’s an angel.Hadhi yake ni ya juu mno .Naamini hata wewe ukimtia machoni utakubaliana nami”
“ Unafahamiana naye? Unamuamini? Unajua sitaki mtu ambaye anaweza kuwa kidomo domo .Si unajua hawa wanawake ikitokea akatembea na rais basi huanzisha matangazo ili ajulikane kila mtaa kuwa anatoka na rais wa nchi”

“ Usihofu kabisa kuhusu hilo mzee.Peniela ni mwanamke ninayefahamiana naye na niamuamini sana.Hana mambo kama hayo ya ajabu ajabu.”

“ Good to hear that then.Nashukuru kwa kunipa uhakika huo.Nakuamini sana Captan na ndiyo maana sijawahi kukuacha katika safari zangu zote za nje ya nchi”

“ Hata mimi nashukuru sana mzee kwa kuniamini na ninatumai sijawahi kukuangusha hata mara moja katika kila kazi unayonipa”
“ Ni kweli Amos hujawahi kuniangusha .Katika safari zote tunazosafiri nje ya nchi umekuwa unaniletea wanawake wazuri wenye hadhi yangu.Nipatapo safari kama hizi za nje ya nchi huwa ni fursa yangu na mimi kujivinjari na watoto wazuri.Kama ujuavyo mama yenu ni mgonjwa sana siku hizi halafu mahaba yamepungua kutokana na umri kwa hiyo ninapokuwa huku nje ninapata nafasi nzuri ya kujivinjari na damu changa.Nashukuru unalifahamu hitaji langu na kila mara umekuwa unaniletea aina ya wanawake ninaowataka” akasema Dr Joshua na Amos akatabasamu

“ Saa tatu za usiku baada ya chakula nitakuwa na maongezi na balozi wetu hapa afika ya kusni kwa hiyo nitamuhitaji Peniela kuanzia saa sita za usiku.Atakapowasili mkabidhi kwa Kareem na yeye atajua namna ya kumleta kwangu” akasema Dr Joshua halafu wakaendelea na maongezi mengne na baada ya muda Amos akaondoka na kumuacha Dr Joshua peke yake.
“ Peniela ..” akasema kwa sauti ndogo huku akitabasamu
“ Jina hili linafanya nijenge taswira ya mwanamke mwenye uzuri zaidi ya tausi.Amos amemsifia sana na kwa sifa zote zile nina hakika uzuri wake utakuwa zaidi ya Cleopatra Yule aliyewahi kuwa mtawala wa Misri ambaye vitabu vinatueleza kwamba alikuwa na uzuri usioelezeka.Halafu kuna kitu nimekuwa nakifikiria kwa muda mrefu.Kadiri siku zinavyozidi kusonga ndivyo mapenzi na mke wangu Flora yanazidi kupungua.Flora hana tena ule mvuto wake wa asili na kutokana na maradh ya moyo yanayomsumbua hana tena ule uwezo wa uweza kuniridhisha kitandani.Japokuwa umri wangu umekwenda lakini bado damu inanichemka na ninao uwezo mkubwa kitandani .Kama ni hivyo basi kwa nini nisitafute mwanamke mzuri mwenye hadhi ambaye atakuwa wangu moja kwa moja? Mwanamke huyo nitakuwa naonana naye kwa siri kila pale ninapokuwa na hamu ya kufanya mapenzi,mwanamke ambaye ataniliwaza na kuniondolea mawazo.Hili niI wazo la msingi na ninatakiwa kulipa uzito wa kipekee.Ngoja nimuone huyo Peniela ni mwanamnke wa aina gani na kama anaweza akanifaa kuwa naye katika mahusiano ya siri.Kama atafanikiwa kuniridhisha na kama ni mwanamke mwenye staha na si wale wanaitwa micharuko basi nitamfanya awe mpenzi wangu wa kudumu.Nitamfanyia mambo makubwa na kufanya aishi maisha ya kifahari “ akawaza Dr Joshua huku akiendelea kupata mvinyo taratibu


SAA SITA USIKU FOUR SEASON HOTEL


Saa sita na dakika saba za usiku gari moja lenye rangi nyeusi likainga katika hoteli ya four seasons .Toka ndani ya gari hilo akashuka daktari wa rais Captain Amos akiwa ameongozana na mwanamke mmoja mwenye uzuri wa kipekee.Alikuwa mwembamba ,mrefu wastani aliyevaa suti nzuri nyeusi iliyomkaa vyema.Moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha rais ambako Captain Amos akakamkabidhi Yule mwanamke kwa Kareem mmoja wa walinzi wa rais.
“ Karibu sana Peniela” akasema Kareem baada ya kutambulishwa.Captain Amos akaondoka na Kareem akamuomba Peniela amfuate.Ulinzi ulikuwa mkali na kila aliyepita eneo lile alipokuwa rais alilazimika kusachiwa kwanza lakini Peniela alipita bila wasi wasi kwa kuwa alikuwa ameongozana na mlinzi wa rais Kareem.Katika mlango wa kuingilia chumba cha rais kulikuwa na walinzi ,Kareem akawapa ishara Fulani nao wakaitika kwa ishara halafu akaufunga mlango na kuingia sebuleni.
Dr Joshua alikuwa peke yake mle sebuleni akitazama Luninga,huku pembeni yake kukiwa na chupa ya mvinyo.Akageuza shingo kutazama mtu aliyeingia mle sebuleni .Kwa sekunde kadhaa akabaki ameduwaa akitazama mlangoni ambako alikuwa amesimama mlinzi wake kareem akiwa na Peniela

“ Oh my Gosh !!!..what a beautifull angel..” akanong’ona Dr Joshua huku akimkazia macho peniela.Alistushwa mno na uzuri wake.
“ Amos wa right.Peniela ana uzuri wa kipekee mno.Katika wanawake wote ambao amekuwa ananiletea kila tuwapo nje ya nchi hajawahi kuniletea mwanamke mzuri kama huyu.This is exactly the the type of woman I want.” Akaendelea kuwaza Dr Joshua huku akimkazia macho Peniela
“ Samahani mzee kwa usumbufu,nimekuletea mgeni.Anaitwa Peniela” akasema Kareem halafu akamgeukia Peniela

“ Peniela huyu ni Dr Joshua ,rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Baada ya utambulisho ule Peniela akatembea kwa mwendo wake wa maringo na kumfuata Dr Joshua akamsalimu kwa adabu.

“ Hallo Mr President” akasema huku akitabasamu
“ Hallo Peniela.Karibu sana.Nimefurahi kukuona”
“ Hata mimi nimefurahi kukuona mheshimiwa rais” akasema Peniela ,halafu Dr Joshua akamgeukia Kareem
“ Kareem ahsante kwa kumfikisha mgeni wangu” akasema na Kareem akaondoka zake.Dr Joshua akaenda katika meza iliyosheheni vinywaji mbali mbali
“ Peniela unatumia kinywaji gani? Akauliza .Peniela akatabasamu na kusema
“ anything that you can choose for me” Sauti laini ya Peniela ikazidi kumpagawisha Dr Joshua.Akachukua chupa ya mvinyo na kumimina katika glasi mbili akampatia moja Peniela

“ Karibu sana peniela.Ninafuraha kubwa mno kuwa nawe kwa usiku huu.Amos alinieleza sifa nyingi juu yako na baada ya kukuona ninakubaliana naye”
“ Amos alikueleza nini kuhusu mimi? Akauliza Peniela

“ Kikubwa alichonieleza ni juu ya uzuri wako.Alinieleza kwamba peniela ni mzuri hata Yule Cleopatra wa Misri hafikii uzuri wako.Baada ya kukuona nakubaliana na kauli yake.You are an angel Peniela” akasema Dr Joshua na kumfanya Peniela atoe kicheko kidogo halafu akasema

“ Thank you”
Dr Joshua akanywa mvinyo funda moja halafu akasema
“ Pamoja na yote aliyonieleza Amos lakini nahitaji kukufahamu zaidi Peniela”

“ Unahitaji kufahamu kitu gani kuhusu mimi Mr President?
“ Just call me Dr Joshua .I need to know everything about you.Your life,relation ship,everything”

“ Why do you wat to know me Mr Presi…..Oh Sorry Dr Joshua? Amos told me its just a one night stand but now it looks like an interrogation” akasema Peniela.Dr Joshua akatabasamu na kusema
“ Usinielewe vibaya Peniela.Ni sawa alivyokueleza Amos ninahitaji mwanamke mrembo kwa usiku wa leo na katika siku hizi chache nitakazokuwa hapa afrika ya kusini kwa mkutano lakini hata hivyo si vibaya kufahamiana zaidi.”
Peniela akanywa funda dogo la mvinyo na kuuliza
“ Don’t you tust Amos?

“ I do trust Amos with my life lakini ukweli ni kwamba nina sababu zangu bnafsi za kutaka kukufahamu kiundani”
“ Can you tell me what are the reasons?
“ The only reason is that I want you to be my woman”
“ Your woman??!” akauliza Peniela
“ Yes my woman” akajibu Dr Joshua

“ Dr Joshua you have a wife so why do you need me to be your woman?

“ Mke wangu ni mgonwa siku hizi na hawezi kunihudumia .Nahitaji huduma za kimwili na kama mke wangu hana uwezo wa kunihudumia basi nalazimika kuzitafuta huduma hizo sehemu nyingine na ndiyo maana nahitaji mwanamke mzuri mwenye hadhi ya kutembea na rais.Peniela nataka uwe mwanamke huyo.Nitakupa kila kitu unachokihitaji katika maisha yako.I’ll make you the most beautifull woman in the world.I’ll give you all luxuries..” akasema Dr Joshua na kunyamaza baada ya Peniela kuangua kicheko.
“ Peniela I’m serious about this.Its not a joke.” Akasema Dr Joshua
“ I know Dr Joshua but if you need love and comfort from me I’m ready to give you but not in exchange for money or anything.Nina kila kitu ninachokihitaji katika maisha yangu labda nilichokuwa nimekikosa ni kutembea na rais wa nchi” akasema Peniela na wote wakaangua kicheko.Dr Joshua akamtazama Peniela kwa sekunde kadhaa na kusema

“ So what do you say Peniela?
“ Say what? Akauliza Peniela
“ Kuwa mpenzi wangu”

“ Naomba unipe muda wa kulifikiri jambo hili Dr Joshua.Unajua kuwa na mahusiano na rais si jambo jepesi kwa hiyo nahitaji kufikiria kwanza kabla sijasema lolote”
“ Are you scared to be in relation with me? Akauliza Dr Joshua na kumfanya Peniela aangue kicheko.
“ Ofcourse I’m scared.You are the most powerfull man in the country so I must be scared.”akasema Peniela.Waliendelea na maongezi mengine na mwishowe wakajikuta kitandani

Dr Joshua akafumba macho baada ya kumbu kumbu ile kumjia kichwani.

“ For the first time in my life I enjoyed sex with her.Sikuwahi kuyafurahia mapenzi hadi nilipo kutana na Peniela.Usiku ule nilipokutana na Peniela ulikuwa ni usiku wangu wa kwanza kuyafurahia mapenzi na Peniela ndiye mwanamke pekee ambaye nakiri kwamba amefanikiwa kunipa penzi lile la kiwango cha juu mno.Ni mwanamke pekee aliyefanikiwa kunichanganya na kuniteka akili.” Akaendelea kuwaza Dr Joshua.



TUKUTANE SEHEMU IJAYO
Nimeweka kambi nitarudi,,,,
 
SEHEM YA 21

maelekezo ya kutomzuia kuingia chumbani kwako kama
kuna
kitu anakitafuta sasa tungewezaje kumzuia ? Alisema
kuna
vitu vya mama yake anakwenda kuvichukua hivyo
tukamruhusu kuingia akachukua alichokitaka.”
“ Oh my God !! alipotoka humu ndani alikuwa
amebeba vitu gani?
“ Alikuwa na masanduku mawili moja kubwa
alilokuwa analikokota na lingine dogo la rangi ya
kama ya
fedha”
Dr Joshua akatoka mbio akawataka walinzi wake nao
wamfuate.Huku akihema kwa nguvu alifika katika mlan
go wa
chubba cha Anna akakinyonga kitasa lakini mlango ul
ikuwa
umefungwa na hakukuwa na dalili zozote za kuwepo kw
a
mtu mle ndani.
“ Vunja mango!! Akaamuru na mmoja wa walinzi
akaurukia teke mlango ukafunguka wakaingia
ndani.Chumba kilikuwa kitupu Anna hakuwemo.Dr Joshu
a
akaanza kupekua kwa fujo kila sahemu na kutupa tupa
vitu
hovyo lakini hakuliona sanduku lenye kirusi.
“ Ametoweka !!! akasema kwa hasira Dr Joshua
akiwa amesimama amejishika kiuno .
“ Siamini eti Anna anaweza akakiiba
kirusi.Yawezekana labda alidhani ni mojawapo ya vit
u vya
mama yake na ndiyo maana akalichkua? Lazima apatika
e
haraka sana.Nahisi atakuwa amekwenda katika nyumba
niliyomjengea kule minazi saba.Ngoja nimfuate huko
huko.Leo nitamsaka kila kona ya jiji mpaka apatikan
e.”
Akawaza Dr Joshua na kuwaamuru walinzi wake waondok
e
waelekee katika nyumba ya Anna eneo la minazi
saba.Alimtaka pia Abel aongozane naye .
Msafara wa rais ulikwenda kwa kasi kubwa na ndani
ya dakika thalathini waliwasili katika nyumba ya An
na
ambayo alijengewa na baba yake.Ilikuwa ni nyumba ku
bwa
ya ghorofa mbili.Geti lilikuwa limefungwa kwa nje n
a
makufuli manne makubwa hali iliyoashiria kwamba
hakukuwa na mtu ndani ya ile nyumba.Dr Joshua akaam
uru
mmoja wa walinzi apande ukuta na aingie ndani akaha
kikishe
kama kweli Anna hayupo.Haraka haraka walinzi watatu
wakapanda ukuta na kuingia ndani na baada ya muda
wakarejea na jibu ambalo liliidi kumchanganya Dr
Joshua,hakukuwa na mtu yeyote ndani ya ile
nyumba.Akajipapasa mfukioni kutafuta simu yake laki
ni
hakuwa nayo akachukua simu ya mmoja wa walinzi wake
akapiga namba za Anna lakini simu ya Anna haikuwa
ikipatikana.Akaamuru warejee ikulu
“ Ni mambo gani haya yananitokea? Nashindwa
kuelewa kwa nini Anna aamue kuchukua lile sanduku ?
Au
yawezekana alihisi kuna fedha ndani yake? Lakini ha
pana
Anna hana tabia hiyo . Kwa nini basi kama alikuwa a
nashida
na fedha asiniambie kuliko kuchukua kitu
asichokifahamu?halafu sanduku lile linafunguliwa kw
a namba
na kwa kuwa hazifahamu namba hizo nina hakika atala
zimika
kulivunja ili kujua kilichomo ndani akifanya hivyo
nina hakika
ataipasua chupa ile yenye kirusi .Nimempoteza mke w
angu
,mtoto na marafiki sasa mwanangu wa pekee aliyebaki
naye
yuko katika hatari ya kuwa mtu wa kwanza kuangamiz
wa na
kirusi Aby.Nitakuwa na furaha gani katika maisha bi
la ya watu
ninaowapenda? Utajiri nilioupata nitautumia na nani
? Juhudi
zote za kupigania utajiri zimekuwa kazi bure,hakuna
tena
furaha bali majonzi tu.Kila kukicha roho za watu zi
napotea
kwa sababu ya kirusi hiki.Nilitegemea leo hii niufu
nge
ukurasa wa kuhusiana nacho lakini badala yake nimeu
fungua
ukurasa mpya.Anna lazima apatikane haraka sana” aka
waza
Dr Joshua huku akitiririkwa na jasho jingi hali ili
yowapa wasi
wasi walinzi wake.
“ Oh Anna !! Anna !! how could she do this to me?
Akajiuliza Dr Joshua
Walirejea ikulu na kwa haraka Dr Joshua akamuita
Abel Mkokasule katika chumba cha maongezi ya faragh
a
“ Abel “ akasema Dr Joshua na kushindwa kuendelea
akainama chini
“ Mzee kuna tatizo gani? Akauliza Abel
‘ Abel..nashindwa hata nianzie wapi”
“ Niambe mzee kuna tatizo gani? Nini kimetokea?
Nimeona mabadiliko ya ghafla.Niambie mzee kuna tati
zo
gani?
“ Abel kuna jambo zito mno limetokea na sijui
nianzaje kukwambia lakini ni wewe pekee kwa sasa am
baye
naamini unaweza kulitatua suala hilokwa haraka”
“ Niambie mzee ni jambo gani hilo? Nakuahidi
kulishughulikia kwa haraka sana”
“ Dr Joshua akainama akafikiri na kusema
“ Mzigo niliotaka kukutuma uupeleke sehemu Fulani
umetoweka katika mazingira tatanishi sana.Jana usik
u
nilikuwa na kikao na wageni katika nyumba yangu kul
e
ufukweni,Anna mtoto wangu akaingia chumbani kwangu
na
kuchukua mzigo huo ambao ni sanduku dogo na ametowe
ka
nalo na sijui mahala aliko.Abel ninakwambia wewe tu
katika
sanduku hilo alilochukua Anna kuna kitu cha hatari
mno
ndani yake,hatari kwake,hatari kwa nchi pia.Yawezek
ana
katika akili yake alidhani labda ndani ya sanduku h
ilo kuna
fedha na atataka kujaribu kulifungua kwa namna anav
yojua
yeye na ikitokea kwa bahati mbaya akaharibu kilicho
mo
ndani we’re all finished.Kwa hiyo Abel nataka kabla
ya saa
nne asubuhi ya leo Anna awe amepatikana na sanduku
hilo
liwe tayari limepatikana .Ninakukabidhi jukumu hili
wewe
kwa kuwa sitaki jambo hili lifahamike kwa watu
wengine.Ninakukabidhi kazi hii nikifahamu kabisa un
ao
uwezo wa kufanya kwa haraka na ufanisi mkubwa.Achan
a
kwanza na mambo mengine yote na uelekeze nguvu kubw
a
kwa sasa katika kumtafuta Anna ambaye ni hatari kus
hinda
hata Kigomba.Chochote unachokihitaji niambie na
nitakupatia” akasema Dr Joshua.
Abel Mkokasule hakutaka maelezo zaidi kwani tayari
alikwisha elewa ni kazi gani anatakwa kuifanya.Alic
hokifanya
ni kuulizwa maswali machache ambayo yangeweza kumpa
mwanga ni wapi anaweza kuanza kumtafutia
Anna.Aliwasiliana na vijana wake wanne anaowaamini
sana
na kuwataka wafike pale ikulu haraka sana.Sehemu ya
kwanza aliyoanzia uchunguzi wake ni katika chumba c
ha
Anna ambako aliamini angeweza kupata kitu chochote
kitakachomuelekeza mahala aliko Anna.Dr Joshua akaa
giza
daktari afike haraka ili apimwe kutokana na mstuko
mkubwa
alioupata
“ Sitaki kabisa kuamini eti Anna anafahamu kilicho
mo
ndani ya lile sanduku na ndiyo maana
akalichukua.Ninachoamini mimi Anna alidhani ndani y
a
sanduku lile kuna fedha nyingi au kitu ha thamani k
ubwa
ambacho anaweza kuuza na kupata fedha nyingi .Kama
alihitaji fedha kwa nini asingenieleza na ningempa
pesa
yoyote anayoihitaji? Utajiri huu wote nilionao ni w
a kwake
,shetani gani kamuingia na kumshawishi afanye hivi
alivyofanya? “ akawaza Dr Joshua huku jasho jingi l
ikiendelea
kumtiririka na alihisi kuishiwa nguvu.
*****************
Kwa takribani dakika kumi Mathew alikuwa amekaa
kitandani akitafakari.Hii ni baada ya kumaliza kuon
gea na
Peniela simuni
“ Lazima nitafute namna ya kufanya ili Dr Kigomba
aweze kunieleza mambo yatakayonisaidia niweze kuufy
eka
kabisa mtandao wote wa Dr Joshua.Nimekwisha
muhakikishia Anna kwamba sintakubaliana na sharti l
a
Kigomba la kumtorosha yeye na familia yake.Kwa kuwa
Dr
Kigomba ana taarifa za muhimu sana ambazo ninazihit
aji
lazima nitafute namna ya kufanya kuzipata taarifa h
izo bila ya
kukubaliana na sharti lake.Hapa lazima nitmie nguvu

Akaendelea kuwaza Mathew
“ Nadhani njia pekee ya kuweza kumfanya Kigomba
akanieleza mambo yote kuhusiana na mtandano wao ni
kwa
kutishia kuiangamiza familia yake.Siku zote linapok
uja suala
la kuangamizwa kwa familia mtu yeyote huwa tayari k
ufanya
jambo lolote kwa ajili ya kuiokoa familia yake.Naam
ini hata
Kigomba hatakuwa tayari familia yake iangamizwe na
atanieleza kila kitu” akawaza Mathew na kuinuka kit
andani
akatoka na kuchukua kisanduku cha huduma ya kwanza
na
moja kwa moja akaelekea katika chumba alimo Dr
Kigomba.Akaufungua mlango na kuingia.Tayari Dr Kigo
mba
alikwisha amka
“ Mathew karibu sana.” Akasema Dr Kigomba huku
sura yake ikionyesha kutokuwa na wasi wasi
wowote.Mathew akaliweka mezani sanduku la huduma ya
kwanza akamtazama Kigomba
“ Unaendeleaje? Akauliza huku akilikagua jeraha la
Kigomba.
“ Naendelea vizuri Mathew.Mungu ananisaidia “
akajibu Kigomba.Mathew akalifungua jeraha lile na
kulisafisha
“ Kigomba mke wako anaitwa nani?
“ Theresa.Anaitwa Theresa”
“ Do you love her?
“ Yes I do” akajibu Kigomba
“ Familia yako wanafahamu kilichokupata?
Uliwataarifu?
“ Hapana sikupata nafasi ya kuwatarifu
kilichonitokea”
“ Good.Ulifanya vizuri .Nina hakika lazima Dr Josh
ua
atakutafuta kwa kutumia familia yako kwani anajua l
azima
familia huwa ya kwanza kuitaarifu pale yanapotokea
masahibu.”
“ Uko sahihi Mathew lazima familia yangu
itaandamwa sana kwa kudhani labda wanafahamu mahala
nilipo”
Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Kigomba your family is in great danger and I’m t
he
only one who can save them right now”
“ Ni kweli Mathew.Niambie nifanye nini ili uiokoe
familia yangu? Akasema Dr Kigomba .Mathew akamalizi
a
kulifunga jeraha halafu akasema
“ Nielekeze walipo nikawatoe na kuwaleta hapa
ambapo ni sehemu salama kwao kwa sasa na halafu
tutaongea zaidi”
Dr Kigomba akamulekeza Mathew nyumbani kwake.
“ Ok Kigomba ninakwenda sasa hivi kuwachukua na
kuwaleta hapa.Dont worry the’ll be safe” akasema Ma
thew
.Dr Kigomba akamuangalia Mathew na kuuliza
“ Mathew why are you doing this?
“ Because you are important to me” akajibu Mathew
na kupiga hatua mbili halafu akageuka
“ One more thing Kigomba.I’m going to help you and
your family escape.Kwa hiyo nitakaporejea nataka uj
iandae
kunieleza kila kitu kuhusiana na mtandao wa Dr Josh
ua
.Endapo nitaridhika na utakayonieleza I swear I’ll
take you
and your family out of the country.” Akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew kwa kulikubali ombi
langu.Nakuahidi kukueleza kila kitu na utapata usha
hidi wa
kutosha wa kumtia hatiani Dr Joshua na wenzake”akas
ema
Dr Kigomba.Mathew akafunga mlango na kutoka.Akatemb
ea
hatua mbili na mara kengele ya getini ikalia
“ Huyu lazima atakuwa ni Peniela kwani ndiye
ninayemtegemea asubuhi hii” akawaza Mathew na kwend
a
kuchungulia katika luninga iliyounganishwa na kamer
a za
ulinzi .Ni kweli aliyekuwa getini alikuwa ni Peniel
a.Mathew
akaenda kufungua geti,Peniela akaingiza gari ndani
na
kushuka
“ Mathew” akasema Peniela baadaya kushuka garini
akamkumbatia Mathew
“ Nimefurahi sana kukuona tena “ akasema
“ hata mimi nimefurahi sana kukuona tena
Peniela.Karibu tena nyumbani” akasema Mathew
,wakaelekea sebuleni
“ Mambo yanakwendaje hapa? Akauliza Peniela
“ Mambo yanakwenda vizuri .Vipi huko ulikotoka
mambo yanakwendaje?
“ Ndiyo maana nimekuja asubuhi asubuhi namna
hii.Mathew kuna mambo mazito mno ambayo unatakiwa
kuyafahamu” akasema Peniela
“ Kabla hujanieleza hayo ya huko naomba kwanza
nikueleze mambo ya hapa” akasema Mathew
“ Ok Mathew tell me the good news” Mathew
akatabasamu na kusema
“ Kubwa la kwanza ni kwamba our mission is
over.Tayari tunacho kirusi Aby”
“ What ??Mathew this is not time for jokes” akasem
a
Peniela
“ It’s not a joke Peniela,its true we already have
the
virus” akasema Mathew
“ Oh My God Mathew..naomba usinidanganye.How
did you get it?
“ Sikudanganyi Peniela.Ni kweli tayari tunacho kir
usi
aby” akasema Mathew na Peniala akamrukia akamkumbat
ia
kwa nguvu
“ Where is it? Can I see it? Akasema Peniela.Mathe
w
akampeleka chumbani kwake akalichukua sanduku lenye
kirusi Aby akalifungua.Peniela akaruka ruka kwa fur
aha na
kutaka kukishika lakni Mathew akamzuia na kulifunga
lile
sanduku.
“ Mathew is this real the Virus?? Akauliza Peniela
kwa mshangao mkubwa
“ Yes it’s the Virus”
“ How did you get it?
“ Ni hadithi ndefu kidogo tutaongea baadae lakini
kwa sasa bado tuna kazi tunatakiwa kuifanya.Awamu y
a
kwanza ya operesheni yetu imemalizika na sasa tunain
gia
katika awamu ya pili ambayo ni kuufyeka mtandao wot
e wa
Dr Joshua na kuwapandisha wahusika wote mbele ya
sheria.Dr Kigomba ni mshirika mkubwa wa Dr Joshua n
a
anaufahamu vyema mtandao wote.Yuko tayari kutoa
ushirikiano wa kutuwezesha kufahamu wahusika wa
Nitarudiii
 
SEHEM YA 40

habari kama ilivyozoeleza,ulipigwa wimbo wa taifa n
a wazi
mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akajitokeza
“ Ndugu zangu watanzania habari za usiku
huu.Nimejitokeza mbele yenu usiku huu kuzungumza na
nyi
kuhusiana na masuala mazito yaliyoikumba nchi yetu
leo.
Ndugu zangu watanzania siku ya leo ni siku ambayo
haitasahaulika katika historia ya nchi yetu.Kumetok
ea
matukio mawili ya mashambulio ya mabomu ambayo
tunaamni yamefanywa na magaidi ambayo yamesababisha
damu ya watanzania wasio na hatia kumwagika.
Tuko la kwanza limetokea saa sita za mchana
ambapo hoteli ya Samawati beach hotel imelipuliwa k
wa
mabomu na idadi kubwa ya watu wamepoteza maisha na
wengine wamejeruhiwa wengi wao vibaya sana ikiwamo
kupoteza kabisa viungo vyao.Miongoni mwa walipoteza
maisha ni raia wa kigeni toka mataifa mbalimbali am
bao
walikuwa wamefikia hotelini hapo.
Baadae mida ya saa tisa za alasiri watu ambao
tunaamini ni magaidi walivamia jengo la kibiashara
la Dar city
shopping mall na kufanya shambulio kubwa ambalo
limesababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.B
ado
hatuna idadi kamili ni watu wangapi walipoteza mais
ha lakini
pindi idadi kamili itakapopatikana tutawafahamisha.
Makomandoo wa jeshi letu walifanikiwa kuingia
ndani ya jengo hilo wakapambana na magaidi hao wali
okuwa
na silaha nzito na kuwamaliza wote.Kwa taarifa nili
zo nazo
mpaka sasa hakuna gaidi hata mmoja aliyebaki hai.Wo
te
wameuawa na uchunguzi unaendelea ili kubaini kama k
una
gaidi yeyote aliyebaki
Wakati magaidi hao wakitekeleza shambulio lao
ndani ya jengo hilo alikuwemo rais wa Tanzania Dr J
oshua
,alikuwemo pia rais mstaafu wa Tanzania Deus Mkozum
i
akiwa na familia yake vile vile alikuwemo binti mfa
lme wa
Saudi Arabia aliyekuja hapa nchini kwa mapumziko ak
iwa
ameongozana na wenyeji wake ambao ni familia ya Deu
s
Mkozumi.
Wanajeshi wetu walifanikiwa kumuokoa rais lakini
kutokana na mapambano makali yaliyotokea kabla ya
wanajeshi wetu hawajafika baina ya walinzi wa rais
na
magaidi ,rais alikuwa amejeruhiwa na ninachukua naf
asi hii
kulitangazia taifa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano
wa
Tanzania Dr Joshua Joakim amefariki dunia wakati
akikimbizwa katika hospitali kuu ya jeshi.Kwa mujib
u wa
taarifa ambazo zimethibitishwa ni kwamba rais msta
afu
Deus Mkozumi na familia yake nao pia ni miongoni mw
a
watu waliopoteza maisha . .
Ndugu watanzania ,taifa letu limepatwa na msiba
mkubwa sana wa kuondokewa na watu hawa muhimu.Lakin
i
pamoja na masahibu hayo makubwa ambayo taifa letu
limeyapata bado kuna jambo lingine limegunduliwa .K
una
kirusi ambacho inasemekana ni hatari sana na kinach
oweza
kusababisha kifo ndani ya kipindi kifupi, na kinach
osambaa
kwa njia ya hewa tayari kimesambaa hewani.Tayari ba
adhi ya
watu waliokuwemo ndani ya jengo la Dar city shoping
mall
wanatajwa kufariki baada ya kuvuta hewa yenye kirus
i
hicho.Tayari timu ya wanasayansi wetu wameanza uchu
nguzi
ili kubaini ni aina gani ya kirusi na namna ya kuwe
za
kukidhibiti.Tayari tumekwisha omba pia msaada wa
wataalamu toka umoja wa mataifa ambao watafika hapa
muda wowote kuanzia sasa ili kusaidia na wale wa kw
etu
katika kukidhibiti kirusi hicho hatari ambacho kina
sambaa
kwa njia ya hewa na huathiri mfumo mzima wa upumiaj
i
.Wakati wanasayansi wetu wakiendelea na uchuguzi
,wanamchi mnatakiwa kuchukua tahadhari za kujiking
a na
kirusi hiki kwa kuziba pua zenu kwa vifaa malum vya
kukinga
pua na mdomo au vitambaa maalum ambavyo mpango
unaandaliwa ili vitolewe bure katika kila hospitali
hapa
nchini. Naziagiza hospitali za mikoa kote nchini ku
tenga wodi
maalum kwa ajili ya wagonjwa watakaokuwa wameathiri
ka
na kirusi hiki
Ndugu zangu watanzania ,pamoja na msiba mzito
tulioupata wa kuondokewa na wapendwa wetu,nawamba
ndugu zangu tuwe watulivu katika wakati huu wa majo
nzi na
kuwaombea wale wote waliopoteza maisha yao katika
mashambulio ya leo wakiwamo viongozi wetu wakuu wa
kitaifa.Pamoja na mashambulio haya napenda
kuwahakikishia kuwa nchi yetu bado iko salama na ms
iwe na
hofu yoyote.Majeshi yetu ya ulinzi na usalama yako
macho
usiku na mchana kwa kulinda mipaka yetu na kuzuia k
ama
kuna mashambulio mengine yamepangwa kutokea hapa
nchini.Tumeshambuliwa na damu ya watanzania wasio n
a
hatia.Tutapambana na yeyote aliyemwaga damu za
watanzania awe mkubwa ama mdogo.Tutachukua hatua
dhidi ya mtu,kikundi au taifa lolote lililoshiriki
katika
kupanga,kufadhili,au kusaidia kwa namna yoyote ile
katika
shambulio la leo.
Natangaza siku kumi na nne za maombolezo ya
kitaifa na katika siku hizo zote bendera zitapepea
nusu
mlingoti.Mtakuwa mkipokea taarifa kupitia vyombo vy
a
habari kuhusu kile kinachoendelea .
Mwisho kabisa narudia kuwaomba ndugu watanzania
tuendelee kuwa watulivu,tudumishe amani na mshikama
no
katika kipindi hiki kigumu bila kusahau kujikinga d
hidi ya
kirusi Aby
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza”
Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
alihitimisha hotuba yake kwa taifa.Kilichofuata baa
da ya
hotuba hiyo ilikuwa ni nyimbo za maombolezo.Baada y
a
kutoa hotuba ile kwa taifa waziri mkuu akaingia kat
ika katika
kizito cha baraza la usalama la taifa ili kujadili
matukio
yaliyotokea na hali ya usalama wa nchi.Kwa kuwa Mat
hew
alikuwa na taarifa nzito na nyeti kwa usalama wa nc
hi,waziri
mkuu alimualika ashiriki katika baraza lile ili vio
ngozi wengine
waweze kufahamu kwa undani nini hasa kilichotokea n
a
kinachoendelea hapa nchini
****************
Kikao cha baraza la usalama wa taifa kilimalizika
saa
nane za usiku.Uwepo wa Mathew katika kikao hiki uli
kuwa na
umuhimu mkubwa sana kwani ni pekee aliyekuwa
anafahamu mambo mazito yaliyokuwa yanafanywa kwa si
ri
na mtandao wa Dr Joshua.Baada ya kumalizika kwa kik
ao kile
ilikuwa taarifa kuwa katibu wa rais Dr Kigomba amep
atikana
akiwa ndani ya mojawapo ya magari yaliyokuwapo kati
ka
maegesho ya jengo la Dar shoping mall wakati vikosi
vya jeshi
vilikuwa vinafanya upekuzi katika magari yaliyoeges
hwa
katika maegesho ya jengo lile.Taarifa ile ilisema k
wamba
baada ya kupelekwa hospitali Dr Kigomba amepimwa na
amegundulika hana maambukizi ya kirusi Aby kwani nd
ani ya
gari alikuwa amefungwa kitambaa puani na mdomoni
ambacho ndicho kilichomsaidia asiweze kuathiriwa.Ta
arifa
nyingine ilisema kuwa Abel Mkokasule naye vile vil
e
amekamatwa kufuatia agizo la waziri mkuu.
Mathew aliondoka maeneo ya ikulu akiwa na ulinzi
aliopewa akaelekea moja kwa moja hospitali kufatil
ia hali ya
Peniela .Jiji la Dar kwa usiku huu lilikuwa kimya k
abisa .Ni
magari ya polisi tu yaliyoonekana kuranda randa kat
ika mitaa
mbali mbali yakifanya doria.
Haikumchukua Mathew muda mrefu kufika hospitali
kutokana na kutokuwapo magari barabarani.Alipokewa
na
Edmund na Chin sun ambao hadi muda huo hawakuwa
wamelala.
“ pole sana Mathew “ akasema Edmund na
kumueleza Mathew kilichoendelea wakati hayupo.Edmun
d
alimfahamisha Mathew kuwa upasuaji ulimalizika na
madaktari walisema kwamba ulikuwa na
mafanikio.Madaktari walifanikiwa kuyaokoa maisha ya
Peniela na kwa muda huo aliwekwa katika chumba maal
um
huku madakari wakiendelea kufuatilia hali yake kwa
karibu
“ Ahsante Mungu” akasema Mathew na kushusha
pumzi
Ulikuwa ni usiku mrefu sana kwao wote
watatu.Waliongea mambo mengi yanayohusiana na maish
a
yao mapya wanayotarajia kuyaanza lakini kikubwa zai
di
walifanya maombi maalum kumuombea Peniela
WIKI TATU BAADAE
Habari kubwa iliyotawala vyombo vyote vya habari
dniani kote siku hii ya alhamisi ni ile ya shirika
la afya duniani
kuithibitisha na kuizindua rasmi kinga ya kupambana
na kirusi
Aby.Toka kirusi Aby kiliposambaa na kusababisha maa
fa
makubwa ,makampuni makubwa ya kutengeneza dawa
walichukua sampuli ya damu ya Peniela ambaye ndiye
pekee
aliyekuwa na kinga dhidi ya kirusi Aby na wakafanik
iwa
kutengeneza kinga ambayo baada ya kufanyiwa majarib
io
ilifanya kazi vizuri. Kwa sababu dawa hiyo ilitokan
a na kinga
iliyochukuliwa toka mwilini mwa Peniela wanasayansi
waliamua kumpa heshima ya kipekee na kuiita kinga h
iyo
yenye uwezo mkubwa wa kupambana na kirusi Aby ,Peni
ela.
Kirusi Aby tayari kilikwisha sambaa katika sehemu
kubwa ya dunia na maelfu ya watu tayari walikwisha
poteza
maisha .Kupatikana kwa dawa ya Peniela ilikuwa ni h
abari
njema kwa dunia nzima.Uzinduzi wa dawa ya Peniela
ulifanyika nchini Tanzania na kuhudhuriwa na viongo
zi wa
mataifa zaidi ya sabini
Peniela ambaye kwa sasa hali yake ilikuwa
inaendelea vizuri kutokana na upasuaji mkubwa aliof
anyiwa
alichukuliwa kutoka hospitali na kupelekwa katika u
kumbi
zilimofanyika sherehe za uzinduzi wa dawa hiyo akiw
a
ameongozana na Mathew.Watu wote wakasimama na
kuwapigia makofi.Walitembea katika zuria jekundu hu
ku
wakipunga mikono kuwasabahi viongozi wale wengi
waliohudhuria uzinduzi ule mkubwa wa dawa iliyosubi
riwa
kwa hamu kubwa na mamilioni ya watu duniani. Viongo
zi
mbali mbali walitoa hotuba zao na kisha tukio kubwa
lililokuwa linasubiriwa likafuata.Dawa ya Peniela i
kazinduliwa
rasmi.Lilikuwa ni tukio kubwa kuwahi kutokea nchini
Tanzania ambalo lilirushwa dunia nzima.Peniela alig
euka
kuwa mtu maarufu mno duniani kwani jina lake lilita
jwa
katika kila kona ya dunia.Mikataba aliyoingia na ma
kampuni
makubwa ya kutengeneza dawa duniani ilimuingizia pe
sa
nyingi mno na kumfanya aingie katika orodha ya watu
matajiri duniani.
Baada ya kukamilika kwa uzinduzi ule Peniela
hakurejea tena hospitali bali walielekea katika mak
azi ya
akina Edmund ambako Mathew alikuwa akiishi kwa sasa
.
Baada ya mapumziko mafupi wote wakakusanyika sebule
ni.
“ Peniela “ akaanzisha maongezi Mathew
Nitarudiiii
 
Dope! Ila mwisho sijaenjoy Peniela kuwa na Mathew, that's all...
 
Dah nimevutiwa na maelezo yako ndugu, Basi nakukaribisha ukisome kitabu cha Hidden Truth nakirusha humu Jamii Forum hivyo kifatilie ndio Kwanza Msimu wa Kwanza sehemu ya 1 (A)
Vp ulikiachia humu?
 
Dope! Ila mwisho sijaenjoy Peniela kuwa na Mathew, that's all...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Penielaa katengeneza historiaa ya ajabu sanaaa dah..
 
Back
Top Bottom