MACHO YA PAKA
JF-Expert Member
- Feb 24, 2015
- 205
- 475
PENIELA SEASON 3
EPISODE 8
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Padre alitumia zaidi ya dakika hamsini ndani ya chumba cha John.Walionekana kuongea na baadae akamuombea na kumpaka mafuta usoni baadae Padre akatoka.
“ Ndugu zangu kama nyote mnavyofahamu kwamba kutokana na ugonjwa wake ndugu yetu hatakuwa na maisha marefu sana kwa hiyo basi nimempatia huduma ya mwisho kabla ya mwenyezi Mungu kumuita.John Mwaulaya amekubali kwa hiari yake kubatizwa na amekuwa mpya tena . John ametubu dhambi zake zote na kwa mamlaka niliyopewa na kanisa nimemuondolea dhabi zake. Amepokea komunyo takatifu na Yesu yuko ndani yake.Kwa sasa hata kama akiitwa na Mungu dakika yoyote tuna hakika atakuwa sehemu salama.Kitu cha msingi ni kuzidi kumuombea ili hata atakapoondoka katika maisha haya aweze kupokelewa Mbinguni” akasema Padre na kuwabariki wote kisha Peniela akamrudisha nyumbani kwake.
ENDELEA…………………
Mlio wa simu ulimstua Mathew toka usingizini .Haraka haraka akaichukua simu yake na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Eva
“ Hallow Eva? Akasema Mathew
“ Mathew habari za asubuhi? Bado umelala?
“ Ahsante sana kwa kuniamsha Eva.Nilikuwa katika usingizi mzito sana.Kuna habari gani? Akauliza Mathew
“ Mathew nimekupigia kukupa taarifa kuhusiana na ile kazi uliyoniomba nikufanyie.Kuna kitu cha ajabu ambacho kimetokea na kunishangaza sana.Hakuna taarifa zinazoonyesha mawasiliano ya simu ya wale wazee kwa muda wa miezi sita ya mwisho kabla hawajauawa.Taarifa hizo zimefutwa kabisa katika kumbu kumbu kwa hiyo ni vigumu kufahamu walikuwa wakiwasiliana na akina nani kabla hawajafariki.Hii imenishangaza sana Mathew.” Akasema Eva.Mathew akakaa kimya kidogo na kusema
“ Thank you Eva.
“Kuna chochote kingine nikusaidie? Akauliza Eva
“ No thank you Eva.Nikihitaji msaada tena nitakujulisha.Ila nashukuru sana kwa msaada huu mkubwa” akasema Mathew na kukata simu.
“ Kwa miezi sita hakuna taarifa za mawasiliano ya simu za wazee wale.Ni wazi taarifa hizi zimeondolewa makusudi kabisa na lengo hapa ni kumficha Yule mtu ambaye alikuwa nyuma yao.Watu hawa wako makini sana kwani walifahamu fika uchunguzi ungefanyika na yangefuatiliwa mawasiliano kati ya wazee wale na mtu huyo angefahamika na ndiyo maana wakawahi kufuta kabisa kumbu kumbu zote za mawasiliano .Lakini hata hivyo kuna njia nyingine ya kuweza kumfahamu mtu huyo ni nani.Ngoja turudi sasa katika lile wazo la Anitha la kumchunguza Habib ambaye anatajwa kutaka kununua karatasi zile.Nina hakika kupitia yeye basi tunaweza kugundua jambo Fulani.Nina rafiki yangu katika shirika la ujasusi la C.I.A yeye anaweza akanisaidia sana katika jambo hili kwani C.I.A wamejipenyeza karibu kila kona ya dunia na ni rahisi sana kumfuatilia mtu yeyote Yule” akawaza Mathew na kutoka mle chumbani.Tayari Anitha alikwisha amka kitambo na alikuwa jikoni akiandaa mlo wa asubuhi.Mida hiyo ilipata saa moja na dakika kumi na saba za asubuhi
“ Hallow Anitha” akasema Mathew huku akifungua kabati na kutoa chupa ya mvinyo akamimina kidogo katika glasi akagugumia yote.Anitha akamtazama na kusema
“ Is something bothering you? I know you.Ukinywa mvinyo kama hivyo lazima kuna jambo linalokusumbua.” Akasema Anitha
“ nataka kuchangamsha mwili tu ,naona umechoka sana” akajibu Mathew.Anitha akaacha shughuli aliyokuwa akiifanya akamtazama Mathew na kusema
“ Ulionana na John jana? Anaendeleaje? Alikuitia jambo gani? .
Mathew akaongeza tena mvinyo katika glasi akanywa na kusema
“ Nothing important.Hali yake si nzuri na kwa mujibu wa uchunguzi wa madaktari john anasumbuliwa na saratani ya ubongo kwa hiyo hakuna tegemeo la kupona.Aliniita na kuniomba msamaha kwa kitendo kile cha kuiteketeza familia yangu vile vile akanitaka nimlinde Peniela na kuhakikisha anakuwa salama siku zote.Thats all” akasema Mathew na kunywa funda lingine la mvinyo.
“ Anything from Kigomba? Akauliza Mathew
“ hakukuwa na simu ya maana aliyopiga tena zaidi ya kuwapigia simu waanwake wawili na akamuahidi mmoja wao kwamba anakwenda kulala kwake.Vile vile alimpiga simu mke wake na kumweleza kwamba hataweza kurejea nyumbani usiku ule kutokana na kuwa na kikao kizito.Kigomba anaonekana ni mpenda wanawake sana.”akasema Anitha
“ Usimweleze jaji Elibariki chochote kuhusiana na simu hizo za Kigomba alizowapigia wanawake wengine,si unajua anavyompenda peniela.By the way Eva amenipigia simu muda si mrefu na amenipa taarifa kuhusiana na kazi ile niliyomuomba anisaidie kuifanya.Hakuna kumbu kumbu zozote za mawasiliano za wazee wale kwa miezi sita kabla ya kufariki kwao.Zimefutwa kwa makusudi kabisa kwa ajili ya kumficha huyo ambaye walikuwa wakiwasiliana naye.Kwa sababu hiyo basi tunarejea katika lile wazo lako la kumchunguza Habib ambaye anatajwa kutaka kuzinunua karatasi zile.”akasema Mathew
“ Nina rafiki yangu mmoja anafanya kazi katika idara ya ujasusi ya marekani C.I.A.Nina hakika anaweza akatusaidia katika suala hili.” Akasema Mathew halafu akaongozana na Anitha hadi ofisini na kumpigia simu huyo rafiki yake afanyaye kazi katika shirika la ujasusi la marekani.Baada ya sekunde kadhaa mwanadada mmoja akaonekana katika luninga kubwa iliyokuwa ukutani.
“ hallow Mathew” akasema mwanadada Yule mwenye asili ya afrika
“ hallow Kerry.habari za siku ?
“ habari nzuri sana .habari za Tanzania?
“ Tanzania kwema.Samahani kwa kukusumbua Kerry,ninashida naomba unisaidie”
“ Bila samahani Mathew.Nikusaide nini?
“ Kuna mtu mmoja ambaye ninahitaji unisaie kumchunguza.Anaitwa Habib soud ni raia wa Saudi Arabia.Ninataka kufahamu kama ana mawasiliano na mtu yeyote kutoka Tanzania.Kuna jambo ninalichunguza na yeye amejitokeza katika picha .Najua ni kinyume na taratibu zenu za kazi lakini naomba unisaidie Kerry,Ni muhimu sana kwangu” akasema Mathew..Kerry akaonekana kufikiri kidogo kisha akasema
“ sawa Mathew nitakusaidia.Nisubiri dakika mbili.”akasema Kerry na kukata simu
“ Unapofanya kazi kama hizi kuna ulazima wa kuwa na marafiki wengi toka katika mashirika mbali mbali ya kijasusi na kipelelezi duniani ili unapohitaji taarifa Fulani basi inakuwa rahisi sana kuipata.Mimi nina marafiki karibu katika mashirika mengi makubwa ya ujasusi duniani.C.I.A,KGB,MOSSAD,MSS la china,BND ujerumani,MOIS Iran,na mengine mengi” Akasema Mathew na mara Kerry akarejea hewani
“ Mathew huyu Habib Soud ni mtu ambaye amekuwa katika orodha ya watu wanaochunguzwa na C.I.A kwa kufadhili vikundi vya kigaidi.Habib ana utajiri mkubwa sana na inasemakana anautumia utajiri huo katika kufadhili ugaidi.Baba yake alikuwa ni mfadhili wa siri wa Alqaeda na aliuawa na vikosi vya Marekani .” akasema Kerry na kusogeza tena taarifa nyingine katika tablet yake.
“ C.I.A tumekuwa tukimfuatilia pia mawasiliano yake .kwa upande wa Tanzania taarifa zinaonyesha kwamba amekuwa na mawasiliano ya mara na mtu mmoja anaitwa Rosemary Mkozumi.Huyu aliwahi kuwa mke wa rais wa Tanzania na ana taasisi yake inayojishughulisha na miradi mbalimbali ya kuwawezesha akina mama kiuchumi .Kupitia taasisi hii amekuwa akipata wadhili toka sehemu mbali mbali duniani na mmojawapo wa wafadhili wa taasisi hii ni Habib.Amekuwa akitoa pesa nyingi kama misaada kwa taasisi hii kwa dhumuni la kuwawezesha wanawake kiuchumi.Habib anafanya hivi ili kuificha ile dhana kwamba anafadhili makundi ya kigaidi.Mathew hizo ndizo taarifa ninazoweza kukupa kwa sasa kuhusiana na habib.Sisi bado tunaendelea kumchunguza na kama kuna lolote ambalo unaona linaweza likatusaidia katika kupata ushahidi wa kutosha kuhusu Habib kujihusisha na makundi ya ugaidi basi naomba unitaarifu mara moja na endapo utahitaji tena msaada wowote mimi niko tayari kukusaidia muda wowote.” Akasema Kerry
“ Kerry nakushukuru sana kwa msaada wako huo mkubwa.Endapo nitapata jambo lolote la kumuhusu Habib katika uchunguzi wangu nitakutaarifu mara moja” akasema mathew na kuagana na Kerry akata simu.Muda huo huo jaji Elibariki akaingia mle ofisini
“ Kuna taarifa yoyote mpya imepatikana? Akauliza jaji Elbarki
“ Ndiyo jaji.Kuna taarifa tumezipata .Kwanza ni kutoka kwa Eva.hakuweza kupata taarifa zozote za mawasiliano za mzee Mustapha na Ktwana.Inaoenaka zimefutwa kabisa kwa makusudi.Tumewasiliana na trafikiyangu mmoja aanayefanya kazi katika shirika la ujasusi la marekani na ametutaarifu kwamba mtu ambaye alitajwa kutaka kuzinunua karatasi zile zilizoibwa ikulu Habib soud amekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Rosemary Mkozumi mke wa rais mstaafu Deus Mkozumi.Amekwenda mbali zaidi na kusema kwamba Habib amekuwa akiifadhili taasisi inayoongozwa na bi Rosemary kwa kuimwagia mabilioni ya fedha .” Mathew akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“ Jana tumemsikia Dr Joshua akimtaja adui yake namba moja katika mpango wa kuiuza package ni Deus mkozumi.Leo tena tunasikia kwamba mke wa Deus mkozumi anapokea mamilioni ya fedha toka kwa mtu anayedaiwa kuufadhili ugaidi.Hapa kuna picha inajengeka.Ninapata picha kwamba package hiyo anayotaka kuiuza Dr Joshua ilikuwepo hata wakati wa uongozi wa Deus na anaifahamu fika na ndiyo maana amekuwa kinyume na mpango wa Dr Joshua wa kutaka kuiuza.Pili nina hakika kabisa kwamba hata hizo karatasi zilizoibwa zilikuwepo ikulu wakati wa uongozi wa Deus na nina hakika kabisa kwamba Rosemary kwa kuwa naye alikuwepo ikulu wakati huo alifahamu uwepo wa karatasi hizo.Ninaweza kutamka bila wasi wasi kwamba Rosemary ndiye aliyekuwa nyuma ya mpango wa kuziuza karatasi zile.Kumbu kumbu za mawasiliano za mzee Kitwana na mzee Mustapha zimefutwa kwa sababu ya kumficha ili asijulikane kama alikuwa akiwasiliana nao.” Akasema Mathew akawaangalia akina Anitha na kusema
“ kama Habib anashukiwa kuufadhili ugaidi basi ni wazi alihitaji sana karatasi zile ili kuweza kuzitumia kanuni zilizomo ndani yake katika kutengeneza kirusi hicho hatari ili kitumike katika mashambulio ya kigaidi.Hii ni sababu pekee ambayo ilimfanya Habib kutaka kuzinunua karatasi zile kwa mabilioni ya fedha.Mnaona namna picha inavyojengeka? Akauliza Mathew
“ Nakubaliana nawe kabisa Mathew.Maelezo uliyoyatoa yanatoa taswira ya wazi ya namna Rosemary Mkozumi alivyohusika katika uibwaji wa karatasi zile ikulu.Kwa mantiki hiyo basi Rosemary naye atakuwa ni mtu wa muhimu sana kwetu .Kuna mambo mengi ambayo tutahitaji kuyafahamu kutoka kwake.” Akasema Anitha
“ Jamani kuna jambo na mimi naomba niliseme.” Akasema jaji Elibariki
“ Ninamfahamu huyu Rosemary Mkozumi .Alikuwa ni mke wa rais mstaafu Deus Mkozumi lakini baada ya Deus kumaliza awamu yake ya pili ya uongozi walitengana.Hakuna sababu iliyowekwa wazi kuhusiana na kutengena kwao.Rosemary anamiliki jumba kubwa la kifahari ufukweni mwa bahari na vile vile anamiliki pia biashara nyingine nyingi kubwa kubwa.Ni mwanamke tajiri na mpaka sasa haijawekwa wazi utajiri wake ameupataje.Ninaweza kukubaliana na maneno ya mathew kwamba Rosemary aliingiwa na tamaa ya pesa na akaamua kusuka mpango wa kuziuza karatasi zile. Edson alitumiwa tu katika kuziiba lakini maelekezo yote yalitoka kwa Rosemary.” Akasema jaji Elibariki na mara ikasikika kengele ya getini.
“ Ngoja nikaangalie nani anagonga” akasema Mathew na kutoka
“ Is Mathew ok? Akauliza jaji Elibariki baada ya Mathew kutoka.Aligundua kwamba Mathew hakuwa sawa.
“ There is must be something bothering him.Jana usiku alipigiwa simu na peniela kwamba john Mwaulaya anamuhitaji.Aliondoka na kwenda hospitali kuonana na John.Nimemuuliza ni kitu gani John alichomuitia lakini bado hajanipa jibu la kweli.Amekuwa akificha ficha.Ninamfahamu Mathew ,kuna jambo aliambiwa na John” Akasema Anitha
“ Umesema alikwenda kuonana na John mwaulaya? Jaji Elibariki akashangaa
“ ndiyo alikwenda kuonana naye jana usiku na….” kabla Anitha hajaendelea akaingia Mathew akiwa ameongozana na peniela.Jaji Elibariki na peniela walipoonana wakajikuta wakikumbatiana kwa nguvu na kupeana mabusu
“ Are you ok my love?akauliza jaji Elibariki
“ I’m ok Elibariki.What about you,are you ok?
“ I’m ok peniela” akasema jaji Elibariki .Anitha na Mathew wakatazamana wakatabasamu
“ karibu sana peniela” akasema Mathew
“ Ahsante sana Mathew.mambo yanakwendaje hapa?
“ mambo yanakwenda vizuri .Anaendeleaje John? Akauliza Mathew
“ Bado hali yake si nzuri.Jana ulipoondoka hali ilizidi kuwa mbaya akaomba tumtafutie padre.Tulifanikiwa kumpata Padre kwa usiku ule na akampatia huduma ya kiroho kumuandaa kwa lolote linaloweza kutokea.Nimeondoka kule saa kumi na moja alfajiri bado hali yake haikuwa nzuri.Nimewapigia tena simu madaktari kabla sijaja huku na wakaniambia kwamba kwa sasa hali yake imezidi kuwa mbaya .Anything can happen at anytime.” Akasema peniela na chumba kikawa kimya.Mathew akauvunja ukimya
“ Tuko pamoja Peniela katika wakati huu mgumu” jaji Elibariki na Anitha wakamuhakikishia peniela kwamba wako pamoja naye pia
“ Ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu.Nimepita hapa ili kufahamu ni kitu gani kinachoendelea kwani toka jana hatukuwasiliana.Vipi ule mpango wetu ulifanikiwa? Akauliza Peniela
“ Ulifanya kazi kubwa sana jana na kila kitu kimeenda vizuri kama tulivyopanga Tayari tunaweza kufuatilia kila kinachofanyika katika simu ya Dr Kigomba.Mfano jana tumeweza kusikia maongezi yote aliyoongea na Dr Joshua akiwa afrika ya kusini.Vile vile tunaweza kufahamu kila mahala aliko Dr Kigomba endapo atakuwa ameivaa ile saa” akasema Anitha na kumuelekeza Peniela namna program ile inavyofanya kazi.Akayafungua maongezi ya simu kati ya Dr Kigomba na Dr Joshua na wote kwa pamoja wakayasikia.
“kumbe Yule mzee ni mtu katili sana.Amekwenda afrika ya kusni shingo upande.Kwake yeye fedha ni muhimu sana kuliko uhai wa binadamu tena mtoto wake mwenyewe” akasema peniela kwa hasira
“ kwa mujibu wa maongezi yao inaonekana wanajiandaa kuifanya biashara hii haraka iwezekanavyo.Alimuachia Dr Kigomba jukumu la kuhakiki kama fedha tayari imekwisha ingia katika akaunti zao za siri nje ya nchi na mara tu wakihakikisha kwamba fedha yote imelipwa basi wataikabidhi hiyo package.Mtu wa muhimu na wa kuchunga sana hapa ni Dr Kigomba kwani ndiye atakayefanya makabidhiano kwa niaba ya Dr Joshua Kwa vile tayari tuna uwezo wa kumfuatilia Dr Kigomba .Peniela unatakiwa ukae karibu sana na Dr Kigomba.Ongeza ukaribu pia na Kaptain Amos ambaye mko naye team SC41 na yuko timu moja na akina Kigomba .Katika team SC41 mmejipanga vipi katika kuichukua hiyo Package? Akauliza Mathew
“ Jana walikuja watu watano kutoka makao makuu ya team SC41 Marekani na dhumuni lao kubwa ni kuja kusimamia suala hilo la uchukuaji wa hiyo Package na kuondoka nayo.Leo kutakuwa na kikao cha watu wote wa team SC41 kwa ajili ya kuweka mikakati ya mwisho kuhusiana na package hiyo.Team SC41 wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaipata package hiyo na katika operesheni hiyo wanatutegemea sana sisi wawili mimi na captain Amos.
"
“ Mpaka sasa hivi hujafanikiwa kufahamu kilichomo ndani ya hiyo Package? Akauliza Anitha
“ Hapana bado.Mpaka sasa hakuna ajuaye ndani ya hipo package kuna nini.Nmejaribu kuwadadisi wale jamaa waliotoka Marekani lakini hawako tayari kuweka wazi.”
“ Ok vizuri.Basi utaendelea kutufahamisha mipango yote ya team SC41 kuhusiana na package hiyo Kitu cha muhimu sana kuzingatia jihadhari wasije wakagundua kwamba unashirikiana nasi” akasema Mathew
“ Ninalifahamu hilo na niko makini sana katika kuhakikisha kwamba hawagundui lolote.Hata nijapo huku huwa ninatumia mbinu za hali ya juu sana. Ili nisiweze ku…..” Peniela akastushwa na mlio wa simu yake.Akaitazama ikiita akaogopa kuipokea.
“Mbona hupokei simu? Akauliza Mathew
‘ Its Josh.Yuko kule hospitali” akasema Peniela kwa wasi wasi
“ Pokea ufahamu anataka kukwambia nini.Yawezekana ana jambo la muhmu sana la kukwambia”akasema jaji Elibariki .Peniela akabonyeza kitufe cha kupokelea na kuweka simu sikioni
“ hallow Josh ” akasema.Zikapita sekunde kadhaa bila ya Josh kuongea kitu
“ Josh are you there? Akauliza peniela
“ Peniela where are you? Akauliza Josh
“ Josh kuna nini?
“ Naomba uje mara moja hapa hospitali” akasema Josh na kukata simu.Peniela akapatwa na wasiwasi mwingi
“ Is everything ok peniela? Akauliza Mathew
“ Josh ananitaka nifike haraka hospitali .Sijui kuna nini.I’m so scared.”akasema Mathew
“ Usiogope peniela .Yawezekana kuna jambo la msingi analokuitia..I’ll take you there.” Akasema Mathew
“ No thank Mathew I can manage” akasema peniela
“ Peniela uko katika mstuko na ni hatari sana kuendesha gari ukiwa katika hali hiyo.Naomba usiweke ubishi katika hilo.Nitakupeleka hospitali.Anitha endelea kumfuatilia Dr Kigomba na kama kuna jambo lolote la dharura utanitaarifu mara moja” akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akavaa kisha akaongozana na Peniela akamuendesha kuelekea hospitali.
“ Anitha ninakubaliana nawe kwamba mathew leo hayuko sawa sawa.Kuna jambo linalomsumbua kichwa chake.” Akasema jaji Elibariki.
“ Ninavyofahamu mimi,Mathew na John Mwaulaya ni maadui wakubwa.Ni John mwaulaya aliyeiteketeza familia ya Mathew.Siku zote Mathew alikuwa akitafuta nafasi ya kulipiza kisasi kwa John Mwaulaya na ndiyo maana aliponiambia kwamba John amemuita hospitali nilistuka sana .Lakini tumuache kwanza atulie na atatueleza “akasema Anitha
Mathew na Peniela wakawasili hospitali.Safari yao haikuwa na maongezi mengi kwani Peniela alionekana kuzama katika mawazo na Mathew hakutaka kumsumbua
“ Mathew ahsante sana .Ulikuwa sahihi.Nisingeweza kuendesha gari kwa hali hii.Miguu inanitetemeka ” akasema Peniela huku akifungau mlango na kushuka wakaelekea katika jengo alikolazwa john.Mtu wa kwanza kuonana naye alikuwa ni Josh.Macho yake yalionekana kuwa mekundu .Peniela akazidi kujawa na wasi wasi.Josh alipomuona akamfuata na kumkumbatia
“ Peniela I’m sorry.He’s gone.John is gone”akasema Josh.Peniela akaishiwa nguvu na kuzirai.Haraka haraka akachukuliwa na kupelekwa kupatiwa huduma ya kwanza .Wakati Peniela akiendelea kupatiwa huduma ya kwanza simu ya Mathew ikaita.Alikuwa ni Anitha
“ hallow anitha.Nilikuwa katika harakati za kukupigia simu kukufahamisha mambo ya huku .Kuna habari gani hapo? Akaulzia Mathew
“ Dr Joshua amempigia simu Dr Kigomba muda si mrefu.Flaviana is gone.She’s dead.” Akasema peniela .Ilimchukua Mathew zaidi ya dakika moja kutamka lolote
“ How’s Elibariki?
“ ameishiwa nguvu.Nimempeleka chumbani kupumzika.”akasema Anitha
“ Ok Endelea kumpa uangalizi wa karbu sana.Huku nako mambo si mazuri.John is gone too” akasema Mathew
TUKUTANE SEHEMUJAYO…
.