Pentekoste iliyochangamka

Mtani, kumbe tofauti zetu ni jukwaa lile tu, Ila huku tupo pamoja 😀🤝
Aah ndo raha ya kuwa mtanzania mtani...hatuwezi kuchinjana kamweee...
Utofauti wetu wa utani ni utani tuu tukitoka huko tunakutana kwny angle zingine tukiwa wamoja...ahaha 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Waisraeli hawa hawa wanaoshirikiana na US kuua watu wasio na hatia GAZA?
 
Yesu Kristu alimwachia Petro kanisa linaitwaje?
 
Huo Ukristu umeufahamu kwa maumivu na safari ndefu iliyopitia Kanisa kwa miaka zaidi ya 2000 mpaka limefika leo, Unajidai kuujua kuliko Mtume Petro aliyeambiwa Juu ya Mwamba huu nitalijenga kanisa langu 😀
Mwananchi naomba ufafanue, hilo kanisa ni kanisa gani!? lilijengwa juu ya mwamba upi? Lilijengwa Yerusalemu au Italy?
 
"Hali ya Pentecoste ni mbaya kuzidi roman"

Tangu Lini Roman Catholic wakawa na hali mbaya?
RC na yenyewe imebadilika baada ya sadaka za Ulaya kuisha.

Waumini wanakaushwa, mwenye nacho anakuwa mungu, masikini hana thamani na hazikwi
 
Kila nikikumbuka injili ya akina Bishop Moses Kulola (Ulokole), Mch.Geoffrey Mbwana (SDA) na Reinhard Bonke (Ulokole) Kisha nikawaangalia Hawa akina sijui Mwamposa, Suguye, Zumaridi, Alex Malasusa na wengineo nasema INJILI ISHAKUFA kifo cha mende.
Kuna IPM, anapenda kafara kule anavyompenda Yesu. Ukimwambia amtumainie Yesu Kristo anaweza kukuua, anataka utumainie KAFARA, ni mwamba fulani hivi mjanja mjanja
 
Offcourse Roman Catholic ndio ilioanzisha hiyo hybrid belief wakaiita Christianity faith kwa kuchanganya holy faith na paganic traditions and practices na wamejitahidi kuitunza kwa nguvu zote ila at the expense of suppressing truth. Kanisa lolote linalochipua kutoka Roman Catholic Christianity faith haliwezi kuwa kanisa genuine la watakatifu.

Imani aliyoianzisha Mungu mwenyewe haikuwa Christianity ila imani ya utakatifu. Hii ndio twaweza sema ni dini ya Mungu mwenyewe; ilifuatwa na manabii kabla ya ujio wa Kristo, Yesu Kristo aliishi, mitume baada ya Kristo waliishi na kuihibiri, pamoja na kanisa la mwanzo lililoanzia Yerusalem siku ya pentekoste hii ndio ilikua foundation faith of the church.

Naomba ujue kuwa hapa najaribu kulizungumzia lile kanisa la watakatifu ambalo Yesu aliahidi kulijenga kutoka kwa Petro, ambalo malango ya kuzimu hayawezi kulishinda (hili kanisa Roman Catholic wameshiriki kulisupress na kujaribu kulieliminate); not hiyo hybrid faith called Christianity from Roman Catholic.

Kwa kujifunza soma kitabu cha matendo ya mitume uone kanisa lisiloshindwa na malango ya kuzimu linafananaje then licompare na kanisa lako la Roman Catholic halafu chukua hatua sahihi.
 
Yesu Kristu alimwachia Petro kanisa linaitwaje?
Katoliki. Yani la ulimwengu. Juu ya mwamba. Ndio maana ata lipitie misukosuko gani, halianguki milele. Soma matendo 11:26
"Alipompata akaja naye mpaka Antiokia. Na wote wawili wakakaa huko kwa mwaka mzima, wakiwafundisha wengi walioamini katika kanisa la Antiokia. Hapo Antiokia ndipo waamini waliitwa ‘Wakristo’ kwa mara ya kwanza"
Sasa neno lilotumika hapo kwenye original antiokia ambapo wanazungumza kigiriki ni "katholikos" yani la ulimwengu kama kristo alivo. Hatjitungii tu vitu mkuu. Kanisa ni moja tu takatifu katoliki la mitume.
 
ACHA KUJITUNGIA VITU
 
Hao sio wapentekoste. Ni wahuni tu
 
Sasa kwani umeona imepingana na nilichosema? Original greek text lililotumika ni katholikos. Ndio wakristo wa kwanza. Soma taratibu mzee. Au nenda catholic.com utapata kuelewa zaidi. Viva eclesia katholikos.
Nilichopost mimi ni tofauti na ulichopost wewe. Huo mtandao wa wakatoliki unataka uandike nini?! Tofauti na wanachotaka kukuaminisha mfuasi wao. Anyways, Injili ua Kistu na mambo ya makanisa wapi na wapi!? Maisha yaendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…