Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

Wanaume by default ni risk takers , kuna siku ahadi zinakwama , plan b lazima ihusike , nasema tena sidhani kama kuna mwanaume rijali hajawahi jaribu punyeto
Huyo jamaa ni manager wa kiwanda cha Soda, sasa hapo anakutoa kwenye reli na wewe unaenda tu kama kiberenge kibovu 😂
 
Soda mbadala wake maji ya baridi au juisi halisi. Kunywa soda kwa mpangilio yaan kwa siku mara moja tu
 
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.
Kwanini umeamua kuacha bajeti inabana au Kuna lingine?
 
Nafkiri nina mwaka sasa sijanywa soda. Nakunywa mavinywaji magumu tuu sijui kwanini
 
Kunyweni soda nyie kufa mtakufa tu

Ndiyo maana babu kisauji alisema aliyegundua sigara na misosi KFC waliishi miaka kibao ila wale waliogundua mazoezi walifariki chini ya 50,Sungura anarukaruka mazoezi kibao lakini anaishi miaka miwili tu na kobe mwendo mdogo mdogo hana zoezi hata moja anaenda hadi miaka 400.

Hakuna kitu ambacho hakina madhara ,ugonjwa upo maana visababishi ni vingi ,unaweza ukaacha soda ukafa kwa cancer!

Cha muhimu wewe kula unachopenda na fanya mazoezi ya kiafya!! Kuna jamaa alipata kisukari hadi mwenyewe nilishangaa ,jamaa ni mwembamba halafu alikuwa saidia fundi na kuchimba mashimo yaani kazi ngumu.
 
Mwaka wa 8 huu sinywi hayo matakataka. Sio soda, sio juice za kopo, sio energy drinks, sio aina yoyote ya kilevi. Vilevi vingine nje ya soda sijawahi kuvigusa toka nizaliwe. Ni maji tu.
Na ndio maana utakufa mapema na kuzeeka mapema na kinga za mwili wako zitakuwa chini, alcohol kiasi ndani yw mwili wa binadamu ina faida kubwa sana kuliko hasara
 
Ninaweza kukaa mwaka mzima nikanywa soda Mara 1 au 2.

Wanywaji wote wa Soda lazima Upate kitambi. Haiwezekani kinywaji chenye Sukari vijiko 10 ugigide ikuache salama.

Lazima Upate kitambi na unaweza kwenda kuua Nyongo (Pancreas) ambayo humwaga Insulin pale mwili unapopokea Sukari nyingi kutoka kwenye soda. Mwisho wa siku Ni kupata kisukari.


Drink Water Guys soda ni hatari.
 
Na ndio maana utakufa mapema na kuzeeka mapema na kinga za mwili wako zitakuwa chini, alcohol kiasi ndani yw mwili wa binadamu ina faida kubwa sana kuliko hasara
Sawa mke wangu. Wewe utaishi milele mama watoto.
 
Back
Top Bottom