Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

Kitu usichokielewa ni bora ukae kimya, mimi spice huwa nanunuwa kwa Muhindi karibu na Co cabs pale kuna mashine wanasaga wao wenyewe natural, spice nyingi zinapatikana hapo.
Ni vizuri kama ni natural, ila anachosema ni kwamba kuna spices za kuchanganya madawa viwandani, na hizo ndizo nyingi madukani
 
Mimi matumizi yangu makubwa Ni maji, kwa 24 hrs nakunywa 1.5 lt chupa 6 au 7. Kwenda kwa watu lazima nibebe maji kwenye begi. Safarini napata tabu Sana maana nalazimika kutokunywa maji ili kuzuia kukojoa Mara kwa Mara. Je hii nayo Ni addiction?
Hiyo haijawekwa kwenye addiction, pengine ndio mahitaji yako sahihi ya maji mfano labda wewe washikaji hukuona kama pande la jitu.
 
Hongera mkuu, tuendelee kupeana moyo, tutafanikiwa na hii kadhia, nimejidhatiti kweli kweli
Mimi sijaacha ila ukitaka kuacha ni rahisi tu ,ukifanya hivi
1) chakula chako kiwe ugali ,kama mjuavyo ugali ni "mboga" basi fanya mboga ya kulia ugali ziwe nzuri ,pia ugali ni adui no 1 wa soda tofauti na vyakula vyote duniani ,mungu katujalia waafrika kwa kuwa na hichi chakula cha ugali .
Njia ya pili
2)kila unapo sikia kiu au hamu ya soda kunywa maji kwanza ukiona hamu ya soda bado ipo ndiyo nunua soda unywe ,mm niligundua kuwa asilimia 80% ya hamu ya kunywa soda tunayo ipata huwa siyo halisi na ukitaka kujua kuwa siyo halisi basi kabla ya kuamua kunywa soda nunua maji unywe kiu ikate kisha sikilizia kama hamu ya soda bado ipo
Hizi njia mbili zinatosha kabisa kuzitumia kuacha soda ,tena ni nyepesi
 
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.

Maamuzi tu ndugu yangu
 
Addiction ni kila mahali, mm siwezi kulala bila kuona hata nembo ya CCM, yaani CCM imejaa rohoni na moyoni, nikisikia mtu anaisema vibaya CCM moyo unaniuma sana, sbb nimezaliwa nayo na nimekulia nayo. Ndio maisha yangu, bila CCM Imara nchi yetu ingeyumba sanaa huenda leo tungekuwa kama nchi za waafrika wenzetu, vita kila kona, CCM daima na milele, Mungu nisaidie, Amen.
We jamaa naona unakusudia kuharibu hali ya hewa.
Ngoja tusubiri.
 
Mimi matumizi yangu makubwa Ni maji, kwa 24 hrs nakunywa 1.5 lt chupa 6 au 7. Kwenda kwa watu lazima nibebe maji kwenye begi. Safarini napata tabu Sana maana nalazimika kutokunywa maji ili kuzuia kukojoa Mara kwa Mara. Je hii nayo Ni addiction?
Napenda maji pia , japo sjiafika kiwango chako ila nakunywa wastani wa lita 5 kwa siku.
Kuna madhara ya kunywa maji mengi pia ,niliambiwa na mtaalamu mmoja kuwa unaweza kupoteza nutrients muhimu kupitia mkojo kama utakuwa unakojia mara kwa mara , japo hili sijawahi kulijua kitaalamu ila naamini wapo humu kutuelimisha .
 
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.
Unafanya hayo yote..na bado unagonga kavu.hhaahhahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.
Soda ni hatari kuliko Bia, fanyeni utafiti.
 
Mimi matumizi yangu makubwa Ni maji, kwa 24 hrs nakunywa 1.5 lt chupa 6 au 7. Kwenda kwa watu lazima nibebe maji kwenye begi. Safarini napata tabu Sana maana nalazimika kutokunywa maji ili kuzuia kukojoa Mara kwa Mara. Je hii nayo Ni addiction?
Kwamba unakunywa 9lts kwa siku? Hilo nalo ni tatizo mkuu, hizo kidney zako zinapiga mzigo zaidi ya kawaida. Lakini pia unapoteza nutrients nyingi kupitia filtration, 9lts per day, unafanya shughuli gani mkuu?
 
Back
Top Bottom