t blj
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 7,035
- 16,705
Hapo kwenye meno ndo majanga yanayonikuta sasa. nimepitia changamoto mbili , moja mie ni mgonjwa wa pumu, nimetumia sana aminophylline ambazo nazo zinaharibu sana meno, pili at time nilikuwa heavy user wa coca cola, kama unachosema ni sahihi basi meno yangu yamepata bahati mbaya ya kutosha!!!Hongera Mkuu, kwa kuachana na matumizi yasofaa ya soda..
Vinywaji kama Soda ,sukari yake ni aina ya Fructose.. Tofauti na Sukari tunayopata kwa Msosi yaan Glucose.
Glucose huwa inatumika na kila seli mwilin ..lkn Fructose yenyewe huvunjwa vunjwa na INI pekeake .
Sasa unapokunywa masoda meeeeengi..
Unaongeza mafructose meeeeeeeeengi.
Haya Ma fructose yanaenda moja kwa mbili kwenye INI..yakifika hapo ndo huvunjwa vunjwa.
Sasa yakiwa meeeeeeengi, INI linayavunja weeeeeee.....
Mengine yatamwagwa kwenye damu..mengine yatabakia kwa INI na baada ya muda husababisha tatizo la kiafya lijulikanalo kama NONALCOHOLIC FATTY LIVER DISEASE.
lkn poaaa haya mafructosee hisababisha mafuta mengi ,MTU anakua mzitoo, uwezekano wa kupata Kisukarii , magonjwa ya moyoooo n.k
Lkn pia nihatari kwa Meno
Yani meno yanafanya kumomonyoka kama ubuyu, kuna muda naweza kula nikatafuna kitu kigumu ,nikahisi ni jiwe au mchanga ,kumbe ni kipande cha jino langu.