Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

Penye nia pana njia: Ni wiki ya 5 sasa sijatia soda mdomoni, kumbe inawezakana kabisa

Hongera Mkuu, kwa kuachana na matumizi yasofaa ya soda..

Vinywaji kama Soda ,sukari yake ni aina ya Fructose.. Tofauti na Sukari tunayopata kwa Msosi yaan Glucose.

Glucose huwa inatumika na kila seli mwilin ..lkn Fructose yenyewe huvunjwa vunjwa na INI pekeake .


Sasa unapokunywa masoda meeeeengi..

Unaongeza mafructose meeeeeeeeengi.


Haya Ma fructose yanaenda moja kwa mbili kwenye INI..yakifika hapo ndo huvunjwa vunjwa.

Sasa yakiwa meeeeeeengi, INI linayavunja weeeeeee.....

Mengine yatamwagwa kwenye damu..mengine yatabakia kwa INI na baada ya muda husababisha tatizo la kiafya lijulikanalo kama NONALCOHOLIC FATTY LIVER DISEASE.


lkn poaaa haya mafructosee hisababisha mafuta mengi ,MTU anakua mzitoo, uwezekano wa kupata Kisukarii , magonjwa ya moyoooo n.k

Lkn pia nihatari kwa Meno
Hapo kwenye meno ndo majanga yanayonikuta sasa. nimepitia changamoto mbili , moja mie ni mgonjwa wa pumu, nimetumia sana aminophylline ambazo nazo zinaharibu sana meno, pili at time nilikuwa heavy user wa coca cola, kama unachosema ni sahihi basi meno yangu yamepata bahati mbaya ya kutosha!!!
Yani meno yanafanya kumomonyoka kama ubuyu, kuna muda naweza kula nikatafuna kitu kigumu ,nikahisi ni jiwe au mchanga ,kumbe ni kipande cha jino langu.
 
Kweli mjini! mna raha sana!! yaani kunywa soda?? mtu unawazaaaa! eti kuacha! huku kwetu kwa mara ya pili tulikunywa Fanta Nyerere alipo kufa! coke ni ya mwenyekiti na jopo lake! na siku ya kwanza! ilikuwa ccm ilipo timiza miaka kumi utawalani baaasi!!

zile chupa za fanta! tuna tumia kuwekea mapambo!! kwenye nyumba zetu! au mfukoni halafu inachomoza kwa juu hivi! ili uonekane wa kisasa zaidi!
 
Hongera mimi nina mwaka wa 5 Sasa sili chipsi kabisa. Ukiamua inawezekana. Sasa naanza na hilo la soda.
Chips kabisa?? Mi naishia kuzibadilisha mapishi tu ila kuacha bado sijaweza

Soda ndio nimefanikiwa kupunguza sana kunywa, naweza kukaa mwezi bila kunywa! Kifupi nimekuwa nikinywa ikibidi tu
 
Chips kabisa?? Mi naishia kuzibadilisha mapishi tu ila kuacha bado sijaweza

Soda ndio nimefanikiwa kupunguza sana kunywa, naweza kukaa mwezi bila kunywa! Kifupi nimekuwa nikinywa ikibidi tu
Chipsi ni mbaya mkuu zina mafuta mengi. Na mafuta hayo mengi sio mazuri. Fikiria pia juu ya hilo ndugu. Ila kwa soda nakupongeza.
 
Mara ya kwanza nilipojaribu nile chakula bila kunywa soda niliona maisha magumu sana, chakula hakishuki, sina hamu ya maji wala juisi ya matumda wala chochote kile, yaani natamani soda tu, hapa ndipo nilipogundua kumbe hii ni shida, ni kama madawa ya kulevya, nina mashaka kuna kitu wanaweka mule, hii si kawaida.

Mwezi uliopita nikasema hata ikibidi nife kwa kukosa soda, so be it, ila sinywi hata iweje, ni wiki ya 5 leo sijanywa soda, napitia wakati mgumu sana, ila namshukuru Mungu, naendelea vizuri.

===============================


===============================
Update: 09/11/2021

Wiki 5 ni wastani wa siku 35, kama ulifanikiwa siku 35 hupaswi kusema unapata tabu unavumilia tu, kubadilisha tabia ni siku 21 tu ndugu yangu, tabu uliipata zaidi wiki ya kwanza,
 
Chipsi ni mbaya mkuu zina mafuta mengi. Na mafuta hayo mengi sio mazuri. Fikiria pia juu ya hilo ndugu. Ila kwa soda nakupongeza.
Sio chips zote zina mafuta mkuu, naona kuwa tatizo linaweza kuwa mapishi zaidi kuliko chips zenyewe
Mfano ukichomea kwenye air frier mafuta kijiko kidogo tu yanaivisha chips za kula hata watu wanne!
 
Ni mwaka wa 4 tangu niache soda, energy drinks and the likes ila sasa naona mbadala wake nimepeleka kwenye juice ambako nako natakiwa kushinda
 
Ukiona mtu anang'ang'ana kuacha kitu fulani basi ujue limemkuta jambo. Vivyo hivyo kwa walevi ukiona anatafuta msaada wa kuacha pombe ni ama imwmfilisi au alijikojolea kitandani au kufanya kitu cha aibu kilichomshuhia heshima au kumfanya aishi kwa hatia moyoni
Hizo sababu ulizo zitaja, sababu moja wapo ndiyo ilinifanya niache pombe kwa kushitukiza ghafla sana bila maandalizi!

Ni miaka 30 sasa, hata kumbu kumbu ishatoweka.

Ila hapo mwanzoni, ndoto za kuota nimekunywa ziliniandama sana, lakini nikapiga moyo konde na kuuheshimu uamzi wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mwaka wa 4 tangu niache soda, energy drinks and the likes ila sasa naona mbadala wake nimepeleka kwenye juice ambako nako natakiwa kushinda
Kunywa natural juice za matunda halisi
 
  • Thanks
Reactions: Zvi
Sio chips zote zina mafuta mkuu, naona kuna tatizo linaweza kuwa mapishi na sio chips zenyewe
Mfano ukichomea kwenye air frier mafuta kijiko kidogo tu yanaivisha chips za kula hata watu wanne!
Ahsante kwa taarifa mkuu ntazijaribu hizo.
 
Acheni kufananisha punyeto na vitu vya kijinga nyie! mademu wenyewe wanatukoma huo ujeuri wetu tukitoka piga nyeto!
Mademu lazima waandamane ili mkatwe mikono hiyo! Au muwekewe kamera kwa lazima ukipiga tu mada kesi unaua watoto wangapi hapo?? kufanya punyeto ni mauaji ya halaiki mkomege!!! me mnaua sana kuliko ke!!
 
Back
Top Bottom