Pep Guardiola aachana na mkewe baada ya miaka zaidi ya 30 kuwa pamoja

Pep Guardiola aachana na mkewe baada ya miaka zaidi ya 30 kuwa pamoja

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Baada ya miaka 30 pamoja, na watoto 3, Pep Guardiola na Cristina Serra wanaonekana kutengana. đź’”
1736796719126.jpg


==

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameachana na mke wake Cristina Serra ambaye wamekaa pamoja kwa miaka 30.

Guardiola ambaye anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha Manchester City alifunga ndoa na mke wake nchini Hispania mwaka 2014, wakiwa wameshakaa pamoja kwa muda mrefu, lakini jana iliripotiwa kuwa wameachana rasmi.

Taarifa ya kuachana kwao ilianza kutolewa na gazeti la Hispania Spanish Sport, likieleza kuwa wawili hao hawapo pamoja kwa miaka mitano tangu Serra alipoamua kuondoka England na kutimkia nchini Hispania akiwa na mtoto wake mmoja Valentina, 17, huku akimuacha Pep Manchester England akiwa na City.

Wawili ambao walikutana rasmi mwaka 1994 wana watoto watatu, Maria, 24, Marius, 22 na Valentina.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa awali hakukuripotiwa taarifa yoyote ya kutofautiana kwa wawili hao kwani pamoja na kuishi nchi mbili tofauti bado mara kwa mara walikuwa wanaonekana pamoja nchini Hispania na England kwa vipindi tofauti.
 
Au Guardiola huwa yuko busy sana hana muda kwa familia? Au pengine kutokana na kazi yake anakuwa ni mtu mwenye msongo wa mawazo kiasi anashindwa kuwa mume/baba bora?

Miaka 30 inasikitisha sana kutengana.
Wazungu linapokuja suala la uhusiano wa kijamii huwa wana matatizo ya ubongo bahati mbaya ndo role model wa jamii ya leo ya Africa..
 
Baada ya miaka 30 pamoja, na watoto 3, Pep Guardiola na Cristina Serra wanaonekana kutengana. đź’”View attachment 3201117
Tukiwaambia wasioe, wanaona kama tunawaonea wivu.

Mwanamke ni shetani, hata baada ya miaka 50 anaweza kuja kukuacha.

Kuna mijamaa itakuja kukwambia sio wote, sawa bhana, huyo wako si umemuumba wewe mwenyewe
 
Back
Top Bottom