Pep Guardiola aachana na mkewe baada ya miaka zaidi ya 30 kuwa pamoja

Pep Guardiola aachana na mkewe baada ya miaka zaidi ya 30 kuwa pamoja

Review ya mikataba ya ndoa inahitajika. Baada ya hapo, pamoja na stress jamaa alizopitia kujijenga kwenye career yake, bado watagawana mali 50-50 na kama hakuweka mambo vizuri atanyang'anywa zaidi ya nusu ya utajiri wake. Ona Roberto Carlos anachopitia, inauma wanaume tumekuwa punching bag la wanawake. Tupigike then wachukue kila kitu.
 
Au Guardiola huwa yuko busy sana hana muda kwa familia? Au pengine kutokana na kazi yake anakuwa ni mtu mwenye msongo wa mawazo kiasi anashindwa kuwa mume/baba bora?

Miaka 30 inasikitisha sana kutengana.
Maneno ya kifeminist ya kujastify talaka ili kupora utajiri wa wanaume, 'mume bora', 'muda na familia'.
 
Hivi kwanini katika utengano watu mnaangalia mali pekee?

Kwanini hamfikirii maumivu wanayopitia? Mnafikiri kutengana na mtu mliyekuwa pamoja kwa miaka 30 ni rahisi namna hiyo?

Mke wake wako pamoja tokea mwaka 94 ina maana Guardiola ndio alikuwa anachipukia, wamekuwa pamoja kipindi chote cha mafanikio yake kama angetaka mali mnafikiri angedumu naye kwa miaka 30?
 
Kawel sual la ndoa asee! hii ni vita kuu isiyoisha kati ya me na ke.Imekaa kama vita ya myahud na mfilisti na inabomoa dunia kisawsaw.Mwanzo huku africa tulikuw tukiskia wazungu wanaoa kwa mkataba tulikuw tunawaona washenz saana. Ila sas hiv hata sisi wa Iselamagazi tunajionea mubashara😂😂.
 
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameachana na mke wake Cristina Serra ambaye wamekaa pamoja kwa miaka 30.

Guardiola ambaye anapitia kipindi kigumu kwenye kikosi cha Manchester City alifunga ndoa na mke wake nchini Hispania mwaka 2014, wakiwa wameshakaa pamoja kwa muda mrefu, lakini jana iliripotiwa kuwa wameachana rasmi.

Taarifa ya kuachana kwao ilianza kutolewa na gazeti la Hispania Spanish Sport, likieleza kuwa wawili hao hawapo pamoja kwa miaka mitano tangu Serra alipoamua kuondoka England na kutimkia nchini Hispania akiwa na mtoto wake mmoja Valentina, 17, huku akimuacha Pep Manchester England akiwa na City.

Wawili ambao walikutana rasmi mwaka 1994 wana watoto watatu, Maria, 24, Marius, 22 na Valentina.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa awali hakukuripotiwa taarifa yoyote ya kutofautiana kwa wawili hao kwani pamoja na kuishi nchi mbili tofauti bado mara kwa mara walikuwa wanaonekana pamoja nchini Hispania na England kwa vipindi tofauti.
ivi najiuliza mpaka saiv amewezaje kukaa na kiumbe cha hatar kwa miaka 30 yote?
 
Back
Top Bottom