Pep Guardiola: Huwa nacheka sana wakisema Ronaldo anahama club kutafuta ili changamoto

raia chambueni kwa umakini iyo kauli jamaa yupo sahihi kwa asilimia Mia............
 
Kumbe pointi kuhama timu sio kigezo cha muhimu ka unafanya kazi yako ipasavyo.
Dan Alves timu zote alizopita amechukua makombe. Kucheza ligi moja haikuondolei ubora wako
Hizo team pia unazohamia una mchango gani? Kuhama team pia kuna mantiki, je utaendelea kuwa na mchango uleule?
 
ndio maana hta madrid wakaona haina haja cz akiwepo asiwepo ufalme wao uko pale pale
 
Kumbe wazungu pia wana wivu kama huu wa kimatumbi kabisaa?
 
Tukitoa magoli aliyofunga Ronaldo Juventus bado atakua bingwa? tutoe magoli aliyofunga Ronaldo akiwa Real Madrid je Real Madrid wangechukua UCL? maisha ya real Madrid baada ya kuondoka CR7 yapo sawa na zamani?
 
Kumbe na wazungu wanakuwaga na wivu? Angekua mweusi ningesema mshirikina huyu.
Sasa Juve kuna changamoto gani misimu karibia 10 Italy hana mpinzani??

Angekuwa anataka changamoto angeenda Inter au Napoli au hata Roma.. Juve hata bila yeye wangeshinda tu Serie A. He is just icing his cake
 
Binafsi alichoongea hakiingii akilini.

Kwanini? Tubase kwenye mfano wa Danilo alioutoa, Danilo kiwango chake hakijawahi kua na consistency, sasa hivi yupo Juve lakini anacheza? Anapata namba? Namba yake inachezwa na midfielde Cuadrado.

Kiwango chake ni kibovu kiasi wao wenyewe City walimtupa.

Turudi kwa Ronaldo. Kiwango chake unakionaje? Msimu huu ana zaidi ya magoli 30 yupo yeye, Lewandowski na Immobile katika hiyo level.

ROnaldo timu ikiwa inachukua ndoo na yeye mchango wake utauona. Hivyo haendi tu kujaza nafasi kwenye benchi, kiwango chake kinaongea. Sasa muulizs Guardiola mara ya mwisho UEFA alichukua na timu gani na nini kinamzuia nyakati hizi.
Ronaldo ameisaidia Juve?? Juve hata kabla yake ni dominant pale, hakuna alichosaidia hata kama anafunga namna gani..

Juve walimchukua Ronaldo awasaidie kushinda CL na sio Serie A. Vipi ameshinda CL akiwa na Juve??
 
Tukitoa magoli aliyofunga Ronaldo Juventus bado atakua bingwa? tutoe magoli aliyofunga Ronaldo akiwa Real Madrid je Real Madrid wangechukua UCL? maisha ya real Madrid baada ya kuondoka CR7 yapo sawa na zamani?
Madrid amechukua Ligi kuu, CL imesimamishwa vipi kuna maneno hapo??

Kabla ya ujio wa Ronaldo Juve, Je Juve walikuwa wanastruggle kuchukua hiyo Serie A? Madrid kachukua La Liga bila ya Ronaldo hili mbona huliongelei??
 
Ronaldo ameisaidia Juve?? Juve hata kabla yake ni dominant pale, hakuna alichosaidia hata kama anafunga namna gani..

Juve walimchukua Ronaldo awasaidie kushinda CL na sio Serie A. Vipi ameshinda CL akiwa na Juve??
Baba tangu Juve ashuke daraja na kurudi amekua dominant lakini individual records za Juve zilikuaje? Dybala akawa mfungaji wao bora, unajua alikua na magoli mangapi? 15.

Ronaldo ana magoli mangapi tangu aende? Individual records za miaka ya 60 ndiyo zinavunjwa leo na Ronaldo. Kudai kwamba wamemleta Ronaldo ili washinde CL sidhani kama ni sahihi, kwakua Buffon mwenyewe aliondoka Juve na kwenda PSG ili ashinde CL kilichompata tunakijua na Juve haikuwahi sema Ronaldo kaja kwaajili ya CL.

Haya msimu uliopita walifanya comeback kwa Atletico, uliuona mchango wa Ronaldo au haukuuona? Na si ni yeye ndiye aliahidi lazima watafanya comeback? Halafu Simeone akasema wakifanya comeback anaenda kuuza matikiti. Comeback ikafanywa, Ronaldo akachangia comeback na Simeone hakwenda kuuza matikiti.

Huo msimu Guardiola akatolewa na Tottenham.

Danilo alikua na mchango gani kwa Madrid? City? Juve? Na Ronaldo anazeeka.
 
Sasa Juve kuna changamoto gani misimu karibia 10 Italy hana mpinzani??

Angekuwa anataka changamoto angeenda Inter au Napoli au hata Roma.. Juve hata bila yeye wangeshinda tu Serie A. He is just icing his cake
Lazima uangalia kwanza hizo team unazo zitaja zinaweza kulipa ada ya uhamisho ya pound ml.100,zinaweza mlipa 1.5 biltsh kwa weak,na huduma nyinginezo za kironaldo.
 
Sasa Juve kuna changamoto gani misimu karibia 10 Italy hana mpinzani??

Angekuwa anataka changamoto angeenda Inter au Napoli au hata Roma.. Juve hata bila yeye wangeshinda tu Serie A. He is just icing his cake
Kuwa dominant kwenye ligi haimaanishi hakuna changamoto.
Kwani mtu akisema natafuta changamoto mpya anamaanisha kuwa anafuata Ugumu wa ligi?

Soka la Italy ni tofauti na la Uingereza na Uhispania vilevile.
Kama Best player ameona ni vyema akaprove ubora wake katika ligi tofauti.
Na imekuwa hivyo katuonyesha
 
Ferguson aliwahi kusema "Nipe Zidane na vipande 10 vya mbao na nitakupa CL" kwa nyakati zetu Zidane wetu ni Messi au Ronaldo. Yeyote mwenye huyo mchezaji ana advantage over other teams.

FisadiKuu Ronaldo ana misimu mingapi amecheza CL akiwa na Juve? Danilo akiwa na City? Juve, City na Madrid zikiwa zinachukua ndoo Danilo anakua na misimu mingapi? Anakua anapata namba?
 
Baba tangu Juve ashuke daraja na kurudi amekua dominant lakini individual records za Juve zilikuaje? Dybala akawa mfungaji wao bora, unajua alikua na magoli mangapi? 15.

Ronaldo ana magoli mangapi tangu aende? Individual records za miaka ya 60 ndiyo zinavunjwa leo na Ronaldo. Kudai kwamba wamemleta Ronaldo ili washinde CL sidhani kama ni sahihi, kwakua Buffon mwenyewe aliondoka Juve na kwenda PSG ili ashinde CL kilichompata tunakijua na Juve haikuwahi sema Ronaldo kaja kwaajili ya CL.

Haya msimu uliopita walifanya comeback kwa Atletico, uliuona mchango wa Ronaldo au haukuuona? Na si ni yeye ndiye aliahidi lazima watafanya comeback? Halafu Simeone akasema wakifanya comeback anaenda kuuza matikiti. Comeback ikafanywa, Ronaldo akachangia comeback na Simeone hakwenda kuuza matikiti.

Huo msimu Guardiola akatolewa na Tottenham.

Danilo alikua na mchango gani kwa Madrid? City? Juve? Na Ronaldo anazeeka.
Nilishasema huko juu, Ronaldo pale Juve he is just decorating his resume. Huwezi seriously kumsifu Ronaldo eti kaishindisha Juve Serie A, ni ukichaa aisee..

Aya hizo comebacks ziliwasaidia nini? Walishinda CL?? Hivi unafikiri Juve ambaye tayari ni dominant EPL angeingia cost za kumnunua Ronaldo na kumlipa mshahara eti ili tu washinde Serie A?? Juve anastruggle sana CL na wanaitaka kwa udi na uvumba sababu pale Italy hawana changamoto yeyote, na hiyo ndio sababu ya kumuongeza Ronaldo kwenye kikosi chao..
 
Sasa Juve kuna changamoto gani misimu karibia 10 Italy hana mpinzani??

Angekuwa anataka changamoto angeenda Inter au Napoli au hata Roma.. Juve hata bila yeye wangeshinda tu Serie A. He is just icing his cake
Na yeye aende kufundisha brentford awape ubingwa wa UCL[emoji23]
 
Back
Top Bottom