Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Baada ya Arsenal kuchezea kichapo cha goli moja kwa bila dhidi ya Nottingham forest ni rasmi ubingwa wa ligi kuu uingereza msimu wa 2022/2023 unakwenda kwa manchester city ambaye anajumla ya point 85 huku anaemfuata Arsenal akiwa na point 81 na amebakiwa na mchezo mmoja mkononi ili kumaliza ligi wakati man city yeye akibakiza michezo miwili.

Ubingwa huu aliochukuwa man city chini ya kocha Pep Guardiola utakuwa ni ubingwa wao wa tatu mfululizo kuchukua chini na Kocha Pep Guardiola akifanya ivyo msimu wa 2019/2020, 2021/2022, 2022/ 2023 Wakati huo huo man city bado yupo kwenye mbio za kugombania makombe mengine fainali kombe la FA Ambayo atamenyana na Manchester United, fainali ya Uefa champion league dhidi ya Inter Milan, Kiufupi Guardiola ameshindikanika.

Licha ya makombe anayozidi kuyakusanya katika club mbalimbali pia guardiola ni kocha anayesifika kwa kufundisha mpira unaovutia kwa watazamaji mpira wa pasi nyingi, ikumbuke ile Barcelona ya akina Iniesta, Xavi na Lionel Messi, ilikuwa ni hatari mpaka Furgeson anatetemeka mikono [emoji1787][emoji1787]. Kumbuka jinsi alivyoweza kuibadilisha Beyern Munich kutoka kwenye piga tukimbizane mpaka mpira wa pasi nyingi.

Haya ni baadhi ya makombe makubwa aliyowahi kuyachukua Mtaalam Pep Guardiola.

1. Uefa champion league..... ×2
2. Uefa Supercup....×3
3. Spanish (Laliga)......×3
4. England premier league.......×5
5. Bundersliga..........×3
6. Fifa club world cup......×3

View attachment 2629308
Nitamtambua Guardiola kama best coach iwapo atafundisha Average team financially kama vile.. Everton, Roma, Valencia, Dortmund, Nk...

Kwa timu alizowahi kuzifundisha kama Barcelona Ileee... Bayern ya akina Rubben...katika ubora wao, Na man city hii ya akina Haaland hata Juma mgunda anaweza kutangazwa kuwa Kocha bora.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Nitamtambua Guardiola kama best coach iwapo atafundisha Average team financially kama vile.. Everton, Roma, Valencia, Dortmund, Nk...

Kwa timu alizowahi kuzifundisha kama Barcelona Ileee... Bayern ya akina Rubben...katika ubora wao, Na man city hii ya akina Haaland hata Juma mgunda anaweza kutangazwa kuwa Kocha bora.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Unajidanganya mpe mgunda Yanga uone ujinga
 
GPep Hana maajabu, sema pesa za mafuta ndo zinampa jeuri.Kamwe hawei fikia viwango vya Fergie, Mourinho na Ancellotti
 
GPep Hana maajabu, sema pesa za mafuta ndo zinampa jeuri.Kamwe hawei fikia viwango vya Fergie, Mourinho na Ancellotti
Haya yako ndio mawazo ya kishamba, wale wachezaji alionao Pep hakuna timu pale Uingereza isiyoweza kuwasajili, Gundogan, Mahrez, Alvarez, Stones, Diaz na wengine wote wale wanaweza kusajiliwa na timu nyingi pale EPL.

Lakini hebu jiulize, ni makocha wangapi wanaweza kuwafanya wale wachezaji wawe moto kama alivyofanya Guardiola? jibu ni HAKUNA.
 
Ni binadamu mwenye ugonjwa WA akili ndio anaweza kusema Gurdiola sio kocha
20230522_160121.jpg


Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Budget ya clubs anazofundisha huwa unaipitia? Ji kweli ni kocha bora sana, ila nae anakuwa na budget kubwa sana. Hata jana Mourinho alisema, una bench lenye 200m, wakati huo upo na quality ya hali ya juu ndani ya uwanja. Huwezi kulinganisha na hawa wanaopewa limited budget.
Ukiisoma documentary ya Guardiola anakwambaia KOCHA BORA ANATENEGENEZWA NA WACHEZAJI WENYE QUALITY KUBWA VICE VERSA IS TRUE. unaweza kuwa na squard ghali sana na usipate mafanikio makubwa ila huyo huyo Guardiola anaweza kumchukua mchezaji anaye onekana wa kawaida na akamfanya kuwa hatari sana, mfano KDB, AKANJI ambaye hata namba dortmund hakuwa nayo hata ya kufikiriwa then angalia wale watoto wake anao watengeneza saivi akina Lewis.....Guardiola is just a master mkuu.

Bielsa mwenyewe anakwambia huyo ndo mwanafunzi wake bora wa muda wote, kwa wale ambao amewafundisha football.
 
Tofauti na Chelsea wachezaji wengi hawajapitia hata pre season na kucheza pamoja na team imepitia mabadiliko katikati, ipitie Chelsea ya nyuma hapa ilikuwa vipi. Guardiola mpe Man U ile ya kina Maguire na hawa Glazers halafu utanambia. Ila all in all, jamaa anajua sana
pep anajua, cancelo kafunzwa kawa maestro kapewa na saba mgongoni kapata kiburi,na dias jee, ake mabadiliko yake kila mtu anashangaa,KDB wa chelsea alivo ingia mikononi mwa pep kawa top balaa,Stone jee alikuwa ivo? saizi hata yeye hajijui ni mido au beki😂, rodri wa atleticle na huyi vip,
team ni kocha tu, potetino psg ilimshinda, na sasa tuchel bayern inamshinda😂 Pep Fundi sana
 
Budget ya clubs anazofundisha huwa unaipitia? Ji kweli ni kocha bora sana, ila nae anakuwa na budget kubwa sana. Hata jana Mourinho alisema, una bench lenye 200m, wakati huo upo na quality ya hali ya juu ndani ya uwanja. Huwezi kulinganisha na hawa wanaopewa limited budget.
Unafikiri kila mtu akipewa bajeti nzito anaweza fanya kama anavyofanya gurdiola?...pale barcelona alikuwa na bajeti ipo kama siyo kuwapandisha vijana kadhaa toka la masia angalia aina ya mpira anaofundisha mkuu!...psg kuna bajeti nzito mbona wanachemsha UCL
 
Pep ni kocha wa kawaida sana,yan kwa hao quality players lazima uwe bingwa,,kama yeye noma aende tot/man u achukue ubingwa.Kile kikosi cha barca alichokua uefa hata mgunda akipewa anakua bingwa,cheki kina morinho wanakua mabingwa na vikos vya kawaida sana.Pep yeye ampaka awe na quality players ndo anakua bingwa
 
Back
Top Bottom