Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

PAt 3..[

Basi bwana,siku moja tukawa tumetoka mimi,kaka Muddy na Bena tukawa tumekaa mahali mara wakaja wakaka wawili wanashida na wao na mchakato,kuna muhaya mmoja much know kama Mwijaku,yeye anafanyaga kazi na kaka Muddy anatafuta vichwa huko anawaconnect wanapiga kazi,basi pale pombe pombe story za michakato ndio nikaanza kugundua siri nzitonzito, ila kwenye zile stori Bena alikuwa kama anazuia sana hizo stori lengo lake nisielewe chochote lakini si unajua tena kuna watu ni vichwa panzi wakishalewa huwezi kuwa control.Basi yule Muhaya akaniomba namba yangu nikampatia akasave nikasave ya kwake pia,
Basi yule muhaya na yeye alikuwa anataka lile lile duka ila yeye anaenda benki nyingine,kwa hiyo akawa anakuja kushinda pale dukani na yule mteja wake na yeye ajue bei ili siku afisa wao akija yeye ndio awe mwenye duka.
Sasa siku hiyo yule mwenzie akapata udhuru hakuna dukani ndio tukashinda pale dukani karibu siku nzima mimi na Muhaya,jioni nikasema ngoja tukale sehemu ndio tuondoke,Tulivyofika kula muhaya akaagiza bapa akawa anakunywa huku tunaweka stori mbili tatu za michakato ugumu na mafanikio yake,pombe bwana hazinaga mambo ya uongo uongo pombe zenyewe zinajisemeaga ukweli!

Muhaya akaanza kuniuliza nanafahamiana na Bena tangu lini?nikamjibu ninamjua siku nyingi kiasi,sasa pombe zilivyokolea akaanza kunipa mafaili ya Bena!
Bena ni tapeli wa kimaitaifa,yeye ana madeni kila kona ya Dar,ndio maana muda wote anavaa cape anajificha!Bena ana misala hakuna cello haijui!sasa siku hizi michezo yake anatafuta vichwa safi,ambao hawana recoding chafu anasimamia show pesa ikitoka anakupanga vizuri halafu anapotea nayo,akasisitiza anatumia sana Ushirikina,kwanza Bena sio mkurya kama alivyokwambia ni Mnyaturu hatari sana.Akaniuliza wewe hujaenda kwa ustaadhi kumsomea manager?nikasema nilienda akasema na wewe ulikuwa unatulizwa akili!nikasema heeee muhudumu ongeza kasichana hapa na Serengeti baridi!
Muhaya akawasagia kunguni ile mbaya wenzie,yeye ndio akawa mwema,akasema amemsikia Bena akijigamba safari hii ameletaa kichwa safi hajui mambo yoyote ya mjini!nikasema ni kweli mimi nilikuwa namuamini tutakuwa washirika Muhaya akasisitiza weweee tumia akili UNAPIGWA hizi hela zikitoka!
Pombe yote iliingia ila zilikata ndani kwa ndani,ile siku ikapita nikiwa tayari nina mwangaza nipo kwenye situation gani ikawa najiuliza Nibwage au niendelee,malaika wa maasi akaja kukaa began akaniambia "TWO CAN PLAY THIS GAME"!Hakuna kutoka unaacha vipi hela wewe Joannah? wape show!

Mwezi wa pili katikati tangu tuanze mchakato afisa akasisitizia wiki hii mzigo utatoka ila itatoka 25M,hiyo ni baada ya nyumba yangu ile kufanyiwa evaluation,Ila yeye na manager wakataka wapewe 1M,nikasema sawa,

Hapo Bena moyoni kabeba roho ya DHULMA,Ananipanga vizuri nikae kwenye target ili iwe rahisi kupita na hela zikitoka,Bena kila siku ushoga umekolea ananiita tu mdogo wangu kwa upendo,ananipa mikakati ya kutumia pesa vizuri ikitoka na mimi nimetulia kimya ndio nikawa nazidi kujifanya mshambaa sielewi chochote nikasema rohoni mwaka huu ndio utajua kama Nina cheti cha UDSM ambao hakinisaidii chochote kipo tu kabatini!

MZIGO UKATOKA!
Nikapigiwa simu na afisa,sister kesho uje asubuhi na mdhamini hela itoke,kesho yake Bena na Muddy saa kumi na mbili wananipigia simu nitoke nisichelewe,wao ndio wa kwanza kufika huko mbagala kabla sijaingia benki wakanimbia mzigo ukishaingia nitoe wote nitoke nao nje,nikasema sawa...msisahau na muhaya akawepo hapo kwenye huo mzunguko,nikazama benki na mdhamini tukawa tunaendelea na process

WALINZI WANGU WAKO NJE;
Baada ya kujua zile taarifa kutoka kwa muhaya siku za nyuma nikampigia mshkaji wangu mmoja mkaka wa Chuga,ila yupo Dar anasukuma maisha huku,huyo ndio mafia balaa mwenyewe anajitaga Patrol,nikampa mchongo mzima,akaniambia aisee acha ufala umpe hela nusu kwa nusu huyo malaya kivipi na benki wanakujua wewe?hamna kumpa hapo unarudisha tu hiyo hela ya mchakato hakuna kutoa hela kizembe! Akasema siku pesa ikitoka niambie nije nisimamie show! Basi ile siku naingia benki akaniambia niko nje nakusubiri ukitoka tu gari nyeusi Harriern,Na hela ikiingia toa milion mbili tu ndio toka nazo!
Basi wale kina Muddy na Bena na Muhaya wako attention utasema fisi wameona mzoga!mpaka saa nane Meseji hiyoo haikuwa 25M kamili ,ilikuwa na makatomakato, kama nilivyopewa maelekezo nikatoa 2M dirishani nikaweeka kwenye pochi nikatoka nje,yule mdhamini kanibana kisawasawa pembeni yangu ile natoka nje namuona Patrol akaniita namkuta ana Harrier mpya nyeusi tinted yuko na mkaka mwingine ambaye simjui anasema panda twende!mdhamini anasema yeye hapandi kwenye gari nyeusi tusogee kwa mguu hapo kwenye baa si mbali,akaanza kuweweseka anawapigia simu kina Muddy,we ghafla hawa hapa !Basi tukatembea mpaka kwenye hicho ki bar tukawa wote,nikawaambia hawa ni kaka zangu kuna sehemu tunaenda wamenifuata,Muddy kaanza kukoroma kwa nini nawaletea watu,nikasisitiza ni kaka yangu,kaka asema kwani vipi mbona unafoka sana bro?[lafudhi ya Arusha]Muddy anasema hapa hakuna namna tufuate makubaliano mzigo uwekwe mezani nusu apewe Bena na tulipie baadhi ya madeni tunayodaiwa!

Patrol akasema toa hela Joh,nikaweka 2M mezani nikasema nyingine sijatoa,we Muddy karukia pochi kufungua hola!ikawa Tafrani na mzozo pale,Bena yupo kimya anajifanya mwema, akaniita pembeni akasema basi kama hivyo anomba kwanza ile 2 tulipie tunavyodaiwa halafu jioni tutapanga vizuri mambo yetu tusiruhusu wanaume watuharibie mipango yetu mizurii,nikasema sawa,basi akatuliza hali ya hewa pale nikakubali kuacha ile 2M pale,Yaani shetani kasimama pale kungekuwa na mtu ana bastola ningekula ya kichwa!Mimi nikaingia kwenye gari ya kaka yangu wa mchongo Patrol huyoo,hawajaamini nimekuwa mtu mwingine kabisa!Namsikia Muddy anamlaumu Bena unaniletea mtu gani huyu Jambazi kabisa!Bena unaniletea majambazi unataka kuniua?mimi huyo nimekaza komwe ndukiiiiiii.
 
Shalom Shalom taifa la Mungu.

Leo natamani tupige mastory ya jiji la Dar es Salaam.Kwanza kabisa nataka kuweka wazi kwamba hii habari ni kweli ila angalizo ni kwamba kuna baadhi ya mambo kama majina halisi ya wahusika, majina ya maeneo,majina ya taasisi n.k nitabadilisha kutokana na nature ya story yenyewe.Kwa hiyo wale kina John kisomo mnaounganishaga dots A na K na mnasema hazijabalance leo you need to relax na kuenjoy story..Hii story ni ndefu sana ila nita summarise ili nisijichoshe na nisiwachoshe!
Hii story itakupa mwangaza kwenye mambo kadhaa yanayofanyika katika jiji letu hili la hekaheka lakini kikubwa ni Utapeli,dhulma, usaliti na shirki!

Lakini pia hii story ina ujumbe mzito ninaotaka ukufikie mpambanaji yeyote kwamba kama hujakatwa kichwa usikate tamaa kuna siku isiyo na jina lolote na chochote kinaweza tokea,kuna muda Mungu anaweza kuamua tu kukubless hivyo ni wewe tu kutumia hizo baraka ulizoshushiwa,wengine wanaita bahati ila binafsi siamini sana kwenye bahati napenda kusema ni NEEMA tu za Mungu akiamua kukumwagia wino akasign jambo lako litafanyika kivyovyote vile ila litafanyika.
Basi twende sasa pamoja.

BASED ON TRUE STORY

"Gri griiii griii "
simu yangu inaita ,nakumbuka ilikuwa Alhamis,kuchek ni rafiki yangu mmoja tangu secondary,huyu nimpe jina Andy.Andy ni mke wa Don flan hapa mjini mume wake ana biashara zake ambazo binafsi siwezi kuelezea ana biashara gani ila naona tu wanaishi ile Gucci life,Andy yeye ana duka Kariakoo anauza vipodozi vya jumla,ni yule rafiki ambaye mnaona kwenye matukio yote muhimu ya huzuni na furaha ila hamko close kivilee yaani mkikutana ndio mnaongea mambo yenu yoteee.,Andy anapenda sana kula bata na vile pesa ipo aaaah hana baya ukikutana nae ni bata is bataling.!
Basi ile napokea simu

Andy:"We kidawa umefichwa wapi?

Me:"Mh Dar sijaona hata pango la mimi kufichwa, nipo tu nashangaa shangaa na jiji,niambie dada Don leo umenimiss?

Andy;"Bado utashangaa sana,!Sikia jumamosi una ratiba gani?Birthday yangu,baba G yupo Moshi nataka tutoke tupumzishe vichwa,vipi una nafasi?

Me;"Niko na wewe kidawa,mpaka baba G atuchape risasi ya visigino ..
Tukapiga story mbili tatu miadi ikawa jmosi.

JUMAMOSI.
Jumamosi ilivyofika mimi huyo nikavaa zangu simple tu kijumamosi maana alisema tukutane ufukwe mmoja wapo hapa jijini,alisema atakuwa na rafiki zake wengine kimsingi mimi nilikuwa siwafahamu,ni wadada wafanyabiashara wenzie jinsi alivyoniambia,nilichelewa kidogo kufika,Nilipofika aisee nilijiona kama sistahili kuwepo pale,Yaani hao madada ni mishangazi mizurii,imevaa mawigi ya bei na Vito vya thamani yaani wamependeza,nyiiie mashangazi ya Tanzania ni mazuri bwana!Hiyo meza sasa ilivyochafuka vinywaji vya gharama nikasema eeeh leo nimendandia mtumbwi wa vibwengo wakisema "SHARE THE BILL" najifanya nimezima siwezi lipa bill laki mbili mimi Abadan!

Tukatambulishana pale vibe lilikuwa kali sana jamani hili jiji watu wanajua kuenjoy bwana asikwambie mtu,wakati bata inaendelea kuna mshangazi mmoja akawa yuko very interested na mimi,huu mshangazi tuupe jina Bena

Bena yeye ni mdada mrembo,muda wote ilikuwa kavaa cape yake nzuri ya NY,yeye tofauti na wenzie alikuwa na utulivu sana anakunywa kinywaji chake ila simuoni kama kalewa kama wenzie ambao wanachezacheza mziki na stori nyingii!Bena akaniambia yeye mwenyeji ya kanda maalumu ana mume na mtoto mmoja,basi tukajikuta kama tume click sana mimi bila kujua kwamba niko kwenye target!kama ni movie basi hapo director Mel Gibson angeshauri niwekewe kale kadoti ka rangi nyekundu kutoka kwenye AK47.

Binafsi mimi huwa sio muongeaji sana hasa kwa watu wapya,hii inanifanya wengine wanione nina maringo,wengine wanione mshamba,sasa nadhani Bena aliniweka kwenye kundi la washamba.Akaanza kuniambia yeye hapendi mitoko ya fujoo na amehisi ameshabihiana sana na mimi kitabia kama sitojali weekend ijayo twende zetu sehemu tulivu..Mmh nikaanza kujiuliza huyu huu urafiki mbona ghafla au anataka kunibaka nini? maana huu mji watu wamachanganyikiwa sana kumbe nilikuwa nawaza ujinga mtupu!Bena yupo kikazi hana hayo mawazo ya kijinga,kifupi huyo Bena hata via vya uzazi nadhani vilishakauka,tukabadilishana number fresh hiyo siku ikaisha kila mmoja akatawanyika!

JUMATANO
Bena akanipigia kunisalimia na kuniuliza nilifika salama?nikasema nilifika salama akasisitizia nitakuchek basi weekend tupeane michongo ya maisha mdogo wangu,nikasema sawa hamna shida,ijumaa akanichek nikamwambia labda jumapili baada ya ibada tunaweza kuonana kwa Mwamedi kitimoto panafaa,basi tukakubaliana tuonane,kumbuka hapo Andy hajui kama marafiki zake tumekuwa marafiki mpaka wa kwenda kula kitimoto pomoja! kama sio USALITI ni nini jamani?hii haina tofauti na kucheat🥲.

JUMAPILI.
Baada ya ibada nikakuta missed calls zake mbili na watsup chat anasema tukutane pale,nikamwambia nakuja chap!Nikafika kama kawaida kavaa Cape yake ya pink nzuri kaishusha fresh huoni macho hadi muwe karibu,safari hii nikamuuliza unapenda sana kofia?akasema unajua mimi nina aibu sipendi kuangaliana na watu machoni,Basi tukapigapiga story huku tunamla mywetu tunashushia na kileo we maisha burudaaaaniiiii,Kumbe kwenye akili ya Bena ananiona mimi ni kageni ka jiji,na kashamba japo kanaishi jijini, Bena yuko tayari na bisu anajiandaa ili achinje mbuzi wake wa kafara!..
Zikaanza story za biashara kila mmoja kamwambia mwenzie mitikasi zake,yeye akawa analalamika biashara zake zimekwama,hivyo anahitaji apate pesa mahala ili arekebishe mambo yake,mimi moyoni "Tobaaaa yaani huyu mdada anataka kunifilisi haka kamtaji kangu ninakokadunduliza?riziki yangu yenyewe ya papatupapatu sasa huyu mbona anataka kunitoa mchezoni?nikawa namsikiliza kimwili nilikuwa nae ila kiroho nilikuwa mbali sana!
Anaongea taratibu ni mstaarabu sana nakumbuka akaniuliza
"Hivi Joh umewahi chukua mkopo benki?
Nikasema hapana nimeshachukua Brack microfinance ndio namalizia marejesho matatu yamebaki.
Akasema aah sawa,Unaonaje tuchukue mkopo wa M30, tugawane tufanye biashara tuwe tunalipa wote?
Nikabaki nashangaa,M30 nachukuaje huko benki kwa Biashara gani?kwa dhamana gani? Sikuwa na majibu ila Bena the master plan alikuwa na majibu yote....
Nimechoka.
Alamsiki.
Story ndefu aliyeelewa alete summary. Watu hatuna muda wa kusoma soma hadithi.
 
Back
Top Bottom