Pesa inaweza kuja kwenye maisha yako bila kutarajia

PAt 3..[

Basi bwana,siku moja tukawa tumetoka mimi,kaka Muddy na Bena tukawa tumekaa mahali mara wakaja wakaka wawili wanashida na wao na mchakato,kuna muhaya mmoja much know kama Mwijaku,yeye anafanyaga kazi na kaka Muddy anatafuta vichwa huko anawaconnect wanapiga kazi,basi pale pombe pombe story za michakato ndio nikaanza kugundua siri nzitonzito, ila kwenye zile stori Bena alikuwa kama anazuia sana hizo stori lengo lake nisielewe chochote lakini si unajua tena kuna watu ni vichwa panzi wakishalewa huwezi kuwa control.Basi yule Muhaya akaniomba namba yangu nikampatia akasave nikasave ya kwake pia,
Basi yule muhaya na yeye alikuwa anataka lile lile duka ila yeye anaenda benki nyingine,kwa hiyo akawa anakuja kushinda pale dukani na yule mteja wake na yeye ajue bei ili siku afisa wao akija yeye ndio awe mwenye duka.
Sasa siku hiyo yule mwenzie akapata udhuru hakuna dukani ndio tukashinda pale dukani karibu siku nzima mimi na Muhaya,jioni nikasema ngoja tukale sehemu ndio tuondoke,Tulivyofika kula muhaya akaagiza bapa akawa anakunywa huku tunaweka stori mbili tatu za michakato ugumu na mafanikio yake,pombe bwana hazinaga mambo ya uongo uongo pombe zenyewe zinajisemeaga ukweli!

Muhaya akaanza kuniuliza nanafahamiana na Bena tangu lini?nikamjibu ninamjua siku nyingi kiasi,sasa pombe zilivyokolea akaanza kunipa mafaili ya Bena!
Bena ni tapeli wa kimaitaifa,yeye ana madeni kila kona ya Dar,ndio maana muda wote anavaa cape anajificha!Bena ana misala hakuna cello haijui!sasa siku hizi michezo yake anatafuta vichwa safi,ambao hawana recoding chafu anasimamia show pesa ikitoka anakupanga vizuri halafu anapotea nayo,akasisitiza anatumia sana Ushirikina,kwanza Bena sio mkurya kama alivyokwambia ni Mnyaturu hatari sana.Akaniuliza wewe hujaenda kwa ustaadhi kumsomea manager?nikasema nilienda akasema na wewe ulikuwa unatulizwa akili!nikasema heeee muhudumu ongeza kasichana hapa na Serengeti baridi!
Muhaya akawasagia kunguni ile mbaya wenzie,yeye ndio akawa mwema,akasema amemsikia Bena akijigamba safari hii ameletaa kichwa safi hajui mambo yoyote ya mjini!nikasema ni kweli mimi nilikuwa namuamini tutakuwa washirika Muhaya akasisitiza weweee tumia akili UNAPIGWA hizi hela zikitoka!
Pombe yote iliingia ila zilikata ndani kwa ndani,ile siku ikapita nikiwa tayari nina mwangaza nipo kwenye situation gani ikawa najiuliza Nibwage au niendelee,malaika wa maasi akaja kukaa began akaniambia "TWO CAN PLAY THIS GAME"!Hakuna kutoka unaacha vipi hela wewe Joannah? wape show!

Mwezi wa pili katikati tangu tuanze mchakato afisa akasisitizia wiki hii mzigo utatoka ila itatoka 25M,hiyo ni baada ya nyumba yangu ile kufanyiwa evaluation,Ila yeye na manager wakataka wapewe 1M,nikasema sawa,

Hapo Bena moyoni kabeba roho ya DHULMA,Ananipanga vizuri nikae kwenye target ili iwe rahisi kupita na hela zikitoka,Bena kila siku ushoga umekolea ananiita tu mdogo wangu kwa upendo,ananipa mikakati ya kutumia pesa vizuri ikitoka na mimi nimetulia kimya ndio nikawa nazidi kujifanya mshambaa sielewi chochote nikasema rohoni mwaka huu ndio utajua kama Nina cheti cha UDSM ambao hakinisaidii chochote kipo tu kabatini!

MZIGO UKATOKA!
Nikapigiwa simu na afisa,sister kesho uje asubuhi na mdhamini hela itoke,kesho yake Bena na Muddy saa kumi na mbili wananipigia simu nitoke nisichelewe,wao ndio wa kwanza kufika huko mbagala kabla sijaingia benki wakanimbia mzigo ukishaingia nitoe wote nitoke nao nje,nikasema sawa...msisahau na muhaya akawepo hapo kwenye huo mzunguko,nikazama benki na mdhamini tukawa tunaendelea na process

WALINZI WANGU WAKO NJE;
Baada ya kujua zile taarifa kutoka kwa muhaya siku za nyuma nikampigia mshkaji wangu mmoja mkaka wa Chuga,ila yupo Dar anasukuma maisha huku,huyo ndio mafia balaa mwenyewe anajitaga Patrol,nikampa mchongo mzima,akaniambia aisee acha ufala umpe hela nusu kwa nusu huyo malaya kivipi na benki wanakujua wewe?hamna kumpa hapo unarudisha tu hiyo hela ya mchakato hakuna kutoa hela kizembe! Akasema siku pesa ikitoka niambie nije nisimamie show! Basi ile siku naingia benki akaniambia niko nje nakusubiri ukitoka tu gari nyeusi Harriern,Na hela ikiingia toa milion mbili tu ndio toka nazo!
Basi wale kina Muddy na Bena na Muhaya wako attention utasema fisi wameona mzoga!mpaka saa nane Meseji hiyoo haikuwa 25M kamili ,ilikuwa na makatomakato, kama nilivyopewa maelekezo nikatoa 2M dirishani nikaweeka kwenye pochi nikatoka nje,yule mdhamini kanibana kisawasawa pembeni yangu ile natoka nje namuona Patrol akaniita namkuta ana Harrier mpya nyeusi tinted yuko na mkaka mwingine ambaye simjui anasema panda twende!mdhamini anasema yeye hapandi kwenye gari nyeusi tusogee kwa mguu hapo kwenye baa si mbali,akaanza kuweweseka anawapigia simu kina Muddy,we ghafla hawa hapa !Basi tukatembea mpaka kwenye hicho ki bar tukawa wote,nikawaambia hawa ni kaka zangu kuna sehemu tunaenda wamenifuata,Muddy kaanza kukoroma kwa nini nawaletea watu,nikasisitiza ni kaka yangu,kaka asema kwani vipi mbona unafoka sana bro?[lafudhi ya Arusha]Muddy anasema hapa hakuna namna tufuate makubaliano mzigo uwekwe mezani nusu apewe Bena na tulipie baadhi ya madeni tunayodaiwa!

Patrol akasema toa hela Joh,nikaweka 2M mezani nikasema nyingine sijatoa,we Muddy karukia pochi kufungua hola!ikawa Tafrani na mzozo pale,Bena yupo kimya anajifanya mwema, akaniita pembeni akasema basi kama hivyo anomba kwanza ile 2 tulipie tunavyodaiwa halafu jioni tutapanga vizuri mambo yetu tusiruhusu wanaume watuharibie mipango yetu mizurii,nikasema sawa,basi akatuliza hali ya hewa pale nikakubali kuacha ile 2M pale,Yaani shetani kasimama pale kungekuwa na mtu ana bastola ningekula ya kichwa!Mimi nikaingia kwenye gari ya kaka yangu wa mchongo Patrol huyoo,hawajaamini nimekuwa mtu mwingine kabisa!Namsikia Muddy anamlaumu Bena unaniletea mtu gani huyu Jambazi kabisa!Bena unaniletea majambazi unataka kuniua?mimi huyo nimekaza komwe ndukiiiiiii.
 
Story ndefu aliyeelewa alete summary. Watu hatuna muda wa kusoma soma hadithi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…