Pesa mtaani zimepotelea wapi? Je, biashara yako inaendaje?

Pesa mtaani zimepotelea wapi? Je, biashara yako inaendaje?

Hii nakuelewa kiasi
Ujui unaye bishana naye ni nani ? Hichi ninacho kuambia ndiyo kinacho sababisha kwa asilimia 100% mafisadi kipindi hiki yapo tayari kununua nyumba yenye thamani ya sh mil 200 kwa shilingi mil1000 = 1bil dubai kuliko kujenga nyumba 5 kama hiyo waliyo nunua dubai nchini.
 
Mbona JPM alikuwa akimwalika Ikulu?
Kwani unadhani alikuwa anamualika ili iweje ?...huyo rostam azizi anacheza tu na upepo ... wewe unadhani ni nini kilitokea hadi mbunge jangiri ambaye ni mdogo wake rostam azizi kukamatwa kwanini akufungwa jela .. huyo jamaa kabobea katika mbinu maana anatumia pesa zisizo zake yeye anachota tu serikalini.
 
Tatizo kubwa ninaloliona ni pesa nyingi kwenda Chin na Japan, maana hata dollar haipatikani muda huu, lazima ukainunue kwenye blaack market, na inauzwa 2,700/=. Shida hapa ni capital nyingi inatumika kuagiza magari na bidhaa nyingine za kijinga jinga toka China na Japan, tunabaki hatuna pesa mtaani, na magari namba E yamefurika barabarani, pesa itatoka wapi?
Tutafanya nini labda kampuni zije kuwekeza huku Tz tynunulie hukuhuku tugawane hizo pesa kupitia ajira na kodi
 
Mnafikiri trilioni mama alizokopa zinarejea vp,anakopa then anakusanya kodi anarejesha alikokopa ndiokinachofanyika wkt mwingine analopa na kwenda rejesha alikokopa mwanzo,our economy ipo hali mbaya ndio maana mfumuko wa bei upo juu sn
 
Cheki hii ndondocha ya CCM. Chadema lini waliongoza hii nchi? Mbona unajitoa ufahamu hivyo? Wizi na ubadhirifu unaofanywa na ccm huoni. Nchi hii Kila kitu ni shida iliyosababishwa na ccm huzion. Unakimbilia kuilaumu chadema.

Chadema ndo wanakusanya Kodi. Ndo watunga sera na Sheria?
 
Kuna tatizo, tunahitaji wataalam wa uchumi watueleze kuna nini.

1. Je kodi inakusanywa lakini hiyo pesa hairudi mtaani kiasi cha pesa kupotea mtaani?

2. Serikali haitoi ajira ya kutosha?

3. Miradi mikubwa zinapewa kampuni za kigeni tu?

4. Mafisadi wanaficha pesa nje?

Sijui mkuu
Jibu ni kuwa majizi na mafisadi yanaiba na kwenda kuficha Hela nje ya nchi..
 
Utawala wa JPM ndo ulikua ovyo kabisa tatizo waTZ unafiki mwingi.... Biashara kubwa zilifungwa, Pesa ilikosekana mitaani,Ongezeko la Nyumba (Ujenzi) lilidorora, Biashara ya Magari ikawa ngumu amejngia ameikuta No C mpaka anaondoka miaka 6 ameacha No D,.. Alishindwa kuajiri ktk kipindi chote, Ata waliokua wameajiriwa alishindwa kuongeza marupurupu na Mishahara...Ilifikia mahala akawa anataifisha fedha za wafanya biashara kwenye MaBank akichungulia akakuta kuna Bilion kadhaa akaunt inafungwa unaitwa Dodoma ili utoe kadhaa lasivyo Panga la uhujumu uchumi litakukumba ikatungwa sheria onevu ya Plea bargaining... JPM akalipeleka Deni la Taifa ktk kipindi chake cha Miaka 6 likawa Kubwa zaidi ya miaka 20 ya Mkapa na JK....Anyway waTZ wengi walikua Brainwashed na mapambio ya lazima ya JPM ata km Vyuma Vilikaza.... Maskini Kaingia Mama wa Watu mambo yameanza kunyooka japo sio sana Leo angalia Sekta ya Majumba yanavoporomoshwa uko Mitaani, Angalia Sekta ya Biashara ya Magari ilivorudi kwa Kasi hadi saivi vijana wanasukuma ma Range... Watumishi karudisha stahiki zao na saivi wanapandishwa madaraja, Ajira zimeanza nk nk.... Tusiwe wanafiki ukisema Biashara zinakufa na maframe yanafungwa sawa funga wewe Achia chumba kesho anaingia mwingine na mishemishe zinaendelea km kawa...
 
Bora wewe umefanya tathmini ukagundua umedrop Kwa kiasi gani? Tangu January 20 upatikanaji wa hela umekua mgumu sana inafika point unajaribu kubalance mambo yaende upate tu hela ya kusurvive
Mi nilidhani kariakoo biashara ni nzuri siku zote ni kupiga pesa tu
 
Kikwete na wanamtandao wenzao walishikwa mfukoni uchumi ukahamia mifukoni mwa matapeli! Ilifia hatua serikali ilikopa hela kwa watu binafsi kulipa mishahara!
Magufuli ndo aliididimiza zaidi nchi kwa kutumia theories zilizoshindwa kwa wengine!

Swali ni jee, hizi data tunazopewa na TRA na BoT zinapikwa? Hakuna reflection katika real life juu ya kinachohubiriwa na hao watu.
Magufuli alididimiza nchi vip wakati alikuwa anarekebisha makosa ya Msoga?Hela zipo kwa watu tena walioiba serikalini ulitaka Magu afanye nini? Kulikuwa na kesi nyingi za ufisadi, ila mahakama wakawa wanazipiga kalenda mpaka Magu kwenye tukio la mahakama kutimiza miaka mia Magu aliomba zile kesi za ufisadi zisikilizwe na zisizungushwe kwani kupitia zile kesi Magu alikadilia serikali ingerudisha zaidi ya Trilioni 300.Hata kama serikali isingepata hizo 300tr sizani kama ingekosa 50tr.

Mkaanza kumlaumu humu anaingilia uhuru wa mahakama. Baada ya kuona mahakama wanamzingua akaamua amalizane nao kihuni kwa kuwaambia wakirudisha kiasi fulani za fedha yy anafuta kesi. Huwezi kumlaumu Magu wakati mfumo wa Mahakama ulioza.Hii changamoto ndiyo aliyo kutana nayo Rais wa Angola nae akawa mbabe kwa kuzikama mali za familia ya aliyekuwa rais aliyepita Dos Santos,kwani hii familia inaukwasi wa kutosha Dos Santos mpaka anatoka madarakani ana utajiri wa zaidi ya 20 Bil USD huku binti yake akiwa mwanamke tajiri Afrika kwa kuwa na 4B USD.Familia kama hii ukiipeleka mahakamani,kama mahakama hawatokupa ushirikiano basi kutoboa ni shughuli sababu wana hela za kuhonga na viongozi na watu kibao alizizuia mali zao.

Hamna mtu aliyekuwa akijenga nidhamu ile ya kula kwa jasho/akili kama Magu na ndio ndio nidhamu ambayo wenzetu wa ulaya wanayo. Magu kupambana na Mgao wa maji na umeme,hata huduma za kijamii ulikuwa unapata kwa haraka,kulikuwa hamna unanijua mimi nani. Sasa hivi tunabadilishiwa nyimbo mara vyanzo vimekauka,mara sijui transmission line mara hivi mara vile, siku hizi raia kwenda kupata huduma za kijamii unapoteza karibia siku nzima.

Ukija kwenye dollar imepotea ghafla na speed yake ya kupanda ni kubwa mno mpaka unaogopa na hili ndilo lina waumiza wafanyabiashara.Magu kun taratibu aliziweka,kidogo zilisaidia kwenye sehemu za kubadilisha fedha na kuimonitor BOT kwa ukaribu ila sasa daah. Juzi namuona Stivu Nyerere wamekodiwa ndege na wenzake kwenda mbuga za wanayama ili kuhamasisha utalii yupo na kundi la watu kama 20+,ile nidhamu ya hela ya serikali hamna.
 
Nimemsikia Leo Mabeyo anasema kabla ya Magufuli kukataa roho aliitwa Mzena akaambiwa Hali mbaya, Magufuli naye akamwambia Mabeyo wewe ni CDF waamuru haw wanirudishe nikafie nyumbani siwezi kupona.

Baada akaomba aitiwe paroko wake wa Saint Peters oysterbay na Kardinali Pengo.

Baadaye ya kukata roho Mabeyo ndiye aliyeambiwa, akamuita waziri mkuu na Bashiru wakaulizana Nani anapaswa kutangaza ikabidi waangalie katiba, hapo Mama aliwekwa pembeni na Mabeyo.

Hadithi hii inatufundisha Mabeyo alipewa fursa na Mungu kuwakombowa Watanzania lakini alishindwa kuitumia.

Kuyaondowa haya mashetani ya CCM itatuchukuwa muda Sana.

Hivi Una mtu kama Dr Kimei na hayumo kwenye cabinet umejaza Wahuni na machawa tu, mnatarajia unafuu upi wa Maisha?
Hiyo paragraph ya mwisho hata mimi huwa na jiuliza yule Kimei ana sifa zote nikitizama alipo itoa CRDB sina shaka juu ya uwezo wake.
 
Back
Top Bottom