Pesa sio kitu pekee cha kumfanya mwanamke atulie na wewe kwenye ndoa au mahusiano

Pesa sio kitu pekee cha kumfanya mwanamke atulie na wewe kwenye ndoa au mahusiano

Zero Competition

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2018
Posts
347
Reaction score
553
Siku hizi kuwa na pesa sio kigezo cha kumfanya mwanamke wako au mke wako atulie kwenye ndoa au mahusiano yenu.

Hili limethibitishwa na alichokifanya yule afisa wa Equatorial Guinea ambae ametembea na wanawake wengi na kufanikiwa kuwarekodi wote na kibaya zaidi hata wale wanawake wenyewe walikua wanajua fika kwamba mwamba anarekodi video na wao wenyewe wametoa ushirikiano wote kuhakikisha video inatoka vizuri.

Umeshajiuliza wale wanawake aliotembea nao jamaa wanakosa nini kwenye ndoa zao ? mana wengi wao wako na wanaume wenye pesa kiasi kwamba pesa kwao sio tatizo lakini wamethubutu kutoka na kwenda kumtunuku mwamba vipochi manyoya.

Watu wengi wanaamini ukiwa na pesa unaweza kumtuliza mwanamke yeyote kitu ambacho sio kweli mana karibu asilimia 80% ya wanawake hawajui wanataka nini.

Wanaume tujitahidi kutafuta pesa ili tukimbie umasikini ila sio kwamba pesa zetu zinaweza mfanya mwanamke akatulia kwenye ndoa au mahusiano.Tafuta pesa uishi maisha ya ndoto zako na watoto wako.

Pesa haiwezi nunua hisia za mtu au akili zake ingawa ni muhimu kuwa nayo.
 
Dah kweli kabisa, unaweza kuwa na pesa na mke wako ukampa kila kitu lakini akakusaliti, inauma sana, tutafute hela kwa ajili yakujipa furaha wenyewe.
 
Back
Top Bottom