Pesa ya Tanzania inatengenezwa na kampuni gani?

Pesa ya Tanzania inatengenezwa na kampuni gani?

Pesa zote duniani zinafuata kanuni ya shirika la pesa duniani, huwezi ukatengeneza pesa kiholela. Kuna wakati sijui kama ni utani, Amin aliprint pesa kwa wingi, ndio maana uchumi uliporomoka na thamani ya pesa ikashuka.
 
Habari wana JF,

Baada ya mihangaiko ya hapa na pale ya kutafuta chochote ilimradi mkono uingize kitu kinywani, nimejikuta najiuliza sana haya maswali kuhusu pesa ya Tanzania

- Je, ni kampuni ipii inahusika kutengeneza na kuprint pesa ya Tanzania?
-Iyoo kampuni ikoo wapi na ni private au goverment?

- Kama serikali inahusika kuprint pesa mbona serikali inadaiwa mabilioni kutoka nje ,kwanin isiprint pesa za kutosha na kuweza kuwalipa wanaotudai

-Kwanini Tanzania isitengeneze kampuni ya kuprint hela, kama kutimiza sera ya mheshimiwa Tanzania ya viwanda?

- Kwanin thamani yetu ya pesa ishuke,na vyuma vikazee (hali ngumu ya maisha kwamba pesa hamna), wakati serikali inahusika kwa asiliamia mia katika kuprint pesa?

-hiyoo kampuni inayotengeneza pesa wafanyakazi wake wanalipwa nini? Kwa sababu huwezi kuwa unazalisha mahindi wakati huo huo ulipwe hayo hayo mahindi kama mshahara.

Natumaini humu JF kuna great thinker na wataalamu wa kutosha kuhusu hayo mambo,,, naomba kueleweshwa kwan mpaka sasa sielewi inakuaje.
Pesa ikiwa nyingi kitaa unaelewa madhara yake lakini? Tuanzie hapa kwanza...
 
Sio kweli, pesa za Tanzania zinachapwa nje ya nchi miaka yote.
BoT wanatengeneza kila kitu. But hyo issue iko chini ya uangalizi wa TISS ndo maana kuna propaganda eti fedha zinatengenezwa nje ya nchi.
 
De La Rue ni Public company iliyosajiliwa UK. Ilianza kutengeneza notes tangu Karne ya 18. Pia inatengezeza vitu vingine Kama makaratasi ya kuchapisha pesa, stamp, passport na kadhalika.

Ingawa hii ni kampuni ya UK lakini walipoteza mkataba wa kuchapisha passport za UK kwa kampuni ya France.

Hilo Kenya ni branch tu ya kuchapisha pesa za Africa.
 
Back
Top Bottom